Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumamosi, Machi 01, 2014

Wanao penda kujifunza electronics designing


Najua kuna watu wengi wanapenda kujifunza Electronics designing;wale walio choka ku-copy na ku-paste already made design;na hivyo wangependa wao wenyewe wabuni vya kwao.

Ikumbukwe kuwa vifaa vya ki-electronic vinavyotumika kutengeneza vyombo ya ki-electronic kama vile Transistors,capacitors,resisto rs,diodes etc.vinaweza vikaunda kitu chochote unacho kitaka Kutegemeana na maamuzi yako,mfano unaweza kutumia vifaa hivyo kuunda TV,Radio,King’amuzi,Simu,Compu ter,.n.k.

Mfano computer imetengenezwa na vifaa hivyo hivyo,na Radio imetengenezwa na vifaa hivyo hivyo.Tofauti inakuja namna ambavyo vimeunganishwa kutegemeana na lengo la muundaji mwenyewe.

Ifahamike kuwa Hakuna tofauti kati ya vifaa vinavyotumika kuunda vyombo vya kidigitali au vile vya kianalogia.Vifaa kama vile Transistors,capacitors,resisto rs,diodes etc ndio msingi mkuu wa vyombo vyote vya kielectronic(digital and Analogy).Kinacho fanyika hapo is just a game of mathematical and functions exchange kutegemeana na matumizi husika.

Jua kwamba nirahisi sana kuwa fundi wa ku-repair vifaa vya kielectronic ila ni vigumu kwa wewe kuwa mbunifu wa vifaa vya kielectronic kama hujui misingi ya ufanyaji kazi wa vifaa mama vya kielectronic kama vile Transistors,capacitors,resisto rs,diodesetc.
Kamwe haiwezekani ukaamka asubuhi na kuanza ku-design project kubwa kama vile kuunda TV,King’amuzi, au computer kama hukuwahi kuanza katika project ndogo.

Umeme unasheria na kanuni zake ni lazima uzifahamu na kuzizingatia katika maisha yako yote katika dunia ya kielectronic.

NANI ANAWEZA KUWA MBUNIFU WA VIFAA VYA KIELECTRONICS
1.Mtu yeyote,kitu cha msingi ajue nguzo kuu za hesabu kama vile kujumlisha,kutoa,kugawanya,kuz idisha n.k

2.Awe mbunifu ajenge mawazo tofauti tofauti juu ya vitu tofauti tofauti na atafute ufumbuzi kupitia taaluma yake ya kielectronics.

3.Asiwe anakata tama mapema.

4.Ubunifu wa vifaa vya umeme ni tofauti na ubunifu kama vile computer programming kwasababu when a mistake has done is PUUUUUUUUUUU!Within a second,electricity never wait to react!Hivyo basi mbunifu lazima azingatie sheria za umeme kwa usalama wake na usalama wa vifaa vyake,ili kuepuka hasara zisizo za msingi.

5.Apende electronics.

FAIDA GANI ZA KUWA MBUNIFU WA KIELECTRONICS.

1.Kujipatia ajira.Unaweza uka-design kitu ambacho jamii ikawa inakihitaji sana na ikawezekana kifaa hicho hata dukani hakuna,au kama kipo ni ghali kuliko cha kwako,hivyo utapata soko lisilo na mshindani

2.Kuunda vitu vyako mwenyewe kwa matumizi yako mwenyewe.Kama vile security systems,operating systems mbalimbali n.k.Mfano mimi kwangu nimefunga vifaa mbalimbali ambavyo nime-design mwenyewe,kiasi kwamba kama ningekuwa naingia dukani kununua it was a lot of Dollars!Forexample music system yangu nayo tumia it is about 1500 wattage,ambayo ningeingia dukani ingeni cost a lot,pia nimefunga Security systems za kila aina,because it is too cheap if you DIY!

3.Kujiongezea taaluma na maalifa zaidi.

MAFUNZO YA KIELECTONIC KWA NJIA YA MTANDAO

Nimekuwa nikitoa mafunzo kwa njia ya face to face.Ila kuna watu wengi wanapenda kujifunza ila wapo mbali na Dar au wanakosa muda wa kuingia darasani.Hivyo nimefikiria kuanzisha mafunzo ya kielectronic kwa njia ya mtandao ili niweze kumfikia kila mmoja.Kile nilicho nacho na wengine wapate.


Mafunzo nitakayo kuwa nafundisha ni ya ubunifu(Electronics designing) tu!Sita fundisha ufundi wa ku-repair kitu chochote ila nitafundisha elimu yak u-design kitu chochote!

Lengo langu ni kuibua vipaji vya wabunifu wa vifaa vya kielectronic na sio wale wanao fanya marekebisho ya vile vilivyo tengenezwa na mzungu vikaharibika.

Japo ni vigumu kufikia kiwango cha juu cha ubunifu wa vifaa vikubwa kutokana na sababu mbalimbali.Ila lengo ni kufanya vile vinavyo wezekana kubuniwa na sisi wenyewe katika mazingira yetu vifanyike.

Lengo langu jingine ni kuunda jamii ya wabunifu na sio warekebishaji tu!Ambapo kwa pamoja tunaweza tukabadilishana mawazo na kuunda vitu mbalimbali.

Mafuzo yangu nitayatoa kwa lugha ya Kiswahili kadri inavyo wezekana,ingawaje kuna baadhi ya misamiati itatolewa kwa lugha ya kiingereza kutokana na ukosefu wa misamiati ya namna hiyo katika lugha yetu ya Kiswahili.

Mafunzo yatagawanyika katika makundi matatu ambayo ni;-

a)Wasio na msingi wa umeme na electronic kabisa
b)Walio na msingi wa umeme na electronic katika kiwango cha kati
c)Walio na msingi thabiti wa umeme na electronic
Kwa wanao taka kujifunza electronic na hawajui wapo kundi gani kati ya hayo waisome sakiti hii hapa chini halafu waniambie ni sakiti ya nini na inafanyaje kazi vilevile wakitambue kila kifaa ndani ya sakiti hii mimi ntajua anakiwango kipi kutokana na majibu yake

Click image for larger version. 

Name: jjco.jpg 
Views: 0 
Size: 200.3 KB 
ID: 141489





-Kila atakayetaka kujifuza lazima anunue vifaa vifuatavyo

1:Multmeter
Name:  hh.jpg
Views: 0
Size:  3.7 KB
2; Soldiering Beat
Name:  images.jpg
Views: 0
Size:  2.8 KB
3;Soldering wire
Name:  bn.jpg
Views: 0
Size:  2.0 KB
4:Unprited circuit board

Name:  jj.jpg
Views: 0
Size:  4.7 KB
5:Kila mwanafunzi atatakiwa awe na software maalumu ya kujaribia michoro ya designing zake za kielectronics kabla ya kuziunda katika circuit board.Software hii itakusaidia kutambua makosa madogo madogo kabla hujaiunda sakiti yako katika dunia halisi.(nitatoa link ya kudownload software hii)

Kwa wale ambao wako tayari kuingia katika dunia hii nawakaribisha tuma jina lako na namba yako ya simu kwenye email efuatayo datetz18@yahoo.com.

Mafunzo yataendeshwa kupitia website maalumu ntakayo itambulisha baadae kwa watakao tuma majina ambapo mwanafunzi atakuwa na uwezo wa ku-log-in au ku-log out kwa kutumia user name na password.

Mafunzo yata base katika ubunifu wa vifaa vya analogia na kidigitali;wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya electronics mnakaribishwa!

Haitakuwa public itakuwa for only members!
Members watatakiwa kulipia fee kidogo ili mwalimu atumie muda wake pamoja nao!


Karibu!


Chanzo: http://www.jamiiforums.com/

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni