Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumatatu, Novemba 14, 2011

Kuimba...NA kwa tafakari!.

Kuimaba ni kitu cha muhimu sana katika kumtolea Mungu sifa. Kuimba nyimbo huzifanya za tafakari. Kwa kutumia maneno machache nyimbo hizi huonyesha msingi wa kweli wa imani, ambao haraka haraka huingia na kukaa akilini. Jinsi ambavyo maneno yanaimbwa kwa mara nyingi, ukweli huu hupenya taratibu ndani ya ubinadamu wetu mzima. Kwa hiyo kuimba kwa kutafakari kunakuwa njia yetu ya kumsikiliza Mungu. Kunamruhusu kila mmoja wetu kushiriki kwa pamoja wakati wa sala na kubaki pamoja katika utulivu tukimsubiri Mungu, bila kuhitaji kujiwekea muda maalumu kwa uhakika sana.

Kufungua njia za kumuamini Mungu, hakuna kinachoweza kukaa badala ya sauti nzuri za binadamu zilizounganishwa pamoja katika nyimbo. Uzuri huu unaweza kutuonjesha chembe za “furaha za mbinguni tukiwa duniani”, kama Wakristo wa Mashariki wanavyoiweka. Na maisha ya ndani yanaanza kuchanua na kung’ara ndani mwetu.

Pia nyimbo hizi husaidia muendelezo wa sala za binafsi. Kwa kupitia nyimbo hizi, kidogokidogo, ubinadabu wetu hupata umoja ndani yetu na Mungu. Zinaweza kuendelea katika ukimya wa mioyo yetu wakati tukiwa kazini, tunapoongea na wengine, au tukiwa tumepumzika. Kwa namna hii sala na maisha ya kila siku ni kitu kimoja. Zinatuwezesha kuendelea kusali katika ukimya wa mioyo yetu, hata tukiwa hatutambui.


“Nyimbo” zinachapishwa katika lugha tofauti tofauti na rahisi, hata hivyo maandalizi yanahitajika ili kuzitumia. Maandalizi haya ni vizuri yakifanyika kabla ya sala yenyewe, ili sala yenyewe ikianza hali ibaki kuwa tulivu na ya kuruhusu tafakari.

Wakati wa sala ni vizuri kwa namna hii kila mtu anaweza kulazimu mtu mmoja kuongoza, Pia, kwa umakini mkubwa sana, kikundi kidogo cha vifaa vya muziki au waimbaji wanao saidia kutia nguvu wengine, wanaweza kuimba, isipokua daima wakumbuke kuwa hawafanyi maonyesho kwa wengine).

Kwani nyimbo zikianzishwa tu hivihivi, sauti itakua ya chini sana. ‘A turning fork or pitch pipe’ vinaweza kusaidia, au vyombo vya muziki kutoa nota ya kwanza au kusindikiza sauti. Na kuhakikisha kasi ya wimbo haiwi ndogo sana, kama inavyotokea wimbo ukiimbwa kwa muda mrefu. Kadiri idadi ya washiriki wa sala inavyoongezeka, kunakua na umuhimu wa kutumia kipaza sauti, na ingefaa zaidi kilongalonga cha kushika kwa mkono, kwa ajili ya kuanzishia na kumalizia wimbo (Wimbo unaweza kumalizwa kwa kuimba “amina” katika nota ya mwisho). Mtu anaye anzisha wimbo anaweza kuwasaidia wengine kwa kuimba kwenye kipaza sauti, lakini kwa uangalifu ili asimeze sauti za wengine. Mfumo mzuri wa sauti ni muhimu kama mkusanyiko ni mkubwa; kama ni muhimu kuukagua, ukaguliwe kabla na fanya majaribio na wale watakao tumia


Nyimbo zilizoko katika lugha mbalimbali ni mwafaka kwa mkusanyiko unaohusisha mataifa mbalimbali toka dunia nzima. Kwa sala zinazo husisha watu wa rika zote kutoka maeneo ya jirani, ni vizuri nyimbo nyingi ziwe katika lugha inayoeleweka na baadhi ya washiriki. Kama inawezekana kila mtu apewe karatasi au kitabu cha nyimbo. Inawezekana pia kuweka nyimbo moja au mbili zinazojulikana vizuri kwa eneo hilo.

Vyombo vya muziki: Gita au kinanda chaweza kusaidia mpangilio mzuri wa nyimbo. Ni vya msaada mkubwa sana katika kuhakikisha sauti si ya juu/chini sana na kasi ya wimbo ni ya kawaida. Gita lipigwe katika mtindo wa ‘classical’ na siyo katika mtindo wa ‘folk style’. Kipaza sauti kinaweza kuwa cha muhimu ili vyombo visikike. Kama nyongeza ya hivi ambayo ni vya msingi, kuna vifaa vingine vya kusaidia katika vyombo vya muziki

Jumamosi, Novemba 12, 2011

Tatizo la KUFIKIRIA kabla ya KUFANYA kitu!






Tuanze kwanza kwa kusikiliza na kutazama nyimbo hizi, kikubwa hapa ni kutafakari ujumbe uliomo ndani ya nyimbo hizi maana tukisema tuanze kuzichambua bado tutakuta ndani kuna vionjo vya Rock and Roll.



 ....na kama hakutakuwa na haja zaidi basi hii itasaidia jambo.



 Ndio kweli yenyewe kwamba:







...naam sasa tuendele.

Ukifikiria hata DHAMBI ,...
....halafu  ukafanya DHAMBI,...
.... labda  LADHA ya dhambi  huongezeka CHACHU!:-(

Swali:
  • Huwa unafikiria kabla ya KUFANYA kitu?
  • Na hufikiri  UKIFANYA bila KUFIKIRIA na UKIFIKIRIA na KUFANYA  kitu kilekile UGALI labda   chaweza kuwa na LADHA mbili tofauti?

Jifunze KUFIKIRIA kwanza ,....
..... na UKISHA kuwa MASTA wa KUFIKIRIA  kabla ya KUFANYA,...
...FIKIRIA halafu FANYA sasa ,...
.... kuna wadaio ndio  WAFANYAO kwa BUSARA wafanyavyo.

Swali:
  • Lakini kwa KUFIKIRIA si yasemekana ndio maana mengi  ya busara kama yangefanyika bila KUFIKIRIA ndio maana WENYE BUSARA hawayafanyi  na kusababisha tatizo liko palepale  kwa kuwa hakuna AFANYAYE TATUZI kwa kuwa wenye TATUZI kitakiwacho kufanyika KIKIFIKIRIWA kwanza HAKIFANYIKIKI?

Ndio,...
.... labda moja ya tatizo la KUFIKIRIA kabla ya KUFANYA kitu,...
..... sio tu kuwa MUDA wa KUFANYA   hautatosha  kwa kuwa muda utatumika pia na KUFIKIRIA kabla ya KUFANYA.:-(

Habari hii ila sio nyimbo za pale juu nimeipata ktk link hapo chini.

http://simon-kitururu.blogspot.com/2011/11/tatizo-la-kufikiria-kabla-ya-kufanya.html

Jumatatu, Novemba 07, 2011

Tabibu na mtaalamu wa saikolojia kutoka nchini Austria aliyeanzisha mtindo wa uchunguzi nafsia...(psychoanalysis).



Sigmund Freud umaarufu wake unatokana na nadharia yake ya uchunguzi nafsia alimochunguza hasa sehemu ya nafsi iliyofichika yaani sehemu zisiziofahamika au zisizofikiwa na akili. Ilikuwa imani yake ya kwamba matatizo ya kiroho na ya kiakili yana msingi katika mvurugo wa kumbukumbu kwenye sehemu hizi ya nafsi zisizoeleweka na mtu mwenyewe. Alibuni njia za kufunua kumbukumbu hizi rohoni kwa majadiliano marefu na kuchungulia ndoto za mtu.

Alizaliwa katika jimbo la Moravia (leo: Ucheki) la Milki ya Austria-Hungaria katika familia ya Wajerumani wa Kiyahudi akapewa jina Sigismund Schlomo Freud na alibadilisha jina hili kuwa Sigmund Freud alipofikia umri wa miaka 21. Familia ilihamia baadaye mjini Vienna alipomaliza shule na kusoma tiba kwenye chuo kikuu na mwaka 1881 alipata digrii ya daktari wa tiba.

Kazi yake ya kwanza ilikuwa katika hospitali kuu ya Vienna alipoendelea kufanya utafiti wa bongo za wagonjwa. Akachungulia pia athira ya dawa ya kulevya kokain kwa roho ya binadamu.
1885 alifanya safari ya masomo kwenda Paris (Ufaransa) alipokaa kwenye hospitali ya magonjwa ya akili alipoangalia hasa matibabu ya hali ya umanyetu (mpagao). Mwaka uleule alimalita tasnifu yake ya profesa akapewa nafasi ya kundisha kozi za magonjwa ya neva na akkili kwenye chuo kikuu cha Vienna.
1886 alifungua kliniki yake ya binafsi akawa pia daktari kiongozi wa idara ya magonjwa wa neva na akili kwenye hospitali ya watoto ya Vienna. 

Mwaka uleule alimwoa Martha Bernays (1861-1951) aliyekuwa binti wa familia ya wataalamu Wayahudi Wajerumani kutoka Hamburg. Aliendelea kuzaa naye watoto sita.
Tangu 1889 alianza kutambua kuwepo kwa nafsi iliyofichika ndani ya roho ya mwanadamu kuwa sababu na chanzo ya mahonjwa mengi ya akili. Aliendelea kutibu na kuandika mjini Vienna hadi mwaka 1938.
Baada ya Ujerumani ya Hitler kuvamia Austria siasa ya Chama cha Nazi ilitisha Wayahudi wote na Freud aliweza kuhamia Uingereza pamoja na familia yake. Lakini dada zake walibaki Austria waliuawa katika makambi ya mauti.

Freud mwenyewe alizaliwa 6 Mei 1856 alikuwa mgonjwa tayari akiwa na kansa iliyoendelea tayari. Mwaka 1939 alimwomba rafiki na daktari yake apewe kiasi kikubwa cha morfini akaaga dunia 21 Septemba 1939.

Hebu jionee mwenyewe The Question of God: 

C.S. Lewis and Sigmund Freud hapa chini.


Jumapili, Novemba 06, 2011

Je unafahamu kuwa Scientology ni dini mpya iliyoanzishwa na L. Ron Hubbard ili kueneza mitazamo na mbinu za Dianetics aliyoibuni mwaka 1950.






Lakini inakubaliwa hadhi ya "dini" katika nchi ya Marekani, Australia na nyingine chache, kwa sababu toka mwanzo imehusishwa na makosa mbalimbali ya jinai, hususan ujasusi, utapeli na kuathiri hali ya nafsi ya wafuasi wake.
Kadiri ya hesabu yake, hao mwaka 2005 walikuwa milioni 8, lakini watu wa nje wanakadiria kuwa ni nusu milioni tu.

Makao makuu ya Scientology yako Marekani, katika kijiji cha Clearwater.
Baada ya Hubbard kufariki mwaka 1986, kiongozi mpya ni David Miscavige.
Jina linatokana na neno la Kilatini "scio" (yaani "najua" kwa maana pana), na neno la Kigiriki "logos" (yaani "somo").Historia ya Scientology inaendana kabisa na maisha ya mwanzilishi wake ambaye tangu miaka ya 1930 aliandika vitabu vya ubunifu mkubwa, mpaka alipojingiza katika masuala ya saikolojia akipinga kabisa misingi na maelekeo ya sayansi hiyo.

Kisha kupata umaarufu wa muda mfupi, akaelekea upande wa roho, aliyoiona haitegemei mwili wala akili, ila inavitumia ili kutenda ulimwenguni.
Kuanzia miaka ya 1960 alifukuzwa na nchi mbalimbali na kuhukumiwa na mahakama tofautitofauti.
Scientology imeitwa "dini ghali" kuliko zote duniani. Kila huduma inatolewa kwa bei iliyopangwa na uongozi wa juu.
Ili kufikia hali ya "Clear", mtu anahitaji kugharimu euro 25.000, na ili kufikia hali bora ya "OT VIII", zinahitajika euro 250,000 hivi.

Kuna kitu unafahamu zaidi?

Jumanne, Novemba 01, 2011

Mkoa na Mlima Kilimanjaro...kwa pamoja.



Mkoa wa Kilimanjaro ni kati ya mikoa 26 za Tanzania. Makao makuu ya mkoa huu ni Moshi. Mlima wa Kilimanjaro, mlima mkubwa kupita yote barani Afrika umo ndani ya mkoa wa Kilimanjaro. Jina la mlima huu ndio limeupatia mkoa huu jina lake.

Mkoa wa Kilimanjaro umepakana na Kenya upande wa kaskazini, Mkoa wa Tanga upande wa Kusini na mikoa ya Manyara na Arusha upande wa magharibi.

Kilimajaro kuna wakazi wapatao 1,381,149 (sensa ya mwaka 2002). Kabila kubwa ndio Wachagga. Makabila mengine mkoani humo ni Wapare na Wamasai

Wilaya

Mkoa wa Kilimanjaro una wilaya 7 ambazo ni: Rombo, Hai, Siha, Moshi Vijijini, Moshi Mjini, Mwanga na Same.


Kilimanjaro ni mlima mrefu kuliko yote Afrika, pia ni wa pili kwa urefu Duniani. Mlima huu uko nchini Tanzania katika Mkoa wa Kilimanjaro. Una urefu wa futi 19,340 (mita 5,895). Hali halisi Kilimanjaro ni zaidi kuliko mlima tu ni kama safu ndogo ya milima mitatu: Kibo, Mawenzi na Shira. Hii mitatu inaonekana kama vilele vitatu vya mlima mmoja hivyo si vibaya kusema Kilimanjaro ni mlima.

Kilimanjaro ni volkeno iliyolala kwa sasa. Kwenye kilele cha Kibo gesi bado inatoka. Kumbukumbu ya wenyeji ina habari ya mlipuko takriban mnamo mwaka 1730.

Kilele cha juu cha Kibo kinaitwa Uhuru Peak. Mtu wa kwanza wa kufika kileleni hapo alikuwa Johannes Kinyala Lauwo kutoka Marangu aliyewaongoza Wajerumani Hans Meyer na Ludwig Purtscheller tarehe 6 Oktoba, 1889 wakati wa ukoloni wa Ujerumani. Wakati ule waliita ncha ya juu  kwa heshima ya Kaisari wa Ujerumani.

Kibo ina theluji na barafuto kadhaa ndogo.

Jumapili, Oktoba 30, 2011

MFUMO WA MAWASILIANO ULIVYO

Mawasiliano ni mchakato ambapo habari hupakiwa na kutumwa na kupashwa na anayetuma kwa anayepokea kupitia kwa njia maalum. Kisha anayepokea hupakua ujumbe ule na kumpatia aliyetuma (ma)jibu. Aina zote za mawasiliano huhitaji anayetuma, ujumbe, na anayepokea. Mawasiliano huhitaji kwamba wale wanaohusika katika mawasiliano wawe na jambo linalowaunganisha kimawasiliano. Kuna njia zinazohusisha kusikia, kama vile unenaji, wimbo, na toni ya sauti, na kuna zile zisizohusisha kusikia, kama vile miondoko ya mwili, lugha ishara, kugusa, kuwasiliana kwa macho, na kuandika.

Mabadiliko katika mawasiliano

Kadri ambavyo wakati umepita , teknolojia imeendelea kukua na kuibua aina mpya ya na mawazo kuhusu mawasiliano. Maendeleo haya ya kiteknolojia yalibadilisha jinsi mawasiliano yanavyofanyika. Watafiti wamegawanya jinsi mawasiliano yalivyobadilika katika hatua tatu.

Mabadiliko ya mwanzo katika Mawasiliano: mawasiliano ya kwanza katika maandishi yalianza na michoro. Maandishi haya yaliandikwa kwenye mawe, ambayo yalikuwa mazito mno kuhamishwa. Wakati huo, mawasiliano katika maandishi hayangeweza kubebwa, ingawa yalikuwepo.

Mabadiliko ya pili katika Mawasiliano: Maandishi yalianza kufanyiwa kwenye karatasi, mavunjo, udongo, nta, nk Herufi za alfabeti zilibuniwa, hivyo basi kuruhusu mfanano wa lugha katika maeneo makubwa. Baada ya muda, shirika la uchapishaji la Gutenberg lilianzishwa. Gutenberg alitayarisha kitabu cha kwanza cha kuchapishwa akitumia mashine yake, na kitabu hicho kilikuwa ni Biblia. Maandiko haya yaliweza kusafirishwa kwa watu wengine duniani ili wayaone. Mawasiliano ya maandishi sasa yanaweza kuhifadhiwa na kubebwa.


Mabadiliko ya tatu ya Mawasiliano: Taarifa sasa inaweza kuhamishwa kupitia mawimbi, na ishara za kielektroniki.


Kwa hivyo mawasiliano ni njia inayotumiwa katika kutoa na kufikisha maana katika jaribio la kusababisha ufahamu wa kijumla. Utaratibu huu unahitaji mkusanyiko mkubwa wa ujuzi wa mawasiliano miongoni mwa na baina ya watu, kusikiliza, kutazama, kuongea, kuhoji, kuchambua, na kutathmini. Ni kupitia kwa mawasiliano ambapo kushirikiana na ushirikiano hutokea......


Pia kuna vikwazo vingi vya kawaida katika mawasiliano. Viwili kati ya vikwazo hivyo vikiwa ni kupasha ujumbe kupita kiasi (mtu anapopokea ujumbe mwingi mno kwa wakati mmoja), na ujumbe changamano. Mawasiliano ni mchakato unaoendelea.

Aina za mawasiliano

Kuna sehemu tatu kuu katika mawasiliano ya binadamu ya ana kwa uso ambayo ni miondoko ya kimwili, toni ya sauti, na maneno. Kulingana na utafiti:

  • 55% ya athari hulingana na miondoko ya kimwili-jinsi mtu alivyokaa, ishara za uso au mikono, na mawasiliano kupitia kwa macho,
  • 38% hulingana na toni ya sauti, na
  • 7% kwa ujumbe au maneno yaliyotumika katika mchakato wa mawasiliano.

Ingawa asilimia ya ushawishi inaweza ikabadilika kulingana na sababu tofauti kama vile mkilizaji na msemaji, mawasiliano kwa jumla hulenga kutimiza lengo moja kwa hivyo, katika baadhi ya matukio, huwa yanafanana kote duniani. Mfumo wa ishara, kama vile sauti, kiimbo au uzito wa sauti, ishara za mikono au uso au ishara zilizoandikwa ambazo huwasilisha mawazo au hisia. Ikiwa lugha inahusu kuwasiliana kwa ishara, sauti, mlio, ishara za uso au mikono, au ishara zilizoandikwa, je, mawasiliano ya wanyama yanaweza kuchukuliwa kama lugha? Wanyama hawana lugha iliyoandikwa, lakini wao hutumia lugha ya kuwasiliana miongoni mwao. Katika hali hiyo, mawasiliano ya wanyama yanaweza kuchukuliwa kama lugha kivyake.

Lugha za Binadamu zinazozungumzwa na kuandikwa zinaweza hufafanuliwa kama mfumo wa ishara (zinazojulikana wakati mwingine kama [[leksia) na sarufi (kanuni)|leksia) na sarufi (kanuni)]]) ambayo ishara hizo huzingatia. Neno "lugha" pia hutumika kurejelea sifa bainifu za lugha. Kujifunza Lugha ni jambo la kawaida katika utoto wa binadamu. Lugha nyingi za binadamu hutumia mifumo ya sauti au ishara ambazo huwezesha mawasiliano baina ya mtu na wenzake. Kuna maelfu ya lugha za binadamu, na huwa na sifa bainifu, ingawa nyingi ya sifa hizi huwa na upekee.


Hakuna mgawanyo dhahiri kati ya lugha na lahaja, lakini mwanaisimu Weinreich Max anatambuliwa kwa kusema kuwa "lugha ni lahaja iliyo na jeshi la nchi kavu na la majini ". Lugha za kuundwa kama vile Kiesperanto, lugha za tarakilishi, na maumbo mbalimbali ya hisabati haziko chini ya sifa bainifu zinazohusisha lugha za binadamu.

Mawasiliano kwa Ishara

Mawasiliano kwa ishara ni mchakato wa kuwasiliana kwa njia ya kutuma na kupokea ujumbe usiohusisha maneno. Ujumbe kama huo unaweza kuwasilishwa kupitia ishara za uso au mikono, miondoko ya kimwili au jinsi ya kukaa; ishara ya uso na kutazamana machoni [[, mawasiliano kwa vitu kama vile mavazi uliyovalia,, jinsi ulivyotengeza nywele, au hata kwa michoro, pia kupitia jumla ya njia zilizoandikwa hapo juu, kama vile mawasiliano kupitia kwa tabia.|, mawasiliano kwa vitu kama vile mavazi uliyovalia,, jinsi ulivyotengeza nywele, au hata kwa michoro, pia kupitia jumla ya njia zilizoandikwa hapo juu, kama vile mawasiliano kupitia kwa tabia.]] Mawasiliano kwa ishara huwa na jukumu muhimu katika maisha ya kila siku ya kila mtu, iwe ni katika uhusiano wa kiajira hadi wa kimapenzi.


Mazungumzo pia huwa na vipengele vya mawasiliano kwa ishara yanayojulikana kama 'paralanguage' au 'viziada-lugha', ambayo huhusisha ubora wa sauti, hisia na mitindo ya kuzungumza, ikiwa pamoja na sifa za kiarudhi kama vile mdundo, lafudhi na msisitizo. Aidha, matini zilizoandikwa zina vipengele vya mawasiliano kwa ishara kama vile mtindo wa kuandika, mpangilio wa maneno, au matumizi ya hisia. Neno lililounganisha maneno ya Kiingereza ya hisia (au emote) na ikoni (icon), kihisishi (an emoticon) ni ishara au muungano wa ishara zinazotumiwa kupitisha hisia katika maandishi.


Aina zingine za mawasiliano kama vile telegrafia huwa katika kategoria hii, ambapo ishara hupitishwa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine kwa njia tofauti. Ishara hizi zinaweza kuwa viwakilishi vya maneno, vifaa au makadirio tu. Majaribio yameonyesha kwamba binadamu wanaweza kuwasiliana moja kwa moja kupitia kwa njia hii bila miondoko ya kimwili, toni ya sauti au maneno.


Kategoria na sifa GW Porter anagawanya mawasiliano kwa ishara katika kategoria nne:


Kimwili. Hii ni aina ya mawasiliano ya kibinafsi. Mawasiliano haya yanahusisha ishara za uso, toni ya sauti, kugusa, kunusa, na miondoko ya mwili.


Ujumi Hii ni aina ya mawasiliano ambayo hufanyika kupitia kwa njia za ubunifu: kucheza ala ya muziki, dansi, uchoraji na uchongaji.


Ishara. Hii ni aina ya mawasiliano, ambayo inajumuisha matumizi ya bendera za ishara, milio 21 ya bunduki, pembe, na ving'ora.


Kiashiria. Hii ni aina ya mawasiliano ambayo inatumia alama za kidini, hadhi, au za kujenga nafsi.


Sifa zisizobadilika


Umbali. Umbali mtu mmoja anaosimama kutoka kwa mtu mwingine kwa kawaida huwasilisha ujumbe fulani. Katika baadhi ya tamaduni hii ni ishara ya mvuto, na kwa wengine inaweza kuonyesha hadhi au umuhimu wa ujumbe unaopitishwa.


Namna ya kujiwasilisha. Watu wanaweza kujiwasilisha kwa njia mbalimbali: uso kwa uso, ubavu kwa ubavu, au hata wakifuatana. Kwa mfano, watu walio na ushirikiano kuna uwezekano watakaa ubavu kwa ubavu na washindani wakati mwingi hutazamana.


Namna ya kukaa. Kwa kawaida mtu anaweza kuwa amelala chini, ameketi, au amesimama. Hivi sio vipengele vya mkao vinavyowasilisha ujumbe. Je, sisi tunatembea kwa kujikokota au tumesimama wima? Tunakunja miguu au mikono yetu? Njia kama hizi za kukaa huwasilisha kiwango cha urasmi na kiwango cha mapumziko katika mawasiliano.


Mgusano wa Kimwili. Kusalimiana kwa mikono, kugusana, kushikana, kukumbatiana, kusukumana, au kupiga kikofi mgongoni, haya yote huwasilisha ujumbe. Huwa yanaashiria urafiki au hisia za (au ukosefu wa) mvuto.



Sifa Badilifu


Ishara za Uso. Tabasamu, kukunja uso, kuinua nyusi, piga miayo, na kukenua, hivi vyote huwasilisha habari. Ishara za uso hubadilika mara kwa mara wakati wa mawasiliano na hufuatiliwa sana na mpokeaji. Kuna ushahidi kuwa maana ya ishara hizo inaweza kuwa sawa katika tamaduni mbalimbali.


Ishara. Mojawapo ya ishara zinazotumiwa, lakini zisizoeleweka, ni vidokezo katika mwondoko wa mkono. Watu wengi hutumia miondoko ya mkono mara kwa mara wakati wanapoongea. Wakati baadhi ya ishara (mfano, kukunja ngumi) zina maana bia, nyingi za ishara huwa kila mtu anajifunza kibinafsi na zina upekee.


Kutazama. Kipengele kikubwa cha mawasiliano ya kijamii ni kutazamana macho. Kipengele hiki kinaweza kuwasilisha hisia, ashiria wakati wa kuzungumza au kuwacha kuzungumza, au chuki. Marudio ya kutazamana yanaweza kuonyesha aidha shauku au kuchoka.

Mawasiliano ya Kutazama

Mawasiliano ya kutazama kama jina linavyopendekeza ni mawasiliano kwa njia ya vielelezo. Ni kupitisha wa mawazo na habari katika aina ambazo zinaweza kusomwa au kutazamwa. Kimsingi yanahusishwa na vipimo vya aina mbili , na yanahusisha: ishara, tipagrafia, kuchora, miundo ya kigrafiki, mchoro, rangi na rasilimali za kielektroniki. Mawasiliano haya hutegemea tu kutazama. Ni aina ya mawasiliano iliyo na athari za kuona. Imejengwa kwenye wazo kwamba ujumbe unaoonekana ukiunganishwa na maandishi huwa na uwezo mkubwa wa kutaarifu, kuelimisha au kumshawishi mtu. Ni mawasiliano kwa kuwasilisha taarifa kupitia vielelezo.


Tathmini ya muundo mzuri wa kutazamwa hujikita kwenye kupima ufahamu na watazamaji, na wala siyo kwenye ujumi au upendeleo wa kisanii. Hakuna-kanuni bia za uzuri na ubaya. Kuna njia mbalimbali za kuwasilisha taarifa kwa kutazama, kama vile kutumia ishara, miondoko ya kimwili, video na TV. Hapa, lengo liko kwenye kuwasilisha matini, picha, michoro, na kadhalika, zikiunganishwa kwenye maonyesho ya tarakilishi. Dhana wasilisho la kutazama hutumiwa kurejelea uwasilishaji halisi wa taarifa. Utafiti wa hivi karibuni katika sehemu hii umelenga miundo ya tovuti na matumizi ya grafiti. Waundaji wa grafiti hutumia mbinu za mawasiliano ya kutazama katika kazi yao.

Aina nyingine ya mawasiliano

Aina nyingine za mawasiliano maalum ni kama vile:

Mawasiliano ya Mdomo

Mawasiliano kwa mdomo ni mchakato ambapo habari hupitishwa kutoka kwa msemaji hadi kwa msikilizaji kupitia kwa mdomo lakini vielelezo vinaweza kutumiwa kusaidia katika mchakato huu .. Msikilizaji anaweza kuwa mtu mmoja, kikundi au hata hadhira. Kuna aina chache za mawasiliano ya mdomo: majadiliano, hotuba, mawasilisho, nk. Hata hivyo, mara nyingi wakati unawasiliana ana kwa ana miondoko ya mwili na toni ya sauti yako huwa na athari kubwa kuliko maneno halisi unayoyasema. Kulingana na utafiti fulani:

55% ya athari hulingana na miondoko ya mwili. Kwa mfano: mkao, ishara, mawasiliano kwa macho, nk.

38% hulingana na toni ya sauti yako

7% hulingana na maudhui ya maneno yako katika mchakato wa mawasiliano.


Unaweza kuona kwamba maudhui au neno unalolitumia silo litakalo amua sehemu ya mawasiliano mazuri. "Jinsi unavyowasilisha ujumbe" huwa na athari kubwa kwa msikilizaji. Ni lazima unase makini ya hadhira na uhusiane na wao. Kwa mfano, watu wawili wanaosema kichekesho, mmoja wao anaweza kuifanya hadhira kuangua kicheko kutokana na miondoko mizuri ya kimwili na toni ya sauti. Hata hivyo, mtu wa pili anayewasilisha kichekesho kile kwa maneno yale yale anaweza kuifanya hadhira itazamane.


Katika mawasiliano ya mdomo, inawezekana kutumia vielelezo ili kukusaidia kuwasilisha habari kwa usahihi zaidi. Mara nyingi, tunaweza kutumia 'PowerPoint' katika mawasilisho yanayohusiana na hotuba zetu ili kuwezesha au kuboresha mchakato wa mawasiliano. Ingawa, hatuwezi kuwasiliana kwa kutumia vielelezo tu kwa sababu sisi hatutakuwa tukizungumza kuhusu mawasiliano ya mdomo tena.

Mipango ya kodi za mawasiliano

Mawasiliano kwa kawaida hufafanuliwa kwa kuzingatia mitazami michache mikuu: Ujumbe (mambo ya aina gani yanayosemwa), chanzo / mtumaji / Msemaji / Mfumbaji (ambaye anatuma), aina (ujumbe ni wa aina gani), njia (unatumwa kupitia njia gani), unapokwenda / mpokeaji / lengo / mpokeaji (anayepokea ujumbe), na lengo au kipengele cha kipragramatiki. Kati ya vikundi, mawasiliano yanahusisha vitendo vinavyotunukia maarifa na tajriba, kupatia mawaidha na amri, na kuuliza maswali. Matendo haya yanaweza kuchukua sura nyingi, katika mojawapo ya njia mbalimbali za mawasiliano. Sura hizi hutegemea uwezo wa kikundi kinachowasiliana. Pamoja, maudhui na sura za mawasiliano kukamilisha ujumbe unaotumwa mahali. Mpokeaji anayelengwa anaweza kuwa msemaji mwenyewe, mtu mwingine au kiumbe kingine, kikundi kingine (kama vile shirika au kikundi cha viumbe).


Mawasiliano yanaweza kuonekana kama mchakato wa kusambaza habari unaoongozwa na viwango vitatu vya sheria za elimu ishara:

  1. Kiwango cha kisintaksia (sifa rasmi za ishara na viashiria),
  2. Kiwango cha kipragmatiki (kinahusika na mahusiano kati ya ishara / maneno na watumiaji wake) na
  3. Kiwango cha kisemantiki (utafiti wa uhusiano kati ya ishara na viashiria na yale vinayowasilisha).


Kwa hiyo, mawasiliano ni mwingiliano wa kijamii ambapo angalau vitu au watu wawili wanaotagusana hutumia seti moja ya ishara na seti moja ya kanuni za kielimu ishara. Sheria hizi zinazozingatiwa wakati mwingine huwa zinapuuza mawasiliano ambayo hutokea bila kupangiwa, yaliwemo mawasiliano ya mtu na nafsi yake kupitia kwa shajara au mazungumzo-nafsi, yote ambayo ni matukio ya sekondari yaliyofuatia kujifunza lugha katika maingiliano ya kijamii.


Katika mfano rahisi, habari au maudhui (mfano ujumbe katika lugha asilia) hutumwa katika njia fulani (kama lugha ya mazungumzo) kutoka kwa mtumaji / msemaji / mfumbaji kwa mahali maalum / mpokeaji / mfumbuaji. Katika njia changamano zaidi, msemaji na mpokeaji huwa wameunganishwa kwa wakati mmoja. Mfano mmoja wa mawasiliano ni kama tendo usemi. Namna ya kutafsiri ujumbe ya msemaji inaweza kuwa tofauti na ya msikilizaji kulingana na desturi na tamaduni za eneo walilomo, au jinsia; mambo ambayo yanaweza kuathiri ujumbe uliokusudiwa. Uwepo wa "kelele za mawasiliano" katika njia inayotumiwa (ikiwa ni hewa, katika kesi hii), mapokezi na ufumbuaji wa ujumbe unaweza kuathiriwa, hivyo basi tendo usemi linaweza kutofikia matokeo yaliyotarajiwa. Tatizo moja la mfano huu wa kupakia-kutuma-kupokea-kupakua ni kwamba mchakato wa kupakia na kupakua huashiria kwamba mtumaji na mpokeaji, kila mmoja ana kitu kinachofanya kazi kama kitabu cha kodi , na kwamba vitabu hivi viwili vya kodi vinafanana kwa kiasi ikiwa si kabisa. Ingawa kitu kama vitabu vya kodi kimetajwa na mfano huu, havijawakilishwa kwenye sehemu yoyote ya mfano huu, jambo ambalo linaibua matatizo mengi ya kuelewa.


Nadharia za urekebishaji-pamoja huelezea mawasiliano kama mchakato wa ubunifu na unaobadilika badilika, unaoendelea wala si kubadilishana tu kwa habari. Mwanataaluma wa vyombo vya habari kutoka Kanada Innis Harold alikuwa na nadharia kwamba watu hutumia njia mbalimbali kuwasiliana na njia watakayochagua kutumia itawapa uwezekano tofauti wa kuumba na kudumisha jamii (Wark, McKenzie 1997). Mfano wake maarufu wa kufafanua haya ni kutumia Misri ya kale na kuangalia vile wao walijijenga wenyewe nje ya vyombo vya habari kwa aina tofauti za mawe na mafunjo. Mafunjo ndiyo aliyoyaita 'Kufunga Nafasi (Space Binding)'. Kufunga huku kuliwezesha kupitishwa kwa maandishi kutoka sehemu moja hadi nyingine na kuwezesha kufanyika kwa kampeni za kijeshi za mbali na utawala wa kikoloni. Mengine ni jiwe na 'Kufunga Wakati (Time Binding)', kupitia ujenzi wa mahekalu na piramidi, wanaweza kuendeleza mamlaka yao kizazi hadi kizazi, kwa kupitia njia hii ya kupitisha habari, wanaweza kubadilika na kuumba ya mawasiliano katika jamii yao (Wark, McKenzie 1997).


Krishi Vigyan Kendra Kannur chini ya Chuo Kikuu cha Kilimo cha Kerala amebuni tawi jipya la mawasiliano ya kilimo linaloitwa Upanuzi kwa Ubunifu (Creative Extension).


Bila mawasiliano ya watu

Mawasiliano katika mingi ya mitazamo yake hayajajifungia tu kwa binadamu, au hata kwa sokwe. Kila mabadilishano ya habari kati viumbe vilivyo hai - yaani kubalishana kwa ishara kunakohusiha mtumaji na mpokeaji walio hai - kunaweza kuchukuliwa kama njia ya mawasiliano. Kwa hivyo, kuna uwanja mpana wa mawasiliano ya wanyama, ambayo yanahusisha mengi ya masuala katika ethnolojia. Pia wanyama waasili kama mwamba tumbawe wanaweza kuwasiliana. Katika ngazi ya kimsingi zaidi, kuna kupatiana ishara kati ya seli, mawasiliano ya seli, na mawasiliano ya kemikali kati ya viumbe asili kama bakteria, na miongoni mwa mimea na himaya za kuvu. Michakato hii yote ya mawasiliano huhusisha mitagusani inayoshirikisha ishara zilizo na ratibu bainifu mbalimbali.


Mawasiliano ya wanyama ni tabia yoyote kwa upande wa mnyama mmoja iliyo na athari ya sasa au baadaye kwenye tabia ya mnyama mwingine. Bila shaka, mawasiliano ya binadamu yanaweza kujumlishwa kama mawasiliano ya wanyama yaliyoendelezwa. Utafiti wa mawasiliano ya wanyama, uitwao zuosemiotiki (zoosemiotics) (tofauti na athroposemiotiki (anthroposemiotics), utafiti wa mawasiliano ya binadamu) umechangia pakubwa katika ukuzaji wa etholojia, biolojia-jamii, na masomo ya uwezo wa mnyama wa kutambua. Jambo hili ni dhahiri kwani binadamu huwa wanaweza kuwasiliana na wanyama, hasa pomboo na wanyama wengine ambao hutumika katika sarakasi. Hata hivyo, hawa wanyama hulazimika kujifunza njia za kipekee za mawasiliano. Mawasiliano ya wanyama, na haswa kuelewa ulimwengu wa mnyama kwa ujumla, ni taaluma inayokua kwa kasi, na hata katika karne ya 21 kufikia sasa, uelewa mwingi wa hapo awali kuhusiana na nyanja mbalimbali kama vile matumizi ya kiishara ya jina, [[hisia za wanyama, utamaduni na kujifunza kwa wanyama|hisia za wanyama, utamaduni na kujifunza kwa wanyama]], na hata tabia za kingono, zilizofikiriwa kwa muda mrefu kuwa zimeeleweka vizuri, zibadilika pakubwa.

Mimea na kuvu

Miongoni mwa mimea, mawasiliano huonekana ndani ya mmea wenyewe , yaani, ndani ya na kati ya seli za mimea, kati ya mimea ya spishi moja au spishi zinazohusiana, na kati ya mimea na viumbe visivyohai, hasa katika sehemu ya mizizi. Mizizi ya mimea huwasiliana na bakteria za rhizobia, na kuvu pamoja na wadudu walio kwenye ardhi. Mitagusano hii sambamba inayohusisha ishara na inayoongozwa na kanuni za kisintaksia, kipragmatiki na kisemantiki hutokea kwa sababu ya "mfumo wa neva" wa mimea uliogatuka. Maana asilia ya neno nyuro katika Kigiriki ni "nyuzinyuzi za mboga" na kama utafiti wa hivi karibuni unavyoonyesha, mengi ya mawasiliano ya ndani ya mmea hufanana na ya nyuro. Mimea pia kuwasiliana kupitia kwa mivuke katika kisa cha tabia za wakati wa mashambulizi na wanyama wala mimea, ili kuonya mimea jirani. Sambamba na hayo, mimea hiyo hutoa mivuke ya kuvivutia vimelea ambavyo huwashambulia wale wanyama. Katika hali ya dhiki mimea inaweza kubadilisha kodi ya kinasaba iliyorithi kutoka kwa wazazi wao na kurudi kwa ile ya mababu zao.


Kuvu huwasiliana ili kuratibu na kupanga ukuaji wao wenyewe na maendeleo yao kama vile malezi ya seli zake na sehemu za kuota. Aidha, kuvu huwasiliana spishi zinazofanana au kuhusiana pamoja na spishi zisizokuvu katika mitagusano ya kimfaano, haswa na bakteria, 'unicellular eukaryotes' , mimea na wadudu. Kemikali za kisemiotiki zinazotumiwa huwa za asili ya kibayotiki na hufanya kuvu kuonyesha athari maalum, ambapo, katika tofauti wakati hata huo kemikali za molekuli huwa si sehemu ya ujumbe wa biotiki unaosababisha msisimko wa viumbe-kuvu. Ina maana kuwa, kuvu zinaweza kutambua tofauti katika molekuli ambazo ni sehemu ya ujumbe wa kibayotiki au kutokuwepo kwa sifa hizi. Hadi sasa kuna molekuli tano tofauti na za msingi zinazojulikana ambazo huratibisha ruwaza tofauti za kitabia kama vile 'nyuzi za hisia', kuzaana, ukuaji, usababishaji wa magonjwa. Uratibu wa tabia na uzalishaji wa vitu kama hivi unaweza tu kufikiwa kupitia michakato fasili: ya kibinafsi au isiyo ya kibinafsi, kiashiria cha kibayotiki, ujumbe wa kibayotiki kutoka kwa spishi zinazofanana, zinazohusiana au zisizohusiana, au hata "kelele", yaani, molekuli zinazofanana lakini hazina ujumbe wa kibayotiki.

Mawasiliano kama taaluma ya kiakademia

Mawasiliano kama taaluma ya kiakademia, ambayo wakati mwingine huitwa "komunikolojia," inahusiana na njia zote tunazozitumia kuwasiliana, hivyo basi inahusisha sehemu kubwa ya utafiti na maarifa. Taaluma ya mawasiliano inahusisha mawasiliano ya kimaongezi na yasiyo ya kimaongezi. Mkusanyiko wa maarifa kuhusu mawasiliano umewakilishwa na kufafanuliwa katika vitabu, machapisho ya kielektroniki, na majarida ya kiakademia. Katika majarida, ripoti za kitafiti ndizo matokeo ya tafiti ambazo ni msingi wa uelewa, unaoendelea kupanuka, wa jinsi sisi wote tunavyowasiliana.


Mawasiliano hufanyika katika ngazi tofauti (hata kwa tendo moja), katika njia mbalimbali, na kwa viumbe wengi, na vilevile kwa mashine fulani. Baadhi ya taaluma za utafiti , ikiwa siyo zote, hutenga sehemu ya mafunzo yake kwa mawasiliano, hivyo basi wakati wa kuzungumza kuhusu mawasiliano, ni muhimu sana kuwa na uhakika kuhusu nyanja ya mawasiliano inayozungumziwa. Ufafanuzi wa mawasiliano hutofautiana sana, baadhi yake ukitambua kwamba wanyama wanaweza kuwasiliana na wenzao na binadamu pia, na baadhi ni finyu zaidi, ukihusisha binadamu katika mitagusano ya kibinadamu iliyo na maana.

*******************************************************

Mawasiliano ni mchakato wa kuhamisha taarifa kutoka chombo kimoja hadi kingine. Michakato ya mawasiliano ni mwingiliano unaohusisha ishara kati ya angalau wakala wawili walio na mkusanyiko wa ishara na sheria za elimu ishara . Mawasiliano kwa kawaida hufafanuliwa kama "kupasha au kubadilishana kwa mawazo, maoni, au habari kwa kunena, maandishi, au ishara". Ingawa kuna kitu kama mawasiliano ya njia moja, mawasiliano yanaweza kueleweka vyema kama mchakato kati ya wahusika wawili ambapo kuna mabadilishano na kukuza kwa fikra, hisia au mawazo (nishati) kufikia lengo lililokubaliwa au mwelekeo uliokubaliwa (habari).

*******************************************************