Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumatatu, Machi 10, 2014

NAFASI YA MUZIKI ULIOPENDWA KATIKA FASIHI YA KISWAHILI


Inkisiri

Nyimbo, kama tanzu ya fasihi yeyote ile zina majukumu mbalimbali ambayo hutekeleza katika jamii. Lengo kuu la fasihi
ni lile la kuielimisha na hata kuiburudisha jamii. Ndivyo ilivyo katika nyimbo kwa sababu kupitia kwazo wanajamii huburudika
na kuelimishwa. Ni kwa sababu hiyo ndipo makala hii inalenga kuangalia nafasi ya nyimbo zinazopendwa katika fasihi ya
Kiswahili. Huu ni utanzu ambao huwafikia watu wengi katika jamii. Kutokana na kutumia lugha ya Kiswahili, utanzu huu
unaweza kueleweka na Wakenya wengi. Nchini Kenya, vyombo vya habari vimeipa fasihi hii nafasi kubwa sana na hivyo basi
kuipanua hadhira yake. Hii ni kutokana na sababu kuwa fasihi hii inathaminiwa sana na wengi na ipewe nafasi kubwa katika
vyombo vya habari hasa katika redio kwa muda mrefu. Ni kutokana na sababu hii ndipo tunajaribu kuonesha nafasi yake katika
fasihi ya Kiswahili.

Makala

Mahusiano ya kijamii hujengwa kutokana na historia, mazingira na shughuli za watu za kila siku na imani yao pia. Watu wa
jamii moja mara nyingi husikilizana kwa lugha, mila na desturi. Misingi hiyo ya utamadununi na utamaduni wenyewe huwa
ni vigezo maalum vya kumfanya mtu aitambue nafasi yake katika jamii na vile vile kutambua wajibu wake na majukumu yake,
Mazrui (1986).

Tanzu mojawapo inayodhihirisha utamaduni wa jamii ni muziki wake. Wasanii hawa, hasa waimbaji wanaoimba kwa
lugha ya Kiswahili nyimbo ambazo twaweza kuziita nyimbo-pendwa wamechukua nafasi kubwa katika kukuza lugha hii,
utamaduni na mawasiliano...

Muziki umekuwa chombo ambacho kimewavutia wanadamu. Jambo hili limewafanya watu wa matabaka mbalimbali wakiwemo
wanafalsafa na watu wa kawaida kujru:ibu kuelewa muziki - lakini hakuna fasili ambayo imeweza kueleza muziki ni nini hasa:
Uasili wake haujulikani, kama anavyodai Schumann katika kofia (1994) kuwa:

"Sayansi hutumia hisibati na umantiki, ushaiii nao hutumia maneno teule..  muziki ni yatima ambaye babake na mamake
hawajulikani kamwe. Hata hivyo, ni huu utata wa uasili wake ambao umefanya muziki uonekane kuwa kitu bora zaidi katika
jamii" (Tafsiii yangu).

Katika kutumia nyimbo, waimbaji hawa wameweza kuhifadhi historia na utamaduni wa jamii zao. Hata hivyo, hivi sasa utaona
kuwa maendeleo ya kisayansi na teknolojia yameanza kuiingiza jamii nyingi katika fasihi ya televisheni na video na hivyo kuonekana kama kwamba jambo hili linafifisha stru:ehe inayopitikana katika nyimbo (Mlacha, 1998}.

Dhamila kuu ya makala haya ni kuangalia nafasi ya nyimbo-pendwa katika fasihi ya Kiswahili. Mabadiliko katika jamii yamesababisha mabadiliko katika nyimbo na hivyo basi nyimbo zimekuwa na maudhui na fani tofauti kutegemea namnajamii ilivyobadilika.

Uchunguzi uliofanywa juu ya nyimbo umeonyesha kuwa nyimbo ni kipengele muhimu sana katika jamii zote ulimwenguni.
Nyimbo ni utanzu uliothaminiwa sana, na zilitawala katika mifumo yote yajamii, Brandel (1959). Akuno (1999) anasema kuwa muziki ni zaidi ya sauti tu ambazo huimbwa na kuchezwa. Muziki sio wazo la dhana fulani bali ni tajriba, ni tukio ambalo huwasilisha mambo mbalimbali yenye umuhimu katika jamii husika Akuno anaona nyimbo/muziki ukiwa na uamali wa kiujozi: Kwanza ni kama kiburudisho, muziki huendeleza uhusiano wa mtu binafsi, humstarehesha na kumwezesha mtu huyu kuwasilisha hisia zake Na kama tambiko, muziki huendeleza uhusiano wa kimazingiia - kwa kuwahusisha wanadamu na viumbe vingine vinavyopatikana katika mazingiia hayo.

Katika kuangalia upande wa kijamii, Akuno anaona muziki kama chombo ambacho hutumiwa kuelezea histmia ya jamii,
hutumiwa kupasha 11iumbe maalum kwa wanajru:nii hasa kutoka kizazi kimoja hadi kingine na hutumiwa hasa kuelezea
histmia, imani, itikadi na kaida zajamii. Nyimbo ni zao la mazingiia ya jamii. Zinaweza kufananishwa na mtoto ambaye
hufinyangwa na mambo mengi katika historia ya jamii yake. Hii inamaanisha kwamba muziki hauibuki katika ombwe tupu na hauwezi vilevile kujiundia mazingira yazo yenyewe. Mabadiliko na maendeleo ya muziki yamekuwa yakifuatana na historia ya watu wenyewe. Nyimbo huathiriwa sana na mambo yanayotendeka ulimwenguni.

Umuhimu wa muziki unadhihirika katika matumizi ya nyimbo katika wakati maalum kama njia mojawapo ya kuanzisha mabadiliko katika tabia za jamii au mtu binafsi, (McAI!ester 1971). Muziki umetumika kama njia mojawapo ya kujifundisha utamaduni na aghalabu hutumiwa katika kuelezea mtu mazingira yake na jinsi anavyoweza kuyatumia na kuyatunza vilivyo Nyirnbo vi1evile
zimekuja kuchukuliwa kama chanzo cha elimu na jinsi ya kujieleza katika jamii na hasa katika sana ya ma.zllngumzo Nyimbo
humfanya mtu kumbukumbu ya vitu au tukio kwa urahisi na kumbukumbu hiyo huweza kudumu kwa muda mrefu sana.
Kwa mfano, masomo shuleni hufanikishwa kupitia nyimbo

Muziki ulioimbwa kwa Kiswahili ni sehemu muhimu sana zirrazojenga utamaduni wa Wakenya. Kwa Wakenya wengi muziki ni neno linaloeleweka kwa wananchi wengi kwa sababu watu hao huwa na upenzi wa muziki Kuhusu muziki ni nini, tunaweza kusema ni taaluma maalum ya sauti inayochanganya kwa usahihi sanaa na sayansi. Muziki ni sanaa katika matokeo na utendaji wake
na ni sayansi katika maandalizi yake na utendaji, (Sekella, 1995).

Wanamuziki wa Kenya wamegawanyika katika makundi mbalimbali:- Watendaji wa muziki wa bendi, kwaya, taarabu na watendaji wa muziki wa kiasili. Karibu kila kundi hutumia lugha ya Kiswahili linapokuwa na ujumbe maalum kwa wananchi. Muziki wa
kiasili nao huweza kugeuzwa maneno ya lugha ya kiasili ya wimbo unaohusika hadi katika lugha ya kiswahili ili ujumbe wake
uweze kueleweka kwa wasikilizaji wengi.

Kenya irnepitia hatua mbalirnbali ya mabadiliko. Hatua hizi zimeathiri nyimbo kwa njia tofauti tofauti. Tunacho kipindi kabla ya wageni au wakoloni. Huu ndio wakati ambapo nyimbo zilizoimbwa zilikuwa nyimbo za kikabila Wanajamii, kulingana na
lugha zao za mama walibuni nyimbo zao. Kipindi cha pili ni cha maajilio ya wazungu. Hiki ni kipindi ambacho mwafrika alidhalilishwa na mzungu. Hii ilikuwa dhuluma ambayo ilivuka mipaka ya uchumi na siasa ikafikia hadi kwenye hali ya kumteka mwafrika kimawazo asiweze kuonea nyimbo zake fahari. Hapa ndipo mwafrika alipojiona kwamba yeye hakuwa na uwezo wa kufanya chochote na hata nyimbo zake hazikuwa na maana yoyote. Kipindi hiki kilishuhudia nyimbo za kutoka nje na ambazo zilianza kuonewa fahari. Watu walianza kwenda katika majumba ya starehe ili kucheza densi. Lugha iliyopendelewa sana ilikuwa ni Kingereza. 

Hata hivyo nyimbo hizi hazikuwafikia watu wengi kwa sababu idadi ya watu waliokifahamu Kingereza ilikuwa ndogo nmo.
Hata hivyo, waimbaji wachache waliendelea kutumia lugha ya Kiswahili katika muziki wao. Waimbaji kama vile Fadhili William,
Daudi Kabaka, John Mwale na wengineo ni baadhi ya wanamuziki ambao bado wanasifika sana katika kuimba kwa Kiswahili..
Hawa ndio watu waliosaidia kufanikisha lugha ya Kiswahili katika miaka ya sitini, na nyimbo zao zikajulikana kama nyimbo
"zilizopendwa" hadi wa sasa. Hivi sasa kuna bendi nyingi zinazoimba kwa Kiswahili, hizi ni pamoja na "Them Mushrooms", Princess Jully", Munishi na nyingine nyingi ambazo zinapendwa na idadi kubwa ya watu. Wananchi, kwa bahati nzuri hupendelea muziki wenye ujumbe na hasa ujumbe ulio katika lugha wanayoielewa ya Kiswahili. Na nyingi ya bendi hizi hutimiza
wajibu huu.

Sanaa ya uimbaji inaonesha uwezo wa binadamu wa kusimulia au kupasha tajriba yake na ya jamii ya kila siku na kujaribu
kuleta maana katika maisha ya kila siku. Mambo haya hufanyika kwa njia ya ukawaida mno - kupitia kwenye nyimbo zilizopendwa. Nyimbo hizi huweza hata kuundwa upya na wananchi wenyewe kwa sababu mbalimbali.

Kama asemavyo Campbell (1976) nyimbo zimeundwa kru:na sanaa nyingine ili kunasa makini yetu. Sanaa hii basi ina ule ukale, uleo na hata ukesho. Kupitia nyimbo zilizopendwa, wanamuziki wa Kiswahili wanaweza kuangalia 'usasa' au dunia ya leo hapo
baadaye, usasa huu utakuwa kama ukale utakao tuelekeza kufahru:nu histmia yetu ya wakati huo. 'Usasa' huu unaweza
kutusaidia katika kutab:iii ukesho na kujua nru:nna ya kukabiliana na ulimwengu ujao.

Muziki umetumiwa katika kupinga ukandamizwaji na uonevu katika jamii. Hapa ni pale ru:nbapo mwanamuziki anaangalia mambo ya kisiasa. Jambo hili lilidhihirika wakati wa ukoloni ambapo mwafrika alitumia nyimbo kama silaha kupigania uhuru. Muziki ulitumiwa kuwahimiza watu. wapinge tamaduni za wakandamizaji. Waafrika walifanya hivi kwa kuchukua nyimbo za kisiasa na kuzipa mahadhi ya kidini ambapo kwa hakika maana ilikuwa tofauti na ile ya kidini Hivi sasa wanamuziki wa nyimbo zilizopendwa wanaimba nyimbo zinazowaelimisha na kuwahamasisha watu ili watekeleze kwa ufanisi sera na maagizo mbalimbali ya chama kinachotawala na serikali kwa jumla. 

Nyimbo nyingi zinazosikika redioni zinahusu kuwahimiza watu kuwa na uwajibikaji, kilimo cha kisasa, uzazi wa mpango, vita dhidi ya Ukimwi, kuchagua viongozi bora na kufanya kazi kwa bidii. Lugha ya Kiswahili imetumika kuimba nyimbo zenye ushauri kuhusu maisha, mapenzi, tabia nzuri na mbaya, ukulima bora na kadhalika Muziki hasa muziki wa 'zilizopendwa' ni sanaa ambayo huwafikia watu wengi kupitia vyombo vya habari hasa redio na hata
televisheni. Kwa hivyo hii ni sanaa ambayo haiwezi kupuuzwa kutokana na majukumu mbalimbali inayotekeleza. Vyombo
vya habari vimetenga masaa kadhaa ya kuwaburudisha watu kwa kutumia nyimbo mbalimbali. Balisidya (1987) anakubali
kuwa sanaa hii ni sehernu mojawapo ya fasihi ya Kiswahili na inahitaji kufanyiwa uchunguza zaidi, kwa jinsi ambavyo watu
wengi wanaweza kuipata.

Nyimbo za kisasa zinaweza kutupa mwangaza kuhusu maisha ya watu duniani.. Finnegan (1970), anasema kuwa nyimbo-pendwa zina majukumu mbalimbali ya kutekeleza hasa katika kuangalia mitazamo ya jamii kiulimwengu, na nyimbo hizi
hutekeleza majukumu haya kama zilivyo nyimbo za kijadi Mtazamo huu umeungwa rnkono na watu kama vile Kabira na
Mutahi (1988), Agovi (1989), na wengine wengi ambao wanaona muziki kuwa utanzu teule inayodhihirika katika jamii hii
inayobadilika. Nyimbo pendwa zimechukuliwa na wasomi wengi kuwa kama muingiliano wa masimulizi jadi na ukweli wa
maisha ya hivi sasa, Nyimbo hizi hushughulikia mambo kama vile ukandamizwaji, kutamauka maishani, unyimwaji wa haki
na umaskini/ubinafsi. Mambo haya ni mambo ya kisasa na huathili wanajamii kwa njia mbalimbali.

Waimbaji wa nyimbo zilizopendwa hushughulikia nyanja tofauti za maisha ya jarnii kama vile dini, uchumi na siasa. Kwa
mfano, wao wanashughulikia ndoa na mapenzi kwa kuonesha mahusiano ya jamii na migongano ya kimawazo baina
ya wazee na vijana au baina ya rnke na mume. Katika nyakati hizi za mabadiliko katika uchumi na siasa waimbaji wamekuwa
wakitunga nyimbo kwa kutuchorea picha ya jinsi mambo yalivyo. Wamekuwa katika mstari wa mbele katika kuwatahadharisha wanajamii kuhusu ugonjwa wa Ukimwi

Muziki uliopendwa katika Kiswahili ni sanaa isiyo kuwa na mipaka ya ukabila. Ni sanaa ambayo huwaunganisha watu wa
makabila mbalimbali kwa kutumia lugha inayoeleweka na kuzungumzia tajriba sawa wanazozifahamu. Nyimbo hizi pia
zimetumika kuimulika jamii kwa kuonesha maendeleo yaliyopatikana katika nyanja mbalimbali Anapoikosoa jamii, mwimbaji huwa anachukuwa jukumu la kuhakiki jamii na hata kuielekeza. Nyimbo hizi pia zinatumiwa kuwazindua watu waweze kufahamu haki zao hasa pale wanaponyimwa, zinatumiwa kama ajenti wa ukombozi.

Katika nyimbo hizi, pia kuna ufasihi hasa upande wa lugha. Sifa moja ambayo hubanisha nyimbo ni matmnizi yake ya lugha hasa zile tamathali za usemi kama vile tashbihi, methali, semi, jazanda taashira na majina ya majazi. Tamathali hizo zinazotumiwa na
nyimbo huwa ama zimebuniwa katika jamii ya mwimbaji au zimebuniwa na mwimbaji mwenyewe lakini akazingatia kanuni za
uundaji wake. Hii inafanya tanzu hii iweze kuchunguzwa kwa makini kiusomi kwa kuchanganua ufani wake kupitia lugha iliyotumika. Hata hivyo, waimbaji wa nyimbo-pendwa wamekumbana na vizingiti vingi. Kutokana na sababu kuwa wao ni wahakiki wa jamii, baadhi ya nyimbo zao zimepigwa marufuku, (mwangi 1992) na hivyo basi haziwafikii watu wengi waliolengwa na haziwezi kutumiwa kama njia ya kuwazindua watu. Katika kule kuihaki jamii, wao-hulenga kuikosa, lakini mara nyingi wao huwa hawaafikiani na viongozi kuhusiana na maongozi yao.

Hitimisho

Nyimbo zinazoimbwa kwa lugha ya Kiswahili huwafikia watu wengi kutokana na sababu kuwa lugha ya Kiswahili ni lugha ya
walio wengi. Nyimbo zilizopendwa zitaendelea kukua kufuatana na mabadiliko ya kihistoria na kifani ambayo yanasababishwa
na watu wengi. Hivyo basi, nyimbo hizi hazina budi kuchukuliwa kama sehemu moja ya Fasihi ya Kiswahili kwa kuangalia mchango wake kimaudhui na kifani. Na zinahitaji kusambazwa ili ziwafikie wanajamii wote. Hii ina maanisha kuwa vyombo
vya habari vina majukumu ya kutekeleza katika kuhakikisha kwamba watu wengi wameweza kuzipata nyimbo hizi. Kwa
upande wa fasihi, haya ni mafanikio makubwa hasa kwa sababu tabia ya kupenda kusoma haijakomaa kwa wengi.

Vyombo vya habari vinatumika kusambaza fasihi hii kwa mamilioni ya watu. Hii ni kutokana na sababu kuwa kundi moja tu la waimbaji linaweza kufundisha idadi kubwa ya watu kwa wakati mmoja kupitia nyimbo zao



Mwandishi: PAMELA M. Y NGUGI


Jumapili, Machi 02, 2014

Muziki ni wa maana kwako kadiri gani?


□ Si wa lazima.
□ Siwezi kuishi bila muziki.

Wewe husikiliza muziki wakati gani?

□ Ninaposafiri
□ Ninaposoma
□ Wakati wote

Ni muziki wa aina gani unaopenda sana?

YAELEKEA sote tuliumbwa tukiwa na uwezo wa kufurahia muziki. Na kwa vijana wengi, muziki ni wa lazima. “Siwezi kuishi bila muziki,” anasema Amber mwenye umri wa miaka 21. “Mimi husikiliza muziki karibu kila wakati, ninapofanya usafi, ninapopika, ninapotembea, au hata ninaposoma.”

Hata muziki wenye mdundo wa kawaida tu unaweza kupenya ndani sana na kuchochea hisia zetu. Kama vile “neno linalosemwa wakati unaofaa ni jema kama nini!” wimbo unaochezwa wakati unaofaa unaweza kuburudisha sana! (Methali 15:23) “Nyakati nyingine unahisi kwamba hakuna mtu anayekuelewa,” anasema Jessica mwenye umri wa miaka 16. “Lakini ninaposikiliza nyimbo za bendi fulani ninayopenda, najihisi kwamba siko peke yangu.”

Je, Muziki Hutokeza Vita au Amani?

Ingawa unapenda muziki, huenda wazazi wako wakawa na maoni tofauti. Kijana mmoja anasema: “Baba yangu husema, ‘Zima hiyo kilele! Inaniumiza masikio!’” Ugomvi unapotokea, huenda ukaona kwamba wazazi wako wanachemka bure. “Ilikuwaje walipokuwa vijana?” anauliza msichana mmoja. “Kwani wazazi wao pia hawakufikiri kwamba muziki walioupenda ulikuwa mbaya?” Ingred mwenye umri wa miaka 16 analalamika: “Watu wazima hawapendi mabadiliko. Ingekuwa afadhali kama wangetambua kwamba kizazi chetu kinapenda muziki tofauti!”

Kuna ukweli fulani katika maneno ya Ingred. Kama ujuavyo, tangu zamani mapendezi ya vijana na ya watu wazima yametofautiana sana. Hata hivyo, haimaanishi kwamba lazima mgombane kwa sababu ya muziki kila siku. Siri ni kujaribu kutafuta maelewano kuhusu muziki. Ikiwa wazazi wako wanaiheshimu Biblia, basi kuna matumaini. Kwa nini? Kwa kuwa Neno la Mungu linaweza kukusaidia wewe na wazazi wako kutambua mambo yanayofaa na yanayotegemea mapendezi ya kibinafsi. Ili kufanya hivyo, unahitaji kuchanganua mambo mawili makuu: (1) ujumbe ulio katika muziki unaosikiliza na (2) muda unaotumia kusikiliza muziki. Kwanza, tufikirie swali hili . . .

Muziki Ninaopenda Una Ujumbe Gani?

Muziki ni kama chakula. Unahitaji aina inayofaa kwa kiasi kinachofaa. Aina mbaya, hata iwe ni kiasi gani, ni hatari. Kwa kusikitisha, katika ulimwengu wa muziki, aina mbaya ya muziki ndiyo inayovutia zaidi. “Kwa nini miziki yote yenye midundo mitamu huwa na maneno machafu hivyo?” alalamika kijana anayeitwa Steve.

Ikiwa unapendezwa na mdundo, kuna haja ya kuzingatia ujumbe uliopo? Ili kujibu swali hilo, jiulize: ‘Ikiwa mtu fulani angetaka ninywe sumu, angetumia mbinu gani ili kunifanya niinywe? Je, angeichovya katika kitu kichungu au katika sukari?’ Yule mwanamume mwaminifu, Ayubu, aliuliza: “Je, sikio halipimi maneno kama kaakaa linavyoonja chakula?” (Ayubu 12:11) Kwa hiyo, badala ya kusikiliza muziki kwa sababu tu unapenda mdundo wake—utamu wake wa kijuujuu—‘pima maneno yake’ kwa kufikiria kichwa cha muziki na maneno yaliyomo. Kwa nini? Kwa sababu maneno yaliyo katika muziki yataathiri kufikiri kwako na mtazamo wako.

Inasikitisha kwamba miziki inayopendwa sana leo ina maneno yanayosifu ngono, jeuri, na matumizi ya dawa za kulevya. Ikiwa huoni kwamba kusikiliza maneno hayo kunaweza kukuathiri, basi “sumu” yake imeanza kukuingia.

Usifuate Upepo

Vijana wenzako wanaweza kukushinikiza usikilize muziki usiofaa. Pia, soko la muziki lina uvutano mkubwa. Kukiwa na redio, Intaneti, na televisheni, muziki umekuwa biashara kubwa. Wataalamu wa mauzo wameajiriwa ili kukuchochea upendezwe na muziki wa aina fulani.

Lakini unapoacha marafiki au vyombo vya habari vikuamulie muziki utakaosikiliza, unapoteza uhuru wako wa kuchagua. Unakuwa mtumwa, mtu asiyetumia akili yake. (Waroma 6:16) Biblia inakuhimiza uepuke uvutano wa ulimwengu katika mambo kama hayo. (Waroma 12:2) Hivyo, unapaswa kuzoeza ‘nguvu zako za ufahamu ili zitofautishe yaliyo sawa na yaliyo makosa pia.’ (Waebrania 5:14) Unaweza kutumia jinsi gani nguvu zako za ufahamu unapochagua muziki? Fikiria mapendekezo yanayofuata:

Chunguza picha na maandishi yaliyo kwenye kasha. Mara nyingi unaweza kujua yaliyomo katika kanda kwa kutazama kasha. Unapoona picha zinazoonyesha jeuri, ngono, au kuwasiliana na pepo, tahadhari. Inaelekea muziki wenyewe pia haufai.

Soma maneno ya wimbo. Ni nini kinachosemwa? Je, kweli ungependa kusikiliza maneno hayo tena na tena? Je, ujumbe wa wimbo huo unapatana na sifa na kanuni za Kikristo?—Waefeso 5:3-5.

Chunguza athari zake. Kijana anayeitwa Philip anasema: “Niligundua kwamba muziki na maneno niliyosikiliza yalinifanya nishuke moyo.” Kwa kweli, muziki unaweza kuathiri watu kwa njia mbalimbali. Lakini muziki unaosikiliza unaamsha hisia gani? Jiulize: ‘Je, mimi huwa na mawazo yasiyofaa baada ya kusikiliza muziki au maneno ya muziki fulani? Je, nimeanza kutumia lugha ya mitaani inayotumiwa katika muziki?’—1 Wakorintho 15:33.

Wafikirie wengine. Wazazi wako wana maoni gani kuhusu muziki unaosikiliza? Waulize maoni yao. Pia, fikiria maoni ya Wakristo wenzako. Je, wengine wanaweza kukwazwa? Kubadili mwenendo wako ili usiumize hisia za wengine kunaonyesha kwamba wewe ni mkomavu.—Waroma 15:1, 2.

Kujiuliza maswali yaliyo hapo juu kutakusaidia kuchagua muziki ambao utakuchangamsha moyo pasipo kuangamiza hali yako ya kiroho. Hata hivyo, kuna jambo lingine la kufikiria.

Ni Wakati Gani Muziki Unapita Kiasi?

Muziki unaofaa kama vile chakula kizuri unaweza kuwa wenye faida. Hata hivyo, methali yenye hekima inaonya: “Je, umepata asali? Kula kiasi cha kukutosha, ili usiile kupita kiasi kisha uitapike.” (Methali 25:16) Asali ni dawa. Lakini kitu chochote hata kiwe kizuri kinapopita kiasi kinaweza kukudhuru. Kwa hiyo, vitu vizuri vinapaswa kufurahiwa kwa kiasi.

Hata hivyo, maisha ya vijana fulani hutawaliwa na muziki. Kwa mfano, Jessica aliyetajwa mapema, anakiri: “Mimi husikiliza muziki kila wakati—hata ninapojifunza Biblia. Mimi huwaambia wazazi wangu kwamba muziki hunisaidia kukaza fikira. Lakini hawaniamini.” Je, umewahi kuwa na maoni kama ya Jessica?
Unaweza kujua jinsi gani ikiwa unapita kiasi katika kusikiliza muziki? Jiulize maswali yanayofuata:

Kila siku mimi hutumia saa ngapi kusikiliza muziki? ․․․․․
Ninatumia pesa ngapi kwa muziki kila mwezi? ․․․․․

Je, muziki unaharibu uhusiano kati yangu na wengine katika familia? Ikiwa ndivyo, andika hapa chini jinsi unavyoweza kurekebisha hali hiyo. ․․․․․

Badili Mazoea Yako

Ikiwa muziki unachukua wakati mwingi kupita kiasi, unapaswa kujiwekea mipaka na kuwa na usawaziko kuhusiana na mazoea yako ya kusikiliza muziki. Kwa mfano, huenda ukahitaji kuacha mazoea ya kuweka masikioni vidude vya kusikilizia muziki siku nzima au mazoea ya kuwasha redio mara tu unapofika nyumbani.
Kwa nini usijifunze kufurahia pindi za utulivu, pasipo kelele yoyote? Kufanya hivyo kutakusaidia katika masomo yako. 

Steve aliyetajwa mapema anasema: “Unaweza kujifunza mambo mengi zaidi ikiwa muziki umezimwa.” Jaribu kusoma bila muziki, na uone iwapo utakazia fikira zaidi mambo unayojifunza.
Pia, utahitaji kupanga wakati wa kusoma na kujifunza Biblia na vitabu vinavyotegemea Biblia. Nyakati nyingine, Yesu Kristo alitafuta mahali patulivu ili kusali na kutafakari. (Marko 1:35) Je, wewe pia hujifunza katika mazingira matulivu, yasiyo na kelele? Ikiwa hufanyi hivyo, huenda unazuia ukuzi wako wa kiroho.

Fanya Uchaguzi Unaofaa

Kwa kweli, muziki ni zawadi kutoka kwa Mungu, lakini unapaswa kujihadhari usiitumie vibaya. Usiwe kama msichana anayeitwa Marlene, anayesema: “Nina muziki ambao ninajua ninapaswa kuutupilia mbali. Lakini ni mtamu wee.” Fikiria madhara anayosababisha katika akili na moyo wake kwa kusikiliza muziki usiofaa! Usinaswe na mtego huo. Usikubali muziki ukupotoshe au utawale maisha yako. Chagua muziki unaopatana na viwango vya Kikristo. Mwombe Mungu akusaidie. Tafuta marafiki walio na maoni kama yako.

Muziki unaweza kukustarehesha na kukuburudisha. Unaweza kukuondolea hisia za upweke. Hata hivyo, hautatui matatizo yako. Isitoshe, nyimbo haziwezi kulinganishwa na marafiki wa kweli. Kwa hiyo, usiruhusu muziki uwe jambo kuu maishani mwako. Furahia muziki, lakini usikubali ukutawale.


Unahitaji kujiburudisha mara kwa mara. Kanuni za Biblia zinaweza kukusaidia jinsi gani unufaike kutokana na pindi hizo zenye kufurahisha?

MAANDIKO MUHIMU

Je, sikio halipimi maneno kama kaakaa linavyoonja chakula?Ayubu 12:11.

PENDEKEZO

Ikiwa unataka wazazi wako waelewe ni kwa nini unapenda muziki au bendi fulani, kwanza jaribu kupendezwa na baadhi ya miziki wanayofurahia.

JE, WAJUA . . .?

Ikiwa hupendi wazazi wako wasikilize muziki unaopenda sana, basi huenda muziki unaosikiliza una kasoro.

HATUA ZA KUCHUKUA!

Ninaweza kuwa na usawaziko kuelekea muziki niki ․․․․․
Vijana wenzangu wakinishurutisha nisikilize muziki usiofaa, nitawaambia ․․․․․
Mambo ambayo ningependa kuuliza mzazi (wazazi) wangu kuhusu habari hii ni ․․․․․

UNA MAONI GANI?

Kwa nini uchaguzi wako wa muziki ni wa maana sana?
Unaweza kuamua jinsi gani ikiwa wimbo fulani unafaa au haufai?
Unaweza kufanya nini ili ujifunze kufurahia miziki ya aina nyingine?

‘‘Wakati mwingine mimi hujikuta nikisikiliza muziki usiofaa. Nauzima bila kukawia. Nisipofanya hivyo mara moja, nitaanza kutafuta visababu vya kuusikiliza.’’—Cameron

Jifunze Kufurahia Miziki ya Aina Nyingine

  Je, unapenda aina nyingi zaidi za chakula leo kuliko ulipokuwa na umri wa miaka mitano? Ikiwa ndivyo, ni kwa sababu umejizoeza kufurahia ladha ya vyakula vipya. Ndivyo ilivyo na muziki. Usisikilize muziki wa aina moja tu. Jifunze kupendezwa na miziki ya aina nyingine.

  Njia moja ya kufanya hivyo ni kujifunza kupiga ala fulani ya muziki. Kufanya hivyo kunaweza kukuchangamsha na kukuridhisha na pia kutakufanya upendezwe na aina nyingine ya muziki mbali na ile inayopigiwa debe na wafanyabiashara. Utapata wapi wakati wa kujifunza? Unaweza kupunguza wakati unaotumia kutazama televisheni au kucheza michezo ya kompyuta. Ona yale ambayo vijana hawa wanasema.

“Kupiga ala ya muziki ni raha na kunaweza kuwa njia bora ya kuonyesha hisia zako. Kujifunza kupiga nyimbo mpya kumenisaidia kupenda aina mbalimbali za muziki.”—Brian, mwenye umri wa 18, ambaye hupiga gitaa, ngoma, na piano.

“Unahitaji kufanya mazoezi ikiwa unataka kujifunza kupiga vizuri chombo fulani cha muziki. Na mazoezi hayafurahishi sikuzote. Lakini kuwa stadi wa kupiga muziki fulani ni jambo lenye kufurahisha na kuridhisha kwelikweli.”—Jade, mwenye umri wa miaka 13, ambaye hupiga fidla.

“Ninapokuwa nimechoka au kushuka moyo, kupiga gitaa hunisaidia kustarehe. Kutunga muziki mzuri na wenye kutuliza na kuburudisha ni jambo lisilo na kifani.”—Vanessa, mwenye umri wa miaka 20, hupiga gitaa, piano, na zumari.

“Nilikuwa nikijiambia, ‘Sitawahi kuwa na ustadi kama fulani wa fulani.’ Lakini niliendelea kufanya mazoezi, na sasa ninapata uradhi ninapopiga wimbo fulani vizuri. Sasa, nawavulia kofia wanamuziki wengine stadi.”—Jacob, mwenye umri wa miaka 20, hupiga gitaa.

Muziki ni kama chakula. Unahitaji aina inayofaa kwa kiasi kinachofaa. Aina mbaya, hata iwe ni kiasi gani, ni hatari

Jumamosi, Machi 01, 2014

Wanao penda kujifunza electronics designing


Najua kuna watu wengi wanapenda kujifunza Electronics designing;wale walio choka ku-copy na ku-paste already made design;na hivyo wangependa wao wenyewe wabuni vya kwao.

Ikumbukwe kuwa vifaa vya ki-electronic vinavyotumika kutengeneza vyombo ya ki-electronic kama vile Transistors,capacitors,resisto rs,diodes etc.vinaweza vikaunda kitu chochote unacho kitaka Kutegemeana na maamuzi yako,mfano unaweza kutumia vifaa hivyo kuunda TV,Radio,King’amuzi,Simu,Compu ter,.n.k.

Mfano computer imetengenezwa na vifaa hivyo hivyo,na Radio imetengenezwa na vifaa hivyo hivyo.Tofauti inakuja namna ambavyo vimeunganishwa kutegemeana na lengo la muundaji mwenyewe.

Ifahamike kuwa Hakuna tofauti kati ya vifaa vinavyotumika kuunda vyombo vya kidigitali au vile vya kianalogia.Vifaa kama vile Transistors,capacitors,resisto rs,diodes etc ndio msingi mkuu wa vyombo vyote vya kielectronic(digital and Analogy).Kinacho fanyika hapo is just a game of mathematical and functions exchange kutegemeana na matumizi husika.

Jua kwamba nirahisi sana kuwa fundi wa ku-repair vifaa vya kielectronic ila ni vigumu kwa wewe kuwa mbunifu wa vifaa vya kielectronic kama hujui misingi ya ufanyaji kazi wa vifaa mama vya kielectronic kama vile Transistors,capacitors,resisto rs,diodesetc.
Kamwe haiwezekani ukaamka asubuhi na kuanza ku-design project kubwa kama vile kuunda TV,King’amuzi, au computer kama hukuwahi kuanza katika project ndogo.

Umeme unasheria na kanuni zake ni lazima uzifahamu na kuzizingatia katika maisha yako yote katika dunia ya kielectronic.

NANI ANAWEZA KUWA MBUNIFU WA VIFAA VYA KIELECTRONICS
1.Mtu yeyote,kitu cha msingi ajue nguzo kuu za hesabu kama vile kujumlisha,kutoa,kugawanya,kuz idisha n.k

2.Awe mbunifu ajenge mawazo tofauti tofauti juu ya vitu tofauti tofauti na atafute ufumbuzi kupitia taaluma yake ya kielectronics.

3.Asiwe anakata tama mapema.

4.Ubunifu wa vifaa vya umeme ni tofauti na ubunifu kama vile computer programming kwasababu when a mistake has done is PUUUUUUUUUUU!Within a second,electricity never wait to react!Hivyo basi mbunifu lazima azingatie sheria za umeme kwa usalama wake na usalama wa vifaa vyake,ili kuepuka hasara zisizo za msingi.

5.Apende electronics.

FAIDA GANI ZA KUWA MBUNIFU WA KIELECTRONICS.

1.Kujipatia ajira.Unaweza uka-design kitu ambacho jamii ikawa inakihitaji sana na ikawezekana kifaa hicho hata dukani hakuna,au kama kipo ni ghali kuliko cha kwako,hivyo utapata soko lisilo na mshindani

2.Kuunda vitu vyako mwenyewe kwa matumizi yako mwenyewe.Kama vile security systems,operating systems mbalimbali n.k.Mfano mimi kwangu nimefunga vifaa mbalimbali ambavyo nime-design mwenyewe,kiasi kwamba kama ningekuwa naingia dukani kununua it was a lot of Dollars!Forexample music system yangu nayo tumia it is about 1500 wattage,ambayo ningeingia dukani ingeni cost a lot,pia nimefunga Security systems za kila aina,because it is too cheap if you DIY!

3.Kujiongezea taaluma na maalifa zaidi.

MAFUNZO YA KIELECTONIC KWA NJIA YA MTANDAO

Nimekuwa nikitoa mafunzo kwa njia ya face to face.Ila kuna watu wengi wanapenda kujifunza ila wapo mbali na Dar au wanakosa muda wa kuingia darasani.Hivyo nimefikiria kuanzisha mafunzo ya kielectronic kwa njia ya mtandao ili niweze kumfikia kila mmoja.Kile nilicho nacho na wengine wapate.


Mafunzo nitakayo kuwa nafundisha ni ya ubunifu(Electronics designing) tu!Sita fundisha ufundi wa ku-repair kitu chochote ila nitafundisha elimu yak u-design kitu chochote!

Lengo langu ni kuibua vipaji vya wabunifu wa vifaa vya kielectronic na sio wale wanao fanya marekebisho ya vile vilivyo tengenezwa na mzungu vikaharibika.

Japo ni vigumu kufikia kiwango cha juu cha ubunifu wa vifaa vikubwa kutokana na sababu mbalimbali.Ila lengo ni kufanya vile vinavyo wezekana kubuniwa na sisi wenyewe katika mazingira yetu vifanyike.

Lengo langu jingine ni kuunda jamii ya wabunifu na sio warekebishaji tu!Ambapo kwa pamoja tunaweza tukabadilishana mawazo na kuunda vitu mbalimbali.

Mafuzo yangu nitayatoa kwa lugha ya Kiswahili kadri inavyo wezekana,ingawaje kuna baadhi ya misamiati itatolewa kwa lugha ya kiingereza kutokana na ukosefu wa misamiati ya namna hiyo katika lugha yetu ya Kiswahili.

Mafunzo yatagawanyika katika makundi matatu ambayo ni;-

a)Wasio na msingi wa umeme na electronic kabisa
b)Walio na msingi wa umeme na electronic katika kiwango cha kati
c)Walio na msingi thabiti wa umeme na electronic
Kwa wanao taka kujifunza electronic na hawajui wapo kundi gani kati ya hayo waisome sakiti hii hapa chini halafu waniambie ni sakiti ya nini na inafanyaje kazi vilevile wakitambue kila kifaa ndani ya sakiti hii mimi ntajua anakiwango kipi kutokana na majibu yake

Click image for larger version. 

Name: jjco.jpg 
Views: 0 
Size: 200.3 KB 
ID: 141489





-Kila atakayetaka kujifuza lazima anunue vifaa vifuatavyo

1:Multmeter
Name:  hh.jpg
Views: 0
Size:  3.7 KB
2; Soldiering Beat
Name:  images.jpg
Views: 0
Size:  2.8 KB
3;Soldering wire
Name:  bn.jpg
Views: 0
Size:  2.0 KB
4:Unprited circuit board

Name:  jj.jpg
Views: 0
Size:  4.7 KB
5:Kila mwanafunzi atatakiwa awe na software maalumu ya kujaribia michoro ya designing zake za kielectronics kabla ya kuziunda katika circuit board.Software hii itakusaidia kutambua makosa madogo madogo kabla hujaiunda sakiti yako katika dunia halisi.(nitatoa link ya kudownload software hii)

Kwa wale ambao wako tayari kuingia katika dunia hii nawakaribisha tuma jina lako na namba yako ya simu kwenye email efuatayo datetz18@yahoo.com.

Mafunzo yataendeshwa kupitia website maalumu ntakayo itambulisha baadae kwa watakao tuma majina ambapo mwanafunzi atakuwa na uwezo wa ku-log-in au ku-log out kwa kutumia user name na password.

Mafunzo yata base katika ubunifu wa vifaa vya analogia na kidigitali;wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya electronics mnakaribishwa!

Haitakuwa public itakuwa for only members!
Members watatakiwa kulipia fee kidogo ili mwalimu atumie muda wake pamoja nao!


Karibu!


Chanzo: http://www.jamiiforums.com/