Mtayarishaji

Morning Star Radio

Ijumaa, Mei 13, 2011

MAJIBU YAFANYAYO KAZI...MAUTI!!


... au kifo ni mwisho wa uhai; kwa lugha ya biolojia mwisho wa michakato yote ndani ya kiumbehai ambayo ni dalili za uhai.

Mauti hutokea kutokana na sababu mbalimbali kama vile

  • umri mkubwa unaosababisha michakato ya kimsingi mwilini kusimama polepole
  • muda mrefu wa maisha unaoruhusu makosa na kasoro kujumuika na kusababisha madhara (mfano: kansa)
  • magonjwa yanaovurugisha michakato ya uhai hadi kuisimamisha
  • ajali zinazoharibu viungo muhimu mwilini
  • ukosefu wa chakula, maji, hewa au kinga dhidi ya mazingira magumu
  • athira haribifu kutoka viumbe wengine (k.m. kushambuliwa) au kutoka mazingira

Kwa binadamu kutokea kwa kifo mara nyingi hakutokei mara moja; katika mazingira ya kawaida kifo kinaonekana kama moyo hausikiki tena na mapafu hayakupumua kwa dakika kadhaa. Lakini hata hivyo kuna uwezekano ya kwamba kazi ya moyo na mapafu ni hafifu kiasi haitambuliki. Penya hospitali nzuri na mitambo ya kiganga mara nyingi mtu anarudi katika maisha kama ameshatazamiwa ameaga dunia mahali pengine. Kama mashine zineendelea kuchukua kazi ya moyo na mapafu si rhbisi kujua kifo kinatokea kini. Wataalamu wengi siku hizi wanaona mara michakato ya kawaida ya ubongo imekwisha kifo kimetokea.

Mauti na utamaduni

Katika utamaduni na imani za watu mauti ni jambo muhimu. Lugha ina njia nyingi ya kuitaja kwa mfano kuaga dunia, kufariki n.k.

Katika dini na falsafa kuna misimamo mbalimbali kuhusu mauti kama vile

  1. Mauti ni mwisho wa binadamu kimwili na kiroho; hakuna kinachobaki baada ya kifo
  2. Mauti ni hatua tu katika mzunguko wa maisha; nafsi au roho inarudi katika maumbile mengine
  3. Kifo ni kupita penginepo: maisha ya milele, mbinguni, upeo wa wafu n.k.
Kama ujuavyo, habari hii ni mahususi kutokana na yaliyowasibu marafiki zetu hawa AMBASADOR OF CHRIST kutoka REMELA, RWANDA.

--------------------------------------------------------

Ndugu msomaji: MAJIBU YAFANYAYO KAZI ni kipengele kinachoongelea masuala ya kiroho zaidi.

Kwa sababu ya upekee na unyeti wa siku, Sio vibaya tukibadilishana mawazo na kuambizana yaliyomuhimu katika maisha hasa ya kiroho.
Na huu utakuwa ni mfululizo kwa kila siku kama hii ya leo...

(Namaanisha JumaMosi)

Pamoja na kwamba weeengi wanaamini hii ni kweli, lakini kweli halisi jionee mwenyewe ambapo

Dr. Carlton P. Byrd

Anapotwambia:

"The truth about suffering and trials".




CHRIST wanatwambia EBALUWA wakiwa na maana katika Kiswahili BARUA. Nani kapewa na ni nani msomaji wa hiyo barua?? RAHA JIPE MWENYEWE mtu wangu.


Jumanne, Mei 10, 2011

Nafsi...Binadamu????

Nafsi ni neno la mkopo kutoka Kiarabu. Linatumika kusisitiza dhati ya mtu (k.mf. "Mimi nafsi yangu"). Hivyo linatumika kutafsiria neno la Kilatini "persona" (kwa Kiingereza "person") ambalo linamtofautisha binadamu (kama kiumbe wa pekee) na wanyama wote na kumpa haki zake za msingi. Tofauti hiyo ilisisitizwa hasa na dini ya Uyahudi iliyomtambua mtu (mwanamume na mwanamke vilevile) kuwa sura na mfano wa Mungu. Ni msamiati muhimu wa ustaarabu wa Magharibi, unaotumika sana katika saikolojia, sheria, falsafa, teolojia n.k. Maendeleo makubwa katika kuuelewa yalipatikana wakati wa mabishano ndani ya Ukristo kuhusu fumbo la Yesu na Utatu.


Binadamu

Binadamu ni neno linalomaanisha "Mwana wa Adamu", anayeaminiwa na dini za Uyahudi, Ukristo na Uislamu kuwa ndiye mtu wa kwanza. Kisayansi jina hilo linaweza kutumika kwa maana ya Homo Sapiens ili kumtofautisha na viumbe wengine wa jenasi Homo ambao wa mwisho wao (Homo Neanderthalensis) walitoweka miaka 35,000 hivi iliyopita. Wanadamu wote walioko leo hii ni spishi ileile na tofauti zinazoonekana kati ya maumbile ya watu katika sehemu mbalimbali za dunia ni kidogo tu. Utafiti juu ya DNA umethibitisha kwamba binadamu wote wametokana na watu waliokuwepo Afrika Mashariki tangu miaka 200,000 hivi iliyopita. Kwa namna ya pekee, upimaji wa DNA ya mviringo, ambayo kila mmoja anarithi kwa mama tu, unaonyesha kuwa binadamu wote waliopo duniani wanachanga mama mmoja aliyewahi kuishi miaka 130,000 hivi iliyopita. Halafu upimaji wa DNA ya mstari, hususan kromosomu Y, ambayo kila mwanamume anarithi kwa baba tu, umeonyesha kuwa wanaume wote waliopo duniani wanachanga baba mmoja aliyewahi kuishi miaka 70,000 hivi iliyopita, kidogo kabla ya watu wa kwanza kuhama bara la Afrika na kuenea Asia kufuatia pwani za Bahari ya Hindi.

Kutoka bara la Asia, watu walienea kwanza Australia na Ulaya, halafu Amerika toka kaskazini hadi kusini. Hatimaye, katika karne ya 20 watu walikwenda kukaa kwa muda katika bara la Antaktika kwa ajili ya utafiti. Ingawa binadamu ana undugu mkubwa wa kibiolojia na sokwe na viumbe vingine, ustawi wake hauna mfano, kiasi cha kufanya wengi waamini tofauti iliyopo inadai kuelezwa kwa uwemo wa roho ndani ya mwili wake; roho ambayo dini hizo zinasadiki imetiwa na Mungu moja kwa moja. Kadiri ya Biblia, binadamu ameumbwa “kwa mfano wa Mungu” (Mwa 1:27), mwenye roho isiyokufa. Ameshirikishwa naye ukuu juu ya viumbe vyote vinavyoonekana. Yeye tu ni nafsi, anaweza kujifahamu, kujitawala, kujitolea na kupendana na wengine. Basi, anapaswa kulinda hadhi hiyo asitawaliwe na tamaa za kila aina. Akifanya hivyo anatimiza mpango wa Mungu juu yake na kupendana naye. Utotoni anasukumwa tu na haja za umbile lake, ambazo ni muhimu kwake na anazilenga bila ya kuhitaji juhudi.


Lakini akikua anaanza kutambua tunu za maadili na dini, ambazo ni njema, ni muhimu kwa zenyewe na zinamdai azifuate kwa nia imara hadi afikie lengo. Kwa bidii za kudumu za namna hiyo anamlenga hasa Mungu, wema mkuu. Anapopitia misukosuko ya ujana asikubali kushindwa na vionjo wala asikate tamaa, kwa kuwa Mungu amemuumba atawale hata nafsi yake na mwili wake. “Mungu aliona kila kitu alichokifanya, na tazama ni chema sana” (Mwa 1:31). Hata hivyo, baada ya dhambi ya asili anadaiwa bidii katika kutekeleza tunu ili wema alionao uzae matunda. Basi, apanie kukuza wema aliojaliwa ili kesho awe mtu bora kama mzazi, raia, kiongozi wa dini na jamii n.k. Penye nia pana njia hata ya kuelekea utakatifu utakaokamilika katika uzima wa milele. Binadamu amekabidhiwa na Mungu dunia, lakini hasa amekabidhiwa nafsi yake mwenyewe. Itamfaa nini kujua na kutawala ulimwengu, asipojijua na kujitawala kweli? Karne XX imeleta maendeleo makubwa katika elimunafsia (= saikolojia). Hivyo anaweza kutambua vizuri mema na mabaya yaliyomo ndani mwake.

Lakini akitaka kujifahamu haitoshi asikilize mafundisho hayo au kusoma vitabu vingi juu yake. Anahitaji kuishi katika mazingira bora ambapo ajisikie nyumbani, huru na mtulivu kwa kupendana na wenzake, kusikiliza watu wanaomfahamu (hasa walezi wake) wanasema nini juu yake, kujipatia muda wa kutulia peke yake na kujifikiria kulingana na maneno yao, kujichunguza kwa makini kuanzia miaka ya utotoni. Kwa kuwa utu unategemea urithi, mazingira na utashi wa kila mmoja, anapaswa kuchunguza hayo yote yaliyochangia kumjenga. Mara kwa mara ajitenge na watu na shughuli ili kutathmini tena maisha yake, kupima maono yake na kuweka maazimio ya kufaa, bila ya kusahau kwamba uhai wake ni fumbo, kwa kuwa unamtegemea Mungu.






Ugali


Ugali ni chakula kinacholiwa na jamii za kiafrika. Chakula hiki chenye virutubisho vya wanga hutokana na unga wa nafaka (kama mahindi, mtama, uwele) au muhogo.

Ugali hutayarishwa kwa njia ifuatayo: kwanza unachemsha maji kwenye sufuria baada ya kuchemka unachanganya unga kidogo na maji ya baridi pembeni, kisha tia mchanganyiko huo kwenye maji ya moto yaliyo jikoni huku ukikoroga. Utatokea mchanganyiko wa unga na maji ambao unaitwa uji, acha uji huo uchemke kwa muda kisha tia unga kiasi kulingana na uji wako huku ukisonga kwa kutumia mwiko. Endelea kusonga mpaka mchanganyiko ushikamane, mchanganyiko huu ndio hutoa ugali.

Ugali huweza kuliwa na mboga ya aina yoyote kama vile mboga majani, sukumawiki, samaki na nyama.

Kawaida ugali huliwa kwa mikono mitupu. Tonge la ugali hufinyangwa kwa mkono wa kushoto kisha kuchovya kwenye maziwa au mchuzi wa maharage, samaki, au nyama ya ng'ombe. Ugali, mapishi yake na jinsi unavyoliwa, hufanana kwa kiasi fulani na foufou toka Afrika Magharibi, na polenta toka Italia. Ugali hujulikana kama nshima nchini Zambia au nsima nchini Malawi.

Jumapili, Mei 08, 2011

MTAYARISHAJI WETU

Nipo katika moja ya majukumu yanayotusibu kila inapoitwa siku, hii nisehemu tu ya kufanikisha kile wasikilizaji wanachokihitaji. Hapa nilikuwa nawasiliana na waimbaji ambao walikuwa njiani kuja kwenye kipindi cha Muziki wa acappella ambacho huwa kinaruka kila ijumaa kuanzia saa 2:00-3:00 usiku na kila jumapili kuanzia saa 10:00-12:00 jioni.









Hawa wanaitwa GRACIOUS SING'ERS. Wanapatikana Kanaan, ni eneo lililopo Mbezi ya Kimara Dar es salaam, kitu kimoja ambacho kinawafanya waonekane tofauti ni pamoja na kushirikiana na Binti mdogo, idadi kamili ya hawa waimbaji wapo 6 na kati ya hao sita kuna Binti (muangalie mwenye tshirt yenye mistari ya rangi nyekundu) Kilichonivutia saaaaaana ni jinsi huyu binti anavyoweza kumudu kuimba sauti 3 kwa nyakati tofauti. Wanajiandaa kurekodi album yao ya kwanza hivi karibuni.

Jumamosi, Mei 07, 2011

MAJIBU YAFANYAYO KAZI..."MTAKATIFU".

Kwa Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki

Makanisa ya Kiorthodoksi yanamuita mtakatifu hasa anayesadikiwa yuko katika paradiso, kuanzia Adamu na Eva, Mose na manabii wengine, lakini pia malaika. Ni Mungu anayefunua watakatifu wake kwa kuitikia sala anazotolewa kwa kuwapitia na kwa kutenda miujiza. Wakristo wanaanza kuwatambua lakini uamuzi wa mwisho unachukuliwa na sinodi ya maaskofu.

Waorthodoksi wanawatendea watakatifu kama watu hai, kwa sababu wanaishi mbinguni pamoja na Kristo mfufuka, ingawa miili yao haijaungana tena na roho zao. Kila mtu anapobatizwa anapewa jina la mtakatifu fulani kama msimamizi kwa maisha yake yote.

Katika Uprotestanti

Madhehebu mengi hayakubali mawazo hayo, yakipenda kusisitiza kwamba wokovu unamtegemea Mungu tu. Hata hivyo mara nyingi waamini bora wanakumbukwa kwa heshima na kuchukuliwa kama mfano (taz. Confessio augustana art. 21). Hasa Waanglikana wanakaribia msimamo wa Wakatoliki na kuadhimisha sikukuu za watakatifu kadiri ya kalenda maalumu.

Katika Uislamu

Ingawa dini hiyo haikubali tofauti kati ya watu, Waislamu wengi wanapenda kuheshimu kwa namna ya pekee marafiki wa Mungu (wali), wakisadiki wana uwezo wa kutabiri, kuombea na kuponya.

Ndugu msomaji: MAJIBU YAFANYAYO KAZI ni kipengele kinachoongelea masuala ya kiroho zaidi.

Kwa sababu ya upekee na unyeti wa siku, Sio vibaya tukibadilishana mawazo na kuambizana yaliyomuhimu katika maisha hasa ya kiroho.
Na huu utakuwa ni mfululizo kwa kila siku kama hii ya leo...

(Namaanisha JumaMosi)

Pamoja na kwamba weeengi wanaamini hii ni kweli, lakini kweli halisi jionee mwenyewe ambapo

Dr. Carlton P. Byrd

Anapotwambia: “Devil Is Alive




Kwa kuwa bado upo nikuongezee nahii kutoka kwa Take 6 katika moja ya nyimbo zao za LIVE wanaposisitiza kuwa Fly Away.