Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumatatu, Novemba 07, 2011

Tabibu na mtaalamu wa saikolojia kutoka nchini Austria aliyeanzisha mtindo wa uchunguzi nafsia...(psychoanalysis).



Sigmund Freud umaarufu wake unatokana na nadharia yake ya uchunguzi nafsia alimochunguza hasa sehemu ya nafsi iliyofichika yaani sehemu zisiziofahamika au zisizofikiwa na akili. Ilikuwa imani yake ya kwamba matatizo ya kiroho na ya kiakili yana msingi katika mvurugo wa kumbukumbu kwenye sehemu hizi ya nafsi zisizoeleweka na mtu mwenyewe. Alibuni njia za kufunua kumbukumbu hizi rohoni kwa majadiliano marefu na kuchungulia ndoto za mtu.

Alizaliwa katika jimbo la Moravia (leo: Ucheki) la Milki ya Austria-Hungaria katika familia ya Wajerumani wa Kiyahudi akapewa jina Sigismund Schlomo Freud na alibadilisha jina hili kuwa Sigmund Freud alipofikia umri wa miaka 21. Familia ilihamia baadaye mjini Vienna alipomaliza shule na kusoma tiba kwenye chuo kikuu na mwaka 1881 alipata digrii ya daktari wa tiba.

Kazi yake ya kwanza ilikuwa katika hospitali kuu ya Vienna alipoendelea kufanya utafiti wa bongo za wagonjwa. Akachungulia pia athira ya dawa ya kulevya kokain kwa roho ya binadamu.
1885 alifanya safari ya masomo kwenda Paris (Ufaransa) alipokaa kwenye hospitali ya magonjwa ya akili alipoangalia hasa matibabu ya hali ya umanyetu (mpagao). Mwaka uleule alimalita tasnifu yake ya profesa akapewa nafasi ya kundisha kozi za magonjwa ya neva na akkili kwenye chuo kikuu cha Vienna.
1886 alifungua kliniki yake ya binafsi akawa pia daktari kiongozi wa idara ya magonjwa wa neva na akili kwenye hospitali ya watoto ya Vienna. 

Mwaka uleule alimwoa Martha Bernays (1861-1951) aliyekuwa binti wa familia ya wataalamu Wayahudi Wajerumani kutoka Hamburg. Aliendelea kuzaa naye watoto sita.
Tangu 1889 alianza kutambua kuwepo kwa nafsi iliyofichika ndani ya roho ya mwanadamu kuwa sababu na chanzo ya mahonjwa mengi ya akili. Aliendelea kutibu na kuandika mjini Vienna hadi mwaka 1938.
Baada ya Ujerumani ya Hitler kuvamia Austria siasa ya Chama cha Nazi ilitisha Wayahudi wote na Freud aliweza kuhamia Uingereza pamoja na familia yake. Lakini dada zake walibaki Austria waliuawa katika makambi ya mauti.

Freud mwenyewe alizaliwa 6 Mei 1856 alikuwa mgonjwa tayari akiwa na kansa iliyoendelea tayari. Mwaka 1939 alimwomba rafiki na daktari yake apewe kiasi kikubwa cha morfini akaaga dunia 21 Septemba 1939.

Hebu jionee mwenyewe The Question of God: 

C.S. Lewis and Sigmund Freud hapa chini.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni