Mtayarishaji

Morning Star Radio

Alhamisi, Juni 23, 2016

SOMA KITABU CHA UJASUSI WA KIDOLA NA KIUCHUMI


Kwa mjibu wa nyaraka za MOSSAD, CIA, RAW na FSB juu ya elimu ihusuyo "kiwango cha hali ya hatari katika eneo la kiraia" ambacho hupimwa kwa kipimo kiitwacho Def Cond, inasema, "Pale majadiliano ya meza yanaposhinwa kuleta jibu chanya, wanamjadala hususia meza, ambapo katika kipimo husomeka Def Cond 0001".

Ikitokea kuwa hata huko walikoamua wanamjadala hao kupeleka hisia zao nako kukazuiwa, hasira ya wanamjadala hao huongezeka na kuwa Def Cond 0002.

Hatua ya mwisho ya wanamjadala hawa huwa ni kwenda kwenye mahakama ya umma, hapa kipimo husomeka Def Cond 0003.

Hiki ni kipimo kikubwa katika medani ya kiusalama kwa mambo ya ndani, ambapo matokeo yake shughuli katika jamii husimama, serikali hushindwa kutawala wala kuongoza. Katika lugha nyingine huitwa mgogoro wa ndani,kisiasa,kikatiba nk...

Zingatia hali hii haizai vita, kwani ili vita kamili ya ndani izaliwe lazima hali ya hatari isomeki Def Cond 0006. Na ili vita kamili izaliwe katika ya taifa na taifa lazima hali ya hatari isomeke Def Cond 0008.

Mzigo ukiwa dukani tayari kwa mauzo,
Bei ya rejareja 30,000/=
Bei ya Jumla 25,000/=

Fika Dukani House of Wisdom Bookshop lililopo Dar es Salaam, Posta, mtaa wa Samora jengo la NHC Ghorofa ya kwanza.

Kwa walio nje ya Jiji la Dar wanaweza kununua kwa M-Pesa +255755865544 Yericko Nyerere. Utaletewa mahali ulipo kwa njia ya Posta.

PIA KWA MAUZO YA JUMLA LIPA KUPITIA BANK YA CRDB
AC NO: 0152241955000.
Name: YERICKO YOHANESY NYERERE.
BRANCH NAME: HOLAND HOUSE
BRANCH CODE: 3319
BANK NAME: CRDB BANK PLC
SWIFT CODE: CORUTZTZ
CURRENCY: TZS.

WANAKARIBISHWA WAFANYABIASHARA WALIOTAYARI KUWEKEZA KATIKA BIASHARA HII.


Wasiliana kwa simu: +255 715 865 544

Jumapili, Juni 12, 2016

UMUHIMU WA ELIMU YA MUZIKI NA ELIMU YA UENDESHAJI WA MUZIKI

Photo By: www.borgenmagazine.com


Asilimia kubwa ya wanamuziki hapa Tanzania wanapiga muziki bila ya kuwa na elimu yoyote ya awali ya muziki, hili si jambo la ajabu kwani hali hii iko sehemu nyingi duniani, lakini kitu ambacho ni wazi kinakosekana ni elimu kuhusu utendaji wa taasnia ya muziki. 

Pamoja na kauli nyingi nzuri za viongozi wa Nchi kusifu sanaa hii na wasanii wa sanaa hii lakini ni nadra kusikia kiongozi akiongelea matayarisho rasmi katika sanaa hii na kwa kweli hata katika sanaa nyingine.

Kumekuwepo na ombwe la elimu ya uendeshaji wa tasnia ya sanaa. Ombwe la elimu kwa wataalamu ambao huwezesha wasanii kufika walipo, kuwaendeleza kukaa walipo, kulinda haki za kimaslahi za wasanii na hata kuwapa maelekezo ya kujitayarisha kwa wakati ambapo umaarufu utakuwa umekwisha.

Tasnia ya muziki huhiyaji shule za kujifunza muziki, vyuo vya uongozi wa muziki, au kozi fupi ambapo taaluma za umeneja, uproducer, upublisher, usambazaji, ujuzi wa sheria za hakimiliki na watendaji wengine wa aina hiyo hupata elimu, ujuzi wa sheria za hakimiliki na watendaji wengine wa aina hiyo hupata elimu. Kukosekana kwa elimu hii kumefanya watu kujifunza kwa vitendo kwa kujaribu na hata kubahatisha hivyo mara chache kufanikiwa.

Kukosa elimu sahihi kumewafanya wasanii wengine wenye uwezo mkubwa kupotea kwenye taaluma na wengine kujikuta wakishindwa kuingia kwenye ulingo huu japo uwezo wanao. Pia kumetoa nafasi ya wasio na uwezo kujikita katika uongozi wa sanaa na kuleta matatizo makubwa kwenye sanaa, aidha kwa kuaminika kuwa wanatoa ushauri sahii na hivyo maamuzi yenye hasara kubwa kufanyika. 

Pamoja na mafanikio yaliyoonekana taifa linakwenda kihobela hobela katika tasnia ya sanaa ya muziki. Ushahidi wa wazi upo kwa kupata elimu ya muziki kuanzia umri mdogo kuna faida nyingi sana. Kwanza humuwezesha motto kukuza sehemu ya ubongo ambayo huhusika na hesabu na pia kukuza uwezo wake wa kutafakari. 

Inaeleweka kuwa ubongo huendelea kupata maendeleo miaka mingi baada ya kuzaliwa, hivyo muziki huendelea kuboresha upande wa kushoto wa ubongo ambao ndio huhusika na ujuzi wa lugha na tafakari na hesabu. Muziki husaidia sana watoto kukumbuka mambo mbalimbali, ndio maana hata matangazo ya biashara ya kawaida husindikizwa na muziki ili kukaa katika kumbukumbu kwa urahisi. Kwa watoto muziki husaidia sana katika kazi zao za elimu ya kila siku.

Wasanii waliopata elimu sahihi huwa na uwezo wa kubuni majibu mbalimbali kwa tatizo moja, hii unaweza kuiona kwa mfano ukiwapa wanamuziki kumi semina kuhusu jambo. Kwa mfano: Ukimwi kasha ukawaambia watunge wimbo kuhusu elimu waliyopewa, utashangaa watakuja na tungo tofauti za mtizamo mpya kabisa wa kuelezea elimu hiyo waliyoipata.

Elimu ya muziki hufungua ubongo kuruhusu kuachana na mawazo mengi yaliyopita na kujaribu mawazo mapya. Wasanii kote duniani huwa waanzilishi wa mambo mengi ikiwemo mitindo ya nguo, uvaaji na mambo mengi katika maisha kutokana na ubongo wao kuwa na uwezo wa kuruhusu kufikiria vitu katika mtazamo mpya.

Elimu ya awali ya muziki imeonesha kuwa wanafunzi wa elimu hii hfanya vizuri zaidi katika masomo mengine tofauti sana na mawazo ya kawaida kuwa muziki huharibu watoto. Katika muziki, kosa huwa ni kosa, ukikosea beat, usipotune chombo chako, ukiimba vibaya ni kosa hakuna mbadala, sauti ikiwa juu mno, au chini mno na kadhalika, na wanamuziki hulazimika kurudia tena na tena mpaka atakapopata kitu sahihi na kabisa.

Elimu hii ikiwa kichani kwa watoto toka umri mdogo humsaidia katika kuboresha mambo yake mengine na kuyafanya vizuri zaidi kila mara. Elimu ya awali ya muziki humjenga motto kujua kufanya kazi na watu wengine kama kundi, kutokana na kuelewa kuwa katika muziki watu wengi hutegemeana ili kuleta ubora katika wimbo mmoja, hii huwasaidia katika maisha kila siku.

Kuna mengi yanayopatikana katika elimu bora ya sanaa, pia kubwa likiwa ni kwenda sambamba kitaaluma na ulimwengu, kuna bahati mbaya sana kwa vijana wetu kutaka kuingia katika soko la muziki duniani lakini bila kuwa na matayarisho yanayostahili kufikia huko, wengi ni ndoto zao hazitatimia kwani elimu ya kufikia huko hawana.

Ni wazi kuna haja ya kuanza kutoa elimu ya sanaa kuanzia ngazi ya shule za awali, kuna haja sasa ya kuwasaidia wanamuziki walioko kwenye taaluma kupata elimu ya haki zao. 

Ni wasanii wangapi wanaojua kuwa katika kila tungo, kuna haki tofauti kumi wanazostahili? 

Watunzi wangapi wanajua wana haki kwa kazi zao kutumika kibiashara? 

Wakati viongozi wakisifia wasanii wan je wakumbuke kuwa kinachowafanya wawe na mafanikio ni kutumia kila njia sahihi kukamua mapato kutoka kwenye haki zao hizo zinazolindwa kisheria.
  
Makala hii ni kwa msaada wa John Kitime

Ijumaa, Juni 03, 2016

UGONJWA WA MKAZO (STRESS)

Photo Credit By:  http://luxuryspablog.com/


Ni ukweli usiopingika kwamba mwanadamu anakabiliwa na changamoto mbalimbali za kiuchumi, kiafya, kijamii na kadhalika. 

Changamoto zote hizo huongezeka zaidi pindi mwadamu anapofikia umri wa utu uzima, kwa maana ya umri wa kubebeshwa majukumu ya kimaisha, kama vile kusaidia wanafamilia, wanaukoo na jamii kiujumla. Hata hivyo, changamoto kubwa za kiafya zinazomkabili mwanadamu huyu, karibu kote ulimwenguni ni ugonjwa wa Mkazo, ambao kitaalamu wanaita Stress pamoja na kupanda kwa Shinikizo la Damu, kitaalamu Hypertension. 

Baadhi ya vitu vinavyosababisha ugonjwa huu wa Mkazo kwa mujibu wa wataalamu wa afya, ni pamoja na hofu au wasiwasi kuhusiana na jambo lolote linaloweza kumkumba mwanadamu, hasa ukosefu wa fedha mfukoni au kutamani utajiri ambao hajui ataupataje. 

 Lakini pia, ratiba za shughuli za kiuchumi na huduma zenye mambo mengi yasiyokuwa na mpangilio huweza kumsababisha ugonjwa huo binadamu, pamoja na ugomvi usiokwisha ndani ya familia, kukumbana na matukio ya kutisha kama vile ya ugaidi na kadhalika.  

Watu wengi ulimwenguni wamezoea kutumia kilevi, kama vile pombe, tumbaku na vileo vingine ili kukabiliana na maradhi hayo ya Mkazo na kupanda kwa Shinikizo la Damu. Hali hiyo, inatokana na wengi wao hao kushidwa hata kula vizuri, huku baadhi yao wakilazimika kutumia muda mwingi kuangalia matukio katika televisheni au kutumia vifaa vya kielektroniki kama vile kompyuta na simu za mkononi kwa muda mrefu ili tu kujisahaulisha na msongo wa mawazo kichwani. 

Mkazo na Kupanda kwa Shinikizo la Damu, ni vitu vinavyoendana sana katika maisha ya mwanadamu, ndiyo maana ili kudhibiti magonjwa hayo, mhusika hushauriwa kudhibiti kwanza hali yake ya Mkazo.

Kituo kimoja cha Matibabu ya Akili kilichoko nchini Uingereza, zinabainisha kwamba katika kila kundi la watu watano ulimwenguni, basi mtu mmoja hukumbwa na maradhi ya Mkazo unaotokana na mazingira ya mahali pake pa kazi. Kwa mujibu wa taarifa hizo, kushindwa kukabiliana na hali hiyo ya Mkazo mwingi, mtu mmoja kati ya watu wanne, hujikuta akilia peke yake bila kupigwa wala kukasirishwa na yeyote, akiwa kazini kwake. 

Hali hiyo inatokana na ukweli kwamba mwanadamu ameumbwa kwa njia ya kipekee kabisa, kwa kuwekewa mifumo mbalimbali mwilini inayofanya kazi mbalimbali usiku na mchana ili tu kumweka vizuri na salama katika maisha yake. 

Kwa mfano, mwanadamu amewekewa mfumo wa hisia za dharura, ambao ni kichochea kikuu cha mwili pindi mwanadamu huyu anapopatwa na Mkazo mwingi. Vichocheo hivyo, ndivyo vinavyomfanya binadamu huyo anapopatwa na hali hiyo aweze kupumua haraka, moyo wake uende mbio na kadhalika hali inayochangia kuongezeka kwa Shinikizo la Damu. 

Aidha, vichocheo hivyo, ndivyo huongeza chembe za damu na sukari kwenye damu. Kwa kawaida, mfumo huo wa hisia za dharura unafanya kazi kubwa ya kumtayarisha mwanadamu kukabiliana na kitu chochote au mtu yeyote anayemsababishia hali hiyo ya Mkazo. 

Hata hivyo, baada ya jambo hilo linalosababisha Mkazo kupita, mwili hurudi katika hali yake ya kawaida, ingawa baadhi ya wataalamu wanaweka wazi kuwa endapo hali hiyo ya hisia za dharura inajirudia mara kwa mara, mtu anaweza akakumbwa na ugonjwa mwingine wa hofu au wasiwasi, ambao kitaalamu unajulikana kama 'Anxiety Disorder'. 

 Kwa hiyo, kwa kila binadamu awaye yeyote yule, ni muhimu kujifunza mbinu za kukabiliana na maradhi hayo Mkazo na kupanda kwa Shinikizo la Damu. Kwa sasa zipo njia kuu rahisi 10 za kukabiliana na hali hiyo. 

mediaphotos/Getty Images


Mosi, ni kuhakikisha unapata muda wa kutosha wa kulala usingizi, Kutopata usingizi wa kutosha kunaathiri hisia, akili, kiwango cha nishati mwilini pamoja na afya kiujumla. Wataalamu wa afya wanashauri mtu mzima apate usingizi wa walau saa nane (8) katika kila saa 24 za siku. 

 Pili, katika kujipangia mipango ya maisha, unashauriwa kutanguliza mambo muhimu yanayokuwezesha kuishi maisha yenye kiasi. Kwa maneno mengine, binadamu anatakiwa kufikiri jinsi ya kurahisisha maisha yake, pengine kwa kupunguza gharama za maisha pamoja na kupunguza muda anaotumia kufanya kazi kazini kwake. 

Tatu, jifunze mbinu za kupumzisha mwili. Kutafakari kwa kina (Meditation), mazoezi ya kuvuta pumzi na yoga ni njia imara za kuondoa Mkazo. 

 Nne, mtu inampasa kuimarisha mtandao wake wa kijamii. Kujiunga na vikundi mbalimbali kama vile vya masomo, kutoa misaada kama vile kwa watoto, yatima na wajane au vikundi vya wajasiriamali. Mwaka 2008, baadhi ya watafiti raia wa Uingereza waligundua njia moja ya kubaki imara pindi mtu anapopatwa na Mkazo. Katika utafiti wao, wanasema moja ya njia ya kubakia imara, ni kujitolea kuwasaidia wengine kwa njia fulani fulani. 

Tano, mtu inampasa kujitahidi kuelewa vizuri hisia za wengine, kitu kitakachomsaidia kupunguza hasira, na wakati huo huo awe mwepesi kusamehe kwa kuwa ni jambo jema pia kimaisha. Utafiti uliofanywa mwaka 2001 nchini Uingereza, ulionyesha kwamba mtu anapokuwa na kinyongo fulani kwa mtu, humsababishia kupanda kwa Shinikizo la Damu pamoja na kuongezeka kwa mapigo ya moyo. Hali hiyo, kwa mujibu wa utafiti huo, inaweza kuondolewa kwa mtu kuwa mwepesi wa kusamehe haraka. 

Sita, kwa gharama yoyote, mtu anatakiwa kujiepusha na ugomvi wa aina yoyote ile. Kugombana na wengine kunaweza kumletea au kumsababishia mtu Mkazo mwingi. Mtu anapokuchokoza jitahidi kutulia, usimwage ugali kwa kuwa yeye kamwaga mboga. Inashauriwa kujitenga naye kwa kukaa faragha, hivyo kusuluhisha mambo kwa hekima na busara nyingi. 

Saba, jipangie ratiba ya matumizi ya muda kwa kuandaa muda wa kutatua matatizo ya familia na ya kazini, kwa kutumia mbinu bora za makubaliano. Aidha, mtu anaweza akatunza muda wake wa kazi na familia kwa ufanisi hivyo kupunguza kiwango cha Mkazo kwake. 

Nane, inampasa mtu ajitahidi kupunguza hali zitakazomwongezea Mkazo kadri awezavyo, kwa kutoruhusu hali zenye kuongeza Mkazo. Kwa mfano, kujiepusha kuwaza mambo mabaya yanayoweza kutokea na kuchota hisia zake. 

Tisa ni kuhakikisha mwili mzima unatunzwa. Baada ya kazi nzito, jitahidi kuukanda mwili kwa maji ya uvuguvugu, kabla ya kula chakula. Mazoezi ya kutembea na kusikiliza muziki unaoifurahisha nafsi yako ni muhimu pia. 10, ni kuondokana na woga wa kuomba msaada kwa jamaa na marafiki au majirani. 

Baadhi ya tafiti zinaonyesha kwamba kuzungumza na marafiki au watu wa familia kuhusu hali inayokupata, husaidia kuondoa ugonjwa wa Mkazo. Hata hivyo, pamoja na njia zote hizo 10 rahisi, inashauriwa na wataalamu wa akili na mifumo ya miili kwamba endapo Mkazo na hali ya wasiwasi itaendelea, ni muhimu kutafuta msaada zaidi kwa Daktari, ikiwezekana upatiwe dawa za kutibu hali hiyo.