Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumamosi, Januari 26, 2013

Majibu Yafanyayo Kazi - MAWE MATANO


Ngoja nikwambie msomaji wangu jambo hili, 
kwamba:
MAJIBU YAFANYAYO KAZI 
Ni kipengele kinachoongelea masuala ya kiroho zaidi.
Kwa sababu ya upekee na unyeti wa siku, Sio vibaya tukibadilishana mawazo na kuambizana yaliyomuhimu katika maisha hasa ya kiroho.
Na huu utakuwa ni mfululizo kwa kila siku kama hii ya leo...
(Ninamaanisha JumaMosi)

Pamoja na kwamba weeengi wanaamini hii ni kweli, kweli halisi jionee mwenyewe ambapo tutatijifunza:

MAWE MATANO (5) YA KUMSHINDA GOLIATH  THE GIANT!

Imeandaliwa na Pr. Filbert Joseph Mwanga

Mwanadamu ni kiumbe kidogo katika ya viumbe walioumbwa na Mungu. Lakini ambaye dunia imemtengenezea silaha kali za nyuklia, mizinga na mabomu, n.k. ili kumuua na kumfutilia mbali. Silaha zimewekwa angani – zote hizo sio kuangusha milima- la bali kumuua mwanadamu.

Ndipo swali linakuja kwangu – je watu hawa akili zao ziko sawa? Mtu ambaye anauwawa na mbu tu wa malaria – ‘anopheles’  kuna haja ya kumtengenezea mabomu yote hayo? Silaha zimewekwa angani yote hiyo ni mwanadamu. Silaha hizi zinamsaka mtu ambaye halingani wa karne kama Goliath? Goliath ni nani? THE GIANT! JITU LA MIRABA MINNE!

Goliath aliongoza kambi ya wafilisti akiwa kama mwanaume wa shoka – mtu wa vita tu! Soma 1 SAMWELI 17:1 – 2. Wafilisti walijipanga kwa ajili ya vita. Mbaya zaidi vikawa ndani ya mipaka ya Yuda. Ikiwa kuna vita vibaya kuliko vyote ni vile ambavyo vinapiganwa NDANI YA KAMBI YAKO! Kisa cha Amerika na Iraq – Technical Defensive Matching. Mchezo huu ni mbaya hata kwa timu za mpira wa miguu. Wanapojihami na kurudi nyuma ndipo wanapofungwa maana mpira unachezewa ndani ya goli lao na hivyo wamekaribisha wameshambulizi wenyewe!

Wapagani hawa wamehamishia vita ndani ya mipaka ya Israeli. Kama kuna vita vibaya vya kiroho ni vile vinavyopiganiwa ndani ya mwili wako. Zipo dhambi zinazotendwa ndani ya mwili na nyingine nje ya mwili. 1 CORINTHIANS 6:18, 16 – 17. 

Paulo anataja dhambi hizo ZINAA. Ndani ya mwili. Bali uongo ni nje ya mwili. Uvunjaji wa kanuni za afya ni NDANI YA MWILI. UBINAFSI ndani ya mwili tena unakula taratibu lakini kwa hakika. Unataka kuhudumia MIMI kwanza! Mzee wa kanisa au kiongozi wa kwaya anapokuwa mzinzi kanisa, familia, watoto au kwaya inapoteza mwelekeo. Maana wamekaribisha adui ndani ya ngome. Kiongozi yeyote anapokuwa MBINAFSI kama ni serikali au kanisa anatafuta kufanya huduma zote yeye tu, ataanza kung’ang’ania madaraka yote, na hata akiona wengine wanafanya vizuri hatopendezwa maana anabaki kuuona MIMI anaguswa. Hivyo vita vyake vitapiganiwa moyoni! Ataanza kuonyesha hasira, uadui, kisha unaanza kujihoji kuwa umefanya nini – unajifikiria kuwa kuna tatizo gani? Hakuna lolote makosa anayokutoa na kashfa anazokupa na mateto – ni sababu ya PIGANO LINALOENDELEA MOYONI UBINAFSI!

Maumivu makali ni yale yanayomuumiza mtu kwa ndani. Unaweza ukamuumiza ndugu yako kwa kumpiga na fimbo au chombo chochote kikali na akabaki na kovu; lakini KOVU baya ni lile linalobaki moyoni. Waswahili walisema maneno ni sumu! Kwanini? Maneno ni vita vinavyokwenda kupiganiwa Moyoni – vita ya ndani!  Ndoa nyingi zina watu wanaojua kutoa maneno mabaya – na hayo ndiyo yanayoleta talaka na wala sio ngumi pekee! Bali masimango kwa mumeo au mkeo au watoto! Maneno ni SUMU!

1 SAMWELI 17:3 Majeshi yote wapo katika milima - Israeli na wafilisti. Milima wakati wote inawakilisha – IBADA. ENEO LA IBADA! Inategemea aina ya Mungu unayemuabudu. Israeli ni Mungu wa mbinguni. Wafilisti ni mungu Dagoni. Mungu atakayeshinda vita ndiye mkuu. Tatizo la Israeli wamepanda kwa Mungu wa kweli – lakini katikati yao kuna bonde la ELLA! Hilo ndiyo tatizo kwa Israeli. Wafilisti walizoea mabonde – Shinari, Timna, Gaza, n.k. unaposoma Biblia bondeni inawakilisha MAPOROMOKO YA KIROHO!

Mfalme wao ambaye ni Sauli – amekuwa na ibada nyingi. Pamoja na kuwa wapo milimani –wapo kaika pigano ambalo halina Mungu wa Kweli kati yao. Wote wakapoteza tumaini lao kwa Mungu – wakaona kushindwa mbele yao. 

Fungu 4. Hebu tumuelewe GOLIATH – the Giant! Israeli pamoja na kupanda juu ya Kilima – hawamuoni Mungu wa Kweli – bali GOLIATH – kushindwa! Kwanini? Goliath ni mtu mrefu wa futi 9. Kizazi chao ni watu wa ajabu. Mwingine alikuwa na vidole 24. (2 SM. 21:19-22). Kabila lake ni mrefai – the Giant. Dirii aliyokuwa amevaa ni kg. 50 – mfuko wa sementi! Kichwa cha mkuki wake ni kg. 7. Unawezaje kupambana na mtu aliyekuzidi urefu, uzito na hata umri wewe mtu uliyemfupi tu wa futi 4 au sana sana 6.5? Tena huna uzoefu wowote?!

Lazima kuna siri kuu. DAUDI mwana wa YESE anajua siri hiyo! Soma 1 SAMWELI 17:45.  Kumbe ni JINA LAYESU! MWAMINI YESU NA MANABII WAKE NAWE UTATHIBITIKA! 2 NYAKATI 20:20. 

Unaweza ukaona kila kitu mbele yako kuwa ni kitu cha kutisha – hata ukapoteza mwelekeo. Huenda ni ugonjwa – the giant! Kukosa ajira – the giant! Kukosa mchumba – the giant! Kutafuta wahubiri ni dhambi inayokusumbua – the giant! Dhambi – zaka na sadaka – the giant! GOLIATH! Hivyo unakata tamaa – unalia moyoni. Maumivu ya kiroho – spiritual anguish! Kila siku ngambo ya pili ukiamka asubuhi unaona Goliath amesimama maneno makali kama mkuki moyoni au ubavuni mwako! Hakuna amani kanisani, nyumbani, kazini na majirani! Badala ya kumuona YESU siku ya Sabato – mlimani kwa Bwana unamuona Goliath! Hutamani kurudi nyumbani unaona ni bonde kubwa utakalozama na kutobolewa macho kama Samsoni. 

Hata ijapokuwa muhubiri anasimama saa tano – wengine ndiyo Goliath – Usingizini anaonekana lakini kwenye masengenyo na mateto  macho yote pima! Hata ijapokuwa YESU ameinuliwa juu ya mlima wa Golgotha – bado hatuwezi kumuona Yesu bali Goliath – the giant! Huku akinguruma kiasi ya kuwa unataka kuacha vita vya kiroho na kuvaa silaha za mwili – giza yaani kutumia UBINADAMU kulikabili TATIZO! Huenda hali ya uchumi imekuwa ngumu – sasa watoto hawana ‘school fees’ – naacha kukaza mwendo naogopa na kuvaa silaha za wizi wa zaka na sadaka ili kutatua tatizo!

Kumbuka Israeli kila siku asubuhi walipojipanga hawamuoni BWANA bali GOLIATH – kwao ni utisho tu. Fungu 8 – 11. Tangazo limetolewa kuwa anatakiwa mtu mmoja tu. Atakayesimama na kupambana na adui mmoja. Katika Israeli mtu aliyekuwa anamkaribia Goliath kwa urefu – the giant ni SAULI sio JESHI lote! (Mtu mmoja sio KANISA LOTE). 

Kumbuka Sauli tayari ana mapepo. 1 SAMWELI 16:23. Je mtu aliye na pepo la ubinafsi, uzinzi, anaweza kuongoza jeshi la Bwana? Hapo ndipo taifa lote limepoteza mwelekeo. Huwezi kumtegemea mtu aliye gizani akuongoze katika vita vya ulimwengu. Unaumwa na una mapepo unaenda kwa MGANGA wa kienyeji? Tegemea anguko. Pia kujiongezea mapepo zaidi.

Daudi mwana wa Yese alijua namna kulikabili JITU! Fungu 40. Usikabiliane na jitu bila kuendea KISIMA CHA MAJI YA UZIMA! YALE MAWE MATANO yapo pale kisimani na wala sio bondeni au tambarare, LA! MAWE MATANO LAINI YAPO PALE YA USHINDI! Baada ya kupata mawe hayo ndipo umwendee Goliath – the giant! Ushindi ni wa LAZIMA! Leo nitaanza na JIWE la kwanza aliokota Daudi. Nalo ni KUAMINI JINA LA YESU! ZABURI 20:7 Tatizo la Israeli waliacha Jina la Yesu wakitumainia Jina la Sauli. MATENDO 4:11-12. Hakuna Jina lingine isipokuwa Jina la YESU MNAZERETI! KISA CHA CAMPOREE KENYA – MTOTO NA KAFARA!

Unaposimamisha Jina la Yesu – hakuna mwanadamu au jeshi litakalosimama. Soma CLEAR WORD  inasema, Israeli na Sauli “walipoteza ujasiri wao baada kuona the ‘giant’ – Goliath.  Huwezi ukamuona mwana wa Adamu ukawa muoga na kupoteza matumaini. Mitume walipomuona YESU aliyeangikwa msalabani na sasa YU HAI walikuwa ‘Courageous’ – walitiwa shime kuhubiri Jina la YESU bila woga. 

Daudi alitumia Jiwe LAINI – NIRA LAINI YA YESU! Tumaini la kushinda tatizo lolote linapatikana kwa YESU anaposema leteni mizigo yenu yote mpate kupumzika. Kila jambo gumu kuna ushindi uliofichika kwa Yesu. Siri kuu ni kumtegemea YESU kwa asilimia 100% sio kutegemea Helmet, Dirii, fumo, n.k. hizo silaha zote hazikumsaidia Sauli. Tambua hili SHETANI hatishiwi na muda mrefu wa kuishi kanisani. Ikiwa hiyo ndiyo ‘Defensive Mechanism ya Kiroho’ nataka nikupe pole maana Shetani ni giant! Daudi alijaribu vyote hivyo akagundua hawezi kumshinda Goliath na mambo hayo! Alikumbuka Yule Simba wa Kabila la Yuda! 

Uzoefu wa kukaa kanisani au kusoma Biblia na kujua mafungu mengi – hauwezi kumtisha Shetani. Bali uzoefu katika kutumia silaha ya Jina la Yesu katika shida zako – ni ushindi usio na mpinzani! Shetani ANALOOGOPA NI JINA LA YESU – JIWE MOJA! JIWE KUU LA PEMBENI! MWAMBA ULIO IMARA! WIMBO 192! MWAMBA WENYE IMARA KWAKO NITAJIFICHA! IMARA – MADHUBUTI. FUNGU 45. KISA CHA MTU ALIYEKUFA KWA AJILI YA NG’OMBE!  Msimamishe Yesu Mnazereti kwa Jina hili ni USHINDI!

SOURCE: INGIA HAPA
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni