Licha ya kuwa na aina za kompyuta lakini bado kuna msingi ambao zote
huutegemea. Msingi huo ni kuwa na sehemu kuu mbili; sehemu kuu ya kutengeneza habari kutokana na
data zilizoingizwa ijulikanayo kama Central Processing Unit au CPU kwa kifupi na sehemu ya
kuingizia data na kutolea habari iliyokwisha tengenezwa kwa ajili ya faida ya mtumiaji
ijulikanayo kama peripheral devices. Kwa hiyo data huingizwa kupitia sehemu zinazofahamika Kama peripheral
devices na kupelekwa ndani ya CPU ambako hunyumbulishwa na kufafanunuliwa na
hatimaye kutoa kile kilichokusudiwa kupitia tena peripheral devices hizohizo. CPU hufanya
kazi ya kufafanua data (processing) kulingana na maelekezo ya mtumiaji. Tuone sehemu mbalimbali
za kompyuta ambazo huifanya kazi ya kompyuta kutekelezeka kwa ufanisi.
Ubongo wa Kompyuta (Central Processing Unit)
Hii ni sehemu maalum kabisa katika kompyuta. Ndiko ambako maamuzi yote
kuhusu data na habari hufanywa ili kuhakikisha kuwa mambo yanakwenda vyema. Ni kama
ubongo wa binadamu ambao huamua mambo yote yanayohusiana na shughuli zote za mwili ili
kumfanya aishi katika afya njema. Sehemu hii ya kompyuta huwa ndani ya kifaa kiitwacho computer
case ambacho kinafunika ‘ubongo’ huu wa kompyuta.
Computer Case inaweza kuwa bapa na
yenye umbo la msitatili au mraba (kwa aina ya personal computers) ambayo huwekwa katika
meza ili iweze kutumika vyema. Aina hii ya computer case inajulikana kama desktop case na
ndiyo maana kompyuta huitwa desktop computer. Pia computer case inaweza kuwa na umbo
lililosimama, kama umbo la mche msitatili na lijulikanalo kama Tower case – na ndiyo huzaa
jina la Tower computer. Lakini kwa notebook computer na palmtop computers computer case huwa
imunganishwa na sehemu ya peripheral kiasi kwamba ni vigumu kuweza kuifafanua vyema.
Ubongo wa kompyuta huwa ni muunganiko wa sehemu mbalimbali ambazo kwa
pamoja huwekwa katika mfumo mmoja ujulikanao kama motherboard. Muundo wa motherboard
hutofautiana kutegemeana na aina ya kompyuta (mtengenezaji) na ukubwa wa kompyuta
yenyewe na hata toleo (version) la kompyuta husika. Kompyuta aina ya desktop ina motherboard
tofauti na kompyuta aina ya notebook. Pia kompyuta toleo la mwaka 1995 ina muundo wa motherboard
ulio tofauti na lile la toleo la mwaka 2005.
Ubongo wa kompyuta (CPU) huwa na
vifaa muhimu vifuatavyo:
Kifaa ambacho ni mkusanyiko wa mamilioni ya sakiti ndogondogo
zijulikanazo kama transistors. Sakiti hizi zinakwa na ukubwa wa chini ya unywele mmoja wa nywele za
binadamu! Kifaa hiki ndicho ambacho kinachukuliwa kama moyo au ‘roho’ ya kompyuta. Bila kifaa
hiki kompyuta haiwezi kufanya lolote. Kifaa hiki kinajulikana kwa jina la microprocessor.
Ni kifaa hiki ambacho hupokea mamilioni ya maelekezo kutoka kwa mtumiaji na kuyafanyia kazi ili
kutoa majibu yanayotakiwa. Kina uwezo wa kufafanua na kunyumbulisha data kwa uwezo wa
hata kufikia maelekezo trilioni moja kwa sekunde! (hii ni kulingana na ukubwa na uwezo
wa microprocessor hiyo kutegemeana na aina ya kompyuta).
Kifaa kingine muhimu ni kitunza kumbukumbu kijulikanacho kama random
access memory chip ambacho hutunza kumbukumbu zinazofanyiwa kazi na kompyuta. Kumbukumbu
hizi huhifadhiwa katika mfumo ambao ni wa muda tu; ikiwa na maana kwamba mfumo huu
hupoteza kumbukumbu hizo mara tu umeme ambao unaozunguka katika sakiti nzima ya kompyuta unapotoweka. Kifaa kijulikanacho kama random acess memory
Kifaa kingine ni mkusanyiko wa nyanya ndondogo sana ambazo huunganishwa
pamoja na kufungwa vyema ndani ya material aina ya plastiki. Kifaa hiki hupitisha
data ndani na nje ya motherboard. Ni kama barabara ambayo inaunganisha mji mkubwa ili kufanya
mawasiliano kuwapo baina ya watu. Kifaa hiki kinafahamika kama system bus.
System bus (utepe manjano)
Pia kuna vifaa mbalimbali ambavyo vinahusika na utoaji wa sauti, picha na
kadhalika. Pia matundu ya aina mbalimbali ambayo huwezesha uunganishwaji wa sehemu za nje ya motherboard
yaani peripheral devices.
Sehemu Za Nje ya Motherboard (Peripheral Devices)
Hizi ni sehemu ambazo zinakamilisha ufanyaji kazi wa kompyuta. Sehemu
hizi ziko nje ya system case na zinakuwepo katika kompyuta kulingana na matumizi ya mtu husika
ingawa kuna sehemu ambazo lazima ziwepo (basic peripheral devices). Sehemu hizi za kompyuta
hujulikana pia kama sehemu za kutoa na kuingizia habari na data au kwa jina la kitaalam kama input
and output devices. Sehemu hizi ni kama zifuatazo:
Sehemu ya kuingizia maneno na maelekezo maalum ijulikanayo kama keyboard.
Hiki ni kifaa ambaco kina mkusanyiko wa herufi (A mpaka Z) na namba 0 mpaka 9. Kifaa
hiki kina mkusanyiko wa vitufe au buttons ambazo herufi au namba hizo huandikwa. Mtumiaji wa
keyboard anapaswa kubonyeza (press) vitufe hivyo ili kuweza kuingiza malekezo haya (herufi
na namba) katika kompyuta. Pia keyboard huwa na buttons maalum ambazo huingiza malekezo
maalum kea ajili ya ufanisi wa kazi wa kompyuta. Tutazungumzia zaidi sehemu hii.
Sehemu ya kukuwezesha kuona nini unakifanya katika kompyuta. Huwezi
kwenda kwa mfano sokoni ilihali hauoni. Unahitaji kuona barabara na kufahamu soko lipo
wapi ili uweze kufika kwa urahisi. Vivyo hivyo unapokuwa unatumia kompyuta au unafanya kazi na
kompyuta unahitaji kuona kile unachokifanya. Unahitaji kusikia kile unachokitarajia. Sehemu
hii ya kompyuta hujulikana kama monitor. Monitor ina umbo kama la runinga ambayo umezoea
kuiona na kwa uhalisia teknolojia ya uundwaji wake ipo sawa na ya runinga isipokuwa
marekebisho kidogo. Monitor ndipo mahala pekee pa kuweza kufahamu nini kinaendelea ndani ya
kompyuta kwani shughuli zote za utengenezwaji na utoji habari huonekana katika kifaa
hiki.
Sehemu ya kuweza kuingiliana na monitor na kufanya kile unachikihitaji na
ambayo hufanya kazi kwa kushirikiana na keyboard ni sehemu ya tatu katika hili kundi la peripheral
devices. Sehemu hii inajulikana sana kama mouse. Mouse ni kifaa ambacho mtumiaji hukitumia
kuwasiliana na kompyuta (CPU) ili kuzaa au kutoa kile kinachotarajiwa. Kifaa hiki huwa
na mahali ambapo unabonyeza kwa kutumia kidole na ubonyezawji wa kidole hiki husafirisha
habari katika kompyuta na kuilekeza ifanye nini. Mouse huonekana katika kompyuta kama mshale na
mshale huu hutembea katika monitor kumuwezesha mtumiaji kuamua nini cha kufanya.
Mshale huu hujulikana kama cursor kwa kimombo.
Sehemu hizi tatu za kwanza katika kundi la peripheral devices
zinategemeana na hujulikana kama basic input & output devices. Hii ina maana kwamba sehemu hizi ni lazima
ziwepo ili kuifanya kompyuta ifanye kazi zilizo za muhimu. Sehemu nyingine muhimu ni zile zinazotoa na kuingiza sauti. Sehemu hizi
hufahamika kama input
and output sound devices. Mfano wa sehemu hizi ni kama speakers,
microphones, webcam, cameras na nyingine nyingi. Pia sehemu za kuingizia picha na kutolea
picha kama cameras. Aina mbalimbali za Microphones
Sehemu nyingine muhimu ambayo ni ya muhimu sana inajulikana kama printer.
Ni kifaa ambacho hutumika katika kuchapa matokeo ya ufafanuzi wa kompyuta ulio katika
mfumo wa maandishi (text) kwa shughuli mbalimbali anazozihitaji mtumiaji. Kifaa hiki kina
uwezo wa kutoa maandishi na picha zilizo na zisizo na rangi. Kifaa hiki kinatofautiana katika
utengenezwaji kulingana na mahitaji ya watumiaji.
Sehumu tulizozizungumzia hapo juu ndizo sehemu zinazojumuisha peripheral
devices. Kwa hakika sehemu hizi ni muhimu katika kuifanya kompyuta iitwe kompyuta kwani ndizo
zinazowezesha kupata matokeo
ambayo binadamu anayahitaji katika maisha yake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni