● Rangi maridadi
inayong’aa juu ya mabawa ya vipepeo fulani hubadilika ikitegemea upande
ambao unatazama. Rangi ya bawa la vipepeo wa aina fulani ni laini na
inang’aa sana hivi kwamba inaweza kuonekana umbali wa mita 805. Ni nini
kinachofanya bawa la kipepeo liwe la kipekee hivyo?
Fikiria hili: Mistari midogo iliyobonyea kwenye sehemu ya juu ya mabawa ya kipepeo anayeitwa green swallowtail (Papilio blumei)
hurudisha nuru kwa njia kadhaa. Kwa mfano, sehemu ya katikati ya eneo
lililobonyea hurudisha nuru yenye rangi ya manjano na kijani, huku
sehemu za nje zikirudisha nuru yenye rangi ya bluu.
Pia, sehemu ya
katikati ya eneo lililobonyea hurudisha nuru moja kwa moja, lakini nuru
inapopiga sehemu za kando inalazimika kupitia kwenye matabaka kadhaa,
ambayo huongeza na kuzungusha mawimbi ya nuru. Mchanganyiko wa mwisho
unaotokea huwa tata sana.
Watafiti
walitumia miaka kumi kutokeza kitu kinachofanana na sehemu ya juu ya
bawa la kipepeo. Wanatumaini kwamba teknolojia hiyo itawasaidia kutokeza
noti za benki na kadi za mkopo zisizoweza kuigwa kwa urahisi na mabamba
yanayoweza kunasa nguvu za jua kwa njia nzuri zaidi.
Hata hivyo, ni
vigumu sana kuiga sehemu ya juu ya bawa la kipepeo. “Ingawa wanasayansi
wanaelewa mambo mengi sana kuhusu elimu ya nuru,” anaandika Profesa
Ullrich Steiner wa Chuo Kikuu cha Cambridge, “unamna-namna wa rangi
wenye kushangaza unaopatikana katika bawa hilo unazidi mambo yanayoweza
kutokezwa kwa kutumia teknolojia.”
Una maoni gani?
Je, sehemu ya juu ya bawa la kipepeo ilijitokeza yenyewe?
Au ilibuniwa?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni