Kwa kawaida vyombo vingi vinavyorahisisha kazi hutumia kazi
hutumia umeme ili viweze kuleta ufanisi katika shughuli mbalimbali. Kompyuta
nayo hutumia umeme katika kutekeleza majukumu yake. Umeme huu huingizwa kwa
kutumia nyanya (cable) ambazo hutoa umeme kutoka katika soketi zilizopo mahali
husika. Umeme huu hupitia chombo maalum kifahamikacho kama power supply.
Chombo hiki huwa kimeunganishwa kuelekea motherboard na sehemu nyingine muhimu. Kwa kawaida umeme huu hubadilishwa kutoka mfumo wa kubadilika
badilika (alternating current a.c) kwenda mfumo wa moja kwa moja (direct
current d.c) ambao kompyuta inaweza kuutumia. Umeme huu hugawanywa katika
kiwango kinachotakiwa kulingana na matumizi ya sakiti husika.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni