Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumapili, Desemba 23, 2012

ASILI NA HALI YA MAISHA YA KIBAIOLOJIA

Photo Credit By: http://www.smithsonianmag.com

Kufanya kazi kwa abayojenesisi hakueleweki kwa ufasaha: nadharia mashuhuri ni pamoja na nadharia ya dunia ya RNA (vitoaji aina sawa katika makao ya RNA) na nadhari ya dunia ya chuma-sulfuri (umetaboli bila Jenitiki). Nadharia ya mabadiliko ya viumbe haijaribu kuelezea asili ya maisha bali utaratibu ambao viumbe tofauti vimepitia katika kipindi chote cha historia kupitia mabadiliko ya ghafla ya kijenitiki na uteuzi wa kiasili.  

Wakati wa mwisho wa karne ya 20, kwa kuzingatia ufahamu kutoka mtazamo wa mbadiliko wa viumbe unaotegemea jeni haswa, wanabaiolojia George C. Williams, Richard Dawkins, David Haig, miongoni mwa wengine, wanahitimisha kwamba ikiwa kuna kazi msingi ya maisha, ni kujinakilisha kwa DNA na kuendelea kuwa hai kwa jeni za mtu. 


Hata hivyo, ingawa wanasayansi wameyachunguza maisha vilivyo Duniani, kuyafafanua maisha kibayana bado ni changamoto. Kimwili, mtu anaweza kusema kwamba maisha "hula entirofi hasi"  ambayo inahusu utaratibu ambao waliohai wanapunguza entirofi yao ya kindani kwa gharama ya aina fulani ya nishati inayochukuliwa ndani kutoka mazingira.


Wanabiolojia kiujumla wanakubaliana kwamba viumbe mbalimbali ni mifumo inayojipanga yenyewe inayosimamia mazingira ya ndani ili kudumisha hali hii ya mpango, shughuli za kimetaboliki hutumika kutoa nishati, na uzazi unaruhusu maisha kuendelea kwa vizazi vingi. Kawaida, maumbile huwa sikivu kwa uchochezi na habari za kijenitiki huelekea kubadilika kutoka kizazi hadi kizazi ili kuruhusu marekebisho kupitia mabadiliko ya kimwili, hizi sifa huongeza nafasi ya kuishi ya kiumbe binafsi na wazao wake kwa mtiririko huo. 

Viwakala visivyokuwa vya seli vinavyozaana, hasa virusi, kwa ujumla si havitazamwi kama viumbe kwa sababu haviwezi kuzaana kwa "kujitegemea" au kuendeza shughuli za kimetaboliki. Pambano hili ni tatizo, ingawa, baadhi ya vimelea na visimbayonti vya ndani ya mwili pia vinaweza kuishi maisha ya kujitegemea. Astrobaiolojia inajihusisha na masomo ya uwezekano wa kuwa na aina tofauti ya viumbe vyenye uhai katika ulimwengu mwingine, kama vile miundo ya kujinakilisha kutoka vifaa vingine visivyo DNA.

Ijumaa, Oktoba 26, 2012

Chenjiagou, sehemu ya chimbuko la mchezo wa Wushu wa Taiji


Wushu ya Taiji ilianzishwa nchini China, na ni kiini cha Wushu ya China. Taiji ni yenye vitendo vyenye nguvu na vitendo laini kwa pamoja, licha ya kuweza kutumika kujilinda, pia inaweza kutumika kuimarisha afya ya mwili. Chenjiagou, ambayo ni sehemu ya chimbuko la Wushu ya Taiji, iko kwenye mlima Qingfeng, wilaya ya Wen, sehemu ya kati ya China. Chenjiagou ni kijiji kimoja kidogo, mtu akitaka kwenda huko kwanza anapaswa kufika Jiaozuo kwa garimoshi au kwa gari kutoka mji wa Zhengzhou, halafu anaweza kupanda teksi na kufika huko. Mto Manjano unapita kusini mwa kijiji hicho, kijiji hicho kina familia 600 hivi na wakazi zaidi ya 2,500. 

Jua linapoanza kuzama, watu wanafanya mazoezi ya wushu. Ingawa Chenjiagou haina mlima maarufu na mto mkubwa, lakini ni mahali penye mabingwa wengi. Tangu Chen Wangting, ambaye ni kizazi cha 9 cha nasaba ya ukoo wa Chen kwenye mji wa Chenjiagou kubuni Wushu ya Taiji mwishoni mwa enzi ya Ming na mwanzoni mwa enzi ya Qing, mabingwa wengi walijitokeza katika vizazi mbalimbali.
Kwenye ukumbi wa kuwekea michoro ya vielelezo vya Wushu ulioko kwenye sehemu ya kuingilia katika kijiji hicho, zimewekwa sanamu za mwanzilishi wa Wushu ya Taiji Chen Wangting, pamoja na mabingwa wa vizazi mbalimbali wa Wushu ya Taiji waliotoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya Wushu. Kwenye kando mbili za sanamu yameandikwa maneno ya "Taiji ya Kidao inakusanya maendeleo ya makundi mbalimbali, undani wa Taiji ni astrotech". Mwongoza watalii Bi. WangJingyu alisema,
"Maneno hayo yanaeleza sayansi ya chanya na hasi ya Taiji, Wushu ya Taiji ni Wushu inayounganisha ubora wa utamaduni mbalimbali, dini ya Kidao na falsafa ya meridian." 

Michoro miwili mikubwa iliyotundikwa kwenye ukuta wa ukumbi wa kuwekea vitabu vya Wushu, inawavutia sana watalii, michoro hiyo miwili ni ya mabingwa wawili wa Wushu waliotofautiana kabisa, mmoja mwenye uso wa kutisha, nywele zimesimama kutokana na hasira, na mwingine ni mpole mwenye uso wa kutabasamu, mikono mingi isiyohesabika yenye nguvu ilinyooshwa kutoka katika miili ya mabingwa hao wawili. Mwongoza watalii Bi. Wang Jingyu alisema,
"Mtu akifanya mazoezi ya Wushu, baada ya kufika kiwango cha juu, kama ana mikono mingi sana mwilini mwake isiyoonekana, anaweza kuangusha kitu chenye uzito wa kilo elfu kumi akitumia nguvu ya nusu kilo moja tu." 

Mtu akitembea kwenye mitaa ya Chenjiagou, anaweza kuhisi jadi kubwa ya Wushu. Kuna msemo mmoja unaosema, "baada ya mtu kunywa maji ya Chenjiagou, anajua kupiga teke la Wushu."
Mazingira maalumu ya Taiji yanafanya kijiji hiki kidogo cha Chenjiagou kionekana kuwa na mambo mengi yasiyofahamika, mashabiki wengi wa Wushu wa nchi za nje wanafika huko kwa kuvutiwa na sifa zake. Daktari wa Marekani Bw Bob mwenye umri wa zaidi ya miaka 50, alianza kufanya mazoezi ya Wushu ya Taiji toka alipokuwa na umri wa miaka 15, mwaka 2004 alipata nafasi ya kufika Chenjiagou, na kujifunza Wushu ya Taiji kutoka kwa bingwa Wang Xian, ambaye ni mmoja kati ya mabingwa wa Wushu wa huko. Bw Bob alisema
"Ingawa anaonekana hakutumia nguvu sana, lakini ngumi yake ni yenye nguvu kubwa. Hii ni tofauti na michezo mingine inayotumia nguvu za misuli, michezo mingine inafanya misuli ya mchezaji iwe mikubwa, lakini Taiji inafuatilia kutojikaza mwilini. Hii ndiyo sababu inayoifanya itumike katika kujilinda, vilevile inafaa kwa kuimarisha afya." 

Kuna mashabiki wengi waliofika Chenjiagou kujifunza Wushu ya Taiji kama alivyo Bw Bob. Toka mwaka 1981, Chenjiagou imeshayapokea makundi zaidi ya 100 ya Wushu kutoka nchi na sehemu zaidi ya 50. Mwezi Mei mwaka 1983, bingwa Wang Xian alitembelea Japan na kufanya maingiliano na wana-wushu wa nchi za nje. Kiongozi wa taasisi ya utafiti wa Wushu ya Wang Xian, Bi Yan Sujie toka muda mrefu uliopita amekuwa akifuatana na bingwa Wang Xian kutoa mafunzo ya Wushu katika nchi za nje, alisema,
"Mashabiki wa Wushu ya Taiji wa nchi za nje hawajabadilisha Wushu waliyoichagua toka mwanzo. Bw Noguti Atsuko kutoka Japan amejifunza Wushu kwa miaka 28 kutoka kwa Wang Xian. Kwa sababu undani wa Taiji una mambo mengi sana, hivyo mtu akifanya mazoezi atakuwa kama anafanya usingaji kwenye viungo vyake mwilini, na anasikia raha sana."

SOURCE INGIA:  H A P A

Alhamisi, Oktoba 25, 2012

UMUHIMU WA KISAIKOLOJIA NA THAMANI KATIKA MAISHA




Kwamba sayansi inaweza kutusaidia kuelewa zaidi kuhusu masuala ya msingi kama vile maana ya maisha ni suala linalozua mabishano mengi katika jamii za sayansi na falsafa ya kisayansi.
Hata hivyo, sayansi inaweza kutupa muktadha fulani na huiweka baadhi ya mipaka ya mazungumzo kuhusu mada zinazolingana.
 
Sayansi huenda ikashindwa kutuambia nini ni cha thamani muhimu maishani, lakini baadhi ya masomo hugusia maswali yanayohusiana: watafiti katika saikolojia chanya (na, mapema na bila umakini mwingi, katika saikolojia ya binadamu) hufanya utafiti kuhusu sababu zinazoleta kuridhika na maisha, kujihusisha vikamilifu katika shughuli, kufanya mchango zaidi kwa kutumia vipawa vya kibinafsi, na maana iliyo na msingi wa kuwekeza katika jambo kubwa kuliko mtu binafsi.

Aina moja ya mfumo wa thamani uliopendekezwa na wanaelimunafsia wa jamii, uitwayo kwa upana Nadharia ya Kupambana na Mambo ya Kutisha, inasema kwamba maana yote ya binadamu inatokana na hofu ya kimsingi ya kifo, ambapo maadili yanachaguliwa yanapotusaidia kuepukana na kumbukumbu ya kifo.

Sayansi ya niurolojia imetunga nadharia ya malipo, raha na msukumo katika masuala ya kimwili kama shughuli za kupitisha ujumbe za kiniuro, hasa katika mfumo wa kilimbi na haswaeneo la kiventrali tegimentali. Ikiwa mtu anaamini kwamba maana ya maisha ni kufanya raha iwe nyingi iwezekanavyo, basi nadharia zinatoa utabiri unaozidi kuongezeka, kuhusu jinsi ya kufanya ili kufanikisha hili.

Somo la kijamii linapima thamani katika ngazi ya kijamii kwa kubuni nadharia kama vile nadharia ya thamani kanuni, anomi, n.k.

Jumatano, Oktoba 24, 2012

Kolonia Santita: RIWAYA YA KISWAHILI YA KIJASUSI INAYOSISIMUA..

 

546935
Kolonia Santita ni shirika la madawa ya kulevya. Panthera Tigrisi ni mfanyabiashara wa madawa ya kulevya, katili kuliko wote katika Hemisifia ya Magharibi. Kitabu hiki Kinahusu Ujasusi, Madawa ya kulevya na ugaidi wa kimataifa. Ukianza kukisoma hutakiweka chini kamwe unless kimeisha… 

Kitabu hiki kimetungwa na mtunzi anayekuja juu akiwa ni mjomba kabisa wa mtunzi maarufu wa Riwaya za Kijasusi Marehemu Elvis Musiba ambaye alitamba na kitabu chake cha kwanza cha Njama.
Enock Maregesi ambaye anaishi na kufanya shughuli zake kwa Malkia Elizabeth anasema kitabu hiki amekifanyia kazi kwa umakini na kitaleta mapinduzi kwenye uandishi wa Riwaya za Kiswahili za Kijasusi.

“Kolonia Santita ni tofauti na hadithi zingine kwa sababu ya wapelelezi wake. Wapelelezi wake ni makomandoo-wapelelezi-wanajeshi.” 

Kwa wapenzi wa vitabu kaeni mkao wa kula kwani kiko njiani na kitapatikana kwenye Bookstores zote.

Jumatatu, Oktoba 22, 2012

UCHANYA WA KIMANTIKI



Wachanya wa kimantiki huuliza: Ni nini maana ya maisha? na mbona kuuliza?Kama hakuna maadili yanayolengwa, basi, hivyo ni kusema maisha hayana maana? Ludwig Wittgenstein na wachanya wa kimantiki walisema: "Linapoulizwa kilugha, swali ni la ubatili"; kwa sababu, maishani taarifa ya "maana ya x", kawaida inaashiria madhara ya x, au umuhimu wa x, au kile ambacho ni dhahiri kuhusu x na kadhalika, kwa hivyo, wakati dhana ya maana ni sawa na "x", katika taarifa ya "maana ya x", taarifa inakuwa ya kujirudia, na kwa hivyo, ya kiupuzi, au inaweza kutaja kama ukweli kwamba maisha ya kibaiolojia ni muhimu ili kuwa na maana maishani.

Mambo (watu, matukio) katika maisha ya mtu yanaweza kuwa na maana (umuhimu) kama sehemu ya uzima, lakini maana isiyobainika wazi ya maisha (hayo), yenyewe, mbali na mambo hayo, haiwezi kubainika. Maisha ya mtu yana maana (kwake mwenyewe, wengine) kama matukio ya maisha yanayotokana na mafanikio yake, urithi, familia, na kadhalika, lakini, kusema kwamba maisha, yenyewe, yana maana, ni matumizi mabaya ya lugha, kwani yoyote ya umuhimu, au ya mwisho, ni muhimu tu "katika" maisha (kwa walio hai), hivyo basi kuifanya taarifa iwe ya kimakosa. Bertrand Russell aliandika kwamba ingawa alipata kwamba chuki yake ya mateso haikuwa kama chuki yake ya mboga ya brokoli, hakupata utaratibu wowote wa kuridhisha, na wa kupimika wa kuthibitisha hili:
Tunapojaribu kuwa na uhakika, kulihusu kile tunachomaanisha tunaposema kuwa hiki au kile ndicho "Zuri," sisi hujipata katika matatizo makubwa sana. Tamko la Bentham, kwamba radhi ndiyo Zuri, lilizua upinzani mkali, na ilisemekana kuwa falsafa ya nguruwe. Yeye na wapinzani wake walishindwa kuibua hoja zozote. Katika swali la kisayansi, ushahidi unaweza kupatikana kutoka pande zote mbili, na mwishowe, upande mmoja unabainika kuwa na hoja bora - au, kama hili halitokei, swali linabaki kama halijajibiwa. Lakini katika swali, kuhusu ikiwa hili, au hilo, ndilo mwisho Mzuri, hakuna ushahidi, kwa vyovyote vile; kila mtetezi anaweza kupendekeza tu hoja kulingana na hisia zake, na kutumia vifaa vya ushawishi ambavyo vitaibua hisia sawa katika wengine. . . Maswali kuhusu "maadili" - yaani, kuhusu kile ambacho chenyewe ni kizuri kibaya , bila kutilia maanani madhara yake - yanapatikana nje ya uwanja wa sayansi, jinsi watetezi wa dini wanavyodai kwa msisitizo. Nadhani kwamba, katika hili, wako sawa, lakini, mimi napata hitimisho zaidi, ambalo hawapati, kwamba maswali kuhusu "maadili" yanapatikana kabisa nje ya uwanja wa maarifa. Hiyo ni kusema, tunaposema kwamba hili, au lile, lina "thamani", sisi tunaeleza tu hisia zetu wenyewe, si ukweli, ambao bado ungalikuwa kweli ikiwa hisia zetu za binafsi zingalikuwa tofauti.

Jumapili, Oktoba 21, 2012

BREAKING NEWS

Photo Credit By: spectrummagazine.org

Wapendwa Viongozi wa Kanisa,

Kufuatia tamko la Serikali la kupiga marufuku mihadhara yote ya dini kwa siku thelathini kuanzia leo Oktoba21,2012, Uongozi wa Kanisa la Waadventista wa Sabato Tanzania Unioni,unaelekeza kwamba tuzingatie maelekezo hayo kwa kuahirisha Mahubiri yote ya hadhara au kuyahamishia makanisani, pale itakapowezekana, mpaka marufuku hiyo itakapoondolewa. Tafadhali fikisheni ujumbe huu makanisani. Tunawasihi tumlilie Mungu ili Hali ya Amani na Utulivu irejee mapema na marufuku hii iondolewe.
 
*********************************  
Dear Adventist Church Leaders,

Following the Statement of the government to ban all religious public meetings for thirty days with effect from today October 21, 2012, Tanzania Union Administration of the Seventh Day Adventist Church Directs that we adhere to this directive by canceling all public evangelistic meetings which were falling within these thirty days from today. Kindly pass this message to all churches today. We shall let you know the moment the ban is lifted.

Pr. Mussa Daniel Mika
Director of Communication- 

TANZANIA UNION OF SEVENTH DAY ADVENTIST CHURCH

Alhamisi, Oktoba 18, 2012

KAMPUNI YABUNI PROGRAMU YA WAZAZI KUDHIBITI SIMU ZA WATOTO WAO!!.

Picha ya mtandaoni ikionesha mtoto akitumia simu.



Hatimaye kilio cha wazazi kote duniani kuhusiana na matumizi ya mabaya ya simu ambayo yamekuwa yakifanywa na watoto wao kwa ajili ya kufanikisha michongo isiyo na tija kwao kimepatiwa tiba, baada ya kampuni moja ya teknolojia kugundua mfumo utakaowawezesha kufuatilia mwendendo wa simu za watoto wao.

Mfumo huo unaojulikana kwa jina la Belimo, ambao kwa kuanzia utaweza kufanya kazi kupitia mtandao wa Vodafone, unatoa fursa kwa wazazi kudhibiti muda wa watoto wao kuweza kuwa hewani, kutuma ujumbe mfupi wa maandishi au hata kupiga simu.

Tofauti na mifumo mingine inayojulikana kwa lugha ya kiingereza kama Application, mfumo huu umetengenezwa katika namna ambayo mtoto anayedhibitiwa hawezi kuukataa kwa namna yoyote ile kwani anayekuwa na uwezo wa kuuendesha na kuuamuru ni mzazi anayeamua kuutumia.

Tayari mfumo huu umeshapata umaarufu hata kabla haujaanza kutumika ambapo asasi moja ya nchini Uingereza yenye kujihusisha na masuala ya uzazi na malezi, imeweka bayana mtazamo wake juu ya kuukubali mfumo huu huku ikisema kuwa “utawawezesha wazazi kudhibiti vijana wao kujihusisha na masuala ya kipuuzi”
Chini ya mfumo huu, mzazi ataweza kununua kifurushi ambacho kinajumuisha kadi ya simu ya kawaida tu kama zilivyo zinazotumika kwenye simu hivi sasa, lakini ikiwa imeunganishwa kwenye mfumo huo, na huduma hiyo itakuwa ya kulipia kwa kadiri mtumiaji anavyopenda kuendelea kuitumia.

“Mfumo huu utawawezesha wazazi kudhibiti kwa mfano, namba zipi ambazo hawapendi ziwe zinawasiliana na mtoto wao, muda wa kupiga simu, kutuma ujumbe na huduma zingine za simu. Lakini pia, wazazi watakuwa na uwezo wa kusoma ujumbe mfupi wa maneno ulioko kwenye simu za watoto wao, bila kuwa na simu za watoto hao” amesema msemaji mmoja wa kampuni inayoandaa mfumo huo.

Hatua hii imekuja ikiwa ni katika zama ambazo taasisi kadhaa za kiutafiti zimetanabaisha kuwa, watoto hasa wa kike barani Ulaya, wamekuwa katika shinikizo la kutuma kwa njia mbalimbali, mambo yenye kuhusu maisha yao ya kimapenzi, jambo ambalo limekuwa likiwakwaza wazazi wao huku maadili pia yakizidi kupotea watoto wao simu kwa watoto wao.

CHANZO CLICK:  H A P A