Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumatatu, Machi 12, 2012

Inaitwa: Hamasa ya 9 Dey.



Mnamo tarehe 9 Dey mwaka 1388 Hijria Shamhsia iliyosadifiana na Disemba 30 mwaka 2009 kulijiri tukio kubwa na la kihistoria nchini Iran ambalo lilikuwa jibu kwa mirengo potofu baada ya uchaguzi wa 10 wa rais nchini. Tukio hilo lilikuwa hamasa ya kudumu ya busara, ufahamu na mwamko wa taifa la Iran mbele ya njama na fitina za ndani na nje ya nchi. 

Uchaguzi wa rais wa Juni 2009 nchini Iran ulikuwa nukta muhimu katika uga wa uchaguzi nchini Iran. Asilimia 84 ya wapiga kura walishiriki Katika uchaguzi huo usio na kifani. Tukio hilo lililojiri wakati wa kuanza muongo wa nne wa Mapinduzi ya Kiislamu, liliashiria kuwa mfumo wa Kiislamu nchini Iran unamilikiwa na wananchi.Tukio hilo lilivuruga kabisa njama za Marekani za kuwachochea Wairani wasishiriki katika uchaguzi na kuitenga Iran kimataifa. 

Hivi karibuni Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani alibainisha wazi njama za Washington dhidi ya Iran pale alipohojiwa na BBC ya Kifarsi na kutangaza rasmi kuwa Marekani ilijaribu kuunga mkono mrengo wa fitina nchini Iran. Kwa hivyo tunaweza kusema kuwa Hamasa ya tarehe 9 Dey inapaswa kuzingatiwa kwa kina kwa mitazamo yote kama harakati ya kudumu ya kujitolea ya wananchi yenye athari za kudumu. 

Habari hii, ili upate mengi zaidi soma... HAPA.

Maoni 1 :

  1. Wenzetu wametuzi sana,unajua hata hapa bongo wameshajua nani atakuja kuwa raisi...

    JibuFuta