Mfano wa maada mango ni jiwe la mwamba, maada kiowevu ni maji, na
maada gesi ni hewa. Hivyo plasma ama utegili ni hali ya nne ambayo si ya
asili katika maisha yetu ya kila siku. Huonekana katika mifumo ya
kimaada iliyo katika joto kali.
Plasma ni hali halisi ya jua.
Lenyewe linafanyika na maada lakini si tena katika hali ya kawaida
tunayoijua hapa duniani. Nayo ni kama gesi inayolipuka masaa yote na
kufanya mnururiko wa nishati inayotufikia kama joto, mwanga na pia
mawimbi ya plasma itufikiayo na kujidhihirisha kama aurora katika ncha ya kaskazini ya Dunia.
Ikiwa gesi ni ya joto kali sana elektroni zake zinaanza kuachana na atomu zao. Tabia ya hali hii ni tofauti na hali ya gesi yenyewe. Elektroni zisizoshikwa na atomu pamoja na atomu hizo katika hali ya ioni zote zinajibu kwa uga wa sumakuumeme.
Asilimia kubwa ya maada ulimwenguni iko katika hali ya utegili kwa sababu imo ndani ya nyota za angani. Kwa ajili ya matumizi ya mitambo hali ya utegili yaani ya kuionika husababishwa pia kwa leza au kwa uga wa sumakuumeme.
Utegili pia: plasma katika lugha ya fizikia, ni hali ya nne ya maada. Hali hiyo ni kama gesi ila ni ya kiioni. Nyinginezo ni hali mango (imara), kiowevu (majimaji) na gesi (kama hewa).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni