Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumatano, Februari 08, 2012

MUUNGANO WA MAKANISA



1. Je, kila dhehebu la Kiprotestanti katika nchi ya Amerika litaingia katika Muungano wa Makanisa unaokuja?

"Makanisa Makuu ya Marekani, yatakapoungana katika mafundisho yale wanayoshirikiana pamoja, watakapoishawishi serikali yao kuyatia nguvu kisheria maagizo yao na kuzipa ruzuku taasisi zao, hapo ndipo Amerika ya Kiprotestanti itakuwa imeunda sanamu ya utawala wa kidini wa Roma, na adhabu ya serikali haitaweza kuepukwa kutolewa juu ya wale wasioafiki." GC 445.



2. Kwa msingi gani makanisa ya Kiprotestanti hatimaye yataweza kuungana?

"Tofauti kubwa ya imani inayojitokeza katika makanisa ya Kiprotestanti inaangaliwa na wengine kama ni ushahidi wa kutosha kuonyesha kwamba hakuna juhudi yo yote inayoweza kufanywa ili kupata umoja utakaolazimishwa. Lakini kwa miaka mingi, katika makanisa yenye imani ya Kiprotestanti, pamekuwa na maoni yenye nguvu, yanayoendelea kukua ambayo yanapendelea muungano uwepo uliojengwa juu ya mafundisho yale wanayoshirikiana pamoja. Kuupata muungano kama huo, mjadala wa mafundisho yale ambayo wote walikuwa hawaafikiani ----- haidhuru yawe ya maana jinsi gani kutokana na msimamo wa Biblia ----- itabidi utupiliwe mbali." GC 444.



3. Ni mafundisho gani makuu mawili yenye makosa ambayo makanisa hayo yameyashikilia kwa pamoja?

"Kwa njia ya makosa makuu mawili ----- imani kwamba roho haifi, na utakatifu wa Jumapili ----- Shetani atawaleta watu chini ya madanganyo yake. Wakati lile la kwanza linaweka msingi wa imani ya mizimu (spiritualism), lile la pili linaleta mapatano ya kushirikiana na Roma." GC 588.



4. Je, Uprotestanti hatimaye utaweza kuungana na Ukatoliki?

a. "Neno la Mungu linafundisha kwamba matukio hayo [ya kuikandamiza Sabato] yatarudiwa wakati ule Wakatoliki wa Roma na Waprotestanti watakapoungana kwa lengo la kuitukuza Jumapili." GC 578.



b. "Kwa jinsi gani Kanisa la Roma linaweza kujinasua kutokana na shtaka la kuabudu sanamu hatuwezi kuelewa.... Na hiyo ndiyo dini ambayo Waprotestanti wanaanza kuiangalia kwa upendeleo mkubwa sana, na ambayo hatimaye itaungana na Uprotestanti." RH, 6-1-1886, uk.338.



c. "Maadam muda wa majaribio bado ungalipo, itapatikana nafasi kwa mwinjilisti wa vitabu kufanya kazi yake. Madhehebu za dini zitakapoungana na upapa ili kuwatesa watu wa Mungu, basi, mahali pale ambapo uhuru wa dini utakuwapo patafunguliwa kwa uinjilisti wa vitabu." 6T 478.



5. Je, kutakuwa na muungano wa makanisa au muungano katika utendaji wake?

a. "Ulimwengu unaojidai kuwa ni wa Kiprotestanti utaungana kwa mapatano na yule mtu wa dhambi (kuasi), hapo ndipo kanisa na ulimwengu vitakuwa katika mwafaka potovu." 7BC 975.



b. "Uroma katika Ulimwengu ule wa Zamani [Ulaya], na Uprotestanti Asi katika ule Mpya [Marekani], watafuata njia ile ile moja katika kuwashughulikia wale wanaoziheshimu amri zote [kumi] za Mungu." GC 616.



6. Je, Roma itabadilika au Uprotestanti ndio utakaobadilika ili kufanya kuunganika tena kuwezekane?

a. "Muungano huo, kwa hali yo yote, hautafanyika kutokana na badiliko katika Ukatoliki; kwa maana Roma haibadiliki kamwe. Inadai kwamba haiwezi kukosea. Ni Uprotestanti, basi, utakaobadilika. Kupokea mawazo mapana yaliyo huru kwa upande wake [Uprotestanti] kutauleta mahali ambapo utaushika kwa nguvu mkono wa Ukatoliki. 'Biblia, Biblia, ndiyo msingi wa imani yetu,' kilikuwa ndicho kilio cha Waprotestanti katika siku zile za Luther, wakati Wakatoliki walipopaza sauti zao, wakisema, 'Mababa, Desturi, Mapokeo.' Siku hizi Waprotestanti wanaona ni vigumu kuyathibitisha mafundisho yao kutoka katika Biblia, hata hivyo, hawana ujasiri wa kimaadili kuweza kuipokea kweli ambayo inaambatana na msalaba; kwa hiyo, kwa kasi wanaufuata msimamo wa Ukatoliki.... Naam, Waprotestanti wa karne ya kumi na tisa wanakaribia kwa kasi kwa Wakatoliki katika kukosa uaminifu wao kuhusu Maandiko." RH, 6-1-1886, uk.338.



b. "Waprotestanti wa Marekani watakuwa mstari wa mbele katika kuinyosha mikono yao juu ya ghuba ili kuushika mkono ule wa Imani ya Mizimu; kisha watainyosha juu ya shimo kubwa lenye kilindi kirefu [bahari] kushikana mikono na Mamlaka ile ya Roma; hapo ndipo, chini ya uongozi wa muungano huo wa utatu [Uprotestanti, Umizimu, na Ukatoliki], nchi hii [ya Marekani] itafuata katika nyayo za Roma kwa kuikanyaga chini ya miguu yake haki ya mtu ya kuamini kama dhamiri yake inavyotaka." GC 588.



c. "Uprotestanti utakapounyosha mkono wake ng'ambo ya ghuba kuushika mkono wa Mamlaka ya Roma, utakapounyosha juu ya shimo kubwa lenye kilindi kirefu kushikana mikono na Imani ya Mizimu [toka Mashariki ya Mbali - India, China, n.k.], hapo ndipo nchi yetu [Marekani], chini ya uongozi wa muungano huo wa utatu, itakapokuwa imeikataa kila kanuni ya Katiba yake kama Serikali ya Kiprotestanti na ya Jamhuri, na kuiweka sheria inayotangaza uongo na adanganyo ya upapa, ndipo sisi tutaweza kujua ya kwamba wakati umewadia kwa utendaji wa miujiza ya ajabu ya Shetani na ya kwamba mwisho u karibu." 5T 451.



d. "Uprotestanti utaipa mkono wa ushirika Mamlaka ile ya Roma. Ndipo itapitishwa sheria dhidi ya Sabato ya Uumbaji wa Mungu, kisha ndipo Mungu naye atafanya 'kazi yake ya ajabu' katika nchi [ulimwengu]." 7BC 910.



e. "Taifa letu [la Marekani] litakapozikataa kanuni za serikali yake hata kuweza kutunga Amri ya Jumapili, kwa tendo hilo Uprotestanti utakuwa umeshikana mikono na Upapa...." 5T 712.



7. Je, Upapa hatimaye utakuwa na nguvu kiasi gani hapa Amerika?

"Waprotestanti... wanafungua mlango kwa upapa katika Amerika ya Kiprotestanti ili upate kushika tena hatamu zake za utawala ambazo umezipoteza katika Ulimwengu ule wa Zamani [Ulaya - tangu 1798]." GC 573.



8. Ni nani atakayewaongoza watu hao watakapoungana ili kuwapinga wafuasi wa Mungu?

"Tunapoikaribia hatari kubwa ile ya mwisho, ni jambo la maana sana kwetu sisi kwamba amani na umoja viwepo miongoni mwa vyombo vya Bwana. Ulimwengu umejawa na dhoruba na vita na ugomvi. Hata hivyo, chini ya kiongozi mmoja ---- Mamlaka ya Kipapa ----- watu wataungana kumpinga Mungu kwa njia ya mashahidi wake. Muungano huo umeimarishwa kabisa na yule
Mwasi Mkuu [Shetani]." 7T 182.



9. Kusema kweli, ni nani hasa anayesimama nyuma ya Papa?

"Mmoja amesondwa kidole katika unabii kuwa ni mtu wa dhambi (kuasi). Yeye ndiye mwakilishi wa Shetani.... Hapa yupo mtu aliye msaidizi mkuu wa Shetani, aliye tayari kutekeleza kazi ile aliyoianzisha Shetani kule mbinguni, ya kujaribu kuirekebisha sheria ya Mungu [AmriKumi]. Na ulimwengu huo wa Kikristo umeziunga mkono juhudi zake kwa kumpokea mtoto huyo wa Upapa ----- yaani, amri hiyo ya Jumapili." 7BC 910; RH, 3-9-1886, uk. 146.



10. Je, tungekuwa tukifanya nini sasa, ili kukabiliana kwa ufanisi na upinzani wa jamii hiyo iliyoungana pamoja ya Mataifa hayo ya Kikristo?

"Ulimwengu wote uko kinyume nasi, makanisa yale yanayopendwa sana na watu yako kinyume nasi, sheria za nchi hivi punde zitakuwa kinyume nasi. Kama ulipata kuwako wakati ambapo watu wa Mungu wangeshikamana kwa karibu sana, ni sasa." 5T 236.




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni