Mtayarishaji

Morning Star Radio

Ijumaa, Oktoba 26, 2012

Chenjiagou, sehemu ya chimbuko la mchezo wa Wushu wa Taiji


Wushu ya Taiji ilianzishwa nchini China, na ni kiini cha Wushu ya China. Taiji ni yenye vitendo vyenye nguvu na vitendo laini kwa pamoja, licha ya kuweza kutumika kujilinda, pia inaweza kutumika kuimarisha afya ya mwili. Chenjiagou, ambayo ni sehemu ya chimbuko la Wushu ya Taiji, iko kwenye mlima Qingfeng, wilaya ya Wen, sehemu ya kati ya China. Chenjiagou ni kijiji kimoja kidogo, mtu akitaka kwenda huko kwanza anapaswa kufika Jiaozuo kwa garimoshi au kwa gari kutoka mji wa Zhengzhou, halafu anaweza kupanda teksi na kufika huko. Mto Manjano unapita kusini mwa kijiji hicho, kijiji hicho kina familia 600 hivi na wakazi zaidi ya 2,500. 

Jua linapoanza kuzama, watu wanafanya mazoezi ya wushu. Ingawa Chenjiagou haina mlima maarufu na mto mkubwa, lakini ni mahali penye mabingwa wengi. Tangu Chen Wangting, ambaye ni kizazi cha 9 cha nasaba ya ukoo wa Chen kwenye mji wa Chenjiagou kubuni Wushu ya Taiji mwishoni mwa enzi ya Ming na mwanzoni mwa enzi ya Qing, mabingwa wengi walijitokeza katika vizazi mbalimbali.
Kwenye ukumbi wa kuwekea michoro ya vielelezo vya Wushu ulioko kwenye sehemu ya kuingilia katika kijiji hicho, zimewekwa sanamu za mwanzilishi wa Wushu ya Taiji Chen Wangting, pamoja na mabingwa wa vizazi mbalimbali wa Wushu ya Taiji waliotoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya Wushu. Kwenye kando mbili za sanamu yameandikwa maneno ya "Taiji ya Kidao inakusanya maendeleo ya makundi mbalimbali, undani wa Taiji ni astrotech". Mwongoza watalii Bi. WangJingyu alisema,
"Maneno hayo yanaeleza sayansi ya chanya na hasi ya Taiji, Wushu ya Taiji ni Wushu inayounganisha ubora wa utamaduni mbalimbali, dini ya Kidao na falsafa ya meridian." 

Michoro miwili mikubwa iliyotundikwa kwenye ukuta wa ukumbi wa kuwekea vitabu vya Wushu, inawavutia sana watalii, michoro hiyo miwili ni ya mabingwa wawili wa Wushu waliotofautiana kabisa, mmoja mwenye uso wa kutisha, nywele zimesimama kutokana na hasira, na mwingine ni mpole mwenye uso wa kutabasamu, mikono mingi isiyohesabika yenye nguvu ilinyooshwa kutoka katika miili ya mabingwa hao wawili. Mwongoza watalii Bi. Wang Jingyu alisema,
"Mtu akifanya mazoezi ya Wushu, baada ya kufika kiwango cha juu, kama ana mikono mingi sana mwilini mwake isiyoonekana, anaweza kuangusha kitu chenye uzito wa kilo elfu kumi akitumia nguvu ya nusu kilo moja tu." 

Mtu akitembea kwenye mitaa ya Chenjiagou, anaweza kuhisi jadi kubwa ya Wushu. Kuna msemo mmoja unaosema, "baada ya mtu kunywa maji ya Chenjiagou, anajua kupiga teke la Wushu."
Mazingira maalumu ya Taiji yanafanya kijiji hiki kidogo cha Chenjiagou kionekana kuwa na mambo mengi yasiyofahamika, mashabiki wengi wa Wushu wa nchi za nje wanafika huko kwa kuvutiwa na sifa zake. Daktari wa Marekani Bw Bob mwenye umri wa zaidi ya miaka 50, alianza kufanya mazoezi ya Wushu ya Taiji toka alipokuwa na umri wa miaka 15, mwaka 2004 alipata nafasi ya kufika Chenjiagou, na kujifunza Wushu ya Taiji kutoka kwa bingwa Wang Xian, ambaye ni mmoja kati ya mabingwa wa Wushu wa huko. Bw Bob alisema
"Ingawa anaonekana hakutumia nguvu sana, lakini ngumi yake ni yenye nguvu kubwa. Hii ni tofauti na michezo mingine inayotumia nguvu za misuli, michezo mingine inafanya misuli ya mchezaji iwe mikubwa, lakini Taiji inafuatilia kutojikaza mwilini. Hii ndiyo sababu inayoifanya itumike katika kujilinda, vilevile inafaa kwa kuimarisha afya." 

Kuna mashabiki wengi waliofika Chenjiagou kujifunza Wushu ya Taiji kama alivyo Bw Bob. Toka mwaka 1981, Chenjiagou imeshayapokea makundi zaidi ya 100 ya Wushu kutoka nchi na sehemu zaidi ya 50. Mwezi Mei mwaka 1983, bingwa Wang Xian alitembelea Japan na kufanya maingiliano na wana-wushu wa nchi za nje. Kiongozi wa taasisi ya utafiti wa Wushu ya Wang Xian, Bi Yan Sujie toka muda mrefu uliopita amekuwa akifuatana na bingwa Wang Xian kutoa mafunzo ya Wushu katika nchi za nje, alisema,
"Mashabiki wa Wushu ya Taiji wa nchi za nje hawajabadilisha Wushu waliyoichagua toka mwanzo. Bw Noguti Atsuko kutoka Japan amejifunza Wushu kwa miaka 28 kutoka kwa Wang Xian. Kwa sababu undani wa Taiji una mambo mengi sana, hivyo mtu akifanya mazoezi atakuwa kama anafanya usingaji kwenye viungo vyake mwilini, na anasikia raha sana."

SOURCE INGIA:  H A P A

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni