Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumatano, Februari 01, 2012

Katika historia zilitokea.

Tufahamu kwamba, utumwa ni mfumo unaotoa fursa kwa binadamu kummiliki binadamu mwenzake kama mali yake. Binadamu anayemilikiwa anakuwa na hadhi sawa na chombo au kifaa chochote kinachoweza kuuzwa. Mfumo huu ulikuwa maarufu kabla ya harakati za ukoloni duniani mathalani karne ya 15 ambapo watumwa walihitajika katika shughuli za kilimo na uchimbaji madini katika sehemu mbalimbali za ulimwengu. Mfumo huu huunda matabaka ya "mabwana" ambao humiliki watumwa na "watwana" ambao ni watumwa wenyewe. Kwa nini nakwambia haya? Hebu endelea kusoma hapo chini

Kuna utumwa tofautitofauti, kivipi:


Katika historia zilitokea. Kulikuwa na utumwa wa muda (yaani mtu huwa mtumwa kwa miaka kadhaa) au kwa maisha yote. Kulikuwa na utaratibu ambako watoto wa mtumwa walikuwa watumwa tena hivyo kuzaliwa watumwa; kulikuwa pia na utaratibu ya kwamba watoto wa watumwa walitazamiwa kama watu huru.

Kulikuwa na jamii ambako watumwa hawakuwa na haki kabisa yaani mabwana waliweza kuwatendea jinsi walivyotaka (vyovyote vile utavyojisikia kutenda) hata kuwaua lakini kulikuwa pia na jamii zilizojua haki fulani za watumwa; watumwa waliweza kuwa na mali ya binafsi na kwa njia hii hata kununua uhuru wao kutoka kwa mabwana. Watumwa katika utumishi wa watawala waliweza kupata nafasi muhimu katika jamii; mfano ni wamameluki wa Misri waliokuwa watumwa wanajeshi wakatawala nchi hii kwa karne kadhaa…hizi habari ukuzifuatilia zinauma!!!

Chanzo cha utumwa

Ni hivi; kilikuwa yaani kutokana mara nyingi ama vita ama madeni. Vitani wafungwa wakauzwa kama watumwa wakihesabiwa kama sehemu ya uwindo wa washindi. Sababu kuu nyingine ilikuwa madeni ya watu waliokamatwa na kuuzwa ili madeni yalipiwe kwa njia hii. Mahitaji wa kiuchumi kwa watumwa wengi yalisababisha biashara ya watumwa.


Biashara ya watumwa ni nini sasa:


Msomaji wangu!!, biashara ya watumwa ni biashara inayohusu watumwa yaani watu wasio huru wakitazamiwa kuwa mali ya wengine. Katika historia ilitokea mara nyingi. Uchumi wa Roma ya Kale ilitegemea watumwa waliokamatwa na kusafirishwa kati ya pande zote za mazingira ya Bahari Mediteranea. Milki za makhalifa wa Uislamu ziliendelea kutegemea watumwa. Waosmani walichukua watoto wa kikristo kutoka nchi za Balkani na kuwapeleka kama watumwa katika sehemu za kusini za milki yao kama Misri walipofanya kazi za wanajeshi.

Mahitaji ya uchumi wa kimataifa tangu karne ya 15 yalisababisha kuongezeka kwa biashara ya watumwa hasa kutoka Afrika; mamilioni walikamatwa na watawala wa milki kwenye pwani za Afrika na kuuzwa kwa wafanyabiashara wazungu waliowapeleka Amerika walipohitajika kwa kazi kwenye mashamba makubwa ya miwa na pamba,,, hebu piga picha.

Biashara hii ilianza kupingwa tangu mwisho wa karne ya 18; Mkutano wa Vienna (1814-15) ilikuwa na nia na ndio chanzo cha mapatano ya kwanza ya kimataifa yaliyolenga kukataa biashara ya watumwa kutoka Afrika. Hata hivyo yaliendelea kwa miaka kadhaa hasa upande wa bahari Hindi ambako wafanyabiashara kama Tippu Tip waislamu waliendelea kukamata watumwa na kuwapeleka pwani.

Ukoloni ulimaliza biashara hii pia kwa njia gani.


Tangu karne ya 20 utumwa na pia biashara ya watumwa zimepigwa marufuku katika mapatano ya kimataifa chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa (japo haijaisha). Lakini miaka za nyuma imeona biashara mpya inayotumia nafasi za usairi wa kisasa; hata kama hakuna utumwa kisheria tena duniani ni hasa wanawake na mabinti wanaouzwa kwa kazi haramu ya ukahaba kati ya nchi na nchi.


Utumwa Kiroho.


Nabii Isaya anaagua neno hili la Mungu wakati Waisraeli wako utumwani. Wana mashaka na wanamlalamikia Mungu maana muda unapita na Mungu hatekelezi ahadi yake. Hatimaye Mungu anaibua kati yao, nabii Isaya awatie moyo akiwakumbusha kuwa ahadi za Mungu ni za milele, hazibadiliki. Anawafundisha kwa kutumia mfano wa mvua inyeshayo kuwa mara inyeshapo hairudi angani bali hurutubisha ardhi ili iweze kuzaa matunda. Kumbe ahadi ya Mungu ya kuwatoa katika utumwa wa kiroho na kimwili haitasimama kamwe na wala haibadiliki. Ndiyo kusema, neno la Mungu tulilolipokea halitarudi bure bali litazaa matunda.

Maoni 1 :

  1. historia iliyoandikwa vitabuni, ina mashaka, historia yenyewe imeandikwa na wakoloni

    JibuFuta