Maisha yana kanuni moja kubwa nayo ni kutodumu kwa vitu. (Labda milima ambayo sijaona ikitoweka ingawa nayo inatajwa kutoweka) Unayoyaona leo kesho unaweza usiyaone kesho na kila linapoondoka moja jingine huja. Ukilia leo kesho utacheka, ukifurahi utahuzunika, ukipata utakosa, ukitajirika utafirisika pia.
Hayo ndiyo maisha ya kila siku ya mwanadamu. Sasa; ili uishi kwa raha kila ulipatalo sema litapita. Pambana na kila hali bila kuumizwa na kukata tamaa. Hayo yanayokusibu yatapita unachotakiwa kufanya ni kuishi wewe kama wewe na kutomtazama mumeo ama mkeo watoto, majirani, ndugu, rafiki, viongozi wa dini kama mkombozi wako.
Hiki kisebule babu kubwa. Wala sikuwa na habari nacho zaidi ya kuona jina la mtayarishaji akichangia kwenye visebule vingine. Good job keep it up.
JibuFutaNitakuwa nikikutembelea nimege hili na lile. Asante sana kwa kuwa mfuatiliaji wa blog yangu.
Umenitafakarisha Mkuu! Sabato njema!
JibuFutaSi unajua ingawa sijaandika komenti siku ijulikanayo kama Jumamosi kwa kalenda zetu hizi zilizobuniwa katika mikutano ya BINADAMU,..
... labda leo ndio JUMAMOSI kikweli aisee!:-(