Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumatatu, Machi 12, 2012

Kutafuta habari kwenye Mtandao – Teknolojia mpya ya Habari

Kwa wengi, ulimwengu sasa umekuwa kama kijiji. Watu wanawasiliana kupitia barua-pepe, mitandao ya kijamii au hata simu za mkononi. Noa Bongo inapigia mbizi suala la Teknolojia ya kisasa ya mawasiliano Ulimwenguni.


Je wewe huwasiliana na jamaa zako nchini Marekani? Je umewahi kutoa maelezo yako mafupi kwenye mtandao wowote wa kijamii? Au je, hutumia mtandao wa Intaneti kufanya utafiti wa kazi zako?
Katika sehemu nyingi Barani Afrika, ukosefu au huduma duni na za pole pole za mtandao wa Intaneti bado ni kikwazo na tatizo kubwa kwa watumiaji wake. Lakini sasa bara hili limo mbioni kurekebisha hali hii.

Na hii ndio sababu Noa Bongo inajaribu kulipigia mbizi suala hili ili kutoa mwangaza zaidi kuhusu matumizi ya teknolojia hii mpya. Kupitia mchezo wa redio, tunasikia hadithi kuhusu kundi la vijana wanaoamua kijitosa katika biashara ya kutoa huduma za teknolojia hii mpya ya mawasiliano. Sikiliza upate kufahamu masaibu yanayowakumba baada ya kuanzisha mkahawa wao wa kutoa huduma hizi za intaneti.

Vipindi vya “Learning by Ear” ‘Noa bongo Jenga Maisha yako, vinasikika katika lugha zaidi ya sita ikiwa ni lugha ya Kiingereza, Kifaransa, Kiswahili, Kihausa, Kireno na Kiamharik. Na vinafadhiliwa na wizara ya mambo ya nchi za kigeni ya Ujerumani.


Una Nyongeza Kuhusu Teknolojia Habari.



Maoni 1 :