Photo Credity By: http://metrology.zeiss.com |
Hakika kompyuta ni kifaa kilichoundwa
katika utaalam wa hali ya juu. Unapokuwa unaitazama kompyuta, yaani unapokuwa
unaiona monitor, keyboard, case na vinginevyo unakuwa unaona sehemu ya ‘nje’
ya kompyuta. Unakuwa unaiona sehemu ijulikanayo kama hardware part. Hardware
part ni sehemu ambayo unaweza kuishika na kuiona kwa macho. Ni sehemu
ambayo ni hard au ‘ngumu’ kwa maana ya kwamba inaonekana na kuweza
kubebwa na kufanyiwa marekebisho. Sehemu hii ya kompyuta haiko peke yake katika
ufanyaji kazi wa kompyuta.
Yenyewe kama ilivyo haiwezi kufanya
lolote; ni kopo lisilo na maana! Ni kama unaponunua baiskeli na kuiweka ndani.
Itakuwa na manufaa kwako endapo tu utaiendesha. Ni kama unapokuwa na gari
ambalo bado halina mafuta. Ili liweze kujongea utahitaji kuliwekea mafuta.
Vivyo hivyo kompyuta haitaweza ‘kujiendesha’ yenyewe bila kuwa na muendeshaji
(ambaye ni wewe). Kompyuta haitaweza kufanya kazi kama itakuwa na hardware
part peke yake. Ni lazima kuwe na muendeshaji wa hardware part hiyo.
Sehemu ya kompyuta ambayo ni muhimu
sana katika kuifanya ifanye kazi iliyokusudiwa ni ile ‘isiyoonekana’. Ni
sehemu ambayo huwezi kuiona na inajulikana kama software part. Tazama
jinsi maneno yalivyotumika: hardware na software ambayo yanatia
msisitizo katika ‘ugumu’ na ‘ulaini’. Sofware ni mkusanyiko wa maelekezo maalum
ambayo kompyuta hupewa ili kuiwezesha kufanya kazi kulingana na maelekezo hayo.
Kwa jina jingine software inafahamika kama computer
Ni namna gani software na hardware hufanya kazi kwa ushirikiano?
Kama nilivyosema hapo awali hardware
part ya kompyuta ni mkusanyiko wa sakiti mbalimbali ambazo zimeunganishwa
katika mfumo maalum unaoiwezesha kompyuta kufanya kazi. Lakini ni lazima sakiti
ya kompyuta ipewe maelekezo maalum ili iweze kufanya kazi. Ni kama kuiamuru
runinga yako ioneshe kituo Fulani cha matangazo ambacho unataka kutazama. Kwa kutumia
dhana hii wataalam wa mambo ya kompyuta waliamua kutumia mkusanyiko wa maelekezo
uitwao software ili kufanikisha hili. Software ni mkusanyiko wa maelekezo
mbalimbali yaliyogawanyika kulingana na kazi yanayotakiwa kufanya. Kuna
maelekezo ya kuwasha kompyuta, kuna maelekezo ya kuizima kompyuta, kuna
maelekezo ya kutoa ishara za hatari, maelekezo ya kutoa mlio na kuacha kutoa
mlio, maelekezo ya kuandaa picha za video na za kawaida, maelekezo ya kuhifadhi
habari zinazoandaliwa na mengine chungu nzima. Hii inamaansiha kuwa kuna
software tofauti tofauti kulingana na kazi zinazotakiwa kufanya. Kuna software
ya kuandikia, software ya kupigia mziki, software ya kuendeshea mitambo,
software ya kutengeneza sauti, softwares za kuendesha mitambo mbalimbali kama robots,
ndege, camera za ulinzi nk.
Mkusanyiko wa software mbalimbali hufanya vipi kazi katika
hardware?
Software zote huunganishwa na
kupangiliwa kufanya kazi kwa kutumia software kuu ijulikanayo kama system
software au operating system kwa kifupi OS. OS ni maelekezo mama ambayo
huingizwa katika kompyuta mara tu kompyuta inapokuwa imetengenezwa. Ni
maelekezo ambayo huiendesha kompyuta katika kupokea na kutoa maelekezo mengine
ambayo binadamu hutaka ifanye. OS ndiyo huiwasha kompyuta na kuiweka katika
hali tayarifu kwa ajili ya kufanya kazi. Kifuatacho ni sehemu ndogo ya kile
ambacho OS hufanya unapotaka kuitumia kompyuta: Unawasha kompyuta kwa kubonyeza
kitufe cha kupokea umeme Umeme hutiririka katika sakiti nzima ya kompyuta OS
hufahamu kuwa umeme umeingia hivyo huiwasha kompyuta OS hutizama kama kila
sehemu muhimu ya kompyuta ipo kwa mfano keyboard, mouse, monitor n.k
Baada ya muda kompyuta inakuwa tayari
imewashwa na iko tayari kufanya kazi ikimsubiri mtumiaji ailekeze nini cha
kufanya. Mtumiaji wa kompyuta hutumia peripheral devices kama keyboard
na mouse katika kuilekeza kompyuta ifanye kile anachokihitaji. Na
hao ndipo panakuwa na maelekezo mengine ambayo niliyazungumzia hapo mwanzo. Kwa
mfano kama mtumiaji anataka kuandika barua basi itambidi aanzishe maelekezo
yatakayomwezesha kuandika barua hiyo. Maelekezo haya madogodogo hutekelezwa na
programu ndogo inayfanya kazi pamoja na programu mama ikijulikana kama application
software. Kwa maana hii tunaweza kusema kuwa software part ya kompyuta imegewanyika
katika sehemu kuu mbili; system software na application software.
Je, maelekezo haya yajulikanavyo Kama application software na
system
software hueleweka
vipi ndani ya kompyuta?
Kwa hakika unaweza kujiuliza ni vipi
maelekezo haya hutambulika na sakiti ndogondogo za kompyuta. Lakini ni dhana rahisi tu kuilewa. Ni kama wewe unapozungumza na mtu ambaye
hatumii lugha unayoizungumza. Itakubidi uzungumze na mtu huyo kwa kutumia
mfasiri (mkalimani). Vivyo hivyo maelekezo ya kompyuta inabidi yatafsiriwe na
kuwekwa katika mfumo ambao hardware ya kompyuta itayaelewa. Lakini jambo
moja la kufahamu ni kwamba maelekezo haya huandaliwa au kuandikwa kwa utaalamu
maalum ili yaweze kueleweka katika kompyuta.
Utaalam huu hutumiwa na wanasayansi wa
kompyuta. Utaalam huu hufahamika kama programming. Utaalamu huu hutumia
lugha maalum ammbazo si kama zile tuzitumiazo katika maisha ya kawaida katika
kuwasiliana. Lugha hizi zina herufi na namba ambazo tunazifahamu (A mpaka Z na
0 mpaka 9) ukijumuisha na alama kadhaa kama mkato, nukta, mabano na nyingine nyingi
ambazo ni nadra kutumika katika maandishi ya kawaida ya lugha. Mkusanyiko wa
herufi na namba hujulikana kama codes na uandikaji wake hufahamika kama coding.
Kwa lugha ya kawaida ya kimombo neno codes humaanisha maneno ya siri
yasiyoweza kufahamika kwa urahisi na watu wengine isipokuwa wale wachache wenye
utaalam maalum waliousomea. Kwa hiyo lugha hizi za kuandikia maelekezo ya
kompyuta hufahamika kama programmming languages. Hivyo ni lugha hizi
ambazo huifanya kompyuta kujengewa maelekezo ambayo itayatambua na hatimaye
kuweza kufanya kazi. Kwa hapa nchini utaalam wa lugha hizi hujifunza katika
vyuo mbalimbali nchini kama kile chuo kuku cha Dar es Salaam. Mfano wa lugha
hizi za kompyuta ni kama Java, Visual Basic, PHP na C.
Je Kompyuta inayaelewa vipi Maelekezo Haya?
Maelekezo yanayowekwa ndani ya
kompyuta hayawezi kuelewekwa moja kwa moja ndani ya sakiti za kompyuta.
Yanapaswa kutafsiriwa katika mfumo ambao kompyuta inaweza kuyaelewa. Katikati
ya hardware part na software ya kompyuta kuna maelekezo maalum
yajulikanayo kama assembler ambayo hufanya kazi ya kutafsiri software
part kwenda katika sakiti ya kompyuta. Sakiti ya kompyuta haiwezi kutambua
maelekezo yanayokuwa na herufi au namba (ambayo software huundwa) bali hutambua
mtiririko wa namba mbili maalum ziandikwazo kama 0 na 1. Kwa hiyo assembler
hubadilisha herufi na namba kwenda namba mbili 0 na 1. Kwa mfano neno ‘do’ linaweza
kutafsiriwa na assember katika tarakimu 01100 ambazo sakiti ya
kompyuta huielewa. Kwa namna hii kompyuta huweza kufanya kazi na kuleta matokeo
yanayotarajiwa.
Je Maelekezo au software hutunzwa wapi ndani ya Kompyuta?
Tuliona kuwa kompyuta hutunza
kumbukumbu. Na ni uwezo wa kompyuta kutunza kumbukumbu ndiyo unaifanya kuwa
chombo cha kipekee katika ulimwengu huu ambacho kinaweza kufananishwa na ubongo
wa binadamu na hata kufanya kazi kwa ufanisi. Kumbukumbu za kompyuta hutunzwa
katika mfumo wa ki-elektroniki katika kifaa maalum kilicho ndani ya system unit
kifahamikacho kama hard disk. Kifaa hiki kina uwezo wa
kutunza kumbukumbu kwa muda mrefu na kimeundwa katika mfumo ambao unaruhusu
kufuta, kurekebisha na kuandika tena kumbukumbu; kuongeza na kupunguza
kumbukumbu. Ni kifaa muhimu katika kompyuta. Huwa kimeunganishwa na motherboard
kwa kutumia waya maalum. Kifaa kifahamikacho kama hard disk
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni