Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumamosi, Oktoba 06, 2012

SATELITE NET EVENT KAMPALA 2012

Picha kwa hisani ya: http://www.hopetv.org



Maneno SATELITE NET EVENT KAMAPALA 2012 yakitumika bila kutafisiriwa yanabeba maana iliyo bora sana kuliko yakitafsiriwa. Kwa kuwa ndiyo maneno yabebayo tukio la satalaiti, ni vizuri kutoa tafsiri ya jumla itakayosaidia wengi kuelewa jambo hili tunalolipigia mbiu. Inawezekana kabisa kuyatohoa na kuyatumia kama yalivyo, lakini kwa faida ya wengi tafsiri rahisi tunayoweza kuitoa ni Mahubiri ya Satalaiti ya Kamapla 2012.

  • Baada ya kuelewa maana hii, makanisa yanaweza:
  • Kuyatohoa na kuyatumia kama yalivyo.
  • Kutumia tafsri tuliyoitoa.
  • Kutumia yote mawili; kuyatohoa na kutumia tafsiri tuliyotoa.


AGIZO LA UTUME WETU
Agizo la utume la kuwafikia watu na habari njema ya injili siyo wazo jipya kabisa katika uelewa wa Waadventista wa sabato. Agizo hili limeelezwa wazi katika maandiko likiwa na msisitizo wa utolewaji wa habari njema kuwa ushuhuda kwa mataifa yote. Agizo hili limeandikwa kwa namna nzuri karibu katika sura tatu tofauti za Biblia; Mathayo 24:14, 28:19-20: na ujumbe wa malaika watatu Ufunuo 14:6-12.

MSUKUMO WA KITEKNOLOJIA
Ni muhimu sana kwetu kuelewa kwamba, jumbe hizi zinapaswa kwenda kwa haraka sana. Hatutaweza kufikia lengo letu la kile ambacho Mungu amekusudia tukifikie isipokuwa tunatumia njia ambazo zinakubalika katika kizazi tuishicho. Teknolojia imetuthibitishia ukweli wajambo hili kwa kadri tuonavyo ushahidi wa uhakika wa kile iwezacho kufanya kupitia nguvu ya Roho Mtakatifu. Kanisa katika ukanda wetu limewahi kupitia uzoefu wa nguvu ya teknolojia katika uinjilisti. Tunaweza kuuita uinjilisti kwa njia ya vyombo vya habari (Media Evangelism)

Idara ya mawasiliano imejiandaa kutumia njia zote za mawasiliano ili kutuoa ujumbe wa matumaini kwa wote wanaoweza kufikiwa. Kwa kuwa tunaishi katika siku za mwisho zenye changamoto mpya kwa kila siku ipitayo, unatiwa moyo kumjulisha rafiki yako, jirani yako, na kila mtu wako wa karibu kuhusu Mahubiri makubwa ya Satalaiti Kampala 2012.

Ninakualika kusoma kwa makini maelezo yafuatayo:

MAHUBIRI:
Mchungaji Blasious Ruguri.

Moto wa NET Event Kampala:
“NDIMI ZA MOTO WA INJILI”.

Kauli mbiu ya Utangulizi:
 “MOTO WA INJILI”.

AFYA, KAYA NA FAMILIA:
Yataletwa na wazungumzaji wenye uwezo na uzoefu mkubwa.
Nyimbo kupitia kwaya na vikundi vya uimbaji zitakuwa sehemu ya tukio.

TAREHE:
Septemba 29-Octoba 13, 2012. Matangazo yatakufikia katika kituo cha kanisani kwako na nyumbani kwako. Morning Star Radio  na redio zingine mbalimbali zitajiunga na mahubiri haya.

MAHALI:
Union ya Uganda.

ENEO LA TUKIO:
Kanisa la Waadventista Wa Sabato Bhunga.

MAWAKALA WA UTANGAZAJI NA KUREKODI:
ECD MEDIA CENTER na HOPE CHANNEL INTERNATIONAL watawajibika kwa pamoja katika uzalishaji. Pia watatoa taarifa na ushauri wa kiufundi kila itakapoonekana vyema.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni