Inkisiri
Nyimbo, kama tanzu ya fasihi
yeyote ile zina majukumu mbalimbali ambayo hutekeleza katika jamii. Lengo kuu
la fasihi
ni lile la kuielimisha na
hata kuiburudisha jamii. Ndivyo ilivyo katika nyimbo kwa sababu kupitia kwazo
wanajamii huburudika
na kuelimishwa. Ni kwa sababu
hiyo ndipo makala hii inalenga kuangalia nafasi ya nyimbo zinazopendwa katika
fasihi ya
Kiswahili. Huu ni utanzu
ambao huwafikia watu wengi katika jamii. Kutokana na kutumia lugha ya
Kiswahili, utanzu huu
unaweza kueleweka na Wakenya
wengi. Nchini Kenya, vyombo vya habari vimeipa fasihi hii nafasi kubwa sana na
hivyo basi
kuipanua hadhira yake. Hii ni
kutokana na sababu kuwa fasihi hii inathaminiwa sana na wengi na ipewe nafasi
kubwa katika
vyombo vya habari hasa katika
redio kwa muda mrefu. Ni kutokana na sababu hii ndipo tunajaribu kuonesha
nafasi yake katika
fasihi ya Kiswahili.
Makala
Mahusiano ya kijamii hujengwa
kutokana na historia, mazingira na shughuli za watu za kila siku na imani yao
pia. Watu wa
jamii moja mara nyingi
husikilizana kwa lugha, mila na desturi. Misingi hiyo ya utamadununi na
utamaduni wenyewe huwa
ni vigezo maalum vya kumfanya
mtu aitambue nafasi yake katika jamii na vile vile kutambua wajibu wake na
majukumu yake,
Mazrui (1986).
Tanzu mojawapo
inayodhihirisha utamaduni wa jamii ni muziki wake. Wasanii hawa, hasa
waimbaji wanaoimba kwa
lugha ya Kiswahili nyimbo
ambazo twaweza kuziita nyimbo-pendwa wamechukua nafasi kubwa katika kukuza
lugha hii,
utamaduni na mawasiliano...
Muziki umekuwa chombo ambacho
kimewavutia wanadamu. Jambo hili limewafanya watu wa matabaka mbalimbali
wakiwemo
wanafalsafa na watu wa
kawaida kujru:ibu kuelewa muziki - lakini hakuna fasili ambayo imeweza kueleza
muziki ni nini hasa:
Uasili wake haujulikani, kama
anavyodai Schumann katika kofia (1994) kuwa:
"Sayansi hutumia hisibati na umantiki, ushaiii nao hutumia
maneno teule.. muziki ni yatima ambaye babake na mamake
hawajulikani kamwe. Hata hivyo, ni huu utata wa uasili wake
ambao umefanya muziki uonekane kuwa kitu bora zaidi katika
jamii" (Tafsiii yangu).
Katika kutumia nyimbo,
waimbaji hawa wameweza kuhifadhi historia na utamaduni wa jamii zao. Hata
hivyo, hivi sasa utaona
kuwa maendeleo ya kisayansi
na teknolojia yameanza kuiingiza jamii nyingi katika fasihi ya televisheni na
video na hivyo kuonekana kama kwamba jambo hili linafifisha stru:ehe
inayopitikana katika nyimbo (Mlacha, 1998}.
Dhamila kuu ya makala haya ni
kuangalia nafasi ya nyimbo-pendwa katika fasihi ya Kiswahili. Mabadiliko katika
jamii yamesababisha mabadiliko katika nyimbo na hivyo basi nyimbo zimekuwa na
maudhui na fani tofauti kutegemea namnajamii ilivyobadilika.
Uchunguzi uliofanywa juu ya
nyimbo umeonyesha kuwa nyimbo ni kipengele muhimu sana katika jamii zote
ulimwenguni.
Nyimbo ni utanzu
uliothaminiwa sana, na zilitawala katika mifumo yote yajamii, Brandel (1959).
Akuno (1999) anasema kuwa muziki ni zaidi ya sauti tu ambazo huimbwa na
kuchezwa. Muziki sio wazo la dhana fulani bali ni tajriba, ni tukio ambalo
huwasilisha mambo mbalimbali yenye umuhimu katika jamii husika Akuno anaona
nyimbo/muziki ukiwa na uamali wa kiujozi: Kwanza ni kama kiburudisho, muziki
huendeleza uhusiano wa mtu binafsi, humstarehesha na kumwezesha mtu huyu
kuwasilisha hisia zake Na kama tambiko, muziki huendeleza uhusiano wa
kimazingiia - kwa kuwahusisha wanadamu na viumbe vingine vinavyopatikana katika
mazingiia hayo.
Katika kuangalia upande wa kijamii,
Akuno anaona muziki kama chombo ambacho hutumiwa kuelezea histmia ya jamii,
hutumiwa kupasha 11iumbe
maalum kwa wanajru:nii hasa kutoka kizazi kimoja hadi kingine na hutumiwa hasa
kuelezea
histmia, imani, itikadi na
kaida zajamii. Nyimbo ni zao la mazingiia ya jamii. Zinaweza kufananishwa na
mtoto ambaye
hufinyangwa na mambo mengi katika historia ya
jamii yake. Hii inamaanisha kwamba muziki hauibuki katika ombwe tupu na hauwezi
vilevile kujiundia mazingira yazo yenyewe. Mabadiliko na maendeleo ya muziki
yamekuwa yakifuatana na historia ya watu wenyewe. Nyimbo huathiriwa sana na
mambo yanayotendeka ulimwenguni.
Umuhimu wa muziki
unadhihirika katika matumizi ya nyimbo katika wakati maalum kama njia mojawapo
ya kuanzisha mabadiliko katika tabia za jamii au mtu
binafsi, (McAI!ester 1971). Muziki umetumika kama njia mojawapo ya kujifundisha
utamaduni na aghalabu hutumiwa katika
kuelezea mtu mazingira yake na jinsi anavyoweza kuyatumia na kuyatunza vilivyo
Nyirnbo vi1evile
zimekuja kuchukuliwa kama
chanzo cha elimu na jinsi ya kujieleza katika jamii na hasa katika sana ya
ma.zllngumzo Nyimbo
humfanya mtu kumbukumbu ya vitu au tukio kwa urahisi
na kumbukumbu hiyo huweza kudumu kwa muda mrefu sana.
Kwa mfano, masomo shuleni
hufanikishwa kupitia nyimbo
Muziki ulioimbwa kwa
Kiswahili ni sehemu muhimu sana zirrazojenga utamaduni wa Wakenya. Kwa Wakenya
wengi muziki ni neno linaloeleweka kwa wananchi wengi kwa sababu watu hao huwa
na upenzi wa muziki Kuhusu muziki ni nini, tunaweza kusema ni taaluma maalum ya
sauti inayochanganya kwa usahihi sanaa na sayansi. Muziki ni sanaa katika
matokeo na utendaji wake
na ni sayansi katika
maandalizi yake na utendaji, (Sekella, 1995).
Wanamuziki wa Kenya
wamegawanyika katika makundi mbalimbali:- Watendaji wa muziki wa bendi, kwaya,
taarabu na watendaji wa muziki wa kiasili. Karibu
kila kundi hutumia lugha ya Kiswahili linapokuwa na ujumbe maalum kwa wananchi.
Muziki wa
kiasili nao huweza kugeuzwa
maneno ya lugha ya kiasili ya wimbo unaohusika hadi katika lugha ya kiswahili
ili ujumbe wake
uweze kueleweka kwa
wasikilizaji wengi.
Kenya irnepitia hatua
mbalirnbali ya mabadiliko. Hatua hizi zimeathiri nyimbo kwa njia tofauti tofauti.
Tunacho kipindi kabla ya wageni au wakoloni. Huu ndio wakati ambapo nyimbo
zilizoimbwa zilikuwa nyimbo za kikabila Wanajamii, kulingana na
lugha zao za mama walibuni nyimbo zao. Kipindi cha
pili ni cha maajilio ya wazungu. Hiki ni kipindi ambacho mwafrika alidhalilishwa
na mzungu. Hii ilikuwa dhuluma ambayo ilivuka mipaka ya uchumi na siasa ikafikia
hadi kwenye hali ya kumteka mwafrika kimawazo asiweze kuonea nyimbo zake fahari.
Hapa ndipo mwafrika alipojiona kwamba yeye hakuwa na uwezo wa kufanya chochote
na hata nyimbo zake hazikuwa na maana yoyote. Kipindi hiki kilishuhudia nyimbo
za kutoka nje na ambazo zilianza kuonewa fahari. Watu walianza kwenda katika
majumba ya starehe ili kucheza densi. Lugha iliyopendelewa sana ilikuwa ni
Kingereza.
Hata hivyo nyimbo hizi hazikuwafikia watu wengi kwa sababu idadi ya
watu waliokifahamu Kingereza ilikuwa ndogo nmo.
Hata hivyo, waimbaji wachache
waliendelea kutumia lugha ya Kiswahili katika muziki wao. Waimbaji kama vile
Fadhili William,
Daudi Kabaka, John Mwale na
wengineo ni baadhi ya wanamuziki ambao bado wanasifika sana katika kuimba kwa
Kiswahili..
Hawa ndio watu waliosaidia
kufanikisha lugha ya Kiswahili katika miaka ya sitini, na nyimbo zao zikajulikana
kama nyimbo
"zilizopendwa" hadi
wa sasa. Hivi sasa kuna bendi nyingi zinazoimba kwa Kiswahili, hizi ni pamoja
na "Them Mushrooms", Princess Jully", Munishi na nyingine nyingi
ambazo zinapendwa na idadi kubwa ya watu. Wananchi, kwa bahati nzuri hupendelea
muziki wenye ujumbe na hasa ujumbe ulio katika lugha wanayoielewa ya Kiswahili.
Na nyingi ya bendi hizi hutimiza
wajibu huu.
Sanaa ya uimbaji inaonesha
uwezo wa binadamu wa kusimulia au kupasha tajriba yake na ya jamii ya kila siku
na kujaribu
kuleta maana katika maisha ya
kila siku. Mambo haya hufanyika kwa njia ya ukawaida mno - kupitia kwenye
nyimbo zilizopendwa. Nyimbo hizi huweza hata kuundwa upya na wananchi wenyewe
kwa sababu mbalimbali.
Kama asemavyo Campbell (1976)
nyimbo zimeundwa kru:na sanaa nyingine ili kunasa makini yetu. Sanaa hii basi
ina ule ukale, uleo na hata ukesho. Kupitia nyimbo zilizopendwa, wanamuziki
wa Kiswahili wanaweza kuangalia 'usasa' au dunia ya leo hapo
baadaye, usasa huu utakuwa
kama ukale utakao tuelekeza kufahru:nu histmia yetu ya wakati huo. 'Usasa' huu
unaweza
kutusaidia katika kutab:iii
ukesho na kujua nru:nna ya kukabiliana na ulimwengu ujao.
Muziki umetumiwa katika kupinga ukandamizwaji na
uonevu katika jamii. Hapa ni pale ru:nbapo mwanamuziki anaangalia mambo ya
kisiasa. Jambo hili lilidhihirika wakati wa ukoloni ambapo mwafrika
alitumia nyimbo kama silaha kupigania uhuru. Muziki ulitumiwa kuwahimiza watu.
wapinge tamaduni za
wakandamizaji. Waafrika walifanya hivi kwa kuchukua nyimbo za kisiasa na
kuzipa mahadhi ya kidini ambapo kwa hakika maana ilikuwa tofauti na ile ya
kidini Hivi sasa wanamuziki wa nyimbo zilizopendwa wanaimba nyimbo
zinazowaelimisha na kuwahamasisha watu ili watekeleze kwa ufanisi sera na
maagizo mbalimbali ya chama kinachotawala na serikali kwa jumla.
Nyimbo nyingi
zinazosikika redioni zinahusu kuwahimiza watu kuwa na uwajibikaji, kilimo cha
kisasa, uzazi wa mpango, vita dhidi ya Ukimwi, kuchagua viongozi bora na
kufanya kazi kwa bidii. Lugha ya Kiswahili imetumika kuimba nyimbo zenye ushauri
kuhusu maisha, mapenzi, tabia nzuri na mbaya, ukulima bora na kadhalika Muziki hasa muziki wa
'zilizopendwa' ni sanaa ambayo huwafikia watu wengi kupitia vyombo vya habari
hasa redio na hata
televisheni. Kwa hivyo hii ni
sanaa ambayo haiwezi kupuuzwa kutokana na majukumu mbalimbali inayotekeleza.
Vyombo
vya habari vimetenga masaa
kadhaa ya kuwaburudisha watu kwa kutumia nyimbo mbalimbali. Balisidya (1987)
anakubali
kuwa sanaa hii ni sehernu
mojawapo ya fasihi ya Kiswahili na inahitaji kufanyiwa uchunguza zaidi, kwa
jinsi ambavyo watu
wengi wanaweza kuipata.
Nyimbo za kisasa zinaweza
kutupa mwangaza kuhusu maisha ya watu duniani.. Finnegan (1970), anasema kuwa
nyimbo-pendwa zina majukumu mbalimbali ya kutekeleza hasa katika kuangalia
mitazamo ya jamii kiulimwengu, na nyimbo hizi
hutekeleza majukumu haya kama
zilivyo nyimbo za kijadi Mtazamo huu umeungwa rnkono na watu kama vile Kabira
na
Mutahi (1988), Agovi (1989),
na wengine wengi ambao wanaona muziki kuwa utanzu teule inayodhihirika katika
jamii hii
inayobadilika. Nyimbo pendwa
zimechukuliwa na wasomi wengi kuwa kama muingiliano wa masimulizi jadi na
ukweli wa
maisha ya hivi sasa, Nyimbo
hizi hushughulikia mambo kama vile ukandamizwaji, kutamauka maishani, unyimwaji
wa haki
na umaskini/ubinafsi. Mambo
haya ni mambo ya kisasa na huathili wanajamii kwa njia mbalimbali.
Waimbaji wa nyimbo
zilizopendwa hushughulikia nyanja tofauti za maisha ya jarnii kama vile dini,
uchumi na siasa. Kwa
mfano, wao wanashughulikia
ndoa na mapenzi kwa kuonesha mahusiano ya jamii na migongano ya kimawazo baina
ya wazee na vijana au baina
ya rnke na mume. Katika nyakati hizi za mabadiliko katika uchumi na siasa
waimbaji wamekuwa
wakitunga nyimbo kwa kutuchorea picha ya jinsi mambo
yalivyo. Wamekuwa katika mstari wa mbele katika kuwatahadharisha wanajamii kuhusu ugonjwa wa Ukimwi
Muziki uliopendwa katika
Kiswahili ni sanaa isiyo kuwa na mipaka ya ukabila. Ni sanaa ambayo
huwaunganisha watu wa
makabila mbalimbali kwa kutumia
lugha inayoeleweka na kuzungumzia tajriba sawa wanazozifahamu. Nyimbo hizi pia
zimetumika kuimulika jamii
kwa kuonesha maendeleo yaliyopatikana katika nyanja mbalimbali Anapoikosoa
jamii, mwimbaji huwa anachukuwa jukumu la
kuhakiki jamii na hata kuielekeza. Nyimbo hizi pia zinatumiwa kuwazindua watu
waweze kufahamu haki zao hasa pale
wanaponyimwa, zinatumiwa kama ajenti wa ukombozi.
Katika nyimbo hizi, pia kuna
ufasihi hasa upande wa lugha. Sifa moja ambayo hubanisha nyimbo ni matmnizi
yake ya lugha hasa zile tamathali za usemi kama vile tashbihi, methali, semi,
jazanda taashira na majina ya majazi. Tamathali hizo zinazotumiwa na
nyimbo huwa ama zimebuniwa
katika jamii ya mwimbaji au zimebuniwa na mwimbaji mwenyewe lakini akazingatia
kanuni za
uundaji wake. Hii inafanya
tanzu hii iweze kuchunguzwa kwa makini kiusomi kwa kuchanganua ufani wake
kupitia lugha iliyotumika. Hata hivyo, waimbaji wa nyimbo-pendwa wamekumbana na
vizingiti vingi. Kutokana na sababu kuwa wao ni wahakiki wa jamii, baadhi ya
nyimbo zao zimepigwa marufuku, (mwangi 1992) na hivyo basi haziwafikii watu
wengi waliolengwa na haziwezi kutumiwa kama njia ya kuwazindua watu. Katika
kule kuihaki jamii, wao-hulenga kuikosa, lakini mara nyingi wao huwa hawaafikiani
na viongozi kuhusiana na maongozi yao.
Hitimisho
Nyimbo zinazoimbwa kwa lugha
ya Kiswahili huwafikia watu wengi kutokana na sababu kuwa lugha ya Kiswahili ni
lugha ya
walio wengi. Nyimbo
zilizopendwa zitaendelea kukua kufuatana na mabadiliko ya kihistoria na kifani
ambayo yanasababishwa
na watu wengi. Hivyo basi,
nyimbo hizi hazina budi kuchukuliwa kama sehemu moja ya Fasihi ya Kiswahili kwa
kuangalia mchango wake kimaudhui na kifani. Na zinahitaji kusambazwa ili
ziwafikie wanajamii wote. Hii ina maanisha kuwa vyombo
vya habari vina majukumu ya
kutekeleza katika kuhakikisha kwamba watu wengi wameweza kuzipata nyimbo hizi.
Kwa
upande wa fasihi, haya ni
mafanikio makubwa hasa kwa sababu tabia
ya kupenda kusoma haijakomaa kwa wengi.
Vyombo vya habari vinatumika
kusambaza fasihi hii kwa mamilioni ya watu. Hii ni kutokana na sababu kuwa
kundi moja tu la waimbaji linaweza kufundisha idadi kubwa ya watu kwa wakati
mmoja kupitia nyimbo zao
Mwandishi: PAMELA M. Y NGUGI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni