Mnamo tarehe 9 Dey mwaka 1388 Hijria Shamhsia iliyosadifiana na Disemba
30 mwaka 2009 kulijiri tukio kubwa na la kihistoria nchini Iran ambalo
lilikuwa jibu kwa mirengo potofu baada ya uchaguzi wa 10 wa rais nchini.
Tukio hilo lilikuwa hamasa ya kudumu ya busara, ufahamu na mwamko wa
taifa la Iran mbele ya njama na fitina za ndani na nje ya nchi.
Uchaguzi
wa rais wa Juni 2009 nchini Iran ulikuwa nukta muhimu katika uga wa
uchaguzi nchini Iran. Asilimia 84 ya wapiga kura walishiriki Katika
uchaguzi huo usio na kifani. Tukio hilo lililojiri wakati wa kuanza
muongo wa nne wa Mapinduzi ya Kiislamu, liliashiria kuwa mfumo wa
Kiislamu nchini Iran unamilikiwa na wananchi.Tukio hilo lilivuruga
kabisa njama za Marekani za kuwachochea Wairani wasishiriki katika
uchaguzi na kuitenga Iran kimataifa.
Habari hii, ili upate mengi zaidi soma... HAPA.
Wenzetu wametuzi sana,unajua hata hapa bongo wameshajua nani atakuja kuwa raisi...
JibuFuta