Nyota za Neutron ni viini vizito zinavyobakia baada ya nyota kubwa kufa na kulipuka huko
angani. Matabaka ya nje ya nyota hurushwa mbali katika milipuko hiyo,
lakini maada katika viini vya nyota hizo husambaratika vyenyewe na
hutengeneza burungutu kubwa la maada. Kinachobakia baada ya hapo ni kitu
kilichokandamizwa chenye mkandamizo mkubwa katika ulimwengu wote nje
shimo jeusi: nyota ya neutron!
Picha
hii mpya iliyopigwa huko angani inaonyesha kundi la nyota lijulikanalo
kama ‘globular cluster’. Ambayo ni baadhi tu ya vitu ambavyo ni vya kale
sana huko angani— umri wake unakaribiana kabisa na umri wa ulimwengu
wenyewe! Hii inamaanisha kuwa nyota nyingi zilizopo ndani yake
zimeshakufa. Na zile kubwa zaidi zimekwishalipuka na kuacha nyota za
neuton.
Kwa kutumia nyota ya neutron katika kundi
hili pamoja na nyingine nyingi, wanaastronomia wameweza kutambua
uhusiano kati ya uzito wa nyota (kiasi cha maada inayobeba) na ukubwa
wake.
Taarifa mpya zinaonyesha kuwa nyota ya
neutron ya kawaida, yenye uzito wa mara moja na nusu ya Jua letu inaweza
kuwa na kipenyo cha kilometa 12. Urefu ambao ni karibu sawa na eneo la
mji mdogo! Likiwa na maada zote hizi zimekandamizwa katika sehemu hiyo
ndogo. Hivyo basi nyota za neutron ni nzito mno. Nguvu ya mkandamizo
(Presha) katika kiini chake ni zaidi ya trilioni kumi kuliko nguvu ya
mkandamizo inayohitajika kutengenezea almasi ndani ya Dunia.
Dokezo: Nyota za neutron
zimepakiwa na kukandamizwa sana hivyo kuzifanya ziwe na duara pete.
Mlima unaoweza kutokea katika uso wake unaweza kuwa na urefu wa milimita
5 tu!
Kwa Taarifa Zaidi
Swahili Space Scoop hii imetokana na Taarifa kwa vyombo vya habari ya Chandra
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni