Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumamosi, Oktoba 06, 2012

SATELITE NET EVENT KAMPALA 2012

Picha kwa hisani ya: http://www.hopetv.org



Maneno SATELITE NET EVENT KAMAPALA 2012 yakitumika bila kutafisiriwa yanabeba maana iliyo bora sana kuliko yakitafsiriwa. Kwa kuwa ndiyo maneno yabebayo tukio la satalaiti, ni vizuri kutoa tafsiri ya jumla itakayosaidia wengi kuelewa jambo hili tunalolipigia mbiu. Inawezekana kabisa kuyatohoa na kuyatumia kama yalivyo, lakini kwa faida ya wengi tafsiri rahisi tunayoweza kuitoa ni Mahubiri ya Satalaiti ya Kamapla 2012.

  • Baada ya kuelewa maana hii, makanisa yanaweza:
  • Kuyatohoa na kuyatumia kama yalivyo.
  • Kutumia tafsri tuliyoitoa.
  • Kutumia yote mawili; kuyatohoa na kutumia tafsiri tuliyotoa.


AGIZO LA UTUME WETU
Agizo la utume la kuwafikia watu na habari njema ya injili siyo wazo jipya kabisa katika uelewa wa Waadventista wa sabato. Agizo hili limeelezwa wazi katika maandiko likiwa na msisitizo wa utolewaji wa habari njema kuwa ushuhuda kwa mataifa yote. Agizo hili limeandikwa kwa namna nzuri karibu katika sura tatu tofauti za Biblia; Mathayo 24:14, 28:19-20: na ujumbe wa malaika watatu Ufunuo 14:6-12.

MSUKUMO WA KITEKNOLOJIA
Ni muhimu sana kwetu kuelewa kwamba, jumbe hizi zinapaswa kwenda kwa haraka sana. Hatutaweza kufikia lengo letu la kile ambacho Mungu amekusudia tukifikie isipokuwa tunatumia njia ambazo zinakubalika katika kizazi tuishicho. Teknolojia imetuthibitishia ukweli wajambo hili kwa kadri tuonavyo ushahidi wa uhakika wa kile iwezacho kufanya kupitia nguvu ya Roho Mtakatifu. Kanisa katika ukanda wetu limewahi kupitia uzoefu wa nguvu ya teknolojia katika uinjilisti. Tunaweza kuuita uinjilisti kwa njia ya vyombo vya habari (Media Evangelism)

Idara ya mawasiliano imejiandaa kutumia njia zote za mawasiliano ili kutuoa ujumbe wa matumaini kwa wote wanaoweza kufikiwa. Kwa kuwa tunaishi katika siku za mwisho zenye changamoto mpya kwa kila siku ipitayo, unatiwa moyo kumjulisha rafiki yako, jirani yako, na kila mtu wako wa karibu kuhusu Mahubiri makubwa ya Satalaiti Kampala 2012.

Ninakualika kusoma kwa makini maelezo yafuatayo:

MAHUBIRI:
Mchungaji Blasious Ruguri.

Moto wa NET Event Kampala:
“NDIMI ZA MOTO WA INJILI”.

Kauli mbiu ya Utangulizi:
 “MOTO WA INJILI”.

AFYA, KAYA NA FAMILIA:
Yataletwa na wazungumzaji wenye uwezo na uzoefu mkubwa.
Nyimbo kupitia kwaya na vikundi vya uimbaji zitakuwa sehemu ya tukio.

TAREHE:
Septemba 29-Octoba 13, 2012. Matangazo yatakufikia katika kituo cha kanisani kwako na nyumbani kwako. Morning Star Radio  na redio zingine mbalimbali zitajiunga na mahubiri haya.

MAHALI:
Union ya Uganda.

ENEO LA TUKIO:
Kanisa la Waadventista Wa Sabato Bhunga.

MAWAKALA WA UTANGAZAJI NA KUREKODI:
ECD MEDIA CENTER na HOPE CHANNEL INTERNATIONAL watawajibika kwa pamoja katika uzalishaji. Pia watatoa taarifa na ushauri wa kiufundi kila itakapoonekana vyema.

Alhamisi, Oktoba 04, 2012

ENEO LINAUZWA














ENEO LIPO MBAGALA SAKU, 
BEI NI MILIONI 18 HAKUNA CHA UDALALI HAPO. 
IKIWA UNA NIA YA DHATI AMA KUPAONA
WASILIANA KWA NAMBA IFUATAYO:
+255 754 553 031

Jumatano, Oktoba 03, 2012

UKOMAVU WA BINADAMU


 Sifa za mtu aliyekomaa

1. Anayatambua mambo yalivyo. Anajitambua na kuwatambua wengine walivyo. Anatambua matukio pia katika sifa na kasoro. Anatambua yale anayoyaweza na yale asiyoyaweza. Hana wivu wala hofu. Anapima hali mbalimbali bila ya kufumba macho mbele ya mambo yasiyompendeza bali anatumia akili akabiliane nayo.

2. Anakubali hali ilivyo. Anajikubali na kuwakubali wengine walivyo. Akiona kasoro hachukii, bali kwanza anakubali hali ilivyo, halafu anajitahidi kuirekebisha iwezekanavyo. Hata akishindwa anakubali na kuvumilia. Vilevile anaweza kuyakubali mabadiliko na mambo mapya bila ya hofu, kwa kuwa anapima yote bila ya kufadhaika kwa kusema, “Itakuwaje?”

3. Anawajibika. Hangoji kuambiwa kila mara afanye nini na vipi, bali anaona mwenyewe anavyotakiwa kutenda, halafu anaamua kwa moyo ayatende. Ndiyo sifa kuu ya mtu aliyekomaa kweli: ana mwongozo wa maisha ndani mwake. Anazingatia pia kanuni za jamii na kusikiliza mashauri, lakini uamuzi wake unatoka ndani.

4 Anajiongoza kwa kuzingatia tunu alizojichagulia. Anaelekeza maisha yake upande fulani alivyoazimia. Katika kuamua la kufanya anafuata tunu hizo, si mkondo kama wanavyofanya kondoo.

5. Anahusiana vema na watu kwa sababu anawakubali, anawaheshimu na kuamini wanaweza kutenda mema. Anaelewa shida zao na kuwatimizia. Anawafanya wajisikie raha na kutokeza sifa zao. Mwenyewe anajisikia salama na kuwafanya washinde hofu zao na hivyo wakomae kwa urahisi zaidi.

6. Anafanikisha mipango. Ana mawazo ya kushangaza kwa kuwa mitazamo yake ni mipana na ya ndani zaidi. Mipango na miradi yake ni mingi, lakini haogopi kujaribu wala kushindwa, kwa kuwa anatambua mambo yalivyo na yanavyoweza kurekebishwa. Hivyo mara nyingi anafaulu kufanya mambo yawe alivyotaka. Mambo yaliyo magumu kwa wengine, kwake ni rahisi.

7. Anajiendeleza aishi kwa ukamilifu. Anatumia vizuri vipawa vyake vyote. Anafurahia mambo mbalimbali ya maisha na kufaidika nayo ili azidi kujiendeleza

Pande mbalimbali za ukomavu wa mtu

1. Wa maono • anakubali maono yake bila ya kutawaliwa nayo; • anaweza kuyajulisha ili kusaidiwa; • anakabili magumu bila ya kuyaepa wala kuhangaika mno; • si mtu wa kujikinga kila mara.

2. Wa nafsi: • anasikiliza wengine, hatimaye anaamua mwenyewe bila ya wasiwasi mkubwa mno; • anaweza kubadili uamuzi wake akipata habari mpya; • anasema ukweli na kuchukua jukumu la uamuzi wake; • anapokea uamuzi wa wengine.

3. Wa jamii: • anaona wema wa wengine, asijifanye lengo la yote; • anafungamana vema na wengine; • ana marafiki wa kufaa; • hawategemei mno ndugu zake; • anafuata taratibu za jumuia; • analinganisha mahitaji yake na ya kikundi chake; • yuko tayari kutimiza sheria halali hata zisipompendeza • anafanya kazi hata ngumu kwa utulivu.

4. Wa maadili: • anapokea mawazo mazuri na kuyaishi; • anafuata malengo yake kwa sababu anayo ya kufaa; • anatimiza busara, haki, nguvu na kiasi; • yuko imara katika imani, tumaini na upendo.

5. Wa roho: • anafungamana vema na Mungu, malaika na watakatifu; • anamtegemea Mungu na kutimiza matakwa yake; • anaelewa wito wake, anauthamini na kudumu kwa hiari kuuitikia

Mambo yanayozuia ukomavu

Binadamu anakusudiwa kukomaa, lakini hafanikiwi sikuzote. Tunawaona watu waliolemaa upande wa mwili, lakini wengi zaidi wamelemaa upande wa nafsi. Sababu ni kwamba mtu akikosa haja zake za msingi hawezi kustawi. Haja hizo zina nguvu sana, nazo zisipotimizwa zinamuacha mtu kilema.

Mambo yanayompata hata akalemaa kinafsi yanaelezwa na mviringo ufuatao usioelekea popote:
1. Hatimiziwi haja za nafsi, ambazo ni za msingi kama zile za mwili, hivyo zisipotimizwa yanaanza matatizo.

2. Hajisikii vizuri, hata kama ni mtoto au haelewi, kwa kuwa mtu akihisi hapendwi, hatakiwi, hayuko salama, basi anajisikia vibaya mpaka ndani.

3. Anapatwa na wasiwasi unaofanya nafsi isistawi, hata kama mwili unaendelea kukua. Ndiyo sababu anashindwa kushirikiana vizuri na watu au anajitenga nao kwa kuona hawampi anayoyahitaji.

4. Kutokana na hofu hashiriki vizuri katika mambo yote. Anatambua kwamba akibaki peke yake hapati nafasi ya kupendwa, lakini anashindwa kukabili hofu yake.

5. Matokeo yake ni kwamba anajihisi hastahili kutimiziwa haja zake. Hatimaye anaweza akajichukia kama kwamba ndiye anayesababisha watu wasimtimizie haja zake.

6. Anafadhaika asijue la kufanya mbele ya matatizo hayo. Anashindwa kupata jibu kuhusu haja zake kutimizwa kesho: ikiwa leo hapati anayoyahitaji hata kwa watu wenye wajibu kwake, je, atayapata lini?

7. Anafuata njia za kujikinga na hofu hizo kusudi asiendelee kufadhaika. Moja ya njia hizo ni kusukuma ndani kabisa mwa nafsi yake yale yasiyompendeza yasielee tena katika kumbukumbu; lakini kadiri mambo hayo yalivyoshindiliwa ndani yanamvuruga na kujitokeza kwa matendo na maneno yasiyotarajiwa. Njia nyingine ya kujikinga ni kutokubali hali halisi, yaani kukataa kukabili jambo la hatari au lisilopendeza. Njia nyingine ni kuhamisha dhihirisho la ono fulani (hasira, chuki n.k.) limlenge mtu tofauti na yule anayekusudiwa. Njia nyingine ni kuishi katika ndoto za mchana badala ya kuwazia hali halisi: mtu anajichorea akilini picha ya ulimwengu mwingine ambapo mambo yanakwenda anavyotaka, hata akaamini ndio wa kweli. Njia nyingine tena ni kujitafutia visingizio ili kutosikia aibu moyoni: mtu anaweza akafikia hatua ya kumshtaki mwenzake kwa kosa alilolifanya mwenyewe. Njia ya mwisho ni kudai kwamba wengine ndiyo wenye hali aliyonayo mwenyewe asiikubali.

8. Kwa kuwa njia hizo hazimtimizii haja zake, hazimsaidii ila zinamtuliza kijuujuu tu kwa muda, yaani zinafunika matatizo yake badala ya kuyatatua. Mtu amejikinga isivyofaa, basi shida inabaki palepale. Hivyo mviringo usioelekea popote umekamilika kwa kurudia namba moja: mtu anahitaji bado kupendwa, kukubaliwa, kuthaminiwa na kuwa salama. Nani atamsaidia?

Dalili za mtu asiyekomaa

1. Anapurukusha tu na kulipua kazi mpaka asimamiwe.
2. Hatimizi vizuri wajibu wake kwa jumla, ni mtegezi.
3. Anachekacheka na kucheza wakati usiofaa.
4. Ana kiburi cha kitoto.
5. Hajui kujiheshimu wala kuwastahi wengine.
6. Ni mbishi, pia kwa makusudi, tena mlalamishi.
7. Hajui kulinda siri za nyumbani, ni mchongezi.
8. Hajali maonyo, anayachukua kimzaha.
9. Hakubali maoni ya wengine.
10. Si mnyofu wala hajui kujieleza wazi alivyo.
11. Anaogopa kutoa mawazo yake mbele ya watu.
12. Haamui kwa utashi imara.
13. Anafuata mkumbo.
14. Katika kuwapenda wenzake ana ubaguzi.
15. Anajipendekeza na kujipendea.
16. Anadai kubembelezwa na kufarijiwa.
17. Hana [[uvumilivu wala moyo mkuu.
18. Anatunza kinyongo.
19. Anakata tamaa kwa urahisi.

 Ukomavu wa binadamu ni hali iliyokusudiwa ifikiwe na mtu kupitia ukuaji wake.

 


Alhamisi, Septemba 27, 2012

TUNAKUZA VIPAJI

Huyu ndiye mwalimu wa muziki katika OMEGA POINT MUSIC ACADEMY iliyopo USHINDI SDA CHURCH.

Hapa ilikuwa ni katika tukio moja hivi.

Calvin mwenye nguo nyeusi kuanzia shati hadi suruali aliyepo nyuma ya pianist akirekebisha mitambo Ushindi SDA Church. Calvin ni rubani wa ndege na hivi sasa yupo kwa Obama anaongeza maujuzi mwanawane .


Huyu mtoto ni kivutia cha wengi kutokana na uwezo wake wa kucheza Piano, ilimchukua muda mfupi sana kuanza kupiga Piano huku akisoma Staff Notation.






Mdada kwa nyuma alikuwa akiimba wimbo uliokuwa ukichezwa na bwana mdogo hapo kwa Piano.


Huyu ndie mkufunzi mwenyewe wa Muziki.


 Mwalimu Heri akitoa maelekezo kwa mwanafunzi





Hapa alipewa paper ngumu, akajiuliza hivi nitaweza kweli kuupiga huu wimbo? Ulimchanganya lakini baada ya kutulia kidogo na kuungalia kwa makini akaanza na akaweza aisee...!!

 Mwalimu Heri akikagua mwanafunzi anachofanya ili kujiridhisha kuwa kaelewa ama anaweza? Ulikuwa ni wimbo mgumu sana.

Hapa anamfunulia ukurasa mwingine ili  kumpima uwezo wake

Dogo hapa kaiva, anapiga piano na kusoma Staff Notation.




Watoto wanaojifunza muziki wakiangalia kwa makini wakati mwalimu Heri akitoa maelekezo.

Hapo je!!


Muziki damuni.

Staff Notation ni moja ya changamoto kwa waimbaji, waalimu na hata wacheza vyombo vya muziki.





UTAPENDA MWANAO AMA WEWE MWENYEWE UJIFUNZE MUZIKI? 
WASILIANA NA MWALIMU HERI KAALE KWA NAMBA HIZI ZIFUATAZO:

+255 713 381883
+255 688 984 442
+255 757 336 090

Jumatano, Septemba 19, 2012

KONGAMANO LA MAISHA BORA



Lile  kongamano la maisha bora, lililoandaliwa na Kanisa la Waadiventista Wasabato USHINDI kwa ajili ya kuwawezesha Watanzania kukabiliana na changamoto za maisha limeshaanza na hivi unavyosoma haya maandishi linaendelea.

Kanisa linatambua wajibu wake kwa jamii na Serikali katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili nchi ili kukabiliana na changamoto hizo, kanisa limeandaa kongamano ambalo litachukua siku kumi kuanzia Septemba 17 hadi 28, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

“Kanisa la Waadventista kama sehemu ya jamii, tunatambua changamoto zinazoikabili nchi yetu, ingawa jitihada kubwa zinafanywa na Serikali, mashirika ya dini pamoja na asasi mbalimbali.

 “Leo kuna watoto wanaoitwa wa mtaani ama idadi ya wanaolelewa na mzazi mmoja inaongezeka kutokana na kuongezeka kwa talaka na ndoa zisizo na furaha na hali hii huathiri malezi ya watoto, elimu yao na maendeleo ya taifa kwa ujumla.”

Kongamano hilo la maisha bora limelenga katika kupanua uelewa ambapo mada mbalimbali zitajadiliwa, ikiwamo ukimwi, maadili kwa jamii, uhuru wa dini, ujasiriamali, mazingira, athari za imani za uchawi na namna ya kudumisha amani katika nchi yetu.

KARIBU WATER FRONT GHOROFA YA 8 KILA SIKU KUANZIA SAA 10 JIONI KWA SAA ZA AFRIKA MASHARIKI.

Jumatatu, Septemba 17, 2012

FAIDA YA JUISI YA MATUNDA MCHANYIKO MWILINI


Katika ulimwengu wa vyakula, inafahamika na kuaminika kuwa chakula ni dawa. Chakula unachokula leo ndicho kinachoamua hali yako ya kiafya kesho. Unaweza kuishi bila kuugua kama ukila vyakula vyote muhimu vinavyohitajika mwilini.

Leo nitakutajia orodha ya juisi zilizotengenezwa kwa matunda na mboga na fadia zake mwilini. Katika orodha hii, utaona kuna mchanganyiko wa matunda au mboga mbili hadi nne na kazi zake mwilini, zikitumika kama tiba au kinga ya magonjwa.

KAROTI, TANGAWIZI NA TUFAHA
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda hayo matatu huondoa sumu mwilini na kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili. Tufaha ndiyo apple kwa Kiingereza.

TUFAHA, TANGO NA FIGILI
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya ni kinga dhidi ya saratani, huondoa lehemu (cholestrol) mwilini, husafisha tumbo na pia huondoa maumivu ya kichwa.

NYANYA, KAROTI NA TUFAHA
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hufanya ngozi ya mwili mzima kuwa nyororo na huondoa harufu mbaya mdomoni.
TANGO CHUNGU,

TUFAHA NA TANGO LA KAWAIDA
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya huondoa harufu mbaya mdomoni na hupunguza joto la mwili.

CHUNGWA, TANGAWIZI NA TANGO
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hung’arisha rangi ya ngozi na kuifanya kuwa laini. Pia hupunguza joto la mwili. Kwa wale wenye matatizo ya kuwa na ngozi kavu, juisi hii itawasaidia sana.

NANASI, TUFAHA NA TIKITIMAJI
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hufanya kazi ya kuondoa chumvi nyingi mwilini, husafisha kibofu cha mkojo na figo. Juisi hii ni nzuri kwa wale wenye matatizo ya kibofu na figo au wanaotaka kujikinga na magonjwa hayo.

TUFAHA, TANGO NA ‘KIWI’
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hung’arisha rangi ya ngozi. Kiwi ni aina ya matunda ambayo hujulikana pia kama ‘matunda-damu’.

PEASI NA NDIZI

Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hurekebisha kiwango cha sukari katika damu. Inawafaa sana wagonjwa wa kisukari na inaweza kuwa sawa na kinga dhidi ya ugonjwa huo.

KAROTI, PEASI, TUFAHA NA EMBE
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya huzuia athari ya sumu mwilini, hupunguza shinikizo la damu na kuondoa mlundikano wa uchafu mwilini.

MASEGA YA ASALI, ZABIBU, TIKITIMAJI NA MAZIWA
Juisi yenye mchanganyiko huu huwa na kiasi kikubwa cha Vitamin C na Vitamin B2 ambazo huimarisha chembechembe hai na kinga ya mwili.

PAPAI, NANASI NA MAZIWA
Juisi hii ina kiwango kikubwa cha Vitamin C, E na madini chuma. Huimarisha rangi ya ngozi na mfumo wa usagaji wa chakula tumboni.

NDIZI, NANASI NA MAZIWA

Juisi hii yenye kiasi kikubwa cha vitamini na virutubisho mbalimbali vyenye faida mwilini, huzuia tatizo la ukosefu wa choo.

Ili kupata faida hizo zilizoainishwa katika kundi la matunda hayo, usafi wa matunda yenyewe hauna budi kuzingatiwa wakati wa kutayarisha juisi yake. Vilevile hakikisha unatumia matunda yaliyoiva vizuri na uyatayarishe kwa kuzingatia kanuni ya ‘mtu ni afya’.

Unaweza kutumia mashine maalumu ya kukamulia matunda (blender) au kutumia njia ya asili ya kutwanga kwa kinu maalumu na kupata juisi hiyo. Kama utaongeza sukari, inashauriwa kuweka kiasi kidogo sana. Ni bora zaidi usipoweka sukari, kwa sababu matunda mengi yana sukari ya asili.