Mtayarishaji

Morning Star Radio

Alhamisi, Februari 09, 2012

HATARI KUBWA MBELE YETU



Bibi White anakielezaje kipindi kile cha dhiki kinachoujia ulimwengu wetu?







(1) "Hatari Kubwa ya Kuogofya."

 "Kazi ambayo kanisa limeshindwa kufanya katika kipindi hiki cha amani na usitawi, litapaswa kuifanya katika kipindi cha hatari kubwa ya kuogofya, chini ya mazingira ya kukatisha tamaa sana, yaani, ya kuogofya sana." Ev.31; 5T 463.






(2) "Hatari Kubwa ya Mwisho."


a. "Katika kipindi hiki cha maovu yanayotapakaa kila mahali tunaweza kujua ya kwamba hatari kubwa ya mwisho imekaribia. Wakati uasi juu ya Sheria ya Mungu utakapokuwa umeenea karibu katika ulimwengu wote, watu wake watakapokuwa wanakandamizwa na kuteswa na wanadamu wenzao hapo ndipo Bwana atakapoingilia kati." COL 178.


b. "Maafa katika nchi kavu na baharini, hali ya kutotulia ya jamii, tetesi za vita, hutuonya juu ya mambo mabaya yatakayotokea mbele. Hubashiri matukio yanayokuja ya kiwango kikubwa mno. "Mawakala wa uovu wanayaunganisha majeshi yao na kuyaimarisha. Wanajizatiti kwa hatari kubwa ile ya mwisho. Mabadiliko makubwa yatatokea mara moja katika ulimwengu wetu, na mabadiliko yale ya mwisho yatakuwa ya haraka-haraka." 9T 11.






(3) "Pambano la maana sana" la vizazi."

 "Hatari kubwa inawangojea watu wa Mungu. Hatari inawangojea walimwengu. Pambano la maana sana la vizazi vyote ndio kwanza liko mbele yetu." 5T 711.






(4) "Hatari ya Vizazi Vyote.

" Tunasimama mlangoni mwa hatari ya vizazi vyote. Kwa mfuatano wa haraka hukumu za Mungu zitakuja moja baada ya nyingine ----- moto, na mafuriko, na tetemeko la nchi, pamoja na vita na umwagaji wa damu. Hatupaswi kushangazwa wakati huu na matukio makuu na ya kukata maneno; maana malaika wa rehema hawezi kuendelea kwa muda mwingi zaidi kuwakinga wale wasiotaka kutubu." PK 278.






(5) Hatari kubwa sana tangu wakati ulipoanza kuwako.

"Tunaukaribia wakati ambao, zaidi ya wakati mwingine wo wote uliopita tangu kuwako kwa ulimwengu huu, utataka kujitoa wakf kikamilifu kwa kila mmoja aliyepata kulitaja jina lake Kristo." GW 323.






(6) "Hatari Kubwa Sana."

"Wakati huu wa sasa ni wakati wa kusisimua mno kwa wote wenye uhai. Watawala na viongozi wa siasa, watu wanaovikalia vyeo vyenye dhamana na mamlaka, wanaume na wanawake wanaotafakari sana wa tabaka zote, mawazo yao wameyakaza juu ya matukio yanayotokea kutuzunguka. Wanaangalia uhusiano uliopo miongoni mwa mataifa. Wanachunguza nguvu inayoingia katika kila kitu cha asili [ardhi, hewa, moto, maji], nao wanatambua ya kwamba jambo fulani kubwa na la kukata maneno li karibu kutokea, ----- ya kwamba ulimwengu huu umefikia ukingoni mwa hatari kubwa sana." PK 537; Ev 703,704, Ed 179.






(7) "Dhoruba."


a. "Dhoruba inaanza kuja ambayo itaupotosha na kuujaribu msingi wa kiroho wa kila mmoja wetu kufikia upeo wake." 5T 129.


b. "Dhoruba inakuja, ina ghadhabu isiyo na huruma. Je! tumejiweka tayari kukabiliana nayo?" 8T 315.



(8) "Tufani."


a. "Mungu amefunua kile kitakachotokea katika siku zile za mwisho, ili watu wake waweze kujiweka tayari kusimama dhidi ya tufani hiyo ya upinzani na ghadhabu." 5T 452.


b. "Tufani inakuja, nasi yatupasa kuwa tayari kukabiliana na ghadhabu yake kwa njia ya kuwa na toba kwa Mungu na imani kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Bwana tasimama kuitetemesha sana dunia hii. Tutaona dhiki pande zote. Maelfu ya meli yatazamishwa chini ya vilindi vya bahari. Majeshi ya wanamaji yatazama chini, na maisha ya wanadamu yatatolewa mhanga kwa mamilioni. Mioto itawaka bila kutazamia, wala hakuna juhudi iwayo yote ya kibinadamu itakayoweza kuizima. Majumba ya kifalme ya duniani humu yatafagiliwa mbali katika ukali wa ndimi za mioto hiyo. Ajali katika njia za reli zitazidi kuongezeka mara kwa mara; kiwewe, migongano, na vifo bila hata taarifa ya dakika moja vitatokea katika njia zote kuu za usafiri. Mwisho umekaribia, mlango wa rehema [karibu] unafungwa. Hebu na tumtafute Mungu maadamu anapatikana, tumwite maadamu yu karibu!" MYP 89,90.



(9) "Pambano la Kuogofya Mno ambalo Halijapata Kushuhudiwa."

 "Pambano ambalo limetufikia sisi litakuwa la kuogofya mno ambalo halijapata kushuhudiwa." 7T 407.



(10) "Pambano la Kutisha."

"Shetani anayakusanya majeshi yake; je! sisi kila mmoja peke yake tumejiweka tayari kukabiliana na pambano la kutisha ambalo li mbele yetu sasa? Je! tunawatayarisha watoto wetu kwa hatari hiyo kubwa?" AH 186.



(11) "Jaribio Kuu."

"Endapo waumini wa ile kweli hawategemezwi na imani yao katika siku hizi za amani linganifu, ni kitu gani, basi, kitakachowainua juu wakati ule wa jaribio kuu utakapokuja na amri kutangazwa dhidi ya wale wote ambao watakataa kuiabudu sanamu ile ya mnyama, wala kuipokea alama yake juu ya vipaji vya nyuso zao au katika mikono yao? Kipindi hicho cha kutisha hakiko mbali. Badala ya kuwa dhaifu na kusitasita, watu wa Mungu wangekuwa wanakusanya nguvu zao na ujasiri kwa ajili ya wakati huo wa taabu." 4T 251.



(12) "Hofu Kuu."

"Uasi karibu sana umefikia kipeo chake. Machafuko yamejaa duniani, na hofu kuu karibu sana itawajia wanadamu. Mwisho umekaribia sana." 8T 28.



3. Je, wakazi wa mbinguni wana habari kuhusu pambano letu linalokuja?

"Malimwengu yote yanaangalia kwa shauku isiyoelezeka kuiona kazi hii ya mwisho ya kufungia pambano kuu kati ya Kristo na Shetani." 5T 526.






4. Je, sehemu kubwa ya wakazi wa dunia hii wana habari juu ya matukio yaliyo karibu kutokea?


a. "Sisi tunaoijua kweli tungekuwa tunajiweka tayari kwa kile kitakachoupata ulimwengu huu hivi karibuni kama mshangao mkubwa mno kwao." 8T 28; 7BC 911.


b. "Wakristo wangekuwa wanajiandaa kwa kile kitakachoupata ulimwengu huu hivi karibuni kama mshangao mkubwa mno kwao, na maandalizi hayo wangeyafanya kwa njia ya kujifunza Neno la Mungu kwa bidii na kujitahidi kuyafanya maisha yao kupatana na amri zake [kumi].... Mungu anataka pawepo na uamsho na matengenezo." PK 626.






5. Je, sisi kama Waadventista Wasabato tunaitambua kweli kweli hatari iliyo mbele yetu?






a. " 'Wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo,' hivi punde utakuja juu yetu; tutahitaji uzoefu ambao hatunao sasa, na ambao wengi ni wavivu mno kuupata. Mara nyingi ndivyo mambo yalivyo ya kwamba taabu inayotarajiwa huonekana kuwa ni kubwa kuliko ilivyo hasa; lakini jambo hilo si kweli kuhusu hatari kubwa iliyo mbele yetu. Maelezo ya wazi kabisa hayawezi kukifafanua kiwango cha ukubwa wa mateso hayo." GC 622.






b. "Sisi tuko ukingoni kabisa mwa wakati ule wa taabu, na mifadhaiko ambayo haijapata kuingia katika mawazo yetu i mbele yetu." 9T 43.






6. Je, yawezekana kwa Wakristo kutojiweka tayari kwa taabu ile inayokuja, ijapokuwa wao wamepata maonyo ya nyuma?

Marko 8:31,32; 9:31; 10:32-34; Mathayo 26:56; Luka 24:6-8.






7. Kwa nini wanafunzi wake walikuwa hawajajiweka tayari kabisa?


A. "Hawakuweza kulistahimili wazo la kwamba yeye ambaye matumaini yao yote yalikuwa yamejengwa juu yake angeweza kuteseka na kufa kifo cha aibu sana. Maneno ambayo walihitaji kuyakumbuka yalikuwa yamefutika katika mawazo yao; na wakati wa kujaribiwa ulipofika, uliwakuta hawajawa tayari. Kifo cha Yesu kikayavunjilia mbali matumaini yao yote kana kwamba alikuwa hajawaonya mapema." GC 594.


B. "Petro hakuwa na hamu ya kuuona msalaba katika kazi yake Kristo." DA 415.






8. Je, Bwana ametupa muhtasari ulio wazi wa matukio yanayoambatana na kufungwa kwa mlango wa rehema?



A "Matukio yale yanayoambatana na kufungwa kwa mlango wa rehema na kazi ile ya maandalizi kwa ajili ya wakati wa taabu, vimeonyeshwa kwa wazi. Makundi na makundi ya watu hawana ufahamu wo wote [hawajui] kuhusu kweli hizi za maana sawa na vile ambavyo zingekuwa hazijapata kufunuliwa kwao kamwe." GC 594.



B "Amepewa ramani inayoonyesha kila alama ya njia katika safari yake ya kwenda mbinguni, wala isingempasa kukisia kitu cho chote." GC 98.




C "Katika historia tunapaswa kuona utimilizo wa unabii,kujifunza mkono wa Mungu unavyofanya kazi katika matapo (movements) makubwa ya matengenezo, na kuelewa maendeleo ya matukio katika kuyakusanya mataifa kwa vita ile ya mwisho katika pambano lile kuu." MH 442; 8T 307.






9. Je, hii ina maana kwamba tunaweza kuelewa kwa undani elezo moja moja la matukio hayo yanayotarajiwa kabla hayajatokea?


a. "Alama ya Mnyama ni sawa kabisa na vile ilivyobainishwa tayari. Si yote kuhusu suala hilo yamefahamika, wala yataweza kufahamika mpaka hapo mbingu zitakapokunjwa kama ukurasa." 6T 17; 8T 159.


b. "Mengi juu ya mambo hayo yameonyeshwa kwangu, lakini mimi naweza kutoa maelezo machache tu kwenu. Enendeni kwa Mungu ninyi wenyewe, ombeni mwelimishwe na mbingu, ili mpate kujua ya kwamba mnaijua hasa kweli ni nini, ili uwezo ule wa Shetani ufanyao miujiza utakapodhihirishwa, kisha yule adui akawajia kama malaika wa nuru, mpate kupambanua kati ya miujiza ya kweli ya Mungu na miujiza ya bandia [uongo] ya mamlaka zile za giza." RH, 12-24- 1889, uk.3.


 



10. Je, ni muhimu jinsi gani kwetu kujifunza unabii ule unaohusu siku hizi za mwisho?


a. "Tunapokaribia mwisho wa kufungwa kwa historia ya ulimwengu huu, unabii ule unaohusu siku hizi za mwisho unataka hasa tuufanyie utafiti wetu." COL 133.


b. "Wangepaswa kuyajua mambo yale ambayo hayana budi kutokea kabla ya kuifunga historia ya ulimwengu huu. Mambo hayo yanahusika na usitawi wetu wa milele, na waalimu pamoja na wanafunzi wao wangeyaangalia kwa makini zaidi." 6T 129.


c. "Kisha mimi nikamwona malaika yule wa tatu. Malaika aliyeandamana nami akasema, 'Kazi yake ni ya kutisha. Ujumbe wake ni wa kuogofya. Huyo ndiye malaika anayechagua ngano kutoka katika magugu, na kuitia muhuri, au kuifunga, ngano hiyo tayari kwa kuwekwa katika ghala ile ya mbinguni. Mambo hayo yangejaa katika mawazo yetu yote, yaani, yangeyavuta mawazo yetu yote.' " EW 118.

d. "Katika majira ya usiku maneno haya yalinenwa kwangu: 'Waagize waalimu katika shule zetu kuwatayarisha wanafunzi wao kwa kile kinachoujia ulimwengu.' " FE 526,527.


e. "Lakini iko siku aliyoiweka Mungu kwa ajili ya kufungwa kwa historia ya ulimwengu huu: 'Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.' Unabii huo unatimia haraka sana. Mengi, mengi sana yangeweza kusemwa juu ya masomo haya ya maana sana." FE 335.



f. "Walinzi na wapaze sauti zao na kutoa ujumbe huu ambao ndio ukweli wa leo. Hebu na tuwaonyeshe watu mahali tulipofikia katika historia ya unabii." 5T 516.


g. "Jitihada kubwa zingefanyika kuliweka somo hili mbele ya watu. Ukweli huu wa kutisha unapaswa kuwekwa sio tu mbele ya watu wa ulimwengu huu, bali pia mbele ya makanisa yetu , ya kwamba siku ya Bwana itakuja ghafula, bila kutazamia. Onyo la kutisha la unabii huu ni kwa kila mtu. Asiwepo hata mmoja anayejisikia kuwa yu salama mbali na hatari ile ya kugutushwa. Tafsiri ya unabii ya mtu awaye yote [isiyopatana na Maandiko] isiwanyang'anye uhakika wa kuyajua matukio ambayo yanaonyesha kwamba tukio hilo kuu limekaribia sana." FE 336.






11. Sisi tumeonywa tusifanye kitu gani hasa?




a. "Uko wakati wa taabu unaowajia watu wa Mungu, lakini hatupaswi kuuweka mbele ya watu daima, na kuwafanya [kusababisha] waweze kupata wakati wao wa taabu mapema. Kupepetwa kuko miongoni mwa watu wa Mungu, lakini huo sio ukweli wa leo wa kuyapelekea makanisa yetu." 1SM 180; 2SM 13.


b. "Ziko nyakati za dhoruba mbele yetu, lakini tusitamke neno hata moja liletalo mashaka au kukatisha tamaa [kwa waumini]." ChS 136.



12. Tukiwa tumeizingatia hatari kubwa inayokuja, tungekuwa tunafanya nini hivi sasa?


"Kama Mungu amepata kunena kupitia kwangu, basi, wakati utakuja mtakapopelekwa mbele ya mabaraza, na kila msimamo wa ile kweli mnayoishikilia utakosolewa kwa ukali sana. Muda ambao wengi sana wanauacha kupotea bure ungetumika kulitii agizo ambalo Bwana ametupa la kujiweka tayari kwa hatari kubwa inayokuja." 5T 717.





13. Ni akina nani pekee watakaosimama imara katika Pambano Kuu la mwisho?


a. "Hakuna watakaoweza kusimama katika Pambano lile Kuu la mwisho isipokuwa wale walioiimarisha mioyo yao kwa zile kweli za Biblia." GC 593.


b. "Jifunzeni Biblia zenu kwa namna ambayo hamjapata kamwe kujifunza kwa siku za nyuma. Msipoinuka na kukifikia kiwango kile cha juu cha utakatifu katika maisha yenu ya kidini, hamtakuwa tayari kwa kufunuliwa [kuja] kwake Bwana wetu." 5T 717.



c. "Tunazikaribia nyakati zile za dhoruba.... Kila msimamo wa imani yetu utachunguzwa; na kama sisi si wanafunzi wakamilifu wa Biblia, tulioimarishwa, tuliotiwa nguvu, na kutulia [katika kweli], basi, hekima ya wakuu wa ulimwengu huu itatufanya sisi tupotee." 5T 546.



d. "Ni wale tu ambao wamekuwa wanafunzi wenye bidii wa Maandiko, na ambao wameipenda hiyo kweli [wameishi kulingana na hiyo kweli], watakaolindwa kutokana na madanganyo yenye nguvu yatakayouteka ulimwengu wote." GC 625.






Hakuna maoni:

Chapisha Maoni