Mtayarishaji

Morning Star Radio

Ijumaa, Desemba 03, 2010

THE SHINE GROUP

HISTORIA YA KIKUNDI CHA THE SHINE

UTANGULIZI:
Kikundi cha THE SHINE kilianzishwa mnamo mwezi wa tano (5), mwaka 2006, kikiwa na wanakikundi watatu, ambao ni SAMWEL SAUL, DEOGRATIUS WASHINGTON na VENANCE H. NYAMBO. Ilipofika mwezi wa saba (7) mwaka huo huo, waliongezeka wanakikundi wengine wawili ambao ni TUMAINI DAUDI na EMANUEL JOSEPH. Hivyo kikundi cha THE SHINE kinaundwa na wanakikundi watano kwa jumla.



CHIMBUKO LA KIKUNDI
SWALI: Je, SAMWEL ukiwa kama mwenyekiti wa kikundi, unaweza kutueleza chimbuko la kikundi cha THE SHINE?
SAMWELI SAUL: Ahsante, manamo mwaka 2005 mwanzoni kabisa mwa mwaka , nilipata njozi ya kuanzisha kikundi cha uimbaji muziki wa ACCAPPELLA, baada ya kuvutiwa sana na uimbaji huu, kilichojulikana kwa jina la, THE HARPVOICE kikundi hiki kilikuwa na wanakikundi zaidi ya kumI (10) nikiwemo pamoja na mimi mwenyewe SAMWEL pamoja na DEOGRATUIAUS WASHNGTON na wengine wengi, ingawaje sikuwahi kusoma elimu ya muziki ila tu ilikuwa ni kipaji kutoka kwa mungu mimi kupenda muziki.

SWALI: Sasa SAMWEL Je waweza kutueleza, vipi kuhusiana na matumizi au kuanzishwa kwa jina la “THE SHINE”?

SAMWELI SAUL: Oh! Mnamo mwaka 2006 mwezi wa 4 kundi hili la “THE HARP VOICE” ulivunjika, kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kama wingi wa wanakikundi uliopelekea migongano ya mawazo na hivyo kutoelewana.
Mara tu baada ya “THE HARP VOICE” kuvunjika kwa kweli bado nilikuwa na njozi ya kuendelea kumtumikia mungu zaidi kwa njia ya uimbaji katika kikundi ambacho kitasimama na kuongozwa na Mungu mwenyewe. Kwa neema ya Mungu ndipo nilipopata njozi na kuanzisha kikundi cha “THE SHINE” bado nilikuwa mwenyewe. Ndipo nilipoungana na mwenangu aitwaye DEOGRATIUS WASHINGTON ambaye baada ya kuvunjika kwa “THE HARP VOICE” hakuwa na pakusimama wala kuimba.

SWALI: Je, mkiwa wawili mmeshawahi kufanya huduma ya uimbaji sehemu yoyote?

DEOGRATIUS WASHINGTON: kwa kweli, hatukuwahi, kufangy huduma ya uimbaji yoyote tukiwa wawili. Tulianza kufanya hudumaya uimbaji tulipokuwa watatu, mara baada ya kumpata mwenzetu aitwaye VENANCE HONEST NYAMBO. Ndipo tulianza kufanya huduma ya uimbaji kanisani yaani MANZESE S.D.A CHURCH pamoja na makanisa mengine ya jirani.

SWALI: Je, vipi kuhusu TUMAINI DAVID MGUTU na EMMANUEL JOSEPH kwenye kikundi?

SAMWEL SAUL: mnamo mwaka huohuo mwezi wa 7 tulifanikiwa kumpata mwenzetu aitwae TUMAINI DAVID MGUTU, na kushirikiana naye kwenye kazi hii ya uimbaji na pia akiwa kama katibu wa hii kikundi.

Mnamo mwaka 2007 mwezi wa 3 tena tulifanikiwa kumpata mwenzetu mwingine aitwaye EMANUEL JOSEPH MBWAMBO AKIWA KAMA mtunza ya kikundi. Na hivyo kutimia mana kikundi watano (5) kuunda neon “SHINE”


SWALI: Waweza kutueleza maan ya neno “SHINE”

TUMAINI DAVIDI MGUTU: Neno “SHINE ” llina asili ya kiingereza limaanishalo MNG’AO, NURU AU MWANGAZA. Yaani, “kungarisha neno la Mungu ulimwenguni kote”. Lakini kila herufi kwenye neno “SHINE” linamaa yake kwa lugha ya kiingereza kama ifuatavyo.
S – Smart
H – Honest
I – Intelligent
E – Experience

LENGO/DHAMIRA KUU
Tangu awali tulipokuwa tumekwisha timia watano basi tukawa na lengu kuu ambalo lilituongoza kwenye suala zima la uinjilisti yaani “kuangaza neno la mungu ulimwenguni kote (To shine the word of the lord all over the world)”. Lengo hili kuu lilituongoza katika malengo mengine madogo madogo yakiwa kama:

- huduma kwa jamii
- kukuza ushirikiano na mahusiano baina yetu na vikundi vingine vya ACCAPELLA pamoja na waimbaji wengine wengi.
- Kurekodi na kuzindua album yetu ya kwanza ilikyokua na AUDIO na VIDEO.
- Kuimba katka makanisa mbalimbali ya ndani na nje, ikiwa ni pamoja na mikutano mbalimbali.
- Ukuaji wa kiroho.
- Kuongoa roho.

MAFANIKIO
Kwa neema ya mungu kutokana na lengo letu kuu pamoja na malengo mengine madogo madogo, Mungu alituwezesha katika mambo yafuatayo kati ya hayo yaliyotajwa hapo juu, nayo ni kamka ifuatavyo:-
Tulifanikiwa kwa njia ya uzinduzi wa album yetu ya kwanzan, kukuza ushirikiano na mahusiano baina yetu na vikundi na waimbaji wengine mbalimbali.


- Mnamo 15/07/2007 tulifanikiwa kuingia studio kwa ajili ya kurekodi, kwenye studio za Morning star Radio. Lakini pia Mnamo 29/06/2008, kwa neema ya mungu, tulifanikiwa kuzindua album yetu ya kwanza pale pale kanisani MANZESE S.D.A CHURCH iliyokkua na AUDIO na VIDEO. Tukio hili liliweza kutukutanisha na watu na vikundi vingi na kukshiriki kwa pamoja.


- Lakini pia tumefanikiw kuimba katika makanisa mbalimbali, kwenye mikutano mbalimbali, pia tumeweza kufikisha ujumbe huu kwa njia ya uimbaji na pia tumeweza kualikwa katika maharusi mbalimbali.



VIKWAZO
Pamoja na mafanikio hayo muda mfupi tuliyoweza kuyapata pia tulikuwa na vikwazo mabalimbali ambavyo viliwezesha kuchelewesha ama kuzuia kabisa kazi ya ujilistu kuendelea. Vikwazo hivi vilikua ni kama:-
- Kikwazo cha kwanza ambacho kiliweza kuchelewesha na kuzuia malengo yetu kwa kiasi kikubwa kilikua ni fedha, fedha iliendelea kuwa tatizo kubwa, kwenye maendeleo yetu.
- Kikwazo kingine kilikuwa ni ukosefu wa eleimu ya kutosha juu ya suala zima la muziki. Lakini pia sisi sote tu wanafunzi wa shule za secondary hivyo tumeweza kukosa muda wa kutosha kwenye mazoezi ya uimbaji kwa ujumla.
- Kucheleweshwa kwa album kutoka studio nalo lilikuwa kati ya suala lililotuchelewesha katika malengo yetu mbalimbali.

OMBI
Tunapenda kuleta ombi letu kwenu ambao kwa namna moja ama nyingine umeweza kuisikiliza/kusoma historia hii,kwamba uweze kutusaidia kwenye maombi, ukituombea juu ya malengo yetu ya kuanga neno la Mungu Ulimwenguni kote, tuombee. Lakini pia kama waweza kutoa sapoti/msaada kwa naman yoyote juu ya malengo ambayo bado tunayo. twaweza kuwasiliana simu hizo chini.

MAWASILIANO
255 713 – 764 713 Mwenyekiti
255 712 – 743 737 Katibu
255 714 – 414 914 Mhazini
255 712 – 229 901
E – mail:
theshineaccappellagroup06@yahoo.com

Maoni 1 :