Nyigu wa kike
ambaye hutoboa miti na kutaga mayai ndani ya misonabari, amewashangaza
sana wanasayansi kwa mbinu yake ya kutoboa miti na kuwachochea kubuni
vifaa bora zaidi vya kufanya upasuaji kwa njia salama zaidi.
Fikiria hili:
Nyigu huyo hutoboa msonobari kwa kutumia mrija ulio kama sindano na
wenye mitaimbo miwili, au “valvu” zilizoingiana, ambapo kila moja
imefunikwa kwa meno yanayoangalia nyuma. Meno ya valvu moja hushikilia
mti na hivyo kumfanya asisonge, na valvu ile nyingine husonga hatua moja
mbele.
Kisha meno ya valvu hiyo ya pili hushikilia mti tena na hivyo ile valvu ya kwanza
inasonga mbele. Katika mwendo huu wa kasi unaofanyika kwa
kurudia-rudia—ambapo valvu hizo hubadilishana kushikilia mti na kusonga
mbele—mrija huo huchimba milimita 20 hivi bila kutumia nguvu nyingi
kwenye sehemu laini ya nje ya mti bila kujipinda wala kuvunjika.
Wanasayansi
wamechochewa na mrija huo hivi kwamba wanabuni kifaa cha kufanya
upasuaji katika ubongo ambacho kitachimba kwa kutumia mbinu hiyo.
Sindano yake ya silikoni ina valvu mbili ambazo husonga mbele na nyuma,
kila moja ikiwa na meno madogo ambayo yanaweza kuingia katika sehemu za
ndani zaidi za ubongo bila kusababisha madhara makubwa. Hata hivyo,
kifaa hicho kitaweza kufanya jambo lingine.
Gazeti New Scientist
linaeleza, “Tofauti na vifaa vingine vya upasuaji visivyoweza
kujipinda, kifaa hiki kitaweza kujipinda kwa kiasi kikubwa hivi kwamba
kitapitishwa katika sehemu salama zaidi za ubongo, bila kugusa sehemu
nyeti wakati wa upasuaji.” Kifaa hicho pia kitafanya iwe rahisi kufikia
sehemu ambazo huwa ni vigumu kufikia bila kukata viungo ambavyo havina
tatizo.
Zaidi INGIA HAPA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni