Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumapili, Januari 27, 2013

Morning Star Television (MSTV) in TANZANIA



Tunapenda kutambulisha  Logo ya Morning Star Tv
Hata Hivyo kama unamaoni tofauti usisite kututumia nasi tutayazingatia na kama kuna mtu anaalternative logo badala ya hii au anadhani kuna maboresho zaidi kwa logo hii, tafadhali tutumie wazo lako likiwa katika PSD format na ulitume kwa mazara@morningstartv.or.tz pia unaweza kuwasilisha ofisini kwetu Mikocheni B lilipo kanisa la Waadventista wasabato Ushindi ama Morning Star Radio.
--------------------------------------------------------------------------------------------------------

 Morning Star Television, yazindua mapango wake wa uchangiaji huko Mwanza na Morogoro.
Je wajua kwa kuchangia uanzishwaji wa MSTV, utawezesha watu Milioni 5 Kufikiwa kwa siku ambapo ingehitaji zaidi ya makanisa 2000
Je wajua, ukitunza kuanzia leo TSH 500 toka kwenye Vocha za simu yako utaweza kuichangia MSTV kiasi kisichopungua TSH 20,000 tarehe 2 March na Hivyo Kuvuka Goli kwa 100% ?
Je wajua kama mshiriki akichangia angalau TSH 10,000 tutaweza kufikia na kuvuka lengo la kuanzishwa MSTV...?





-------------------------------------------------------------------------------------------------------
Sasa unaweza kuchangia ujenzi wa kituo cha Televisheni ya Morning Star, MSTV kupitia
AIRTEL MONEY                                          0686 977 711,
M-PESA                                                         0755 476 266 na pia
TIGO PESA                                                   0655 977 719.

Pia unaweza kuchangia kupitia NBC A/C      0261 0100 2126,
Jina la account TANZANIA ADVENTIST MEDIA CENTER
-------------------------------------------------------------------------------------------------------
Anza leo kukusanya sadaka yako kwa jili ya kufikisha ujumbe kwa watu wote maana kilele cha zoezi hili ni Hapo tarehe 2 March 2013.
-------------------------------------------------------------------------------------------------------

Kwa maelezo zaidi tembelea H A P A

ENDELEA KUCHANGIA
 

Jumamosi, Januari 26, 2013

Majibu Yafanyayo Kazi - MAWE MATANO


Ngoja nikwambie msomaji wangu jambo hili, 
kwamba:
MAJIBU YAFANYAYO KAZI 
Ni kipengele kinachoongelea masuala ya kiroho zaidi.
Kwa sababu ya upekee na unyeti wa siku, Sio vibaya tukibadilishana mawazo na kuambizana yaliyomuhimu katika maisha hasa ya kiroho.
Na huu utakuwa ni mfululizo kwa kila siku kama hii ya leo...
(Ninamaanisha JumaMosi)

Pamoja na kwamba weeengi wanaamini hii ni kweli, kweli halisi jionee mwenyewe ambapo tutatijifunza:

MAWE MATANO (5) YA KUMSHINDA GOLIATH  THE GIANT!

Imeandaliwa na Pr. Filbert Joseph Mwanga

Mwanadamu ni kiumbe kidogo katika ya viumbe walioumbwa na Mungu. Lakini ambaye dunia imemtengenezea silaha kali za nyuklia, mizinga na mabomu, n.k. ili kumuua na kumfutilia mbali. Silaha zimewekwa angani – zote hizo sio kuangusha milima- la bali kumuua mwanadamu.

Ndipo swali linakuja kwangu – je watu hawa akili zao ziko sawa? Mtu ambaye anauwawa na mbu tu wa malaria – ‘anopheles’  kuna haja ya kumtengenezea mabomu yote hayo? Silaha zimewekwa angani yote hiyo ni mwanadamu. Silaha hizi zinamsaka mtu ambaye halingani wa karne kama Goliath? Goliath ni nani? THE GIANT! JITU LA MIRABA MINNE!

Goliath aliongoza kambi ya wafilisti akiwa kama mwanaume wa shoka – mtu wa vita tu! Soma 1 SAMWELI 17:1 – 2. Wafilisti walijipanga kwa ajili ya vita. Mbaya zaidi vikawa ndani ya mipaka ya Yuda. Ikiwa kuna vita vibaya kuliko vyote ni vile ambavyo vinapiganwa NDANI YA KAMBI YAKO! Kisa cha Amerika na Iraq – Technical Defensive Matching. Mchezo huu ni mbaya hata kwa timu za mpira wa miguu. Wanapojihami na kurudi nyuma ndipo wanapofungwa maana mpira unachezewa ndani ya goli lao na hivyo wamekaribisha wameshambulizi wenyewe!

Wapagani hawa wamehamishia vita ndani ya mipaka ya Israeli. Kama kuna vita vibaya vya kiroho ni vile vinavyopiganiwa ndani ya mwili wako. Zipo dhambi zinazotendwa ndani ya mwili na nyingine nje ya mwili. 1 CORINTHIANS 6:18, 16 – 17. 

Paulo anataja dhambi hizo ZINAA. Ndani ya mwili. Bali uongo ni nje ya mwili. Uvunjaji wa kanuni za afya ni NDANI YA MWILI. UBINAFSI ndani ya mwili tena unakula taratibu lakini kwa hakika. Unataka kuhudumia MIMI kwanza! Mzee wa kanisa au kiongozi wa kwaya anapokuwa mzinzi kanisa, familia, watoto au kwaya inapoteza mwelekeo. Maana wamekaribisha adui ndani ya ngome. Kiongozi yeyote anapokuwa MBINAFSI kama ni serikali au kanisa anatafuta kufanya huduma zote yeye tu, ataanza kung’ang’ania madaraka yote, na hata akiona wengine wanafanya vizuri hatopendezwa maana anabaki kuuona MIMI anaguswa. Hivyo vita vyake vitapiganiwa moyoni! Ataanza kuonyesha hasira, uadui, kisha unaanza kujihoji kuwa umefanya nini – unajifikiria kuwa kuna tatizo gani? Hakuna lolote makosa anayokutoa na kashfa anazokupa na mateto – ni sababu ya PIGANO LINALOENDELEA MOYONI UBINAFSI!

Maumivu makali ni yale yanayomuumiza mtu kwa ndani. Unaweza ukamuumiza ndugu yako kwa kumpiga na fimbo au chombo chochote kikali na akabaki na kovu; lakini KOVU baya ni lile linalobaki moyoni. Waswahili walisema maneno ni sumu! Kwanini? Maneno ni vita vinavyokwenda kupiganiwa Moyoni – vita ya ndani!  Ndoa nyingi zina watu wanaojua kutoa maneno mabaya – na hayo ndiyo yanayoleta talaka na wala sio ngumi pekee! Bali masimango kwa mumeo au mkeo au watoto! Maneno ni SUMU!

1 SAMWELI 17:3 Majeshi yote wapo katika milima - Israeli na wafilisti. Milima wakati wote inawakilisha – IBADA. ENEO LA IBADA! Inategemea aina ya Mungu unayemuabudu. Israeli ni Mungu wa mbinguni. Wafilisti ni mungu Dagoni. Mungu atakayeshinda vita ndiye mkuu. Tatizo la Israeli wamepanda kwa Mungu wa kweli – lakini katikati yao kuna bonde la ELLA! Hilo ndiyo tatizo kwa Israeli. Wafilisti walizoea mabonde – Shinari, Timna, Gaza, n.k. unaposoma Biblia bondeni inawakilisha MAPOROMOKO YA KIROHO!

Mfalme wao ambaye ni Sauli – amekuwa na ibada nyingi. Pamoja na kuwa wapo milimani –wapo kaika pigano ambalo halina Mungu wa Kweli kati yao. Wote wakapoteza tumaini lao kwa Mungu – wakaona kushindwa mbele yao. 

Fungu 4. Hebu tumuelewe GOLIATH – the Giant! Israeli pamoja na kupanda juu ya Kilima – hawamuoni Mungu wa Kweli – bali GOLIATH – kushindwa! Kwanini? Goliath ni mtu mrefu wa futi 9. Kizazi chao ni watu wa ajabu. Mwingine alikuwa na vidole 24. (2 SM. 21:19-22). Kabila lake ni mrefai – the Giant. Dirii aliyokuwa amevaa ni kg. 50 – mfuko wa sementi! Kichwa cha mkuki wake ni kg. 7. Unawezaje kupambana na mtu aliyekuzidi urefu, uzito na hata umri wewe mtu uliyemfupi tu wa futi 4 au sana sana 6.5? Tena huna uzoefu wowote?!

Lazima kuna siri kuu. DAUDI mwana wa YESE anajua siri hiyo! Soma 1 SAMWELI 17:45.  Kumbe ni JINA LAYESU! MWAMINI YESU NA MANABII WAKE NAWE UTATHIBITIKA! 2 NYAKATI 20:20. 

Unaweza ukaona kila kitu mbele yako kuwa ni kitu cha kutisha – hata ukapoteza mwelekeo. Huenda ni ugonjwa – the giant! Kukosa ajira – the giant! Kukosa mchumba – the giant! Kutafuta wahubiri ni dhambi inayokusumbua – the giant! Dhambi – zaka na sadaka – the giant! GOLIATH! Hivyo unakata tamaa – unalia moyoni. Maumivu ya kiroho – spiritual anguish! Kila siku ngambo ya pili ukiamka asubuhi unaona Goliath amesimama maneno makali kama mkuki moyoni au ubavuni mwako! Hakuna amani kanisani, nyumbani, kazini na majirani! Badala ya kumuona YESU siku ya Sabato – mlimani kwa Bwana unamuona Goliath! Hutamani kurudi nyumbani unaona ni bonde kubwa utakalozama na kutobolewa macho kama Samsoni. 

Hata ijapokuwa muhubiri anasimama saa tano – wengine ndiyo Goliath – Usingizini anaonekana lakini kwenye masengenyo na mateto  macho yote pima! Hata ijapokuwa YESU ameinuliwa juu ya mlima wa Golgotha – bado hatuwezi kumuona Yesu bali Goliath – the giant! Huku akinguruma kiasi ya kuwa unataka kuacha vita vya kiroho na kuvaa silaha za mwili – giza yaani kutumia UBINADAMU kulikabili TATIZO! Huenda hali ya uchumi imekuwa ngumu – sasa watoto hawana ‘school fees’ – naacha kukaza mwendo naogopa na kuvaa silaha za wizi wa zaka na sadaka ili kutatua tatizo!

Kumbuka Israeli kila siku asubuhi walipojipanga hawamuoni BWANA bali GOLIATH – kwao ni utisho tu. Fungu 8 – 11. Tangazo limetolewa kuwa anatakiwa mtu mmoja tu. Atakayesimama na kupambana na adui mmoja. Katika Israeli mtu aliyekuwa anamkaribia Goliath kwa urefu – the giant ni SAULI sio JESHI lote! (Mtu mmoja sio KANISA LOTE). 

Kumbuka Sauli tayari ana mapepo. 1 SAMWELI 16:23. Je mtu aliye na pepo la ubinafsi, uzinzi, anaweza kuongoza jeshi la Bwana? Hapo ndipo taifa lote limepoteza mwelekeo. Huwezi kumtegemea mtu aliye gizani akuongoze katika vita vya ulimwengu. Unaumwa na una mapepo unaenda kwa MGANGA wa kienyeji? Tegemea anguko. Pia kujiongezea mapepo zaidi.

Daudi mwana wa Yese alijua namna kulikabili JITU! Fungu 40. Usikabiliane na jitu bila kuendea KISIMA CHA MAJI YA UZIMA! YALE MAWE MATANO yapo pale kisimani na wala sio bondeni au tambarare, LA! MAWE MATANO LAINI YAPO PALE YA USHINDI! Baada ya kupata mawe hayo ndipo umwendee Goliath – the giant! Ushindi ni wa LAZIMA! Leo nitaanza na JIWE la kwanza aliokota Daudi. Nalo ni KUAMINI JINA LA YESU! ZABURI 20:7 Tatizo la Israeli waliacha Jina la Yesu wakitumainia Jina la Sauli. MATENDO 4:11-12. Hakuna Jina lingine isipokuwa Jina la YESU MNAZERETI! KISA CHA CAMPOREE KENYA – MTOTO NA KAFARA!

Unaposimamisha Jina la Yesu – hakuna mwanadamu au jeshi litakalosimama. Soma CLEAR WORD  inasema, Israeli na Sauli “walipoteza ujasiri wao baada kuona the ‘giant’ – Goliath.  Huwezi ukamuona mwana wa Adamu ukawa muoga na kupoteza matumaini. Mitume walipomuona YESU aliyeangikwa msalabani na sasa YU HAI walikuwa ‘Courageous’ – walitiwa shime kuhubiri Jina la YESU bila woga. 

Daudi alitumia Jiwe LAINI – NIRA LAINI YA YESU! Tumaini la kushinda tatizo lolote linapatikana kwa YESU anaposema leteni mizigo yenu yote mpate kupumzika. Kila jambo gumu kuna ushindi uliofichika kwa Yesu. Siri kuu ni kumtegemea YESU kwa asilimia 100% sio kutegemea Helmet, Dirii, fumo, n.k. hizo silaha zote hazikumsaidia Sauli. Tambua hili SHETANI hatishiwi na muda mrefu wa kuishi kanisani. Ikiwa hiyo ndiyo ‘Defensive Mechanism ya Kiroho’ nataka nikupe pole maana Shetani ni giant! Daudi alijaribu vyote hivyo akagundua hawezi kumshinda Goliath na mambo hayo! Alikumbuka Yule Simba wa Kabila la Yuda! 

Uzoefu wa kukaa kanisani au kusoma Biblia na kujua mafungu mengi – hauwezi kumtisha Shetani. Bali uzoefu katika kutumia silaha ya Jina la Yesu katika shida zako – ni ushindi usio na mpinzani! Shetani ANALOOGOPA NI JINA LA YESU – JIWE MOJA! JIWE KUU LA PEMBENI! MWAMBA ULIO IMARA! WIMBO 192! MWAMBA WENYE IMARA KWAKO NITAJIFICHA! IMARA – MADHUBUTI. FUNGU 45. KISA CHA MTU ALIYEKUFA KWA AJILI YA NG’OMBE!  Msimamishe Yesu Mnazereti kwa Jina hili ni USHINDI!

SOURCE: INGIA HAPA
 

Alhamisi, Januari 24, 2013

YASABABISHAYO MSONGO WA MAWAZO FAMILIANI



Family stressors

Kuzidiwa na majukumu
Mmoja kutoyaelewa majukumu yake 
Mgongano katika kuyatimiza majukumu ya kifamilia (rule conflict) 
Mapungufu katika kuyatekeleza majukumu ya mmoja 
Ukosefu wa kupeana zawadi au vichochezi pale mmoja anapofanya vema, (suprises and motivators)  
Mahusiano mabovu 
Ukosefu wa fedha 
Kutotoshelezeshwa katika tendo la ndoa

Tabia binafsi ambazo zaweza kuchangia katika kuleta msongo wa mawazo 

Mmoja kujisikia au kujithamini zaidi ya mwezake 
Kiwango cha juu cha hasira 
Mmoja kuchukulia kazi yake kuwa ya muhimu zaidi ya ile ya mwenzake 
Mapungufu katika mbinu za mahusiano, Mfano; mmoja hana tabia yakusema asante, au kutoa zawadi au hata kusema neno “nakupenda” 
Udhaifu katika afya ya mmoja

Dalili za kukuonyesha kuwa misongo ya mawazo ipo ndani ya familia 

Mahusiano nje ya ndoa 
Muda mwingi kazini hata kama hakuna kinachofanywa huko 
Malumbano kuzidi 
Mmoja kutokuwa tayari kumhudumia mwenzake katika tendo la ndoa “sexual withdrawal” 
Kuanza au kuzidi kwa matumizi ya vilevi 
Hali ya mmoja kupooza na kukosa raha wakati mwingi 
Uadui baina ya wanandoa

Matokeo ya kuzidi kwa dalili hizi 

Talaka au kutengana 
Mmoja kunyanyasika au wote kunyanyasana 
Unyanyasaji wa watoto (child abuse) nk. 
Visababishi toka nje ya familia (extrafamily stressors) 
Kazi 
Mahangaiko ya maisha 
Familia kubwa (extended family) 
Kukosa kazi 
Mshahara mdogo kazini 
Matatizo ya shule (hasa kwa wale wanaosoma wakiwa ndani ya ndoa) 
Kukosa elimu (kwa wale ambao hawakubahatika kusoma)

Matokeo ya misongo hii kiafya baina ya wanandoa 

Kuongazeka kwa matatizo ya shinikizo la damu 
Kuongezeka kwa matatizo ya misuli (muscle tention) 
Kuongezeka kwa mapigo ya moyo 
Kuongezeka kwa kasi ya mfumo mzima wa upumuaji (breathing system)

Hali hii inapozidi kwa wanandoa tunategemea yafuatayo 

Magonjwa ya moyo 
Shinikizo la damu 
Vidonda vya tumbo (ulcers) 
Maumivu makali na ya mara kwa mara ya kichwa 
Maumivu ya mara kwa mara ya mgongo 
Hypertension 
Saratani (cancer) 
Hofu kubwa katika baadhi ya vitu ( allergic reaction)

Msongo wa mawazo juu ya masuala ya uzazi wa mpango
 

Pangeni ninyi wawili kukutana na kuzungumza na mshauri, hili sio jambo la mmoja wenu bali wote. Fanyeni chaguzi fasaha ni njia ipi ya uzazi wa mpango mtaiweza na mtaipenda. Tafuteni taarifa Muhimu za kuhusu uzazi wa mpango toka kwa wataalamu, marafiki, ndugu, vitabu, na vujarida husika, msitegemee taaria za uzushi zisizoweza kuaminika. Yamkini njia nyingine zitakingana na imani au misimamo yako binafsi, basi pata ushauri toka kwa kiongozi wako wa dini. Katika kuyatimiza haya yote shirikianeni kwa upendo katika kuelekezana na kukumbushana juu ya ushauri mlioupata.

Msongo wa mawazo unaosababishwa na mzazi mmoja kuwa mbali na familia 

Panga kuitembelea familia yako kila upatapo nafasi zaidi ya kwenda maeneo mengine. Wasiliana nao kwa simu mara kwa mara, hii inaruhusu muda wa maongezi na kujuliana hali. Njia nyingine isiyo ya gharama sana ni kutumiana barua, hapa ninatia msisitizo katika barua na sio kadi. Kadi kama za siku za kuzaliwa na nyingine hazina uzito mkubwa wa mawasiliano kama ule uliopo katika barua. Lazima familia yako ijue kuwa unatumia jitihada zako zote katika kuwasiliana nao hii itawajengea haja moyoni ya kutaka kukujibu.

Misongo ya mawazo inayoletwa na masuala ya fedha 

Stress zinazisababishwa na masuala ya fedha ni mbaya sana, zaweza kuvunja mahusiano baina ya wanafamilia, zaweza kuleta matatizo kiafya hasa pale matibabu yanapocheleweshwa mpaka mgonjwa azidiwe sana, kwasababu ya ukosefu wa fedha. Hali hii huwafanya wanafamilia kuwa na hisia mbaya, kutojithamini, na kutojipenda, hali ya kujitawala kwao hushuka maana hamna mwenye uhakika na maisha.

Jinsi ya kukabiliana na misongo hii.

Jifunzeni kuwa na bajeti ya mapato na matumizi ya familia, bajeti hii itawasaidia kupunguza madeni, ambayo kama yasipolipwa huleta stress zaidi na maranyingine kushitakiwa kisheria. Bajeti pia itawasaidia ninyi kutawala fedha zenu zaidi ya fedha zenu kuwatawala ninyi. Namna nzuri ya kuandaa bajeti ni kupiga picha nyuma, nijinsi gani mlitumia fedha mwakajana, au mwezi uliopita. Angalia vyanzo vyenu vya mapato, vile vikubwa na vile vidogovidogo. Wakati wote jitahidi sana matumizi yasije yakawa ya kasi kubwa kuliko kasi ya kuingiza. Fahamu ni vitu vipi hutumia fedha zenu zaidi, matumizi haya yawe ya lazima na yakishatimizwa yote ndio mwaweza kufikiria matumizi mengine ya anasa.


Jumatano, Januari 23, 2013

Namba Zenye Athira ya Kisiasa



Tangu mwaka ule swali la takwimu ya kidini Tanzania limejadiliwa sana inaonekana ni swali lenye uzito wa kisiasa pamoja na upande wake wa kitaalamu. Kwa miaka mingi makadirio ya kawaida yalikuwa Watanzania ni theluthi 1 wafuasi wa dini za jadi, theluthi 1 Waislamu na theluthi 1 Wakristo

Lakini ni wazi ya kwamba dadi ya wafuasi wa dini za jadi imeendelea kupungua. Baadhi ya viongozi na wanaelimu-jamii wanakadiria kwamba jumuia za Kikristo na Kiislamu zipo sawa tu kwa ukubwa, zote huhesabiwa kiasi cha asilimia 30 hadi 40 kwa idadi ya wakazi, na waliosalia ni waumini wa imani zingine, dini za jadi, na wale wasio na dini kabisa.

Lakini wataalamu wengine wanasema uwiano huo unashikiliwa kisiasa kwa sababu uhusiano kati ya Wakristo na Waislamu ni jambo la siasa ya taifa kwa hiyo makadirio yanaelekea kutaja uwiano sawa kati ya pande hizi mbili

Jumanne, Januari 22, 2013

BAHARI SAYARI YA MARS



Na Leon Bahati

WANASAYANSI wa anga kwa muda mrefu wamekuwa wakitafuta uwezekano wa maisha katika sayari nyingine, mbali na dunia. Kuna imani kuwa kwenye sayari hizo, huenda zikapatikana raslimali nyingi kwa urahisi kuliko duniani ambako binadamu wameishi mamilioni ya miaka hadi sasa.

Wataalamu hao wa anga wamekuwa wakifanya hivyo kwa muda sasa na moja ya mambo muhimu waliyoangalia ni upatikanaji wa maji. Popote maji yanapopatikana, wanaamini maisha yanawezekana.Moja ya sayari ambayo wamekuwa wakiichunguza kwa miaka mingi sasa ni Mars, ambayo ni ya nne kutoka kwenye jua. Dunia ni ya tatu.

Sababu kuu za kuichagua sayari hii tofauti na zingine ni kwamba, hali ya hewa inatofautiana kidogo sana na ya dunia. Sayari nyingine kama Mercury na Venus, zipo karibu zaidi na jua na hali ya joto iko juu kiasi kwamba hali ya maisha inaweza kuwa taabu. Mars ambayo wanasayansi wanaipa jina la sayari nyekundu, ipo karibu na dunia, hivyo ni rahisi kufika iwapo wanasayansi watathibitisha iwapo maisha yanawezekana huko.

Wanaiita sayari nyekundu kwa sababu eneo kubwa la uso wake ni wa rangi nyekundu, tofauti na nyingine zilizomo kwenye mfumo wetu wa sayari. Hakuna mwanasayansi ambaye amethubutu kusafiri hadi kwenye sayari hiyo kutokana na ugumu wa kupata vyombo vya kuaminika, vinavyoweza kusafirisha watu kutoka duniani hadi Mars na kurudi salama.

Hata hivyo, hilo siyo tatizo kwa sababu wakibaini mazingira mazuri, utengenezaji wa vyombo hivyo hauwezi kuwapa taabu. Kazi ya uchunguzi imekuwa ikifanywa kwa vyombo maalumu ambavyo havina watu lakini, vina uwezo wa kuleta mawasiliano duniani.

Pia wanatumia viona mbali katika mchakato huo kuchunguza hali ilivyo kwenye sayari hii, ambayo kumekuwapo na hisia kwamba huenda waliwahi kuishi viumbe hai mamilioni ya miaka iliyopita lakini baadae mazingira yakabadilika na kuwa mabaya.

Uchunguzi unaonyesha kuwa, sayari hii ina mabonde mengi ambayo yanakila dalili kuwa awali yalikuwa yanatiririsha maji kama ilivyo mito hapa duniani. Kwa muda mrefu, wanasayansi wamekuwa wakiichukulia sayari hiyo kuwa na mazingira ya jangwa yanayotokana na ukame wa muda mrefu.
 

WAGUNDUA MAJI

 
Mwezi januari 2009 wanasayansi hao walikuja na maelezo kwamba sayari hiyo ina kiwango kikubwa cha maji na mengi yapo mita chache kutoka uso wake. Mmoja wa wanasayansi waliochunguza sayari hiyo ni Profesa Jay Melosh wa Chuo Kikuu cha Purdue, nchini Marekani.

Yeye alisema uchunguzi huo umewapa imani kwamba siyo tu kwamba Mars ina maji bali kuna viumbe wadogo, mfano wa jamii ya bacteria ambao wanaendelea kuishi humo hadi leo hii. Ni uchunguzi ambao waliamini una matumaini tofauti na taarifa za uchunguzi ulizopita na kizuri zaidi pia ni kubaini moja ya miezi yake miwili, maji yapo kwa wingi zaidi.

Miezi inayoizunguka sayari ya Mars ni Demos na Phobos. Phobos ndio mwezi uliogundulika kuwa na kiwango kikubwa cha maji na ndio ulio karibu zaidi na sayari hiyo. Kwa sababu hiyo, wanaamini kwamba maisha yakianza kwenye sayari ya Mars, kuna uwezekano pia wengine wakahamia kwenye mwezi huo wa Phobos.

Taarifa za uwepo wa maji kwenye sayari hii zilitolewa kwenye mkutano wa wanasayansi wanaochunguza anga za mbali, uliofanyika Austria Juni mwaka 2009. Moja ya dalili za uwepo wa maji ni vimondo ambavyo vimekuwa vikianguka kwa wingi kwenye uso wa sayari hiyo. Mtaalamu wa Uhandisi na Mambo ya Anga, Profesa Kathleen Howell alisema picha walizopiga maeneo ambayo vimondo vimegonga uso wa Mars, zilionesha dalili kama za mtu aliyetupa jiwe kwenye eneo lenye tope.

“Sehemu kimondo kilipoigonga sayari ya Mars, aina ya kitu kama tope kiliruka na kusambaa pembeni,” anasema Profesa Howell. Hali hiyo wakaitafsiri kuwa maji yaliyokaribu na uso wa sayari hiyo yaliruka pamoja na udongo wakati, kimondo kilipozama ndani na kusambaa pembeni.
 

HALI IKOJE?

 

Utafiti huo unaashiria kwamba, sayari hiyo ina bahari kubwa iliyoenea chini kwa chini kwenye miamba mita chache kuingia ndani. Milipuko ya volkano ya miaka mingi iliyopita ni kiashirio kingine kwamba, sayari hii ina maji. Uchunguzi unaonyesha kwamba mlipuko huo uliandamana na maji.

Ripoti ya utafiti huo ambao ulichapishwa pia na jarida la Geology, unaonesha kuwa kiwango cha maji kilichopo Mars kinakadiriwa kuwa sawa au kimezidi kile kilichopo hapa Duniani. “Kimsingi, kiwango cha maji tunayoyazungumzia kinalingana ama ni zaidi ya kile kilichopo kwenye uso wa dunia,” Alisema Kiongozi wa Jopo la Wanasayansi hao, Profesa Francis McCubbin, ambaye pia ni Mtaalamu wa Anga Chuo Kikuu cha Mexico.

“Si jambo la kushangaza kwamba, kwenye sayari hii waliwahi kuishi viumbe hai miaka iliyopita,” alisema Profesa Howell na kuongeza:  “Tatizo tutakalokabiliana nalo ni iwapo tayari muda umepita sana kiasi cha kutotambua vyema hali hiyo.  “Lakini, hata kama hautapatikana uthibitisho wa kisayansi wa viumbe kuwahi kuishi miaka iliyopita, jambo muhimu ni uwezekano wa kiumbe kuweza kuishi kwa sasa.”  
 

HATARI KWENYE MARS!


Hatari iliyopo ni kwamba, ni moja ya sayari ambayo imekuwa ikigongwa mara kwa mara na vimondo vinavyoanguka. Ni vimondo vichache sana ambavyo viliwahi kutua kwenye uso wa dunia. Vinapoanguka kuelekea uso wa dunia hukabiliwa na safari ndefu na kutokana na mwendo mkali wa mwanguko, hujikuta vinapata msuguano mkali na hewa, ambao husababisha joto kali linaloimomonyoa udongo hadi inakwisha.

Sayari hii ambayo ipo karibu na ukanda wa vimondo, uso wake una makovu mengi yanayoashiria athari za vimondo vyenye ukubwa tofauti vilivyotua. Vimondo hivi ndivyo vimeweka wazi dalili za kuwapo kwa maji kwenye sayari hii ambayo uso wake unaonekana kama vile jangwa, kwa kutokuwa na miti na ishara ya ukame wa muda mrefu.
 
DALILI ZAONYESHA KUNA VIUMBE HAI
 JE, NI HATUA NZURI YA UWEZEKANO WA BINADAMU KWENDA KUISHI?

Lamu Kisiwa Ambacho Kimedumu Bila Kubadilika



Na mleta habari wa AMKENI! kutoka KENYA.

UPEPO mwanana wenye chumvi ulipiga matanga ya turubai, na kusukuma mbele meli ndogo ya mbao. Juu kwenye sitaha, akishikilia mlingoti, mlinzi alitazama hadi upeo wa macho ili aone nchi kavu, akikaza macho yake kutazama tu Bahari ya Hindi. Ilikuwa karne ya 15 W.K., na mabaharia hawa walikuwa wanatafuta kisiwa cha Lamu.

Dhahabu, pembe za tembo, vikolezo, na watumwa—Afrika ilikuwa na vyote. Wakivutiwa na hazina za Afrika na hamu ya kuvumbua, wanaume jasiri walisafiri kwa mashua hadi kwenye pwani ya Afrika Mashariki kutoka nchi za mbali. Mabaharia walivumilia bahari zilizochafuka na pepo za ghafula wakitafuta hazina. Walifunga safari ndefu, wakiwa wamesongamana ndani ya meli za mbao.

Mabaharia hao pamoja na meli zao dhaifu walipata bandari yenye kina iliyokingwa na mwamba-tumbawe walipofika juu katikati ya pwani ya Afrika Mashariki, palipo na kikundi kidogo cha visiwa, jamii-visiwa ya Lamu. Walipofika hapa mabaharia hao waliweza kupakia upya merikebu zao maji safi na chakula.

Kufikia karne ya 15, kisiwa cha Lamu kilikuwa kituo cha kibiashara chenye mafanikio. Mabaharia Wareno waliofika katika karne ya 16 walikuta wafanya-biashara matajiri waliovalia vilemba vya hariri na kanzu kubwa-kubwa. Wanawake waliokuwa wakitembea-tembea kwenye barabara nyembamba walijiremba kwa bangili za dhahabu mikononi na kwenye vifundo na kujipaka marashi. Kandokando ya maegesho, meli za matanga zikiwa matanga yake ya pembe tatu yamekunjwa zilielea majini, huku zimejazwa pomoni bidhaa za kupelekwa nchi za kigeni. Watumwa waliofungwa pamoja na kuwekwa katika vikundi, walingoja kuingizwa kwenye majahazi.

Wavumbuzi wa mapema wa Ulaya walishangaa kupata usafi wa kiafya wa hali ya juu na usanifu-majengo katika Lamu. Nyumba za mjini zinazokabili bahari zilijengwa kwa matufali ya matumbawe yaliyochongwa kwa mkono katika machimbo ya mawe ya karibu, na milango mizito ya mbao, iliyochongwa kwa uangalifu mwingi, ililinda njia zao za mwingilio. Nyumba zilipangwa vizuri katika safu zilizokusudiwa kupitisha upepo mwanana wa baharini kwenye barabara nyembamba na kutuliza watu kutokana na joto kali.

Nyumba za watu waliokuwa matajiri zaidi zilikuwa kubwa na zenye nafasi ya kutosha. Bafu zilikuwa na maji safi ya mfereji yaliyopitishwa kwa mifumo ya kale ya mabomba. Vilevile mfumo wa kuondoa takataka ulikuwa wenye kuvutia na wa hali ya juu kuliko wa nchi nyingi za Ulaya wakati huo. Mifereji mikubwa iliyochongwa kutoka kwa mawe, iliteremka kuelekea baharini na kubeba maji machafu hadi kwenye mashimo yaliyochimbwa mchangani yaliyokuwa mbali na vyanzo vya maji safi. Matangi ya maji yaliyotengenezwa kwa mawe yaliyokuwa na maji safi ya kutumiwa nyumbani yalikuwa na samaki wadogo waliokula mabuu ya mbu, na hivyo kupunguza idadi ya wadudu hao wanaouma.

Kufikia karne ya 19, majahazi ya baharini yalipata pembe za tembo, mafuta, mbegu, ngozi za wanyama, kaka la kobe, meno ya kiboko, na watumwa wengi kutoka Lamu. Hata hivyo, baada ya muda, ufanisi wa Lamu ulianza kudidimia. Tauni, kushambuliwa na makabila jirani yenye uhasama, na vikwazo kwa biashara ya utumwa vilifanya Lamu ididimie kibiashara.

Kuchunguza Wakati Uliopita
Kusafiri kwa mashua hadi kwenye bandari ya Lamu leo ni sawa na kuchunguza wakati uliopita. Upepo huvuma bila kukoma kutoka Bahari ya Hindi iliyo kubwa ya rangi ya samawati. Mawimbi mepesi ya feruzi huosha fuko zenye mchanga mweupe. Majahazi ya mbao ya muundo wa kale hunyiririka kandokando ya pwani, huku matanga yake yenye umbo la pembetatu na ya rangi nyeupe yakifanana na vipepeo wanaopuruka. Yakiwa yamepakiwa samaki, matunda, nazi, ng’ombe, kuku, na abiria, yaelekea kwenye bandari ya Lamu.

Gatini, michikichi inayovuma kwenye upepo mwanana wenye joto hutokeza kivuli kidogo kwa wanaume wanaopakua shehena kutoka kwenye meli za mbao. Soko limejaa pilikapilika za watu wenye kelele wanaofanya biashara ya kubadilishana bidhaa. Wafanya-biashara hao hawatafuti dhahabu, pembe za tembo, au watumwa, bali ndizi, nazi, samaki, na vikapu.

Chini ya kivuli cha mwembe mkubwa, wanaume wanasokota kamba ndefu za makonge na kushona matanga ya vitambaa yanayoendesha majahazi yao ya mbao. Barabara ni nyembamba na zimejaa watu wanaoelekea kila upande. Wafanya-biashara waliovalia kanzu ndefu kubwa-kubwa waita watu kutoka kwenye maduka yao yasiyo na mpangilio, wakiashiria wateja waje na kujionea bidhaa zao. Punda, anayejikaza kuvuta mkokoteni wa mbao uliojaa magunia mazito ya nafaka, apita katikati ya watu wengi. Wakazi wa Lamu waelekea kutoka upande mmoja wa kisiwa hadi mwingine kwa miguu, kwa kuwa hakuna magari ya kusafiria kisiwani. Njia pekee ya kufika kisiwani ni kwa kutumia mashua.

Jua lifikiapo upeo katikati ya mchana, wakati huonekana kuwa umesimama. Katika joto kali, ni watu wachache ambao hutembea, na hata punda husimama bila kusonga wakiwa wamefunga macho yao kabisa ili kujituliza na joto hilo.

Jua lianzapo kushuka na halijoto kupungua, kisiwa hicho chenye utulivu hujaa utendaji. Wafanya-biashara hufungua wazi milango yao mizito iliyochongwa kwa mbao ili kuanza biashara, na taa zao zitaendelea kuwaka hadi usiku wa manane. Wanawake huosha watoto wao na kuwasugua kwa mafuta ya nazi mpaka ngozi zao zinaanza kung’aa. Wanawake huanza kutayarisha chakula wakiwa wamekalia mikeka iliyofumwa kwa makuti ya nazi. Hapa wanawake bado hupika kwa kutumia mafiga, wakitayarisha vyakula vyenye ladha tamu vya samaki waliokolezwa vikolezo vyenye kunukia vizuri na wali uliopikwa kwa tui. Watu ni wenye urafiki, wakarimu, na wapole.

Ijapokuwa Lamu haina fahari kama zamani, utamaduni wa Kiafrika wa zamani uliokuwako kabla ya karne ya 20 ungali unasitawi hapa. Chini ya jua la kitropiki, maisha yanaendelea kama yalivyokuwa karne nyingi zilizopita. Ukiwa hapa unaweza kuona mambo ya kale na ya wakati wa sasa pia. Kwa kweli, Lamu imeokoka enzi iliyopita kwa njia ya kipekee, ni kisiwa ambacho kimedumu bila kubadilika.

Ziara Yetu LAMU
  Hivi karibuni, tulizuru Lamu tukiwa kikundi, lakini hatukuwa tumeenda kununua au kuuza vitu. Tulienda kuwatembelea akina ndugu na dada zetu Wakristo, Mashahidi wa Yehova wenzetu. Ndege yetu ndogo ilisafiri kuelekea kaskazini juu ya pwani ya Kenya yenye mawemawe. Chini kabisa, kulikuwa na mawimbi shwari kwenye pwani iliyo na misitu mingi ya kitropiki yenye ukingo wa mchanga mweupe. Kisha, kwa ghafula, tuliona jamii-visiwa ya Lamu ikimetameta kama vito kwenye bahari ya feruzi. Kama tai mkubwa wa Afrika, tulizunguka visiwa hivyo kisha tukatua kwenye barabara ya ndege katika bara. Tulishuka, tukatembea kwenye ukingo wa maji, na kupanda jahazi la mbao ili kutusafirisha hadi Lamu.

  Ilikuwa siku nzuri yenye jua, na upepo wa bahari ulikuwa na joto na uliburudisha. Tulipokaribia kisiwa hicho, tuliona kwamba gati ilikuwa imejaa watu furifuri. Wanaume wenye nguvu waliinua mizigo mizito kutoka kwenye mashua, na wanawake walibeba mizigo yao kwa kuisawazisha barabara vichwani. Tukiwa tumebeba mizigo yetu, tulipenya katikati ya umati wa watu na kusimama chini ya kivuli cha mchikichi. Baada ya dakika chache, ndugu zetu Wakristo walituona, na tulikaribishwa kwa uchangamfu kwenye makao yao yaliyo kisiwani.

  Tuliamka vyema asubuhi kabla ya jua kuchomoza ili kukutana na akina ndugu na dada ufuoni. Safari ya kuhudhuria mikutano ya kutaniko ilikuwa ndefu na ingechukua muda wa saa kadhaa. Tulikuwa tumejitayarishia maji ya kunywa, kofia pana, na viatu vinavyofaa kwa safari. Kulipoelekea kupambazuka, tulifunga safari hadi bara, ambapo mikutano ilifanyiwa.

  Akina ndugu walichukua fursa ya kuhubiria watu waliokuwa mashuani, na hadi tulipofika, tulifurahia mazungumzo fulani ya Biblia na kuangusha magazeti kadhaa. Barabara isiyokuwa na watu ilikuwa na joto na vumbi. Tulipokuwa tunatembea kichakani, tulishauriwa kuwa macho kwa sababu ya wanyama wa mwituni, kutia ndani tembo waliovuka barabara pindi kwa pindi. Akina ndugu walikuwa na furaha na uchangamfu huku tukitembea polepole mahali tulipokuwa tunaenda.

  Punde si punde, tuliwasili kwenye kijiji kidogo ambapo tulikutana na wengine wa kutaniko waliokuwa wametembea kutoka mbali. Kwa sababu ya umbali, mikutano minne ya kutaniko ingefanywa siku hii moja.
  Mikutano ilifanywa katika shule ndogo iliyojengwa kwa mawe yasiyo laini, bila milango au madirisha yaliyokamilishwa kwa ustadi. Ndani ya darasa moja, 15 kati yetu tuliketi kwenye benchi nyembamba na kufurahia programu nzuri inayotegemea Biblia, iliyokuwa yenye kutia moyo na kufundisha. Hakuna aliyebabaishwa na joto kali lililokuwa likitoka kwenye paa ya mabati juu ya vichwa vyetu. Wote walifurahi kuwa pamoja. Baada ya saa nne za mikutano, tuliagana kisha kila mtu akaenda zake. Kufikia wakati tuliporudi Lamu, jua lenye rangi ya kidhahabu lilikuwa likitua kwenye upeo wa macho.

  Jioni hiyo, kwenye baridi ya usiku, tulifurahia mlo sahili pamoja na familia za Mashahidi wanaoishi Lamu. Katika siku zilizofuata tulitembea pamoja nao katikati ya barabara nyembamba zenye kujipinda, tukihubiri na kutafuta watu walio na njaa ya kweli ya Biblia. Tulitiwa moyo na bidii na ujasiri wa ndugu na dada hao wachache.

  Hatimaye siku ilifika ambapo tulihitaji kuondoka. Akina ndugu walitupeleka ufuoni, na tukaagana kwa huzuni. Walituambia kwamba walitiwa moyo na ziara yetu. Tulijiuliza ikiwa walijua jinsi walivyokuwa wametutia moyo! Tuliporudi bara, punde si punde tulipanda ndege yetu ndogo. Tulipopaa juu kabisa angani, tulitazama chini na kuona kisiwa maridadi cha Lamu. Tulifikiri juu ya imani yenye nguvu ya akina ndugu wanaoishi huko, umbali wanaosafiri ili kuhudhuria mikutano, na bidii na upendo walio nao kwa ajili ya kweli. Zamani za kale unabii ulirekodiwa katika Zaburi 97:1: “BWANA ametamalaki, nchi na ishangilie, visiwa vingi na vifurahi.” (Italiki ni zetu.) Kwa kweli, hata kwenye kisiwa cha mbali cha Lamu, watu wanapewa fursa ya kushangilia katika tumaini kubwa zaidi la paradiso ya wakati ujao chini ya Ufalme wa Mungu.—Imechangwa.

SOURCE: CLICK HAPA

Jumanne, Januari 01, 2013

Asili na hatma ya mwisho wa ulimwengu

Ingawa mfano wa Mlipuko Mkubwa ulipambana na mashaka mengi ulipozinduliwa kwa mara ya kwanza, shaka iliyochangiwa na uhusiano na dhana ya dini ya uumbaji, imekuja kuungwa mkono na uchunguzi kadhaa wa kujitegemea. Hata hivyo, fizikia ya sasa inaweza kuelezea tu ulimwengu wa mapema kutoka sekunde 10_"43 baada yaMlipuko Mkubwa (ambapo muda sufuri unawiana na kipimo joto kinafikia idadi isiyopimika), nadharia fulani ya mvuto wa kikwontamu huenda ikahitajika kurudi nyakati zazaidi. 

Hata hivyo wanafizikia wengi wamedadisi kuhusu nini kinachoweza kuwa kimetangulia kikomo hiki, na jinsi ulimwengu ulivyoanza. Baadhi ya wanafizikia hudhani kuwa Mlipuko Mkubwa ulitokea kiajali, na wakati kanuni ya kianthropiki inapozingatiwa, mara nyingi hutafsiriwa kama kuashiria kuwepo kwa ulimwengu maridhawa.

Hata hivyo, haijalishi jinsi ulimwengu ulikuja kuwepo, hatma ya binadamu katika ulimwengu huu ni maangamizi kwani - hata kama ubinadamu utaishi muda huo wote - maisha ya kibaiolojia hatimaye yatashindwa kujiendeleza, iwe kupitia Kuthelujika Kukubwa, Kuraruka Kukubwa au Kupasuka Kukubw]. Ni bayana kuwa njia pekee ya kuishi milele itakuwa kuuongoza mtiririko wa nishati kwenye Kiasi cha Kikosimki na kuibadilisha hatma ya ulimwengu.