Moja kati ya kampuni nyiiingi iliyopo
Florida nchini Marekani imekuja na wazo la kujenga meli iitwayo ‘Freedom Ship’
itakayokuwa na kila kitu cha kuifanya iwe jiji
linaloelea juu ya maji.
Wabunifu wa wazo la meli hiyo wametoa michoro ya picha za meli hiyo itakavyokuwa pindi itakapokamilika.
Roger M Gooch,
ambaye ni mkurugenzi na makamu wa Rais wa kampuni ya Freedom Ship International ambao ndio wenye mradi huo, amesema hiyo meli itakuwa
ndio meli kubwa kuwahi kujengwa, iliyo na muonekano wa jiji la kwanza linaloelea kwenye
maji.
Kutakuwa na uwanja wa ndege juu ya meli hiyo, uwanja utakaowezesha ndege kuruka na kutua wakati wakati meli inatembea
Mkurugenzi na makamu wa Rais wa kampuni hiyo Gooch, amesema
kampuni yake inaendelea kukusanya kiasi cha yuro milioni 600 ni sawa na dola bilioni moja zinazohitajika
kuifanya ndoto hiyo iwe kweli aliongeza.
Meli hiyo
inayotegemewa kuwa na ghorofa 25, itakuwa na uwezo wa kuwapa makazi ya
kudumu watu 50,000, lakini itakuwa na nafasi ya ziada ya kupokea wageni
wengine 30,000, makazi 20,000 ya wafanyakazi wa meli, na mengine 10,000
kwaajili ya wageni wa usiku mmoja. Freedom Ship, itakuwa na huduma zote za jiji kama vile Shopping center, shule, hospitali, uwanja wa ndege, casino, maegesho ya magari na mengine mengi.
Hii ndio njia inayotarajiwa kutumiwa na meli hiyo kuizunguka dunia
|
Meli hiyo
itakapokamilika inatazamiwa kuzunguka dunia nzima kupitia nchi moja hadi nyingine, bara
moja hadi jingine Afrika ikiwemo na haitakuwa ikikaa sehemu moja
kwa muda mrefu.
Meli hiyo itakuwa
na huduma zote za muhimu zinazopatikana katika majiji mbalimbali
zikiwemo hospitali, shule, maduka, parks, casino, aquarium, kiwanja cha
ndege chenye njia ya kuruka na kutua ndege ndogo zenye uwezo wa kubeba
watu 40, kitakachokuwa juu kabisa kwenye paa la meli hiyo.
Hii meli itakuwa ikitumia umeme wa solar pamoja na ule wa wave energy.
Itakapokamilika, itakuwa na upana wa futi 750, urefu wa kwenda juu futi 350,
pamoja na urefu wa futi 4,500 ikiwa ni mara nne ya Queen Mary II Cruise ship
iliyokuwa na urefu wa futi 1,132.
Cha ajabu zaidi wageni na wenyeji wanauwezo wa kuondoka na kuingia kwenye jiji hilo linaloelea majini kwa ndege au boti ziendazo kasi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni