Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumatatu, Desemba 20, 2010

BARAZA LA SANAA TANZANIA


Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), liko mbioni kuachia mikakati mizito ya kukuza sekta ya sanaa hapa nchini Tanzania ikiwiwa ni pamoja na kujenga jumba la sanaa litakalokuwa na hosteli za wasanii kwa ajili ya kuishi wakati wakiandaa kazi zao za sanaa.

Akizungumza Katibu Mtendaji wa BASATA jijini Dar es Salaam Ghonche Materego alisema ya kwamba, lengo la nyumba hiyo ya sanaa ni kuwatengenezea sehemu ya eneo maalumu kwa ajili ya wasanii ili wawe na mahali pazuri pa kuandalia kazi zao na kufanya maonyesho.

Mbali na jumba hilo la sanaa, Materego aliongeza kwa kusema kwamba, BASATA iko kwenye hatua za mwisho za kukamilisha ukumbi mkubwa na wa kisasa wa sanaa na burudani wenye uwezo wa kuingiza watu zaidi ya 1,000 wakiwa wamekaa, ambao unatarajiwa kwamba utafufua rasmi sanaa za maonyesho ya jukwaani, ambazo zimekuwa katika hatari ya kutoweka kutokana na kukosekana kwa eneo maalum la kuzionesha na kuziuza.

“Ni matarajio ya Baraza la sanaa Tanzania kwamba, nyumba na ukumbi huo wa sanaa na burudani ulio katika hatua za mwisho utakapokamilika, kutakuwa na uhai mkubwa wa sekta hii hapa nchini, kiasi cha kuanza kuamsha ari na pia kumeesha mizizi kwa Watanzania wengi hususan wale ambao hawathamini sanaa za nyumbani kwao.”

Akizungumzia suala la haki na wizi wa kazi za wasanii, Materego alisema kwamba, pamoja na kuwepo mamlaka nyingine inayoliangaza jambo hilo, BASATA katika mipango na mikakati yake inakusudia kuunda kitengo maalumu cha kulifuatilia, hasa kwenye sanaa za asili ili kuhakikisha tatizo la wizi za wasanii zinapungua na kuimarisha kipato cha wasanii.

Aidha, Materego alieleza zaidi kwamba, muda umefika sasa wa kuwepo kwa sera ya sanaa inayojitegemea, badala ya ilivyo sasa, ambako sekta hiyo inayokua kwa kasi na kuwa tegemeo la vijana wengi.

“Baraza linakusudia kushawishi kupitia njia mbalilmbali, ili sera ya taifa ya sanaa iundwe na baadaye kuleta mageuzi makubwa katika tasnia hii.

Hakuna sababu ya sekta ya sanaa kufichwa ndani ya sera ya utamaduni, kwani kwa sasa imekua sana na kuhitaji muongozo huru wenye kuhitaji uratibu wa kitaifa wa moja kwa moja,” hapa alisisitiza kweli kweli.

Alizidi kusema kwamba, pamoja na sekta ya sanaa hapa nchini kuongozwa na sera ya utamaduni ya mwaka 1997, bado sheria za Bunge na zile ndogondogo zinazosimamia sekta hii ni za 1984, hali inayohitaji kufanyiwa marekebisho makubwa.

Baraza la Sanaa la Taifa ni shirika la umma lililoundwa kwa sheria ya Bunge namba 23 ya mwaka 1984 na kazi zake kubwa ni kuratibu matukio ya sanaa nchini, kusimamia na kukuza sekta ya sanaa nchini kupitia kuhimiza ubunifu wa sanaa bora asilia.

Sasa, kazi kwako mwana sanaa.

Jumapili, Desemba 19, 2010

ACAPPELLA KWANZA

Baadhi ya viongozi wa A CAPPELLA KWANZA TANZANIA, Kutoka kushoto ni Maduhu (Katibu), Amani (Mwenyekiti), Enosi(Mratibu/Mawasiliano) na Yusuph (Makamu Mwenyekiti)

A cappella Kwanza ni kikundi cha kijamii chenye makao makuu yake jijini Dar es salaam,kinachojihusisha na shughuli za sanaa ya muziki wa A cappella. Ni kikundi kilicho na lengo la kusimamia,kukuza na kuendeleza fani ya muziki wa A cappella ikiwa kama sehemu mojawapo ya kuhubiri neno la Mungu na kutoa elimu kwa jamii juu ya uwepo wa utajiri wa kihistoria wa sanaa ya muziki wa A cappella.

Ninapozungumzia A cappella ninamaanisha uimbaji usiotumia ala za muziki.

Msingi wa A cappella ni wa kihistoria ulianza karne nyingi zilizopita,Ulianza ambapo jamii za makabila mbalimbali zilikuwa zikiimba nyimbo za kidini,muziki huu pia ulianza zamani kabla ya hata ya ugunduzi wa vyombo vya muziki.

Mpaka sasa hakuna taasis ama kikundi chochote ambacho kimekuwa kikijihusisha na maendeleo ya muziki wa A cappella nchini Tanzania mbali na kikundi cha A CAPPELLA KWANZA kilichosajiliwa mwaka 2006 na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Morning Star radio na AWR-Morogoro.

Hapa Tanzania aina hii ya uimbaji imekuwa ikitumiwa sana na kwaya ama vikundi vya makanisa mbalimbali kama vile, Kanisa la waadventsita, kanisa la kiinjili la kirutheri, kanisa la baptist n.k

Vikundi ambavyo vimekuwa vikiimba muziki wa A cappela kwa haraka haraka baadhi wakati wa miaka yaaa 2006 kurudi nyuma ni The Voice, Tukumbukeghe Singers, Royal Advent Quartet, Ilala Male Chorus, Busy Bee Quartet, Magomeni Trio, Zanzibar Brothers, Magomeni Heralds, Sonda ya Dilu Singers n.k

Kwa mara ya kwanza hapa nchini A CAPPELLA KWANZA ilifanya kongamano la uimbaji wa A cappella katika ukumbi wa Msimbazi Center jijini Dar es salaam March 11,2007 ambapo Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Mhe.Hulda Kibacha alikuwa mgeni rasmi.

Hata hivyo tumeanzisha umoja wa A cappella TANZANIA na Januari 1, 2011 umoja huo utaanza kazi rasmi. Kuna Programme tumeanzisha inayoitwa ACAPPELLA MTAANI.

STAY TUNE

105.3 fm-Dar es salaam.

MENGI TUTAKUJULISHA HUMU HUMU NA KWENYE KIPINDI AMBACHO HURUKA KILA IJUMAA KUANZIA SAA 2:00-3:00 USIKU NA KILA JUMAPILI KUANZIA SAA 10:00-12:00 JIONI.

...kwa mawasiliano zaidi tumia namba ama email ktk Profile ktk Blog hii.


MTIZAMO KUHUSU BINADAMU

Binadamu wote ni sawa lakini tunatofautiana kimawazo, fikra, kiutendaji, kipawa nk. Haya nilikuja kuyadhitisha katika kufuatilia fikra za Mwanafalsafa aliyekuwa maarufu sana kwa uchambuzi wa fikra na mawazo ambaye alikuwa anaitwa Plato.
Katika kazi yake ya "Republic" Plato alisema kuwa kila binadamu ameubwa tofauti kutokana na wengine kuwa na akili nyingi ambaye yeye aliwaita "golden boy" ambao yeye hawa aliwaelezea kuwa ni wale wanaweza kuwa viongozi wa nchi yaani (Philosphers, Gvern Planners and Rulers)

Wengine wanaakili ya kawaida "Silver boy" kwa mujibu wa Plato hawa ni wale wanaotakiwa kuwa walinzi wa nchi yaani askali jeshi na polisi pia alisema kundi la mwisho wa wale ambao wanaakili finyu "Iron Boy "hawa Plato alisema kuwa kwa kuwa wanauwezo mdogo wa kupambanua mambo kazi yao ni kulima na kuwa wazalishaji wa bidhaa za nchi.

Hii ilikuja pale nilipojaribu kufanya uchunguzi wangu na kugundua kuwa kumbe hata katika suala la upendo binadamu tuko tofauti wengine wanapenda wanene wengine wembamba na wengine weupe wengine weusi.

Katika makabira wengine wanapenda kabira fulani, kama mimi ninapenda wachaga na wengine hawapendi wachaga wengine wasomi wengine hawapendi wasiomi kwahiyo kutokana na hili binadamu tuko tofauti.

Je, katika mtazamo wako wewe unaona je? tujadili.

YOUTH COUNCELING

Helping youth cope with personal difficulties through interviews and other procedures, with the aim of allowing them to reach solutions to those difficulties themselves. the Counselling covers a wide spectrum of therapeutic activity, from practical advice given during one or two meetings to sympathetic attention over months or years. Youth counseling may specialize in particular areas, such as bereavement, trauma after battle or disaster, or living with serious illness...

Visit:www.sdamagomeni.org

Alhamisi, Desemba 09, 2010

WAGENI MELODIES SDA SING'ES



From Wikipedia, the free encyclopedia
Gospel music is
music that is written to express either personal, spiritual or a communal belief regarding Christian life, as well as (in terms of the varying music styles) to give a Christian alternative to mainstream secular music. ________________________________

Like other forms of Christian music, the creation, performance, significance, and even the definition of gospel music varies according to culture and social context. Gospel music is composed and performed for many purposes, including aesthetic pleasure, religious or ceremonial purposes, and as an entertainment product for the marketplace. However, a common theme of most gospel music is praise, worship or thanks to God, Christ, or the Holy Spirit.


Style Gospel music in general is characterized by dominant vocals (often with strong use of harmony) referencing lyrics of a religious nature, particularly Christian. Subgenres include contemporary gospel,
urban contemporary gospel (sometimes referred to as "black gospel"), Southern gospel, and modern gospel music (now more commonly known as praise and worship music or contemporary Christian music). Several forms of gospel music utilize choirs, use piano and/or Hammond organ, drums, bass guitar and, increasingly, electric guitar. In comparison with hymns, which are generally of a statelier measure, the gospel song is expected to have a refrain and often a more syncopated rhythm.


Many attempts have been made to describe the style of late 19th and early 20th century gospel songs in general. Christ-Janer, et al. said "the music was tuneful and easy to grasp... rudimentary harmonies... use of the chorus... varied metric schemes... motor rhythms were characteristic.... The device of letting the lower parts echo rhythmically a motive announced by the sopranos became a mannerism..." Patrick and Sydnor emphasize the notion that gospel music is "sentimental", quoting
Sankey as saying, "Before I sing I must feel", and they call attention to the comparison of the original version of Rowley’s "I Will Sing the Wondrous Story" with Sankey's version. Gold said, "Essentially the gospel songs are songs of testimony, persuasion, religious exhortation, or warning. Usually the chorus or refrain technique is found."
Source --------------------------------------------------------

Description above from the Wikipedia article Gospel music, licensed under CC-BY-SA, full list of contributors here. Community Pages are not affiliated with, or endorsed by, anyone associated with the topic.

Ijumaa, Desemba 03, 2010

THE SHINE GROUP

HISTORIA YA KIKUNDI CHA THE SHINE

UTANGULIZI:
Kikundi cha THE SHINE kilianzishwa mnamo mwezi wa tano (5), mwaka 2006, kikiwa na wanakikundi watatu, ambao ni SAMWEL SAUL, DEOGRATIUS WASHINGTON na VENANCE H. NYAMBO. Ilipofika mwezi wa saba (7) mwaka huo huo, waliongezeka wanakikundi wengine wawili ambao ni TUMAINI DAUDI na EMANUEL JOSEPH. Hivyo kikundi cha THE SHINE kinaundwa na wanakikundi watano kwa jumla.



CHIMBUKO LA KIKUNDI
SWALI: Je, SAMWEL ukiwa kama mwenyekiti wa kikundi, unaweza kutueleza chimbuko la kikundi cha THE SHINE?
SAMWELI SAUL: Ahsante, manamo mwaka 2005 mwanzoni kabisa mwa mwaka , nilipata njozi ya kuanzisha kikundi cha uimbaji muziki wa ACCAPPELLA, baada ya kuvutiwa sana na uimbaji huu, kilichojulikana kwa jina la, THE HARPVOICE kikundi hiki kilikuwa na wanakikundi zaidi ya kumI (10) nikiwemo pamoja na mimi mwenyewe SAMWEL pamoja na DEOGRATUIAUS WASHNGTON na wengine wengi, ingawaje sikuwahi kusoma elimu ya muziki ila tu ilikuwa ni kipaji kutoka kwa mungu mimi kupenda muziki.

SWALI: Sasa SAMWEL Je waweza kutueleza, vipi kuhusiana na matumizi au kuanzishwa kwa jina la “THE SHINE”?

SAMWELI SAUL: Oh! Mnamo mwaka 2006 mwezi wa 4 kundi hili la “THE HARP VOICE” ulivunjika, kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kama wingi wa wanakikundi uliopelekea migongano ya mawazo na hivyo kutoelewana.
Mara tu baada ya “THE HARP VOICE” kuvunjika kwa kweli bado nilikuwa na njozi ya kuendelea kumtumikia mungu zaidi kwa njia ya uimbaji katika kikundi ambacho kitasimama na kuongozwa na Mungu mwenyewe. Kwa neema ya Mungu ndipo nilipopata njozi na kuanzisha kikundi cha “THE SHINE” bado nilikuwa mwenyewe. Ndipo nilipoungana na mwenangu aitwaye DEOGRATIUS WASHINGTON ambaye baada ya kuvunjika kwa “THE HARP VOICE” hakuwa na pakusimama wala kuimba.

SWALI: Je, mkiwa wawili mmeshawahi kufanya huduma ya uimbaji sehemu yoyote?

DEOGRATIUS WASHINGTON: kwa kweli, hatukuwahi, kufangy huduma ya uimbaji yoyote tukiwa wawili. Tulianza kufanya hudumaya uimbaji tulipokuwa watatu, mara baada ya kumpata mwenzetu aitwaye VENANCE HONEST NYAMBO. Ndipo tulianza kufanya huduma ya uimbaji kanisani yaani MANZESE S.D.A CHURCH pamoja na makanisa mengine ya jirani.

SWALI: Je, vipi kuhusu TUMAINI DAVID MGUTU na EMMANUEL JOSEPH kwenye kikundi?

SAMWEL SAUL: mnamo mwaka huohuo mwezi wa 7 tulifanikiwa kumpata mwenzetu aitwae TUMAINI DAVID MGUTU, na kushirikiana naye kwenye kazi hii ya uimbaji na pia akiwa kama katibu wa hii kikundi.

Mnamo mwaka 2007 mwezi wa 3 tena tulifanikiwa kumpata mwenzetu mwingine aitwaye EMANUEL JOSEPH MBWAMBO AKIWA KAMA mtunza ya kikundi. Na hivyo kutimia mana kikundi watano (5) kuunda neon “SHINE”


SWALI: Waweza kutueleza maan ya neno “SHINE”

TUMAINI DAVIDI MGUTU: Neno “SHINE ” llina asili ya kiingereza limaanishalo MNG’AO, NURU AU MWANGAZA. Yaani, “kungarisha neno la Mungu ulimwenguni kote”. Lakini kila herufi kwenye neno “SHINE” linamaa yake kwa lugha ya kiingereza kama ifuatavyo.
S – Smart
H – Honest
I – Intelligent
E – Experience

LENGO/DHAMIRA KUU
Tangu awali tulipokuwa tumekwisha timia watano basi tukawa na lengu kuu ambalo lilituongoza kwenye suala zima la uinjilisti yaani “kuangaza neno la mungu ulimwenguni kote (To shine the word of the lord all over the world)”. Lengo hili kuu lilituongoza katika malengo mengine madogo madogo yakiwa kama:

- huduma kwa jamii
- kukuza ushirikiano na mahusiano baina yetu na vikundi vingine vya ACCAPELLA pamoja na waimbaji wengine wengi.
- Kurekodi na kuzindua album yetu ya kwanza ilikyokua na AUDIO na VIDEO.
- Kuimba katka makanisa mbalimbali ya ndani na nje, ikiwa ni pamoja na mikutano mbalimbali.
- Ukuaji wa kiroho.
- Kuongoa roho.

MAFANIKIO
Kwa neema ya mungu kutokana na lengo letu kuu pamoja na malengo mengine madogo madogo, Mungu alituwezesha katika mambo yafuatayo kati ya hayo yaliyotajwa hapo juu, nayo ni kamka ifuatavyo:-
Tulifanikiwa kwa njia ya uzinduzi wa album yetu ya kwanzan, kukuza ushirikiano na mahusiano baina yetu na vikundi na waimbaji wengine mbalimbali.


- Mnamo 15/07/2007 tulifanikiwa kuingia studio kwa ajili ya kurekodi, kwenye studio za Morning star Radio. Lakini pia Mnamo 29/06/2008, kwa neema ya mungu, tulifanikiwa kuzindua album yetu ya kwanza pale pale kanisani MANZESE S.D.A CHURCH iliyokkua na AUDIO na VIDEO. Tukio hili liliweza kutukutanisha na watu na vikundi vingi na kukshiriki kwa pamoja.


- Lakini pia tumefanikiw kuimba katika makanisa mbalimbali, kwenye mikutano mbalimbali, pia tumeweza kufikisha ujumbe huu kwa njia ya uimbaji na pia tumeweza kualikwa katika maharusi mbalimbali.



VIKWAZO
Pamoja na mafanikio hayo muda mfupi tuliyoweza kuyapata pia tulikuwa na vikwazo mabalimbali ambavyo viliwezesha kuchelewesha ama kuzuia kabisa kazi ya ujilistu kuendelea. Vikwazo hivi vilikua ni kama:-
- Kikwazo cha kwanza ambacho kiliweza kuchelewesha na kuzuia malengo yetu kwa kiasi kikubwa kilikua ni fedha, fedha iliendelea kuwa tatizo kubwa, kwenye maendeleo yetu.
- Kikwazo kingine kilikuwa ni ukosefu wa eleimu ya kutosha juu ya suala zima la muziki. Lakini pia sisi sote tu wanafunzi wa shule za secondary hivyo tumeweza kukosa muda wa kutosha kwenye mazoezi ya uimbaji kwa ujumla.
- Kucheleweshwa kwa album kutoka studio nalo lilikuwa kati ya suala lililotuchelewesha katika malengo yetu mbalimbali.

OMBI
Tunapenda kuleta ombi letu kwenu ambao kwa namna moja ama nyingine umeweza kuisikiliza/kusoma historia hii,kwamba uweze kutusaidia kwenye maombi, ukituombea juu ya malengo yetu ya kuanga neno la Mungu Ulimwenguni kote, tuombee. Lakini pia kama waweza kutoa sapoti/msaada kwa naman yoyote juu ya malengo ambayo bado tunayo. twaweza kuwasiliana simu hizo chini.

MAWASILIANO
255 713 – 764 713 Mwenyekiti
255 712 – 743 737 Katibu
255 714 – 414 914 Mhazini
255 712 – 229 901
E – mail:
theshineaccappellagroup06@yahoo.com

Ijumaa, Novemba 26, 2010

VIONGOZI ECD NA TZ UNION

VIONGOZI WAPYA WA KANISA LA WAADVENTISTA WASABATO KATIKA UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI NA KATI: WAKURUGENZI WALIOCHAGULIWA KUSIMAMIA NA KUONGOZA IDARA MBALIMBALI KATIKA KANDA YA AFRIKA MASHARIKI NA KATI.
1. JP Mulumba - Elimu na Mafunzo ya Uongozi.
2. Elkana Kerosi - Uhusiano, Uhuru wa dini na UtumeUlimwenguni.
3. Uwakili - William Bagambe.
4. Vijana na mambo ya Kiroho - Magulilo Mwakalonge.
5. Huduma ya uchungaji na Familia - Rudatinya Mwangachuchu.
6. Afya na Mratibu wa VVU na UKIMWI - Dr. FesahaTsegaye.
7. Philip Gai - Uchapishaji ,Sauti ya Unabii na Roho ya Unabii.
8. Steven Bina - Mawasiliano na Uinjilisti kwa njia ya Satelite.
9. Elimu - Andrew Mutero.
10. Idara ya Wanawakike na watoto - Debbie Maloba.
11. Elam Musoni - Huduma za Washiriki na Shule ya Sabato.

WATAKAONGOZA IDARA MBALIMBALI KATIKA KANISA LA WAADVENTISTA WASABATO NCHINI TANZANIA TUKIANZA NA NGAZI YA JUU KABISA KAMA VILE RAIS MAKAMU NA WAZIRI:

1.Mwenyekiti - Godwin Ole Lekundayo
2.Katibu - Davis Fue
3.Mhazini - Dennis Wairaha

WAKURUGENZI WA MAIDARA:
1. AFYA, KIASI, VVU NA UKIMWI - GODFEY MABUBA.

2. VIJANA NA MAMBO YA KIROHO - JOSEPH D'ZOMBE.

3. HUDUMA ZA KICHUNGAJI NA FAMILIA - MUSA MITEKALO.

4. ELIMU, UHUSIANO NA UHURU WA DINI - ELIAS KASIKA.

5. MAWASILIANO, MORNING STAR RADIO, AWR NA SAUTI YA UNABII - MIKA MUSA.

6. WANAWAKIKE, WATOTO NA SHULE SABATO - WINFRIDA MITEKALO.

7. UCHAPISHAJI NA ROHO UNABII - ANNA MUHOHO.

8. UWAKILI - JEREMIAH IZUNGO.

Jumatano, Novemba 24, 2010

NI MUHIMU KUFANYA MAZOEZI

Ni muhimu kufanya mazoezi,
ni kwamba unauweka mwili wako safi na pia unaepukana magonjwa madogo madogo
Bibi anasema, usidhani wewe tu unaweza.
Hata mimi naweza usidhani umri ni kitu ha ha ha ha:-)!!!!
...Mmmmmhhh!!
Nawaza kwa sauti hivi huyu bibi ana mifupa kweli?

Riwaya

KIZUNGUMKUTI

HAFSA Hashimu alikuwa na kila kitu chenye kumfanya ayafurahie maisha. Elimu nzuri. Kazi nzuri. Mume aliyempenda kwa dhati ya moyo wake. Alikuwa mwenye furaha ya ndoa yake.
Aliamini hakuna kitu kitakachoharibu furaha ya ndoa yao zaidi ya maradhi na kifo.
Aliamini hivyo, hadi jinamizi la Benito, rafiki yake wa kiume wakiwa shule ya sekondari lilipojitokeza na kumweka katika wakati mgumu zaidi.



HAYA MAISHA

TEKLA Mbena, asingeweza kuisahau maishani mwake siku moja iliyoubadilisha mwelekeo wote wa maisha yake. Alitoka kwenye familia bora. Lakini haya yaliyeyuka mithili ya pande la barafu kwenye pipa la maji yachemkayo.
Mapenzi. Kijana Jimmy anayaharibu matarajio ya Tekla katika maisha yake.
Kila kitu kinamharibiakia Tekla.
Hata mambo yanapomnyookea tena, kivuli cha makosa yake ya nyuma hakimwachi akayafurahia maisha.
Kila kitu kilipopotea kutoka mikononi mwake, anaweza kufanya jambo moja tu.
Kulipa kisasi.


WAKATI FULANI

JANE Siame, anachaguliwa kuwa Waziri Mkuu wa kwanza mwanamke Tanzania. Wanawake wote wananyanyua mikono yao kwa ushindi huo. Wanalazimika kuishusha huku vichwa vyao vikiwa chini kashfa kubwa inapoibuka kuhusiana na historia ya mwenendo wa maisha ya Jane.
Kamati Maalumu ya Maadili ikihusishwa wananchi na viongozi wa dini na siasa wanaoheshimika zaidi inaundwa kumhoji mheshimiwa Waziri Mkuu kabla hajaondolewa wadhifa wake. Kamati hiyo inakutana na mengi yanayoifanya ifikirie mara mbili. Nchi nzima inakuwa katika mkanganyiko mkubwa. Je, aondolewe wadhifa wake na kudharauliwa, ama apongezwe?


Kaa mkao wa kula ukisubiri ujio wa riwaya hizo zenye kukusisimua, na kukufanya usichoke kufungua kurasa kiasi kwamba ufikapo ukurasa wa mwisho, unatamani simulizi iendelee.
http://fadhymtanga.blogspot.com

Bonge la Zoezi

HAYA SASA!! KAZI KWAKO.

Milima ya Alps ,


Uswis 15/10/2010.
Uchimbaji wa barabara chini ya milima ya Alps ambayo itakuwa barabara ndefu duniani kupita ndani ya mlima imemalizika.

Uchimbaji huo amabo ulianza miaka 15 iliyopita ulimalizika leo kwa kuunganisha barabara hiyo na barabara ambayo iliyopo Gottard Base.
Barabara hiyo itaunganisha kusini na kaskazini mwa Ulaya kiusafiri hasa ule wa mizigo mikubwa.

Picha hapo juu anaonekana mmoja ya wafanyakazi akiwa kazini kuanza ujenzi wa reli itakayo tumika kubebea mizigo.

Mtayarishaji: UHABA WA SAFARI

Mtayarishaji: UHABA WA SAFARI

UHABA WA SAFARI


Mambo ya kutafakari kuhusu usalama wetu

Mambo ya Kiva

Saturday morning would mark the official end of Jonothan's KivaWalk. A group of nearly 40 supporters gathered at the Ferry Building to begin a full-day walk through and around beautiful San Francisco. The event would conclude at the Sports Basement in the Presidio, but not before a very important stop at the shoreline of the Pacific. With Jonathon and Kanoa leading the way, the group ran down to the waters edge to witness the end of an epic cross-country adventure. Jonathon eagerly jumped in the ocean, taking a brief moment to think about what he had accomplished: 3,030 miles on foot, from coast to coast , in support of Kiva. It was a wonderful moment to be shared.

Dubai, UAE - 30/10/2010.

Makachero wa UAE na makachero wa kimataifa wa nchi za Uingereza na Amerika wamefanikiwa kuukamata mizigo ambao inasadikiwa ilikuwa ndani ya ndege tayari kuelekea Amerika. Kwa mujibu wa habari zilizo patikana zinasema "mizigo hiyo ilikuwa imetokea nchini Yamen. Mizigo hiyo likutwa na aina fulani ya unga PETN ambao unasadikiwa ungetumika kuleta madhara." Picha hao juu inaonekana moja ya ndege ya kubebea mzigo ikiwa inafanyiwa ukaguzi mara ya habari kupatikana ya kuwa kuna moja ya ndege za kubebea mizigo imebeba mzigo wenye bomu.
http://launite.blogspot.com

Hawa Ndio Wabunge Wako

Huu ndiyo mtazamo wa bunge jipya!
http://innobanzi.blogspot.com

Jumapili, Novemba 21, 2010

MPANGO WA MUZIKI WA ACAPPELLA TANZANIA

NI BAADHI YA VIKUNDI NA CHOIR ZINAZOJIHUSISHA NA MUZIKI WA ACAPELLA, MSIKILIZAJI ENDELEA KUNIJULISHA IKIWA UNAFAHAMU KUNDI AMA CHOIR POPOTE DUNIANI HASA WANAOJIHUSISHA NA AINA HII YA MUZIKI, ACAPPELLA.
  1. WATEULE - KIBAMBA SDA DSM TANZANIA
  2. VOICE OF SANCTIFICATION - BUGURUNI SDA DSM TANZANIA
  3. GRACIOS VOICE - KANANI SDA TANZANIA
  4. AGAPE CHOIR. AKERI LUTHERAN PARISH TANZANIA
  5. THE HOPE SCORES - MACHIMBO S.D.A DSM TANZANIA
  6. MABALOZIWA YESU - BOKO SDA DSM TANZANIA
  7. GLORYSHINE - MONGOLANDEGE SDA DSM TANZANIA
  8. SOUL INFLUENCE - SOUTH AFRICA
  9. PASUWA - MOSHI TANZANIA
  10. NO LIMITS - SOUTH AFRICA
  11. KINGS HERALD - USA
  12. SDA SOUTH AFRICA CORAL
  13. LADY SMITH BLACK MAMBAZO - SOUTH AFRICA
  14. ACAPPELLA COMPANY - USA
  15. FINAL TRUMPET - DSM TANZANIA
MCHAKATO UKO HIVI:
KATIKA SIMU YAKO YA KIGANJANI SEHEMU YA UJUMBE MFUPI ANDIKA NENO MATUMAINI ACHA NAFASI ANDIKA NENO AC ACHA NAFASI ANDIKA JINA LA KIKUNDI AMA CHOIR NA MAHALI WANAPOPATIKANA ANDIKA PIA MAWASILIANO YAO KAMA UNAYO KISHA TUMA KUWENDA NAMBA 15551. ZOEZI HILI NI KWA WALE WAOOOTE WALIOPO TANZANIA.

Nitaendelea Kukupatia Majina ya Vikundi na Mahali Yanapopatikana.