Jamii
ni namba moja (kaya na wakazi ktk eneo) cha pili ni serikali. Kwani
serikali ni nani? Hata vijijini porini watu hutumia video kama kipato na
burudani nako kuna uovu pamoja na kuwa na wazee wa mila.Nishati
mbadala (solar power) kwa sasa, betri na generator za umeme
zimefanikisha haya.Machimboni ndio balaa watoto huona makubwa maana
video na mapombe huko hatari.
Ukiwa
vijijini, ukiuliza matatizo makuu ya wananchi kijijini hapo linakuwa
mojawapo kati ya makubwa ni 'watu wazima na watoto wadogo kuangalia
video za mapenzi (matusi)'. Pamoja na za kuonyesha mpira za mapenzi ni
mojawapo. Uliza kwa nini huwa hivyo, wazee wa mila wapo? Viongozi jee,
watumishi wa umma.....? Kama watu wana mila zao na dini zao za maadili
na wanafanya hivyo, utahitaji polisi na social welfare workers wangapi
kukagua nyumba hadi nyumba mtaani, kitongojini maporini kijijini haya
yasitokee.
Kama madhara wanayajua na wanaona ni tatizo-wazazi, wazee wa
mila wapo wapi? Apangishaye nyumba na kuweka bar mtaani na vilabu vya
pombe ktk makazi na dangulo ni mzazi. Na akataae kuchanga hela 500 kwa
wiki au kulipia uchafu 100/= directly kwa gari la
uzoaji taka ni yule mwenye bar au mama ntilie, saluni ya nywele ambae
hutupa malundo ya uchafu usiku mtaroni au barabarani au mwenye hoteli
anayekataa kuunganisha katika sewer line anaunganisha usiku kiwizi mtaro
wazi. yanajaa, yananuka na matakataka yanajazana kisha unaona ktk
TV-serikali ije izibue, ituondolee huu uchafu unanuka, unatusumbua,
unazalisha mbu. Mmefanya nini kuondoa tatizo-tumeita serikali haiji,
tunateseka!!
Ukienda na kampuni hapo kuvunja maunganisho ya mambomba
hayo kuziba yamwakigie huko yatokako-atatiririsha barabarani,
atakayemfuatilia kumshitaki-atatolewa bastora baada ya muda ataokotwa
maiti mtaroni. Ya video na vilabu mtaani nyumba hadi nyumba ni sisi,
uchafu na chuki za visafi sheria inapochukua mkondo wake-ni sisi, rushwa
na njia za mkato ni sisi-tutabadilika lini watanzania?
Inaumiza
sana.
Mungu atusaidie tubadilike.
Kweli inaumiza sana mkuu. Ni ombi tu, maandishi hatuyaoni kutokana na hii rangi nyeusi,na wengine haya majembe yamfungwa huwezi ku-edit, au kufanay lolote zaidi ya kusoma. Ila ujume umefika
JibuFuta