Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumatatu, Oktoba 15, 2012

INAUMIZA SANA

 
Jamii ni namba moja (kaya na wakazi ktk eneo) cha pili ni serikali. Kwani serikali ni nani? Hata vijijini porini watu hutumia video kama kipato na burudani nako kuna uovu pamoja na kuwa na wazee wa mila.Nishati mbadala (solar power) kwa sasa, betri na generator za umeme zimefanikisha haya.Machimboni ndio balaa watoto huona makubwa maana video na mapombe huko hatari.  
Ukiwa vijijini, ukiuliza matatizo makuu ya wananchi kijijini hapo linakuwa mojawapo kati ya makubwa ni 'watu wazima na watoto wadogo kuangalia video za mapenzi (matusi)'. Pamoja na za kuonyesha mpira za mapenzi ni mojawapo. Uliza kwa nini huwa hivyo, wazee wa mila wapo? Viongozi jee, watumishi wa umma.....? Kama watu wana mila zao na dini zao za maadili na wanafanya hivyo, utahitaji polisi na social welfare workers wangapi kukagua nyumba hadi nyumba mtaani, kitongojini maporini kijijini haya yasitokee. 
Kama madhara wanayajua na wanaona ni tatizo-wazazi, wazee wa mila wapo wapi? Apangishaye nyumba na kuweka bar mtaani na vilabu vya pombe ktk makazi na dangulo ni mzazi. Na akataae kuchanga hela 500 kwa wiki au kulipia uchafu 100/= directly kwa gari la uzoaji taka ni yule mwenye bar au mama ntilie, saluni ya nywele ambae hutupa malundo ya uchafu usiku mtaroni au barabarani au mwenye hoteli anayekataa kuunganisha katika sewer line anaunganisha usiku kiwizi mtaro wazi. yanajaa, yananuka na matakataka yanajazana kisha unaona ktk TV-serikali ije izibue, ituondolee huu uchafu unanuka, unatusumbua, unazalisha mbu. Mmefanya nini kuondoa tatizo-tumeita serikali haiji, tunateseka!! 
Ukienda na kampuni hapo kuvunja maunganisho ya mambomba hayo kuziba yamwakigie huko yatokako-atatiririsha barabarani, atakayemfuatilia kumshitaki-atatolewa bastora baada ya muda ataokotwa maiti mtaroni. Ya video na vilabu mtaani nyumba hadi nyumba ni sisi, uchafu na chuki za visafi sheria inapochukua mkondo wake-ni sisi, rushwa na njia za mkato ni sisi-tutabadilika lini watanzania? 
Inaumiza sana.
Mungu atusaidie tubadilike.

Maoni 1 :

  1. Kweli inaumiza sana mkuu. Ni ombi tu, maandishi hatuyaoni kutokana na hii rangi nyeusi,na wengine haya majembe yamfungwa huwezi ku-edit, au kufanay lolote zaidi ya kusoma. Ila ujume umefika

    JibuFuta