Photo Credity By: http://www.micron.com |
Hakika
nguvu ya binadamu katika kufanya kazi hutegemea sana ubongo. Ubongo ndiyo
huungoza mwili na ndiyo kama injini ya kila lifanyikalo katika mwili wote.
Katika hali sawa na hiyo, kompyuta nayo inategemea kifaa maalum kifahamikacho
kama processor au microprocessor. Kifaa hiki ndicho ambacho
hufanya kazi zote zinazotakiwa na sehemu nyingine zote za kompyuta. Kifaa hiki
pamoja na sehemu ya kutunzia kumbukumbu pindi kompyuta ifanyapo kazi –kumbukumbu
za muda; yaani Random accessory memory; ndizo huweza kutanabahisha nguvu
ya kompyuta. Na bila shaka umekwisha sikia mtu akisema ‘kompyuta yako ni
pentium ngapi’ au ‘kompyuta yako ina RAM kiasi gani’. Hapa anakuwa anazungumzia
uwezo wa processor na RAM.
Microprocessor
hufanya kazi kwa haraka sana kulingana na jinsi ilivyoundwa. Mpaka leo hii processor
ina uwezo wa kufafanua maelekezo (execute instructions) yapatayo bilioni
moja kila sekunde,
kwa kompyuta aina ya PC. Uwezo huu hupimwa kwa kutumia kiwango kifahamikacho kama
Hertz. Microprocessor katika kompyuta aina ya personal za siku
hizi zina uwezo wa mpaka 4.0 Gigerhertz (GH).
Nyingi
ya processor zinatengenezwa na kampuni ifahamikayo kama INTEL. Kampuni hii
huziitza processor zake kwa majina ya Pentium. Na nyingi ya kompyuta
aina ya PC hutumia processor za aina hii na ndiyo maana si ajabu ukakuta
watu wengi wanafahamu kompyuta kwa kupima kiwango cha ‘pentium’
ilichonacho. Hii ni kwa sababu processor hizi zina matoleo tofauti
kuanzia Pentium I, II, III, IV na M na kila moja huwa na nguvu ya juu kuliko
ile zilizoitangulia. Kwa hiyo mtu anaposema pentium IV anamaanisha kuwa anataka
kompyuta ambayo ni bora zaidi kuliko Pentium I kwani hata muundo wake huonekana
tofauti.
Pia
katika upande wa utunzaji kumbukumbu kuna kipimo ambacho huitwa megabyte,
kwa kifupi MB.
Hiki ni kipimo cha utunzaji kumbukumbu ambacho kinaeleza ni kwa kiasi gani
maelekezo au data zote zinazotakiwa kusshughulikiwa na zinazotoka kama
habari hutunzwa kwa pamoja. Kadiri kipimo hiki kinavyokuwa kikubwa ndivyo
kompyuta inakuwa na uwezo wa kufanya kazi kwa haraka na kwa urahisi zaidi. Kwa
kawaida utakutana na kompyuta zenye RAM kiasi cha 256 MB au 512MB na zaidi. Pia
kama kompyuta ina processor yenye kiwango cha 2.0 GH au zaidi inakuwa
nzuri kea shughuli zote.
Na
kwa kawaida kompyuta huuzwa kulingana na viwango hivi viwili, pamoja na kipimo
cha tatu ambacho ni utunzaji wa kumbukumbu zisizoweza kupotea (permanent data)
katika hard disk. Hii hupimwa kwa kiwango cha Gigabyte (GB).
Utakutana na kompyuta aina yenye hard disk kiasi cha 40 GB au 80 GB.
Hivyo unaweza kukutana na kompyuta yenye uwezo (specifications) kama
ifuatavyo:
Hard disk 80 GB, RAM 512 MB, Processor speed 2.6 GH Intel Pentium
M aina ya Dell.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni