Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumatatu, Septemba 03, 2012

KUKABILIANA NA KUMBUKUMBU YA MAISHA YETU

PHOTO BY: African lens

 "Kazi ya kila mtu inachunguzwa mbele za Mungu na inaandikwa kama ni ya UAMINIFU ama ya KUKOSA UAMINIFU. Mbele yake kila jina katika vitabu vya mbinguni huandikwa kwa usahihi kabisa kila neno baya, kila tendo la uchoyo [ubinafsi], kila kazi isiyotimizwa, na kila dhambi ya siri, na kila unafiki uliofanywa kwa werevu.

Maonyo yaliyotumwa kutoka mbinguni na makaripio YALIYOPUUZWA, wakati uliopotezwa bure [kucheza karata, bao, n.k.], nafasi ambazo hazikutumiwa vizuri, mvuto uliotolewa kwa WEMA au kwa UBAYA, pamoja na matokeo yake yafikayo mbali, vyote hivi vinawekwa katika kumbukumbu zenye tarehe na malaika yule anayetunza kumbukumbu hizo.

HEBU TAFAKARI JAMBO LILILOTOKEA HIVI KARIBUNI:
WAANDISHI, WANANCHI DODOMA WALAANI MAUAJI YA MWANDISHI - Dodoma Yetu
This Day Magazine: Jukwaa la Sanaa lamkumbuka Mwandishi aliyeuawa Iringa

 Hali hii ni ya HATARI SANA kwa  wale ambao, wakiwa WAMECHOKA KUKESHA, wanageukia VISHAWISHI vya ulimwengu huu. Mathayo 24:42-5l. 

Wakati mtu wa BIASHARA amezama mawazo yake yote yako katika KUTAFUTA FAIDA, wakati MPENDA ANASA anaendelea kutafuta kujiridhisha katika hiyo, wakati BINTI WA MITINDO anapanga MAPAMBO yake ----- huenda ni katika SAA hiyo HAKIMU WA DUNIA YOTE atakapotamka hukumu hii, "UMEPIMWA KATIKA MIZANI [AMRI KUMI] NAWE UMEONEKANA KUWA UMEPUNGUKA." Danieli 5:27.

Maoni 1 :