Mtayarishaji

Morning Star Radio

Alhamisi, Oktoba 18, 2012

KAMPUNI YABUNI PROGRAMU YA WAZAZI KUDHIBITI SIMU ZA WATOTO WAO!!.

Picha ya mtandaoni ikionesha mtoto akitumia simu.



Hatimaye kilio cha wazazi kote duniani kuhusiana na matumizi ya mabaya ya simu ambayo yamekuwa yakifanywa na watoto wao kwa ajili ya kufanikisha michongo isiyo na tija kwao kimepatiwa tiba, baada ya kampuni moja ya teknolojia kugundua mfumo utakaowawezesha kufuatilia mwendendo wa simu za watoto wao.

Mfumo huo unaojulikana kwa jina la Belimo, ambao kwa kuanzia utaweza kufanya kazi kupitia mtandao wa Vodafone, unatoa fursa kwa wazazi kudhibiti muda wa watoto wao kuweza kuwa hewani, kutuma ujumbe mfupi wa maandishi au hata kupiga simu.

Tofauti na mifumo mingine inayojulikana kwa lugha ya kiingereza kama Application, mfumo huu umetengenezwa katika namna ambayo mtoto anayedhibitiwa hawezi kuukataa kwa namna yoyote ile kwani anayekuwa na uwezo wa kuuendesha na kuuamuru ni mzazi anayeamua kuutumia.

Tayari mfumo huu umeshapata umaarufu hata kabla haujaanza kutumika ambapo asasi moja ya nchini Uingereza yenye kujihusisha na masuala ya uzazi na malezi, imeweka bayana mtazamo wake juu ya kuukubali mfumo huu huku ikisema kuwa “utawawezesha wazazi kudhibiti vijana wao kujihusisha na masuala ya kipuuzi”
Chini ya mfumo huu, mzazi ataweza kununua kifurushi ambacho kinajumuisha kadi ya simu ya kawaida tu kama zilivyo zinazotumika kwenye simu hivi sasa, lakini ikiwa imeunganishwa kwenye mfumo huo, na huduma hiyo itakuwa ya kulipia kwa kadiri mtumiaji anavyopenda kuendelea kuitumia.

“Mfumo huu utawawezesha wazazi kudhibiti kwa mfano, namba zipi ambazo hawapendi ziwe zinawasiliana na mtoto wao, muda wa kupiga simu, kutuma ujumbe na huduma zingine za simu. Lakini pia, wazazi watakuwa na uwezo wa kusoma ujumbe mfupi wa maneno ulioko kwenye simu za watoto wao, bila kuwa na simu za watoto hao” amesema msemaji mmoja wa kampuni inayoandaa mfumo huo.

Hatua hii imekuja ikiwa ni katika zama ambazo taasisi kadhaa za kiutafiti zimetanabaisha kuwa, watoto hasa wa kike barani Ulaya, wamekuwa katika shinikizo la kutuma kwa njia mbalimbali, mambo yenye kuhusu maisha yao ya kimapenzi, jambo ambalo limekuwa likiwakwaza wazazi wao huku maadili pia yakizidi kupotea watoto wao simu kwa watoto wao.

CHANZO CLICK:  H A P A

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni