Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumanne, Mei 10, 2011

Ugali


Ugali ni chakula kinacholiwa na jamii za kiafrika. Chakula hiki chenye virutubisho vya wanga hutokana na unga wa nafaka (kama mahindi, mtama, uwele) au muhogo.

Ugali hutayarishwa kwa njia ifuatayo: kwanza unachemsha maji kwenye sufuria baada ya kuchemka unachanganya unga kidogo na maji ya baridi pembeni, kisha tia mchanganyiko huo kwenye maji ya moto yaliyo jikoni huku ukikoroga. Utatokea mchanganyiko wa unga na maji ambao unaitwa uji, acha uji huo uchemke kwa muda kisha tia unga kiasi kulingana na uji wako huku ukisonga kwa kutumia mwiko. Endelea kusonga mpaka mchanganyiko ushikamane, mchanganyiko huu ndio hutoa ugali.

Ugali huweza kuliwa na mboga ya aina yoyote kama vile mboga majani, sukumawiki, samaki na nyama.

Kawaida ugali huliwa kwa mikono mitupu. Tonge la ugali hufinyangwa kwa mkono wa kushoto kisha kuchovya kwenye maziwa au mchuzi wa maharage, samaki, au nyama ya ng'ombe. Ugali, mapishi yake na jinsi unavyoliwa, hufanana kwa kiasi fulani na foufou toka Afrika Magharibi, na polenta toka Italia. Ugali hujulikana kama nshima nchini Zambia au nsima nchini Malawi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni