Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumanne, Septemba 13, 2011

UTAMADUNI


Neno la Kilatini lenye maana ya utamaduni ni Cultura ambalo lina usuli wake katika neno colere, linalo maanisha "kulima") Neno hili lina fafanuzi nyingi. Kwa mfano, mnamo mwaka 1952, Alfred Kroeber na Clyde Kluckhohn walikusanya orodha ya vijelezi 164 vya neno "utamaduni" katika kazi yao: Culture:a Critical Review of Concepts and Definitions.  Hata hivyo, neno "utamaduni" linatumika kimsingi katika njia tatu zifuatazo:
  • Maonjo ya hali ya juu katika sanaa, vilevile hujulikana kama utamaduni wa juu
  • Mkusanyiko wa maarifa ya kibinadamu, itikadi na tabia ambao hutegemea sana uwezo wa kuwasilisha mawazo na mafunzo ya kijamii kiishara
  • Ni jumla ya mitazamo, kaida, malengo na maadili yanayotambulisha asasi, shirika au kikundi Fulani
Dhana hii ilipoibuka kwanza katika karne ya kumi na nane na kumi na tisa barani Ulaya, ilimaanisha mchakato wa kulima au kuboresha kilimo au kilimo cha mboga. Katika karne ya kumi na tisa dhana hii ilimaanisha kuboreshwa kwa mja kupitia kwa elimu na hali kadhalika ilimaanisha kutekelezwa kwa maazimio ya kitaifa au maadili. Katikati mwa karne ya kumi na tisa, wanasayansi wengine walitumia dhana ya utamaduni kurejelea uwezo wa kiubia wa binadamu.




Katika karne ya ishirini, "utamaduni" ilijitokeza kama dhana ya kimsingi katika somo la Anthropolojia. "Utamaduni" ulihusisha mambo yote yaliyomhusu binadamu ambayo hayakufungamana na matokeo ya kimaumbile. Dhana ya utamaduni katika Anthropolojia ya Kimarekani ilikuwa na maana mbili: 

(1)        Uwezo wa kibinadamu wa kuainisha na kuwasilisha tajiriba za kibinadamu kiishara na kutenda mambo kiubunifu; na

(2)        Namna mbalimbali watu wanaoishi katika sehemu mbalimbali ulimwenguni huainisha na kuwasilisha tajiriba zao za maisha na kutenda mambo kiubunifu. Kufuatia vita vya pili vya dunia, dhana hii ilipata umaarufu ingawa na fafanuzi tofautitofauti katika taaluma kama vile sosholojia, Mafunzo ya utamaduni, saikolojia ya mipangilio na mafunzo ya usimamizi.

Jumatatu, Septemba 12, 2011

NI KWELI Imetokea DHAHIRI.

 
Ni kweli imetokea hadi kupelekea Mubelwa Bandio Kuandika kwenye wall yake ktk facebook. Jisomee mwenyewe kwa ku-Click  HAPA.
Ninairejea kwa kuinukuu: VODACOM....Ni kweli kuwa hasara ambayo mngeipata kwa KUAHIRISHA Miss Tanzania ni kubwa kuliko uhai wa mamia ya watu waliopotea? 
Ni kweli kuwa WATEJA WENU ambao kila siku mnasema mnawajali, si miongoni mwa waliofariki ama kufiwa kutokana na ajali hiyo?

NANI ANASEMA VODACOM INAWAJALI WATEJA WAKE??
Nawawaza kwa sauti tu "wapendwa" wangu VODA.
Mwisho wa kunukuu.
******************
Sijui kwa upande wako wewe msomaji. 
Mimi ninasema kwamba: 
Ukiona Majibu Yanakua Mengi,
Ujue Hakuna Jibu la Uhakika.

Jumamosi, Septemba 10, 2011

Dhambi ya asili

Wakristo wa madhehebu mbalimbali wanaita hivyo dhambi ya kwanza ya watu ambayo imekuwa asili ya dhambi zote (Rom 5:12) na ya uharibu wa dunia (Rom 8:19-25).

 
Michelangelo alivyochora katika kuta za Cappella Sistina huko Vatikano dhambi ya Adamu na Eva na adhabu iliyofuata ya kufukuzwa bustanini.


Dhambi ya Asili katika Biblia

Kitabu cha Mwanzo sura ya 3 inasimulia dhambi hiyo. Kwa njia ya hadithi hiyo tunaambiwa hali yetu mbaya haitokani na Mungu, bali na uasi wetu na wa wazee wetu (Hek 2:23-24). Pia tunafundishwa kukataa toka mwanzo vishawishi vyetu tukiamini maagizo yote ya Mungu yametolewa kwa upendo mkuu.
Shetani ndiye aliyeanzisha kishawishi. Eva alipaswa asimsikilize. Kosa lake la kwanza ni kumjibu: hivyo shetani akamdanganya kwamba, eti Mungu ana kijicho, hataki watu walingane naye, ndiyo sababu aliwakataza (Yoh 8:44). Tukianza kuzingatia kishawishi tunakubali shaka juu ya wema wa Mungu kwetu katika kutuelekeza. Kwa namna hiyo walianguka watu wa kwanza waliokuwa watakatifu; kwa urahisi zaidi tutaanguka sisi wenye tabia mbaya kutokana na dhambi hiyo na nyingine nyingi.
Hata baada ya dhambi Mungu anamtafuta mtu kwa upendo, ila huyo kwa aibu anamkimbia, au akijisikia analaumiwa na dhamiri, basi anatafuta visingizio hata kumlaumu Mungu kana kwamba ndiye aliyesababisha. Kwa utakatifu wake Mungu hawezi kuvumilia maovu, na kwa haki yake anataka makosa yalipwe. Ndiyo sababu tunakuta matatizo maishani, kama vile uchungu wa uzazi, kuhusiana kwa mabavu, kupata riziki kwa shida, na hasa kufa: hayo yote ni matokeo ya dhambi.
Pamoja na hayo Mungu hapendi mtu yeyote apotee (2Pet 3:9), hivyo toka mwanzo aliahidi kwamba mzawa wa Eva atamponda kichwa shetani (Mwa 3:15). Ndiyo habari njema ya awali kuhusu wokovu ujao.

Maendeleo ya dhambi

Baada ya dhambi ya asili watu walianza kuzaa. Mwa 4:1-16 inatuchorea picha ya Kaini na Abeli kama wazaliwa wa kwanza waliotofautiana kiadili (1Yoh 3:11-12). Toka mwanzo mwovu na mwadilifu waliishi pamoja, wa kwanza akimdhulumu wa pili hata kumuua bila ya kujali udugu. Ikisikitishwa kufikiria mzaliwa wa kwanza kuwa muuaji wa mdogo wake, inafurahisha kwamba wa kwanza kufa alikuwa mwema, kielelezo cha Yesu aliyeuawa bila ya kosa (Eb 12:24).
Toka mwanzo hao walimuabudu Mungu kwa njia ya dini, ibada na sadaka mbalimbali. Hata hivyo Mungu akakubali zile tu zilizotolewa kwa ukarimu (Eb 11:4). Tangu hapo Biblia inatuonyesha jinsi alivyopendelea wadogo kuliko wakubwa.
Kuhusu Kaini tunaonyeshwa ustawi wa dhambi ndani mwake na uongozi wa Mungu aliyemtaka ashinde dhambi bado mlangoni. Hata baada ya dhambi hiyo ambayo ni kubwa kiasi cha kumlilia Mungu alipe kisasi, yeye alizidi kumhifadhi Kaini.
Baadaye (Mwa 4:17-24) kukawa na maendeleo ya aina mbalimbali: ujenzi, ufundi, muziki, lakini hasa dhambi. Picha yake ni Lameki, mtu wa kwanza kuwa na mitara, mkatili kama nini.
Ingawa hali ilikuwa ya kukatisha tamaa, kwa baraka ya Mungu watu wakazidi kuzaa na kati ya watoto wao wakapatikana waadilifu kama Henoko aliyestahili kutwaliwa na Mungu.
Hata hivyo ongezeko la dhambi likasababisha maisha ya binadamu yafupike (Mwa 6:3) kwa kuwa ni kusogea mbali na Mungu, chemchemi ya uhai.

Jumanne, Septemba 06, 2011

Dini

Dini (kutoka Kiarabu اﻟدﻴن, tamka ad-din) inamaanisha jumla ya imani ya binadamu kadhaa pamoja na mafundisho wanayotoa kuhusu yale ambayo wanayazingatia ama kuyasadiki, yaani mambo ya roho, kama vile kuhusiana na Mungu, maisha na uumbaji.

Ibada ni nguzo mojawapo iliyo dhahiri miongoni mwa dini kadhaa katika kuunganisha dhamira za mwenye kushika dini na mhimili wa imani, lakini dini inahusu pia mafundisho kuhusu maadili, mema na mabaya, imani na jinsi ya kushiriki katika jumuiya za waumini.

Kwa maana nyingine "dini" inataja jina kielelezo juu ya aina mbalimbali za imani jinsi inavyopatikana duniani, yaani jumuiya za kidini.

Dini kama jumuiya kubwa

Dini kwa maana hiyo yenye wafuasi wengi duniani ni:

Pamoja na hizi kuna dini mbalimbali zinazojulikana tangu karne nyingi duniani hata kama idadi ya wafuasi si kubwa sana kwa mfano:

Pia kuna imani ambazo zinafanana kwa namna fulani, hivyo mara huhesabiwa kama imani mbalimbali za pekee, mara huhesabiwa kama kundi la dini zenye misingi ya pamoja au kama matawi ya imani moja. Zikitazamiwa pamoja idadi ya wafuasi ni kubwa kiasi lakini zikihesabiwa moja-moja idadi ya wafuasi si kubwa sana, kama vile:

Dini au Falsafa?

Hasa Asia ya Mashariki zimetokea mafundisho ambayo mara huhesabiwa kati ya dini mara kati ya falsafa. Mifano yake ni:

Wafuasi wao mara nyingine hufuata pia k

wa wakati mmoja dini zingine kama vile U

buddha au Ukristo.

Dini mpya


Historia inajua pia dini zilizotokea mara kwa mara katika nchi mbalimbali. Mfano wa dini iliyoanzishwa katika karne ya 19 na kusambaa kote duniani ni Baha'i. Kuna mifano mingi mingine. Si rahisi kuzitaja zote.

  • Kundi la "Scientology" ni mfano wa kundi dogo lililoangaliwa sana kwa sababu wafuasi kadhaa ni watu maarufu Marekani na Ulaya kutokana na filamu au magazeti.
  • Lakini miendo mipya yenye wafuasi wengi zaidi huko China (kama Falungong) haikuangaliwa ipasavyo kwa sababu wafuasi wake wako mbali zaidi na waandishi wa habari.
  • Rastafari ilianzishwa kama mwendo unaohesabiwa mara kama tawi la Ukristo, mara kama dini mpya kati ya wakazi wa Jamaika wenye asili ya Afrika tangu miaka ya 1930. Kupitia wapenzi wa muziki wa Jamaika imejulikana sana duniani. Jina na desturi zake kadhaa zimetumiwa kama mwendo wa kiutamaduni hata katika sehemu zingine za dunia ingawa idadi ya wafuasi wa dini hiyo ni ndogo.
  • Miendo ya kidini inayokua katika sehemu mbalimbali za dunia mara nyingi hazijulikani, hasa zikisambaa kati ya wasemaji wa lugha moja au katika sehemu fulani ya nchi moja tu. Mfano wake ni Dini ya Musambwa katika Kenya ya Magharibi tangu miaka ya 1940.

Zaidi ya hayo kuna miendo yenye tabia za kidini, ambayo hakuna makubaliano ya wataalamu kama ni dini au la, kwa mfano New Age na Yoga.

Dini kwa kipindi kirefu cha maisha ya mwanadamu imekuwa kitovu cha ustaarabu wa jamii husika. Hivyo kadiri jamii inavyobadilika ndivyo mambo mengi huongezwa ama kutolewa katika mapokeo yake ili hali kuakisi mazingira ya nyakati.

Katika wakati wa sasa, kumekuwepo kwa jitihada mbalimbali zinazopokea na kuchunguza misingi ya dini na maisha katika sura ya kisomi na hata kiudadisi.


Elimu ya Dini

Kuna masomo mbalimbali ambayo huangalia na kuchunguza dini kwa kutumia mbinu za kitaaluma. Kati ya hizo kuna:

  • Teolojia ama tauhidi, ambayo ni matumizi ya mbinu za kiuanazuoni ndani ya dini fulani, kwa mfano teolojia ya Kiyahudi, ya Kikristo, ya Kiislamuu, n.k.
  • Falsafa ya dini inajaribu kutazama muundo wa fikra na mafundisho ya kidini. Inatumia mbinu na maswali ya falsafa ikitazama maswali kama: - je tunaweza kusema juu ya Mungu? - namna gani? - kuna maisha au uhai kupita kifo? - jinsi gani tunaweza kujua habari za mambo yajayo, uzima wa milele, asili na lengo la dunia?
  • Elimu ya dini inatazama dini mbalimbali na kuzilinganisha: jinsi zinavyobadilika, jinsi ibada zao zinaendelea, jinsi jumuiya zao zinakua au kupungua, nafasi ya dini katika maisha ya jamii n.k.
  • Takwimu ya dini ni somo linalojaribu kuhesabu idadi ya wafuasi wa dini mbalimbali.
  • Saikolojia ya dini inajaribu kuchunguza jinsi gani aina mbalimbali za imani zinahusiana na aina za roho za kibinadamu.
  • Ulinganisho wa dini unatazama hasa mafundisho na hali halisi ya dini mbalimbali jinsi zinavyofanana au kutofautiana: kwa mfano fundisho la Mungu mmoja katika Uyahudi-Ukristo-Uislamu-Uhindu; au fundisho la maono ya kiroho katika umistiki (Ukristo), kabbala (Uyahudi), usufi (Uislamu), tantra (Uhindi, Ubuddha).
  • Ukosoaji wa dini uko karibu na falsafa ya dini ukiwa na mwelekeo wa kuuliza maswali, kutamka wasiwasi, kuchunguza madai ya matamshi ya dini kulingana na misingi ya akili ya binadamu.