Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumatano, Oktoba 17, 2012

NI KWA NINI UHALALI KWA UKABILA, UDINI, UKANDA NK?Wapendwa katika Bwana,

NDUGU Wakristo umefika wakati tumeonelea kuwa ipo haja ya kuwaelezeni machache ili kuona maendeleo yetu na mafanikio tuliokwisha yapata hapa Zanzibar, yanaendelezwa na hayarudi nyuma kwa namna yoyote. Hapana shaka kuwa munaelewa kuwa idadi yetu hadi sasa ni ndogo sana na wengi wetu tungali katika kiwango na hadhi ya wahamiaji na sio Wazanzibar kama wanavyosema wenyewe.


MAFANIKIO YETU


KABLA kugusia yale ambayo tunahisi ndio lengo la waraka huu hapana budi kuwatajieni mambo machache ambayo tumefanikiwa kuyapata hadi sasa. Pamoja na jitihada zetu za muda mrefu bado tunapaswa tumsifu Bwana kwa msaada wake mkubwa kwetu dhidi ya maadui zetu. Tunaamini kuwa kupitia nguvu ya Roho Mtakatifu, Bwana atatupa ushindi na mafanikio makuu zaidi ya haya na atawafumba macho maadui zetu wazidi kulala ili mipango yetu yote ya kuibadilisha Zanzibar kidemografia ifanikiwe katika kipindi kifupi kijacho. 


Mafanikio yetu yameenea katika kila upande - katika uchumi, siasa, huduma za jamii, umiliki wa ardhi, ujenzi, elimu na kadhalika ili kupata picha kamili ni vyema tuorodheshe kwa ufupi mafanikio hayo:
Nafasi yetu kwa upande wa elimu imekuwa ya kuridhisha kupitia nafasi za serikali. Hivi sasa ni rahisi na limekua jambo la kawaida katika kila matangazo ya wito wa masomo kusikia majina ya Wakristo. Kati ya vijana 7 hadi 10 ni lazima upate vijana wawili hadi watatu kutoka katika makanisa yetu.


Sambamba na matangazo ya elimu, vijana wetu wamekuwa wanapata nafasi nyingi za ajira katika serikali ya Zanzibar. Hali ya kutoelewana kisiasa baina ya Wazanzibari imetoa mwanya kwetu kuingiza vijana wa Kikristo wenye asili ya bara kwa wingi kwani wamekuwa wanaaminika zaidi kuliko vijana wa Zanzibar. Hali tulioieleza juu imetuwezesha kuwa na Wakristo wengi katika nafasi za juu serikalini na katika chama tawala. Hali hii ni lazima iendelezwe katika ngazi zote kwani ndiko kunako mambo mengi ya kila siku.


Tumepata fursa ya kutumia 


Taasisi za serikali kwa uendeshaji wa ibada zetu. Hali hii imefanya tuzidi kukubaliwa na Waislamu na kuvumiliwa na inaweza kutupa nafsi ya kuwavuta katika NENO LA BWANA Kwa upande wa mashamba (vijijini) tumepata wasaa mzuri wa kununua ardhi toka kwa Waislamu ambao hadi sasa bado hawajashtuka. Ardhi hizi zimetuwezesha kujenga makanisa kadhaa ambayo hapo awali hayakuwepo. Idadi ya skuli na vituo vyetu (ambavyo licha ya picha ya juu kuwa haviendeshwi kwa misingi ya Kikristo lakini kiukweli ni vituo vya kimisionari) vimeongezeka kwa hali ya kuridhisha. Skuli hizi ni kuanzia kwa watoto wadogo hadi vituo kama hichi kilichopo mji mkongwe (Stone Town Youth Centre) na zinafanya kazi vizuri katika kupandikiza mila za Kikristo.

Sera zilizopo hivi sasa kwa upande wa uingiaji na utokaji 


Zanzibar imetusaidia sana katika uingizaji wetu (Wakristo) kutoka Bara na hivyo kusaidia kufuta ile imani ya kuwa Zanzibar ni kisiwa cha Waislamu eti Wazanzibari kwa zaidi ya asilimia 99 ni Waislamu.  Ujaji wa Wakristo kwa wingi kutoka Bara umewezesha kuongezeka kwa idadi ya mabaa na kilabu za pombe. Hivi sasa ni jambo la kawaida kuona magari ya aina mbalimbali yanayomilikiwa na eti Waislamu yamebeba kreti za bia na pombe kali.

Kujiingiza kwetu katika taasisi za dola katika ngazi za mitaa kumetuwezesha kupata nafasi ya kutangaza Ukristo kwa njia ya mihadhara na wakati huo huo kudhibiti mihadhara ya wazi ya Waislamu kwa kutumia madai ya kashfa na kutatanisha maelewano mazuri baina ya watu wa dini tofauti. Tumefanikiwa kupata viwanja vingi katika maeneo ya mjini ambayo yangali mapya. Maeneo haya ni kama Tomondo, Mombasa,
Mwanakwerekwe na kadhalika ambayo tayari tumeshajenga makanisa yetu ingawaje kwa sasa hayajawa na waumini wengi wa kuyatumia na bado yanaonekana ni matupu.


Ndugu wapendwa katika Bwana,  


Mafanikio hayo yasitufanye tukalewa na kusahau jukumu la kanisa la kuona kuwa utawala wa Bwana unashuka Zanzibar haraka iwezekanavyo. Kosa lolote utakalofanya hivi sasa litaweza kuturudisha hatua kadhaa na huenda nafasi hii tuliyonayo hivi sasa tusiipate kwa karne
mpya ijayo. Mambo ya kufanya yanayotukabili ili kuimarisha nafasi yetu ni kuona yale tuliyokwisha yapata hayatutoki na kuyafanya dira kwa karne ijayo ni haya yafuatayo:


Tusahau tofauti zetu dhidi ya adui  


Ingawaje tupo madhehebu nyingi lakini tunawajibika kuelewa kuwa Waislamu na Uislamu wao ni adui yetu namba moja ambaye hatutofaulu kupambana nae mmoja mmoja. Uislamu hapa Zanzibar ni dini iliofungamana na mila na utamaduni hivyo kila itakavyowezekana tusahau tofauti zetu ndogo ndogo na hata kubwa kukabiliana nao, vingienvyo tutarudi kama wakati wa Karume.

Tuhakikishe tunapata ardhi  


Hii ni mbinu kongwe katika usambazaji wa Ukristo. Wazee wetu walipoleta Ukristo Zanzibar na katika Afrika, jitihada waliyofanya ni kupata ardhi kuwa kwa ajili ya ujenzi wa maeneo yetu, majengo ya hospitali, shule, zahanati na vituo vya chekechea, makanisa na kadhalika. Tunahitaji ardhi kubwa ili kuziweka huduma hizo mahala pamoja kwa ajili ya kueneza injili ya Bwana na Muokozi wetu.

Tununue nyumba na viwanja kwa ujenzi wa Makanisa 


Inaonekana Waislamu wenye siasa kali na baadhi ya watendaji kwenye serikali wameanza kushtuka na ongezeko kubwa la makanisa katika kisiwa cha Unguja. Kuna dalili kuwa tunaweza kupata ugumu katika kupata viwanja kwa ajili ya makanisa. Njia tunayoweza kuitumia kwa muda huu ni kununuwa viwanja vitupu au nyumba za Waislamu kwa bei kubwa itakayowashawishi kuziuza na baadaye tukaweza kuvijenga au kugeuza nyumba hizo kuwa makanisa.

Tujenge shule na hospitali kwa wingi  


Hizi ni taasisi ambazo tunaweza kueneza neno la Bwana kwa Waislamu walio wengi hapa Zanzibar. Kwa kutumia umaskini unaowakabili wengi ya Wazanzibari na uchache wa huduma hizo tunaweza kujitangaza vizuri, tujitahidi kutoa huduma nzuri kuweka vifaa vya kisasa kuweka bei ndogo, kuweka upendo ili vituo vya Waislamu au hata vile vya serikali visiweze kuvikaribia vyetu. Shule ni sehemu muhimu ya kupandikiza mafundisho yetu zaidi kwa watoto wadogo (Nursery).

Tunadai muda zaidi katika vyombo vya habari (TV na Radio) 


Kwa muda mrefu sasa Uislamu na Waislamu wamehodhi vyombo hivi vya habari mbali na kuwa siku ya Ijumaa ambayo yote humilikiwa na vipindi vya Kiislamu vyombo hivyo hutenga siku nyingine kadhaa kwa vipindi vya Kiislamu na hata kuthubutu kutia adhana kila wakati wa sala hali hii inaudhi na inatoa picha ya wazi ya serikali kupendelea Uislamu ingawaje inadai kuwa haina dini. Wakati wa kusherehekea miaka 25 ya TVZ tulizungumzia suala hili lakini halikupata mtu wa kulifanyia kazi. Sasa tuhakikishe kuwa Ukristo unapata muda zaidi katika vyombo hivyo au Uislamu nao upunguziwe nafasi.

Tuongeze mhadhara wa wazi  


Wakati Waislamu wamezuiliwa kufanya mihadhara ya wazi, sisi tujitahidi kuhakikisha kuwa mihadhara yetu inaongezeka kwa kiwango kikubwa. Kwa kuwa Waislamu hawahudhurii mihadhara hiyo, lazima tuone Wakristo wa mjini na mashamba wanahamasishwa na kupatiwa nyenzo ili kuhudhuria. Vipaza sauti vitumike kuhakikisha kuwa neno la Bwana linafika kila pahala. Mihadhara ifanyike karibu na nyumba, Misikiti na kwenye viwanja vya wazi.

Tuendelee kutumia shule na sehemu za umma  


Ili kuwafanya Waislamu watuzoee na kuondosha chuki yao kwetu ni lazima kuendelea kutumia mashule na sehemu za umma zilizo wazi kwa mambo yetu ya ibada kwa kipindi kirefu hali hii inaweza kuwafanya washindwe kuona tofauti yetu na wao. 

Tufanye suala la uhamiaji Zanzibar kuwa jepesi 

Uzoefu unaonesha kuwa ni jambo gumu kuwabatiza Wazanzibari Waislamu. Hali hii inafanya ongezeko la Wakristo kuwa dogo au halipo kabisa ukitoa wale wanaozaliwa katika familia za Kikristo.  Njia pekee ya kuhakikisha ongezeko la makanisa na taasisi zetu ni kuongezeka kwa Wakristo. Jambo hili litawezekana kwa kuingiza Wakristo wengi kutoka Tanzania Bara au wapagani ambao tutaweza kuwabatiza kwa kutumia udugu wetu wa kikabila au asili ya Bara. Kwa kuwatumia ndugu zetu waliomo serikalini (SMZ au SMT) tuhakikishe kuwa suala la uhamiaji linabakia wazi na rahisi na linaendelea kwa kila hali.

Tuzuie jaribio lolote la kadi za uraia au vitambulisho 


Wakrsito tunapaswa kuelewa kuwa iwapo serikali ya Zanzibar itaamua kufanya chochote ili, kuwa na vitambulisho au kadi za uraia kwa Wazanzibari basi jambo hilo litaathiri sana mipango yetu ya muda mrefu kwa Zanzibar. Jitihada zozote za kuiimarisha Zanzibar kama Zanzibar na nje ya Utanzania ni lazima tuelewe kuwa Uislamu utapata nguvu na kuwa tishio kwa hapa Zanzibar na hata Bara. Iwapo tutawajibika kuunga mkono ni kadi za Uraia na vitambulisho vya Watanzania kwa ujumla na sio Zanzibar peke yake.

Tujipenyeze na kushika nafasi muhimu  


Lazima tuelewe kuwa chama chochote cha siasa kinalenga kukamata serikali ili kiweze kutekeleza yale yanayoaminika kuwa mazuri kwa chama hicho. Tunapozungumzia vyama vya siasa kwa Zanzibar tunahusisha zaidi kwenye CCM na CUF. Watu wetu wamefaulu kuingia kwa wingi katika chama tawala na katika jumuiya zake.

Tuunge mkono sera za utalii 


Hadi sasa wengi wa watalii wanaoingia Zanaibar hutokea nchi za Kikristo. Desturi za watalii hupingana na zile za Kizanzibari na hata za Kiislamu. Watalii wanasaidia kuongezeka kwa mabaa na vivazi ambavyo Waislamu wanataka visivaliwe hasa na wanawake. 

Uwafuate Wakristo waliosilimu ili warudie Ukristo 
Watu wa aina hii wanakuwa bado hawajatulia na mara nyingi huwemo katika matatizo. Pana haja ya kuwalenga watu hawa ili kuwarudisha kabla hawajatulia au kupata elimu nzuri. Matatizo yao ndipo mahala pa kuanzia ili Bwana atawateremshie roho ya utulivu. Uzima wa Ukristo ni kuwa na wafuasi wengi kadiri iwezekanavyo. Tuwafuate wanawake kwa misaada  Jumuiya zisizo za kiserikali zinaungwa mkono duniani kote na hasa zile za wanawake na watoto tujiweke pamoja ili tuweze kuwavutia kwa jina la kuwasaidia.

Tuongeze vituo vya mafunzo ya Kikristo 


Kituo cha vijana cha mji mkongwe (Stone Town Youth Center) kimekuwa kikifanya kazi yake vizuri kwani hadi sasa lengo lake la ndani bali halijaeleweka na vijana wanaohudhuria hapo kwa shughuli mbalimbali, jitihada zifanyike ili kuwa na vituo vya aina hii katika maeneo mengine. Lengo kuu liwe ni vijana na wanawake bila ya kuonesha dalili za kidini. Tuwaoe wanawake wao kwa kusilimu kimajina  Jitihada za makusudi zifanyike ili kila itakapowezekana kuwaoa wanawake wa Kiislamu ili tuweze kuwabatiza baadae, njia nzuri iwapo patakuwa na ugumu ni kusilimu kiuongo ili kuruhusiwa kuwaoa wanawake wao.

Tuanzishe NGOs na sisi tuwe viongozi  


Kwa kuwa hivi sasa wafadhili wengi wameonesha hamu ya kuzisaidia NGOs moja kwa moja badala ya serikali ni lazima tujitahidi kuunda jumuiya zetu ambazo zitawashirikisha Waislamu lakini uongozi wa juu ni lazima uwe mikononi mwetu. Hii itatuwezesha kuona sera zetu na malengo yanatelekezwa kwa kivuli hicho. 

Tujenge ukaribu na viongozi ili kuwadhibiti 

Waislamu  Mambo yetu mengi yamekuwa yanakwenda vizuri katika maeneo mbalimbali baada ya wenzetu kuwemo katika kamati za masheha, na matawi ya vyama, na kamati za maendeleo za maeneo mbalimbali. Hali hii ni lazima iongezeke ili udhibiti wa shughuli za Waislamu uwe mzuri zaidi na wakati huo huo kuona kuwa mambo yetu yanakwenda yakiwa na baraka ya vyombo vya dola na vyama vya siasa.

Tuwachonganishe Mashehe wenye msimamo mkali  


Mashehe wenye misimamo mikali wamekuwa ni tatizo kwa Ukristo kwani wana wafuasi wengi na wamekuwa wakisema wazi na kushutumu maendeleo yetu. Mashehe hao ni lazima wachonganishwe na serikali ili hali ikiruhusu wazuiliwe kuendesha shughuli zao. Wakati tukifanya hivyo hatuna budi kuwaunga mkono Mashehe wote ambao wamekuwa wakitusaidia kwa njia mbalimbali. 

Tulenge kuifuta Tabligh  

Pamoja na kuwa na Tabligh sio hatari moja kwa moja kwa Ukristo lakini bado inastahili kupigwa vita kwa sababu ina aina pekee ya mihadhara ya Waislamu inayoruhusiwa humu Zanzibar. Tabligh inaweza kuwazindua baadhi ya Waislamu ambao ni vema kubaki bila ya kuzinduliwa.

Tudai turudishiwe taasisi zetu  


Serikali ya Zanzibar bado inaonekana kuwa ngumu katika milki ya makanisa, ardhi na taasisi zetu. Dalili za huko nyuma zilionekana nzuri kwani tulifanikiwa kupata hospitali yetu Walezo na eneo la Kiugani hata hivyo panakuwepo na ugumu wa kurudishwa shule zetu. Kwa kuwatumia wenzetu waliomo serikalini na baraza la wawakilishi tuzidishe harakati na madai ya taasisi zote zilizobaki.  

Tulete waumini kutoka mashamba kuanza makanisa

Hivyo sasa pameibuka wasi wasi kuhusiana na wingi wa makanisa ambayo hayajapata waumini wa kuyajaza. Ili kuficha dosari hii na hoja kadhaa utaratibu uliopo hivi sasa chini ya baadhi ya makanisa ni lazima uungwe mkono. Wakristo wahamiaji wengi hufikia mashamba hivyo pawekwe na utaratibu wa kuwaleta mjini ili kujaza makanisa.


Neno la mwisho


Wapendwa katika Bwana.  


Miongozi hii ni mikubwa na inaweza kuwatisha baadhi ya waumini wa Kikristo hasa wale ambao bado hawajampokea Roho Mtakatifu vizuri. Hata hivyo, kwa uwezo wa Bwana Mungu wetu ni mpango rahisi. Suala la muhimu ni haya kufahamika na kila Mkristo apendae kumtumikia Bwana. Pia hatuna budi kuishukuru awamu ya nne ya serikali ya Mapinduzi ambao imefungua milango kwa Ukristo na kushuhudia ongezeko la makanisa. Bwana awe nasi!
--
SOURCE:  Jukwaa la www.mwanabidii.com

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni