Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumamosi, Februari 04, 2012

MAJIBU YAFANYANYAYO KAZI....MIBARAKA YA KUTUCHANGAMSHAJinsi zilivyo nyingi fadhili zako ulizowawekea wakuchao; 
Ulizowatendea wakukimbiliao mbele ya wanadamu! Zaburi 31:19. 
Mungu anaimwaga mibaraka yake katika njia yetu yote ili kuifanya safari yetu iwe ya
furaha na kuiongoza mioyo yetu kumpenda na kumsifu, Naye anatutaka sisi kuteka maji
yetu katika visima vya wokovu ili mioyo yetu ipate kuburudika. Twaweza kuimba
nyimbo za Sayuni, twaweza kuichangamsha mioyo yetu sisi wenyewe, tena twaweza
kuichangamsha mioyo ya wengine; tumaini letu laweza kuimarishwa, na giza kugeuzwa
kuwa nuru. Mungu hajatuacha sisi katika ulimwengu huu wa giza ----- kama wasafiri na
wageni watafutao nchi iliyo bora, ile ya mbinguni ----- pasipo kutupa sisi ahadi zake za
thamani ili kuufanya kila mzigo mzito tuliobeba kuwa mwepesi. Kingo za njia yetu
zimepambwa kwa maua mazuri ya ahadi zake. Yanachipua pande zote yakitoa harufu
nzuri sana. ----- Letter 27, 1886.

Ni mibaraka mingapi tunayoipoteza kwa sababu tunaidharau na kuipuuza kutoitilia
maanani mibaraka tunayopokea kila siku, tukiitamani sana ile ambayo hatunayo kwa
sasa. Fadhili za kawaida ambazo zinamwagwa huku na huko katika njia yetu
zinasahaulika na kuthaminiwa kidogo tu. Twaweza kujifunza mengi kutoka kwa vitu vya
kawaida katika viumbe vya asili. Ua lililo mahali penye giza na palipo duni hupokea
mwanga wote linaoweza kuupata, na kutoa majani yake. Ndege aliyefungiwa katika
kitundu anaimba katika kitundu cha gereza lake, ndani
ya nyumba zisizopata mwanga wa jua, kana kwamba yuko katika jengo la kimwinyi,
lenye mwanga wa jua. Mungu anajua iwapo sisi tutaitumia mibaraka yake kwa hekima na
kwa vizuri; kamwe hataweza kutupatia mibaraka hiyo ili tupate kuitumia vibaya.
Mungu anaupenda moyo wenye shukrani, unaoyasadiki kabisa maneno yake yenye ahadi,
ukijikusanyia faraja na tumaini na amani kutokana nayo; Naye atatufunulia sisi vina
virefu zaidi vya upendo wake. ----- RH, Aprili l2, 1887.
  
  

Endapo tungelisifu jina takatifu la Mungu kama ipasavyo, basi, mwali wa moto wa
upendo ungewashwa ndani ya mioyo mingi.... Sifa kwa Mungu inapaswa kuwa mioyoni
mwetu daima na vinywani mwetu. Hii ndiyo njia iliyo bora sana ya kulipinga jaribu lile
la kushiriki katika maongezi yasiyofaa na ya upuuzi. ----- Letter 42, 1900.

Bwana angependa sisi tuwe tunatazama juu, na kuwa na shukrani kwake kwamba
mbingu iko.... Hebu na tuzishikilie sana kwa imani hai ahadi nyingi sana za Mungu, na
kuwa na shukrani kuanzia asubuhi mpaka usiku. ----- RH, Aprili 12, 1887.

********************************
Ngoja nikwambie msomaji wangu jambo hili, kwamba:
MAJIBU YAFANYAYO KAZI ni kipengele kinachoongelea masuala ya kiroho zaidi.

Kwa sababu ya upekee na unyeti wa siku, Sio vibaya tukibadilishana mawazo na kuambizana yaliyomuhimu katika maisha hasa ya kiroho.
Na huu utakuwa ni mfululizo kwa kila siku kama hii ya leo...
(Namaanisha JumaMosi)

Pamoja na kwamba weeengi wanaamini hii ni kweli, lakini kweli halisi jionee mwenyewe ambapo

Miami Temple Seventh-day Adventist Church

Inapotuletea: Divine Service - Sermon 10-22-11

SABATO NJEMA MKUUHakuna maoni:

Chapisha Maoni