Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumanne, Machi 22, 2011

Vizuri kwa kushiriki...NIAMBIE

Mvuvi alimpandisha msomi kwenye mtubwi.!
Wakawa wanavuka maji ya mto.!
Msomi akamuuliza mvuvi.!
Je? Umewahi kupanda ndege.!
Mvuvi akajibu sijawahi.!
Msomi akasema umepoteza asilimia 30% ya maisha yako.
Msomi akauliza tena.!
Je? Umesoma shule.!
Mvuvi akajibu sijasoma.!
Msomi akasema.!
Umepoteza asilimia 40% ya maisha yako.
Mara mtubwi ukaanza kuzama.!
Mvuvi nae kamuuliza msomi.! Je?
Msomi unajua kuogelea.!
Msomi akajibu Sijui.!
Mvuvi akasema umepoteza asilimia 100% ya maisha yako.
Basi msomi akazama majini na mvuvi akaogelea akatoka nje.

Je? Umejifunza nini hapo?..!

Jumatatu, Machi 21, 2011

VYAKULA VINAVYOZUIA KANSA

Rafiki leo ni jumatatu, kuna jambo ambalo linagusa hisia za wengi sana hivyo ikapelekea kushawishika kuweka jambo hili hapa kijiweni ili mwenye kusoma apate maarifa na ufahamu na labda itakuwa msaada kwa wengi. Kama una maoni ushauri mapendekezo usisite kusema.

1.CHAI
Inaelezwa kuwa chai ya kijani na nyeusi ni chanzo kizuri cha kirutubisho kiitwacho ‘catechins’ chenye uwezo mkubwa wa kudhibiti ukuaji wa saratani mwilini. Vile vile chai ina uwezo wa kupunguza hatari ya mtu kupatwa na saratani ya ini, ngozi na tumbo. Taasisi ya Saratani nchini Marekani inaendelea na utafiti kuhusu uwezo wa chai ya kijani na nyeusi katika kupambana na ugonjwa huu hatari usio na tiba. KIUHALISIA CHAI INA SUMU INAYOUA TARATIBU LAKINI KWA UHAKIKA MNO SANA SUMU YAKE HAITOFAUTIANI NA ILIYOMO KWENYE SIGARA.

2. BOGA
Vyakula vingine vinavyotajwa kuwa na uwezo mkubwa wa kuzuia saratani ni Maboga pamoja na karoti, machungwa, viazi vitamu, pilipili nyekundu na za njano. Jamii ya vyakula hivi vina kiwango kikibuwa cha kirutubisho aina ya ‘beta carotene’ na vinapoliwa mara kwa mara vinapunguza hatari ya mtu kupatwa na aina mbalimbali za saratani.

3. SPINACHI
Mboga za majani zenye rangi ya kijani, Spinachi ikiwa inaongoza, ni vyakula ambavyo vina uwezo mkubwa wa kutoa kinga mwilini au kuondoa hatari ya kupatwa na saratani ya ini, kizazi, utumbo mpana na kibofu cha mkojo.

Mboga za majani zinapaswa kuwa katika orodha ya vyakula tunavyokula kila siku, hasa ukizingatia umuhimu wake katika mapambano dhidi ya magonjwa ya kansa na kuwepo kwa kiwango kingi cha Vitamin E, ambayo nayo ni muhimu kwa kinga ya mwili.

4. KITUNGUU SAUMU
Bila shaka kitunguu saumu kinajulikana na kila mtu kutokana na kutumika majumbani karibu kila siku kama kiungo cha mboga. Lakini kitunguu saumu ni zaidi ya kiungo kwani nacho kimeonesha uwezo wa kuondoa hatari ya kupatwa na saratani ya tumbo, koo na matiti kwa mtu anayetumia mara kwa mara. Ili kukiongezea uwezo wake wa kupambana na saratani, kikatekate dakika 10 kabla ya kukipika.

5. NANASI
Nanasi nalo ni chanzo kikuu cha Vitamin C ambayo hutoa kinga mwilini. Mbali na hilo, nanasi pia lina kimeng’enya aina ya ‘bromelain’, ambacho ni muhimu sana katika kutoa kinga dhidi ya saratani ya matiti na mapafu.

6. EPO (apple)
Mbali ya kuwa na uwezo mkubwa wa kutoa kinga mwilini, Epo lina kirutubisho muhimu kiitwacho ‘quercetin’ ambacho kimeeonesha kuwa na uwezo mkubwa wa kupunguza hatari ya mtu kupatwa na saratani ya mapafu na ina uwezo wa kupunguza kasi ya kukua ama kuongezeka kwa seli za kansa ya kibofu. Japo bei ya tunda hili kwa sasa ni kati ya shilingi 500 na 700, lakini ni muhimu kwa afya zetu.

Vyakula vyote vilivyoorodheshwa hapo juu, vina uwezo wa kupambana na saratani kwa njia ya kipekee, lakini utafiti umeonesha kuwa yanapoliwa yote kwa pamoja, hutoa kiwango kikubwa zaidi cha kinga. Hivyo basi, pendelea kula vyakula vyenye uwezo mkubwa wa kutoa kinga mwilini dhidi ya saratani, ambavyo ni matunda, mboga na nafaka, huku vikitiliwa mkazo vyakula vilivyoorodheshwa hapo juu.

HABARI HII NIMEIPATA HAPA:
http://zeeducator.blogspot.com/2010/01/vyakula-vinavyozuia-kansa.html

MWISHO.

Jumamosi, Machi 19, 2011

MAJIBU YAFANYAYO KAZI

Hii ni Moja ya Kazi ya Mikono yangu, Ona Nilivyoshika Mic.

UKURASA WA SIMULIZI HALISI KILA JUMAMOS

Mwaka mzima nimekaa nahangaika nikitamani wazo langu liwe katika halisia, wakati kila mwanzo unapojitokeza dhamira in­­­­­aanza kuwa na maswali .

Mara njiani katika safari zako unakutana na mpita njia! Baada ya kupishana hatua chache mbele wazo linakuijia kwamba huenda ulishawahi kukutana nae mahali.

…Ingawa tunaweza lakini Wakati flani unajiuliza!!

Ningewaona vijana wenzangu na kusema, “Hawa ni Marafiki wa Kufa na Kuzikana. Ningependa kuwa Mmoja wao.” Lakini…

Haikuwa Vigumu Kupata Marafiki Shuleni. Kwa Hiyo Hata Hivyo Mara kwa Mara Nilijikuta Katika Matatizo. Kuna Ugumu Sana wa Kuwa: Isitoshe tuwe:

Fikiria jambo flani ambalo umekuwa ukiahirisha-ahirisha kulifanya, kwa sababu tu hutaki kukosea. Kisha weka tarehe ya kumaliza kulifanya. Halafu unajikuta umekosea!.

Kufanya yote uwezayo na kufanya mambo kikamilifu ni mambo mawili tofauti; la kwanza linaonesha mlingano na la pili ukosefu wa mlingano.

Kupambana na Kutoridhika!!. Je, umewahi kuwaepuka watu kwa sababu hawafai machoni pako? Au je, watu wazuri wamewahi kukuepuka kwa sababu viwango vyako vya urafiki? Yaani ni vya juu mno visiweze fikiwa?

Kwa kadri unavyoendelea njiani katika safari yako uliyozianza ulipokutana na mpita njia! Baada ya kupishana hatua chache mbele wazo lilipokuijia kwamba huenda ulishawahi kukutana nae mahali, na mara baada ya kusimama na kugeuka ili kuthibisha wazo lako hilo jipya unagundua kwamba...

“Hakuna mtu anayependa kuwa rafiki ya watu wanaomfanya aone hafai.”

Nikianza kujiona kwamba sifai nitaaa…! Nikianza kuwa mwenye kudai mengi mno kutoka kwa wengine nitaa…! Majibu yafanyayo kazi.

Kwa sababu ya upekee na unyeti wa siku, Sio vibaya tukibadilishana mawazo na kuambizana yaliyomuhimu katika maisha hasa ya kiroho. Na huu utakuwa ni mfululizo kwa kila siku kama hii ya leo...(NAMAANISHA JUMAMOSI)

Pamoja na kwamba weeengi wanaamini hii ni kweli, lakini kweli halisi jionee mwenyewe kuhusu

Satanism in Hip Hop and Hollywood

HALAFU UTAFAKARI.


Nakutakia SABATO njema R a F i K i.



Ni katika mambo gani maishani wewe hujiwekea miradi isiyoweza kufikika??

Jumatano, Machi 16, 2011

Dunia Isiyo na Njaa...KILIMO KWANZA!?.

Mtizamo wetu:
Niii kuwepo kwa dunia isiyokuwa na njaa na ukosefu wa lishe bora – Dunia ambayo kila mtu ana hakikisho la chakula kistahilicho na kinachofaa ili kuwa na afya bora. Mwono huu uwe ni wa dunia inayotoa na kulinda heshima ya kila binadamu wake wote. Hii ni dunia ambamo watoto wote wanaweza kukua, kusoma, na kusitawi, na kuendelea hadi kuwa watu wenye afya na watu wenye kujali maslahi ya wengine katika jamii na wenye maadili mema hasa ya kiroho.

Kumekuwepo na mafanikio: kwamba, katika kupunguza njaa na ukosefu wa lishe bora duniani, hata hivyo haijafanikiwa kuwa na ulimwengu ambao watu wote hawasumbuliwi na njaa. Tunapewa elimu na habari kwenye masuala yanayohusu njaa ya ulimwengu, kuwepo kwa chakula, na lishe bora kuwa mambo yatakayofanikisha ukweli huu. Kwa hivyo tunakita nguvu zetu kimawazo tu kwa vijana, waalimu na viongozi wao na dini katika nchi zao.

------------------------------------------------------------

Ikiwa kila mwaka watoto kote duniani watatangulizwa kwa pamoja kwa makala tofauti yanayofundisha kuhusu njaa na ukosefu wa lishe na kinachohitajika kufanywa wakati wa siku ya chakula duniani (16 Oktoba) wanaweza kukua wakielewa utegemeano wa dunia na uwepo wa MUNGU ikiwa watafundishwa masomo kutoka sehemu mbalimbali za dunia na kwenye vitabu vya maarifa na hekima hasa kutoka tamaduni mbalimbali na hali, yumkini watakuwa tayari kushirikiana katika kutatua matatizo ya njaa na ukosefu wa vyakula. Kuna njia yoyote ambayo kwayo kikundi cha vijana kinaweza kufundishwa ili kujenga uraia wa kidunia lakini hasa MBINGUNI wenye dhima???.

Tunaamini:

Kuwa...majibu kwa maswali haya yote ni “NDIYO”. Kama walimu na viongozi hata na wa dini mko katika nafasi nzuri na bora kuwaeleza vijana jinsi ya kujali na kuingia katika mapambano dhidi ya njaa. Makisio, mawazo na nguvu za vijana vinawakilisha hazina muhimu ya kuendeleza jamii na mataifa yao. Ninyi waalimu na viongozi lakini pia wazazi na wananchi kwa ujumla tunaweza kusaidia katika kuleta mabadiliko kupitia utoaji wa habari, kushirikiana katika habari, kuhimiza kushiriki na kuonesha vijana kuwa wana jukumu muhimu la kutekeleza katika kupata dunia isiyo na njaa.

UNAITIZAMAJE KILIMO KWANZA...!!?

Jumapili, Machi 13, 2011

Aibu ya vijana wenye nguvu kulelewa.

------------------------------------------------------------------------------------------------
UHUSIANO ni suala binafsi linalohitaji uamuzi wa mtu husika kwa hiari yake mwenyewe, pengine bila kupangiwa wala kuamuliwa.

-------------------------------------------------------------------------------------------------

Hata hivyo yawezekana ukawapo msukumo kutoka kwa mtu au sababu fulani za msingi na zinazoweza kumfanya mhusika kuingia katika uhusiano huo, pengine kwa kuhitaji kusaidiwa kitu na wala si kwa nia au upendo wa kweli kwa mhusika. Hali hiyo mara nyingi inachangiwa na ukata wa fedha, ambapo si tu wasichana ndio hujikuta wakiingia mikononi mwa wanaume kwa ajili ya kumaliza shida zao, bali siku hizi imekuwa hata wanaume nao wanajirahisisha kwa akina dada au akina mama kwa nia ya kusaidiwa. Hali hiyo ya wanaume kujirahisisha inafahamika zaidi kwa jina la ‘kulelewa’, ikiwa na maana kwamba wanakuwa ni watu wa kulelewa ambapo kwa jina maarufu huitwa ‘Maloo’. Utakuta baadhi ya vijana, hasa wanaoonekana kuwa ni wenye haiba ya mvuto wanakuwa na fikra za kupata akina mama wakubwa au hata wasichana wenye kazi zao ili wapate fedha za matumizi. Vijana hufikia kupangiwa nyumba na pengine hata kupewa magari na wanawake hao ili wayaendeshe. Fikra za kufanya kazi za kutumia nguvu, ikiwa ni pamoja na kujituma katika jua na mvua mara nyingi ni ndogo kwao, kwa kuwa kutokana na ile hali ya ‘ubishoo’ wanayokuwa nayo inawafanya kujiona kuwa ni watu wa gharama na ambao watakutwa na baraka za kupendwa na kulelewa, kwa lugha ya mtaani vijana huita ‘zali la mentali’.

***************************************************************************

Inashangaza zaidi kuona kuwa baadhi yao ni vijana wenye miraba minne, nikiwa na maana wana nguvu na hata uwezo wa kufanya kazi za kutumia nguvu ili waweze kuishi. Wapo wengine ambao angalau hujishughulisha na shughuli za ulinzi wa kumbi mbalimbali za burudani, huku wengine wakijishughulisha na masuala ya uanamitindo.

***************************************************************************

Suala la kijana mwenye nguvu, hasa wa kiume, kutegemea kulelewa kwa asilimia zaidi ya 70 ni hatari, si tu kwa familia zao bali pia kwa taifa zima kiujumla kwa kuwa nguvukazi inapungua. Kulelewa huko kunawafanya kupenda kukaa bila kufanya kazi na tena hasa wakiwa na fikra ya kuwa na maisha bora yenye kila aina ya ufahari, huku wakiwasema vibaya wenzao wanaochakarikia kazi. Mmoja kati ya vijana ambao wanapenda tabia hizo, Michael alipozungumza nami aliniambia haya kwamba wapo wenye kupenda hali hiyo, lakini pia kuna baadhi ya akina mama na akina dada ambao hujipendekeza kwao. Anasisitiza kwamba; ...suala la uhusiano ni la binafsi na linamhusu au kuwahusu watu binafsi na akaongeza kuwa kama akina dada wanatongozwa basi hakuna ubaya kwa wao kama vijana pia kukubali kuwa na akina mama au akina dada wanaowataka. Anafafanua kuwa kukaa bila shughuli muhimu ya kufanya ni kitendo kinachowafanya baadhi ya vijana wa aina hiyo kutegemea zaidi wanawake, hasa wenye fedha nyingi, kwa kuwa mtaji wao unakuwa ni ile hali ya haiba ya mvuto waliyo nayo wao vijana. Anasema kwamba yeye binafsi amewahi kukutana na hali kwamba, mama mmoja mwenye kichele chake cha kutosha, akifanya kazi benki alimtaka. Naye hakuwa na hiyana, akakubaliana naye kwa sababu mwanamama huyo, kwa kuwa suala la fedha za matumizi, hakuwa na tatizo, huku kijana husika akizihitaji. Mwanamama huyo alikuwa ameolewa na mumewe alikuwa ni mtu mzima asiyependa masuala ya ujana. Mwanamama huyo alikuwa na miaka 35, kijana akiwa na miaka 30 wakati mume wa mama huyo alikuwa na miaka 52. Anasema kuwa wakati akiwa na mwanamama huyo tayari yeye alikuwa na mpenziwe mwenye umri wa miaka 24, mwanafunzi tu asiyekuwa na chanzo chochote cha mapato. Anasema kuwa yeye mwenyewe licha ya kila mara kusifiwa na mwanamama huyo kuwa ni kijana mwenye mvuto na kupewa karibu kila alichokihitaji – fedha za matumizi, usafiri na mahitaji muhimu, alihakikisha anakuwa makini. “ Najua unajua tena mwenye kuwa na usawa ni mgumu hali ngumu ya maisha lakini wakati huo huo uelewe kuwa suala la upendo ni muhimu, kwa hiyo mtu akinihitaji mimi sina noma na kwa kuwa ninakuwa makini na uhusiano wangu lakini napata ‘chenji’,” anasema Michael. Pia mwanamama mmoja aliyekubali kuwa na tabia kama hizo za kupenda vijana, Mercy, anasema kuwa kama ilivyo kawaida kwa akina baba watu wazima na waliooa kutembea na wasichana wadogo, ndivyo wao pia huwa na uhusiano na vijana. Anafafanua kuwa ni vigumu kwao kukaa na baadhi ya waume ambao wamejichokea au ambao mara nyingi huwa na kazi nyingine nyingi za kufanya kwa muda mrefu. Anasema kuwa kutokana na uwezo wao wa kifedha, akina mama kama yeye wanaamua kuwarubuni vijana hao na kuwatumia watakavyo, ikiwezekana kuwafungia ndani kabisa. “Ah bwana eh! Kulelewa kulelewa, yaani sisi akina mama tukiwalea hao maloo basi inakuwa ni kosa, tena kubwa? Wao wana haki ya kupendwa na hata sisi kama akina mama tukihitaji vijana basi ni haki yetu kwa kuwa wengine waume zetu wenyewe ni ugonjwa wa moyo,” anasema Mercy. Baba mmoja mwenye umri wa karibu miaka 50 alipata kusimulia jinsi alivyopanda kwenye basi ‘daladala’ jijini Dar es Salaam, na baada ya muda dada aliyekuwa ameketi kando yake kidogo, akiisha kumtazama akachukua simu, akaandika ujumbe halafu akampa ile simu yake. Baada ya bwana huyo kupokea simu kwa mshangao na kuanza kusoma ujumbe, alikuta dada huyo akiwa amemwandikia kwamba amempenda na angependa mwisho wa safari hiyo waende wote wakafanye mapenzi. Baba huyo alimkatalia, akamwambia angependa kwenda lakini hana fedha, na msichana huyo akakata mawasiliano.SWALI:

Maana hao wazazi na wao unaweza kuta wanachaguo lao kwako kwamba yumkini kuna binti waliemuona kuwa atakufaa au wanakwambia oa ktk kabila lako.

Kama kweli mke mwema hutoka kwa Mungu kwa mujibu wa mafundisho ya namna ya kuchagua mchumba tuliyoyapata na neno lake linavyosema, kijana anapopata mwenza mtarajwa/mchumba halafu akawaeleza wazazi, hatmaye wafikie hatua ya wazazi kumkatalia kijana wao.

Je, hilo ni dhihirisho kuwa mke mwema hutoka kwa Mungu?

Ijumaa, Machi 11, 2011

Tusipozungumzia Vikwazo vya Maisha...!!


Matarajio ya watu wengi wanapoingia kwenye ndoa huwa ni kupata faraja, ni wachache kati yao hufikiria kukutana na vikwazo vya kimaisha.

Tafiti zinaonyesha kuwa wakati mtu anapotafuta mwenzi huamini toka moyoni kuwa akiwa na waridi wake matatizo ya upweke, kukosa msaada wa hili na lile yatakwisha lakini baadaye anakuja kubaini kuwa aliyokusudia kuyapata hayapati tena na hivyo kujuta kwa kauli kama hizi.


“Kama ningejua kama mwanaume mwenyewe yuko hivi nisingekubali kuolewa.”


Kauli kama hizi mara nyingi hutokea kwa watu ambao hawazungumzii matatizo na vikwazo wanavyokutana navyo katika mapenzi na kuviondoa.


...sio kwamba naongelea ndoa au mahusiano!!!

Kwa sababu ya upekee na unyeti wa siku, Sio vibaya tukibadilishana mawazo na kuambizana yaliyomuhimu katika maisha hasa ya kiroho. Na huu utakuwa ni mfululizo kwa kila siku kama hii ya leo...(NAMAANISHA JUMAMOSI)

Pamoja na kwamba weeengi wanaamini hii ni kweli, lakini kweli halisi jionee mwenyewe kuhusu SATANISM IN HIP HOP HALAFU UTAFAKARI.



Nakutakia SABATO njema R a F i K i.


U m E o N a E e e...!!!!

Tujipe moyo kupitia Prince Amos ambaye ni mtayarishaji wa Music na Video, mmoja wa marafiki zangu muhimu sana hapa Duniani anaposema "AMENIFANYIA NJIA".

Jumanne, Machi 08, 2011

Wototo wetu si wapumbavu

Ni lazima watanzania tufahamu kuwa maamuzi ya watoto yanategemea yale wanayoyapokea kutoka kwa wazazi , mazingira , shule na marafiki . Kudhani kwamba watoto hawatatilia maanani yale wanayoyaona kwenye jumuia yetu iliyotawaliwa na matangazo ya anasa (Consumerism) ni kuwachukulia kuwa watotto wetu ni wapumbavu.

Tunapaswa kuwaelewa watoto wetu kikamilifu . Tuelewe ni binadamu waliojaa hisia . wanauwezo wa kufikiri na kujiunza .

Kiakili wanakua kulingana na wanayoyapokea katika mazingira wanyoishi .

Mazingira anayokulia mtoto ndio yanayomtofautisha na wengine. Sisi waswahili tunasema "Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo".

Tuwaimarishe watoto wetu kwa nguvu ya hoja tunapowalea ili washawishike kujifunza mema.

Hata hivyo kama hatutawapenda na kuwafurahia wakati wote hawataweza kujifunza yale tunayo wapa. Kuwapigapiga na kuwatishia acheni! Acheni!

Bila kuwajengea mazingira yanayofaa kwa malezi hakutatufikisha mbali. Kupiga watoto kila mara ni kuwafundisha woga, chuki na kulipiza kisasi.

Je mazingira ya Tanzania ya leo yanafaa kwa malezi ya watoto?

Kama tulivyoona mazingira yetu yanatawaliwa na anasa za matumizi .

Vyombo vya habari hujali biashara na sio malezi ya kufaa watoto.

Ulaya wanakabiliwa na mmomonyoko wa maadili kwa sababu ya ‘uhuru wa habari’.

Hatuna budi kujiuliza hivi tunakwenda wapi?


Inatia hofu ingawa hili halionekani kuwa tatizo la kitaifa kama tunapoangalia jamii yetu itamezwa na mila na desturi bomu zinazoletwa na vyombo vya habari bila uthibiti yakinifu. Kuthibiti habari kwa manufaa ya watoto sio kuingilia haki ya kupata taarifa tunaangalia zaidi zile habari zinazoweza kuwapa watoto hisia za ukatili, ngono au kudumisha tamaduni za nje.

Lengo la kuthibiti habari ni kulinda malezi ya watoto ambayo kwa kiasi kikubwa hutegemea mazingira, Nyumbani inatakiwa vyombo vya habari vithibitiwe na wazazi kwa manufaa ya watoto. Mtoto anahitaji kupata muda wa kujifunza, kucheza na kupumzika, sio halali kuwaacha watoto waangalie Televison masaa ishirini na nne.