Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumanne, Machi 08, 2011

Wototo wetu si wapumbavu

Ni lazima watanzania tufahamu kuwa maamuzi ya watoto yanategemea yale wanayoyapokea kutoka kwa wazazi , mazingira , shule na marafiki . Kudhani kwamba watoto hawatatilia maanani yale wanayoyaona kwenye jumuia yetu iliyotawaliwa na matangazo ya anasa (Consumerism) ni kuwachukulia kuwa watotto wetu ni wapumbavu.

Tunapaswa kuwaelewa watoto wetu kikamilifu . Tuelewe ni binadamu waliojaa hisia . wanauwezo wa kufikiri na kujiunza .

Kiakili wanakua kulingana na wanayoyapokea katika mazingira wanyoishi .

Mazingira anayokulia mtoto ndio yanayomtofautisha na wengine. Sisi waswahili tunasema "Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo".

Tuwaimarishe watoto wetu kwa nguvu ya hoja tunapowalea ili washawishike kujifunza mema.

Hata hivyo kama hatutawapenda na kuwafurahia wakati wote hawataweza kujifunza yale tunayo wapa. Kuwapigapiga na kuwatishia acheni! Acheni!

Bila kuwajengea mazingira yanayofaa kwa malezi hakutatufikisha mbali. Kupiga watoto kila mara ni kuwafundisha woga, chuki na kulipiza kisasi.

Je mazingira ya Tanzania ya leo yanafaa kwa malezi ya watoto?

Kama tulivyoona mazingira yetu yanatawaliwa na anasa za matumizi .

Vyombo vya habari hujali biashara na sio malezi ya kufaa watoto.

Ulaya wanakabiliwa na mmomonyoko wa maadili kwa sababu ya ‘uhuru wa habari’.

Hatuna budi kujiuliza hivi tunakwenda wapi?


Inatia hofu ingawa hili halionekani kuwa tatizo la kitaifa kama tunapoangalia jamii yetu itamezwa na mila na desturi bomu zinazoletwa na vyombo vya habari bila uthibiti yakinifu. Kuthibiti habari kwa manufaa ya watoto sio kuingilia haki ya kupata taarifa tunaangalia zaidi zile habari zinazoweza kuwapa watoto hisia za ukatili, ngono au kudumisha tamaduni za nje.

Lengo la kuthibiti habari ni kulinda malezi ya watoto ambayo kwa kiasi kikubwa hutegemea mazingira, Nyumbani inatakiwa vyombo vya habari vithibitiwe na wazazi kwa manufaa ya watoto. Mtoto anahitaji kupata muda wa kujifunza, kucheza na kupumzika, sio halali kuwaacha watoto waangalie Televison masaa ishirini na nne.

Maoni 3 :

  1. Umenena kaka!!si kilakitu ni maendeleo!yapo mema na mazuri ya kuwafundisha watoto ambayo yanaonekana yamepitwa na wakati!Uhuru wa watoto usipitilize wawe na kiwango .Wamiliki wa Tv wawe na matangazo ,lakini mengine yasiyofaa kwa watoto yawe usiku sana,nasi tulazimike kuwapangia muda watoto wa kullala mapema na mengine mengi!.

    JibuFuta
  2. I wish kila mtu angeisoma hii , hasa wazazi...kuna hekima na maadili mema hapa. Hongera na nashukuru sana mkuu!

    JibuFuta