Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumanne, Novemba 01, 2011

Mkoa na Mlima Kilimanjaro...kwa pamoja.



Mkoa wa Kilimanjaro ni kati ya mikoa 26 za Tanzania. Makao makuu ya mkoa huu ni Moshi. Mlima wa Kilimanjaro, mlima mkubwa kupita yote barani Afrika umo ndani ya mkoa wa Kilimanjaro. Jina la mlima huu ndio limeupatia mkoa huu jina lake.

Mkoa wa Kilimanjaro umepakana na Kenya upande wa kaskazini, Mkoa wa Tanga upande wa Kusini na mikoa ya Manyara na Arusha upande wa magharibi.

Kilimajaro kuna wakazi wapatao 1,381,149 (sensa ya mwaka 2002). Kabila kubwa ndio Wachagga. Makabila mengine mkoani humo ni Wapare na Wamasai

Wilaya

Mkoa wa Kilimanjaro una wilaya 7 ambazo ni: Rombo, Hai, Siha, Moshi Vijijini, Moshi Mjini, Mwanga na Same.


Kilimanjaro ni mlima mrefu kuliko yote Afrika, pia ni wa pili kwa urefu Duniani. Mlima huu uko nchini Tanzania katika Mkoa wa Kilimanjaro. Una urefu wa futi 19,340 (mita 5,895). Hali halisi Kilimanjaro ni zaidi kuliko mlima tu ni kama safu ndogo ya milima mitatu: Kibo, Mawenzi na Shira. Hii mitatu inaonekana kama vilele vitatu vya mlima mmoja hivyo si vibaya kusema Kilimanjaro ni mlima.

Kilimanjaro ni volkeno iliyolala kwa sasa. Kwenye kilele cha Kibo gesi bado inatoka. Kumbukumbu ya wenyeji ina habari ya mlipuko takriban mnamo mwaka 1730.

Kilele cha juu cha Kibo kinaitwa Uhuru Peak. Mtu wa kwanza wa kufika kileleni hapo alikuwa Johannes Kinyala Lauwo kutoka Marangu aliyewaongoza Wajerumani Hans Meyer na Ludwig Purtscheller tarehe 6 Oktoba, 1889 wakati wa ukoloni wa Ujerumani. Wakati ule waliita ncha ya juu  kwa heshima ya Kaisari wa Ujerumani.

Kibo ina theluji na barafuto kadhaa ndogo.

Maoni 1 :

  1. mlima Kilimanjaro pamoja na sifa zote ulizonazo bado uharibifu wa mazingira katika hifadhi ya mlima Kilimanjaro ni mkubwa na unatishia usalama wa mlima wenyewe jitihada zinahitajika kuulinda sio tunakimbilia tuu kuchukua hela pindi watalii wanapokuja,
    Mkoa Kilimanjaro uliongozwa na manispaa ndo mji msafi Afrika Mashariki na Kati, pia ndo Mkoa ukikamatwa unatupa takataka hata kama ni karatasi ya vocha au mate faini ni kuanzia elfu hamsini

    JibuFuta