Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumatano, Novemba 24, 2010

Riwaya

KIZUNGUMKUTI

HAFSA Hashimu alikuwa na kila kitu chenye kumfanya ayafurahie maisha. Elimu nzuri. Kazi nzuri. Mume aliyempenda kwa dhati ya moyo wake. Alikuwa mwenye furaha ya ndoa yake.
Aliamini hakuna kitu kitakachoharibu furaha ya ndoa yao zaidi ya maradhi na kifo.
Aliamini hivyo, hadi jinamizi la Benito, rafiki yake wa kiume wakiwa shule ya sekondari lilipojitokeza na kumweka katika wakati mgumu zaidi.



HAYA MAISHA

TEKLA Mbena, asingeweza kuisahau maishani mwake siku moja iliyoubadilisha mwelekeo wote wa maisha yake. Alitoka kwenye familia bora. Lakini haya yaliyeyuka mithili ya pande la barafu kwenye pipa la maji yachemkayo.
Mapenzi. Kijana Jimmy anayaharibu matarajio ya Tekla katika maisha yake.
Kila kitu kinamharibiakia Tekla.
Hata mambo yanapomnyookea tena, kivuli cha makosa yake ya nyuma hakimwachi akayafurahia maisha.
Kila kitu kilipopotea kutoka mikononi mwake, anaweza kufanya jambo moja tu.
Kulipa kisasi.


WAKATI FULANI

JANE Siame, anachaguliwa kuwa Waziri Mkuu wa kwanza mwanamke Tanzania. Wanawake wote wananyanyua mikono yao kwa ushindi huo. Wanalazimika kuishusha huku vichwa vyao vikiwa chini kashfa kubwa inapoibuka kuhusiana na historia ya mwenendo wa maisha ya Jane.
Kamati Maalumu ya Maadili ikihusishwa wananchi na viongozi wa dini na siasa wanaoheshimika zaidi inaundwa kumhoji mheshimiwa Waziri Mkuu kabla hajaondolewa wadhifa wake. Kamati hiyo inakutana na mengi yanayoifanya ifikirie mara mbili. Nchi nzima inakuwa katika mkanganyiko mkubwa. Je, aondolewe wadhifa wake na kudharauliwa, ama apongezwe?


Kaa mkao wa kula ukisubiri ujio wa riwaya hizo zenye kukusisimua, na kukufanya usichoke kufungua kurasa kiasi kwamba ufikapo ukurasa wa mwisho, unatamani simulizi iendelee.
http://fadhymtanga.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni