Muonekano wa Windows. |
Tumesema
kuwa software ni maelekezo mama katika kuifanya kompyuta iweze kufanya
kazi. System software ni kama injini ya kompyuta. Ndiyo huendesha
kompyuta. Na kama nilivyosema software huandikwa na wataalam kwa kutumia
programming languages. Waandishi ama wandikaji wa software hizi
huajiriwa na makampuni mbalimbali yanayoendeshwa kibiashara. Mojawapo ya makampuni
maarufu duniani ambayo yanahusika na uundaji wa software ni lile
lijulikanalo kama Microsoft. Kampuni hii inajihusisha na uandikaji wa software
mama (system software au Operating system) zijulikanazo kama Windows.
Hizi
ni software maarufu sana na zinatumiwa na watu wengi duniani kuliko software
nyingine zilizopo sokoni. Mmoja wa waanzilishi wa kampuni ya Microsoft ni
bilionea bwana Bill Gates ambaye aliwahi kuwa tajiri namba moja duniani. Yeye mwenyewe
ni mtaalam wa uandishi wa softwares. Sababu ya kuifanya software ya
Windows kutumika zaidi duniani ni urahisi wake katika kuitumia na hata kuiweka
katika kompyuta bila masharti mengi. Software hii imeundwa katika namna ambayo
inamfanya mtumiaji wa kompyuta kuilewa kwa muda mfupi kwani inatumia picha
zifahamikazo kama graphical tools ambazo huweza kukumbukwa kwa urahisi,
tena zikiwa na majina.
Windows
software zilianza kutolewa tangu mwanzoni mwa miaka ya 1980 na mpaka leo kuna matoleo
kadhaa ambayo yamekuwa yakiboreshwa zaidi na zaidi. Matoleo haya ni kama
Windows 95, Windows 97, Windows 98, Windows NT, Windows 2000, Windows XP and
Windows 7
Je kuna aina nyingine za system software?
Bila
shaka. Kila kompyuta ina maelekezo yake kulingana na muundo wa hardware yake. Kompyuta
aina ya personal au PC hutumia mara nyingi Windows (ambazo hapa Tanzania tunaziona
kila mahali). Lakini kompyuta kubwa kama supercomputers na kompyuta nyingine maalum
kama simu za mkononi na kompyuta za viganjani zijulikanazo kama PDAs hutumia operating
system maalum kulingana na uwezo wa kutunza kumbukumbu wa kompyuta husika. Zifuatazo
ni aina ya Operating System zinazotumika katika kompyuta mbalimbali:
Mac
OS ambayo hutumika katika kompyuta aina ya Apple
Linux
ambayo hutumika katika kompyuta aina ya personal na pia mainframe
Palm
OS ambayo hutumika katika kompyuta aina ya palmtop.
Je
kompyuta zinatambulika vipi katika soko la kibiashara?
Kama
ambavyo kila bidhaa ina jina lake inapoingia sokoni ndivyo ilivyo hata kwa
kompyuta. Kompyuta inatengenezwa kwa kutumia teknolojia mbalimbali kulingana na
matumuzi yanayokusudiwa. Hapa nitazungumzia teknolojia ya utengenezaji wa
kompyuta aina ya PC. Katika soko la biashara ya kompyuta kuna watengenezaji
mbalimbali wa kompyuta ambayo ni makampuni makubwa katika nchi zilizoendelea
kama Japan, China, Marekani na Korea. Mojawapo ya majina makubwa katika
utengenezaji wa kompyuta ni DELL, TOSHIBA, INTEL, IBM, HP na SIEMENS. Kwa
kawaida kompyuta huwa na jina lake ingawa inaweza kuwa na mchanganyiko wa vifaa
vya ndani ambavyo hutoka kwa watengenezaji mbalimbali.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni