Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumapili, Novemba 23, 2014

SAIKOLOJIA NA MAUMBILE




Wataalam wa mambo ya saikolojia na maumbile wamezisoma tabia mbalimbali za binadamu na hatimaye wamewagawanya binadamu katika makundi makuu manne yenye kategoria kuu mbili. Kategoria hizo ni:

1. INTROVANT: Watu wenye uwezo mkubwa kiakili na wanaotafakari mambo kwa kina, katika eneo hili hapa kuna makundi mawili nayo ni; 1.Melancolin 2. Fragmetic

2. EXTROVANTS: Wana uwezo wa kawaida kiakili na hawana tafakari za kina katika mambo yao
Hapa pia kuna makundi mawili nayo ni; 1. Sanguine 2. Colerick
Sasa tuangalie tabia za kila kundi na mienendo yao

1.MELANCOLIN

Watu wa kundi hili (females and males) wana sifa zifuatazo
-wana uwezo mkubwa kiakili (high intelligence Quotient)
-ni wagunduzi wa mambo makubwa ya kisayansi
-wanamudu vizuri masomo ya sayansi na hesabu
-ni watu wenye pole pole na wasio na maneno mengi
-wana hisia kali za upendo na ni kundi linalosadikika kuwa na upendo wa dhati
-Wanawajali sana wenzao hasa wanapokuwa katika shida na matatizo(i.e ndio maana hawa huwa waombaji –wanamaombi wazuri sana kiimani)
-Wana huruma sana na hawapendi kuona wengine wakionewa
-Wanajitolea kwa haraka na kwa dhati katika mambo ya wengine
-Huondoa uchungu wao kwa machozi (wakiumizwa hulia haraka, hasa kwa upande wa wanawake/wasichana)
-Hawajiamini kwa mambo wanayoyafanya (hata wakiwa darasanu si wepesi wa kunyoosha vidole ili kujibu maswali)
-Wanahesabu kushindwa kuliko kufanikiwa (mfano akitaka kuanzisha duka; badala ya kuwaza itakuwaje nikipata faida wanawaza itakuwaje kama duka litaibiwa ama kuungua moto, kwa maswali hayo anajikuta hata anafikia katika uamuzi wa kuahirisha uanzishaji wa mradi huo)
-Wakata tamaa wanapokosolewa.
-Wanapenda sana kutiwa moyo kiuhalisia.
-Wanapenda kusoma, kusikiliza, na kusimulia mambo yenye tafakari na uchambuzi wa kina (hawapendi umbea)
-Wanapotoa mawaidha mahubiri ama ushauri wengi(wanaosikiliza) huwa wanaguswa nao na hubadilika haraka kutokana na mawaidha hayo ama ushauri ama mahubiri hayo
-Hawapendi kuvunja taratibu, sheria za eneo husika.
-Wanapenda usafi na mpangilio mzuri wa vitu vyao
-Ni wa vumilivu sana katika hali mbalimbali (mfano wanapoonewa ama kuumizwa)
-Hawapendi kufuatilia mambo ya wengine pasipo sababu za msingi.
-Ni kundi mojawapo linaloathiriwa sana na magonjwa ya mashinikizo kutokana na kuwa wanawaza sana
-Ni wagumu wa kusahau na hiyo imewasababishia kuwa wagumu wa kusamehe
-Wanaumia sana wanapokosea ama kushindwa jambo Fulani
-Wanajeruhika mioyo yao kirahisi (i.e wakiingiwa na pepo wabaya si rahisi kuwatoka kwa sababu ya kutunza uchungu kwa muda mrefu mioyono mwao)
-Wana busara na hekima nyingi
-Ni watu ambao wakiishika imani fulani wanajitahidi kuitimiliza sheria yote.
-Ni wepesi wa kutubia makosa yao na kutubu kwa ajili ya wengine.
-Wana aibu nyingi sana hasa kwa watu wasiowafahamu wala kuzoeana nao
-Ni kundi la watu wanoridhika haraka
-Masikini wengi kiuchumi duniani ni wa kutoka katika kundi hili kutokana na uoga wao wa kuanzisha mambo kwa kuhofia kushindwa
-Watoto wanaozaliwa katika kundi hili inasadikiwa ni wengi huwa na ndoto za kufanikiwa mapema lakini ni wachache mno ambao huweza kutimiliza ndoto zao kutoka na uoga wa kuanzilisha mambo mapya.
-Kundi linalopenda amani na utulivu
-Wanaogopa sana matatizo, vikwazo na changamoto
-Katika familia baba na mama wakiwa melancolin upo uwezekano mkubwa kwa watoto kuharibika maadili kwa sababu hawa melancolin si wepesi wa kuadhibu
-Mara nyingi hupenda kuonesha sura za tabasamu hata kama wapo katika matatizo makubwa
-Hawapendi kumueleza kila mtu mambo yao binafsi
-Ni kundi la watu wenye marafiki wachache
-Wakati mwingine hupenda kujikataa.
-Ni waaminifu na wasema ukweli
-Wanapenda kusaidia wengine kupita hata uwezo wao
-Ni waaminifu sana kwa mambo ya kawaida na yale ya kiimani
-Hawapendi kujionesha mbele ya macho ya watu
-Hawa hawafai kuwa viongozi (si wazuri sana) kwa sababu wanapenda kusikiliza na kutafakari kila wanachoshauriwa hivyo hujikuta kuwa wanayumba kimisimamo. (mfano kama mkurugenzi/mwenyekiti wa eneo Fulani akiwa ni melancolin yafaa sana msaidizi wake awe ni colerick
-kingine kinachowanyima sifa ya kuwa viongozi wazuri ni kutokuwa na uwezo wa kujieleza kwa kujenga hoja zenye ushawishi mkubwa [Musa wa biblia alikuwa ni mmoja ya watu wa kundi hili, alikuwa hajiamini, anakata tama mapema, mlalamishi, asiyeweza kujieleza, licha ya kupewa msaidizi na Mungu bado tabia zake zilimuathiri na akajikuta anakosa nchi ya ahadi-Kaanani]
-Wanauhesabu upendo wa dhati kutokana na mambo wanayofanyiwa na sio kuambiwa (wanafurahia sana vitendo kuliko maneno}
-Kwa upamnde wa wasichana inasemekana kuwa ndio ambao wanasumbuliwa zaidi na maumivu ya hedhi, na kujifungua

2: FLAGMETIC

-Wana uwezo mkubwa kiakili baada ya melancolin
-Uwezo wao katika utendaji wa mambo inasemekana ni kati ya asilimia moja na sitini
-Ni mabingwa wa kuahirisha mambo (mfano kama akitaka kwenda kupalili shamba, akafika na kukuta kuwa majani ni -machache atabeba zake jembe na kurudi nyumbani hata kama ni msimu wa kupalilia)
-Wanapenda sana kupuuzia mambo ikiwa hawakuyaelewa ama kuyaona kwa macho yao wenyewe
-Hawapendi kukubali ama kusifia mafanikio ya wenzao
-Ni kundi la watu wabishi sana na ambao ni mahiri wa kujenga hoja kwa jambo wanalolitetea
-Katika ushindani hasa wa hoja huwa hawakubali kushindwa kirahisi (anaweza kusema mti ni gari akajenga hoja akazitetea na wote mkakubali hata kama ni kwa shingo upande)
-Mawakili majaji na mahakimu mahiri duniani ni wale wanaotoka katika kundi hili
-Ni watu wanaopenda kutafiti na kufuatilia mambo mbalimbali ndio maana maongezi yao mengi hatawaliwa na mifano na takwimu halisia
-Wanapenda kufuatilia mambo ya wengine pasipo hata msingi wowote (wanapenda sana ushushushu)
-Wapelelezi mahiri hutoka katika kundi hili
-Ni watu wasioumizwa kufanya makosa
-Hawapendi kuwaamini wenzao
-Ni wepesi wa kupokea lakini ni wagumu wa kutoa ama kujitolea kwa mambo mbalimbali
-Wanatafakari mambo kwa kina na kuyatolea uamuzi wa uhakika
-Mapenzi (love affairs) si kitu kinachowaumiza sana (kundi linaloongoza kwa kuwa single na ambalo ni rahisi kukubali talaka pale inapotokea migogoro katika ndoa zao)
-Wanasamehe haraka sana kwa sababu hawajali (they don’t care)
-Ni wagumu wa kuomba msamaha (i.e mara zote hutaka kuonekana kuwa wapo sahihi) ndio maana hupoteza nguvu za Mungu kirahisi (imani zao zikipoa huwa si rahisi sana kuamka)
-Ni wagumu wa kupokea mambo mapya hasa yahusuyo imani na sera, vile vile si rahisi kuachana na imani ama sera walizozipokea
-Si watu wanaojali muda na ratiba
-Ni rahisi kukatisha mahusiano ya aina yeyete pindi wanapogundua kusalitiwa ama kurubuniwa.
-Hawaogopi kumkosoa mtu ama kumuumbua hata kama ni hadharani
-Hawaumizwi na maneno ya watu dhidi yao
-Ni wasuluhishi wazuri wa migogoro ya kijamii na ya kimataifa na wenye ushawishi wa kina (i.e karama ya utele kwa neno la upatanisho ipo kwao)
-Ni kundi linalifanya mambo mengi lakini kwa ufanisi wa wastani
-Ni kundi la watu ambao sio wakereketwa wa masuala ya usafi na unadhifu (i.e kimavazi na kiutaratibu)
-Wakianzisha jambo huweza kuliachia njiani bila kulimaliza na wala wasiumizwe na kukwama huko
-Ni watu wasiopenda vurugu hasa demokrasia ya ushuluhishi wa hoja inapokwama
-Wapo tayari kusalimisha chochote walicho nacho ilimradi wabakie na amani (wanafahamika kama peace makers)
-Watu waliojaa dharau na ambao muda wote huona wao ni bora kuliko wengine katika mambo yote
-Hawapendi kuelekezwa na mara nyingi eidha huwadharau viongozi wao ama hutengeneza mitazamo na hoja za kupinga matendo, kujitolea na maagizo ya viongozi wao.
-Wanapenda kutekeleza maagizo wanayopewa uso kwa uso na sio yale ya jumuia
-Wakiwa viongozi huweza kujikuta wakichukiwa na watu hasa pale watakapoendekeza tabia yao ya kutojali haja na matakwa ya wale wanaowaongoza.

3.SANGUINE

-Wana uwezo wa kawaida kiakili (mara nyingine mdogo)
-Ni wacheshi sana
-Watu walio na maneno mengi na wasiopumzika kuongea
-Wanajisikia raha sana pale wanapokuwa wakiongea na watu wengine wakiwasikiliza
-Wanapenda kuanika mambo yao binafsi mbele ya wengine
-Waigizaji wa kuchekesha wengi ni wakutoka katika kundi hili
-Wanapenda sana kujisifu na kujikweza
-Wanapenda sana kusifiwa hata kwa mambo ambayo hayana uhalisia
-Wanataka sana kuonekana mbele ya watu kwa kila jambo wanalolifanya.
-Wanavipaji vingi vizuri lakini wanahitaji kusifiwa na kuhamasishwa ndipo huvionesha kwa uhakika
-Wana hisi za zima moto (i.e wanahamasika haraka na kusahau haraka. Ikitokea ajali huwa watu wa kwanza kujitokeza eneo la tukio na kuanza kutoa msaada; lakini akiondoka pale anasahau kila kitu na hata kama ametumwa akalete ambulance, anaweza kuanza kufanya shughuli zake nyingine)
-Muda wote wako nadhifu (ni wakereketwa wa masuala ya usafi na unadhifu)
-Wana kiherehere sana.
-Wagumu wa kuelewa na wepesi wa kusahau
-Ni vinyonga katika tabia zao (wanuwezo wa kuigiza tabia zisizo zao kiuhalisia na watu wasiowajua wasiwagundue kirahisi)
-Wanashawishika haraka sana kupokea mambo mapya lakini ni rahisi kuyaacha
-Wasichana wa kundi hili si rahisi kurubuniwa kimapenzi kwa silaha ya ushawishi wa maneno, kwa sababu na wao wana maneno mengi
-Ni kundi linaloathiriwa sana na love affairs (i.e wao ni multiple lovers-ni kawaida kumkuta sanguine akiwa na wapenzi zaidi ya mmoja: __inasemekana kutokana na maneno yao mengi na ufundi wa kuigiza hisia na tabia wavulana wanaume wa kundi hili huwanasa wasichana kirahisi bila kutumia mtaji mkubwa.)
-Wawapo kwenye jamii hukubalika sana hasa kutokana na ucheshi wao na ukarimu walio nao.
-Wanapenda sana kuwasaidia watu ingawa ni kwa kujionesha
-Ni wahamasishaji wakubwa na wenye ushawishi wenye kukubalika kirahisi
-Ni kundi la wainjilisti wanaoongoza kwa kurudisha kondoo wengi kwa Bwana (wengi wana karama za kuhubiri kwa mvuto na ushawishi wa pekee)
-Hawaumii wanapokosolewa, ama wanaposhindwa jambo
-Ni kundi la watu waoga sana (wanajiamini sana kwa maneno lakini kivitendo ni kunguru)
-Si watunzaji wazuri wa siri (waropokaji)
-Wanapenda kujaribu kila jambo linalokuja mbele yao
-Wanaamini kuwa wao ndio watu bora kuliko wengine
-Wanapenda sana kusimulia mambo ya wengine
-Hawana aibu hata mbele ya watu wasiowafahamu wala kuwazoea
-Wanaume wa kundi hili huamini kuwa walizaliwa kwa ajili ya kuwasaidia wanawake
-Ni wavivu wa kufanya kazi, wanapenda sana starehe na anasa na ndoto za kufanikiwa kwa miujiza huwa zimewatawala (wanapenda kuwaza jinsi ya kupata bahati nasibu, kuzawadiwa fedha na hata kuokota fedha ama madini)
-Ni watu wasiojua namna ya kupanga na kuimudu bajeti kwa ustadi)
-Ni watu wa mipango isiyoona mbali (wakurupukaji) (Ministers of emmergency affairs)
-Ni wazuri katika kusifia(i.e wanazikubali kazi za wengine kirahisi na kwa dhati)
-Kutokana na porojo zao hujipatia marafiki wengi na hivyo kuwa maarufu
-Wanapenda kusikiliza na kusoma vitu ambavyo havina uchambuzi wa kina.
Mfano ni Petro mtume wa Biblia: alipenda kujaribu kila kitu (alipomwona Yesu anatembea juu ya maji alitaka na yeye kufanya hivyo) alipenda kufahamu kila kitu (aliuliza habari za siku za mwisho) alipenda kujionesha kuwa ni jasiri (aliahidi kuteswa na Yesu), alikuwa ni muoga sana (alimkana Yesu mara tatu kwa kuhofia kuteswa na wayahudi), alikuwa ni mwinjilisti wa kutumainiwa (alihubiri siku ya Pentekoste), alikuwa ni mwepesi wa kukubali pindi anapokosolewa (alikiri makosa baada ya kuonywa na Paulo juu ya upotoshaji wake wa kuhubiri kuwa hakuna wokovu kwa wasiotahiriwa)

4. COLERICK

-Wana uwezo wa kawaida kiakili
-Ni wa wakali na wakaidi
-Hawana huruma wala unyenyekevu
-Watu wasiopenda kudharauliwa ama kuonewa
-Wanapenda kuwatawala wenzao muda wote
-Ni viongozi kwa asili ya kuzaliwa
-Wanawaza kufanikiwa pekee na wala sio kushindwa
-Watu wasiokata tamaa mapema
-Wanajiamini kupita kiasi
-Hawana uoga ni majasiri sana
-Hisia zao hasa za upendo, mapenzi hazionekani kwa uwazi(hidden emotions)
-Kundi la watu wenye nguvu nyingi
-Ni madikteta
-Hawapendi kabisa kupingwa wala kukosolewa
-Watu wa kulipiza visasi
-Watu wa vitendo kuliko maneno
-Ni waonevu, wanapenda dhuruma na ubabe
-Ni watu wakulazimisha mambo hata kama hayawezekani
-Huwa wanatumiwa sana kwa ajili ya kuzima ghasia, uasi ama kuanzisha jambo lenye upinzani eneo fulani
-Wanafaa sana kuwa viongozi kutokana na uhodari wao wa kuwaongoza watu kwa sera za ushawishi wenye mlengo -wa kiukandamizaji
-Hawajui kubembeleza
-Hawaongei wala kucheka ovyo
-Wanapotenda jambo huwa wanawaza namna ya kunufaika na hata kama akimsaidia mtu anawaza namna ya kurudishiwa hicho alichokitoa
-Ni kundi la watu matajiri sana duniani hasa kutokana na uimara wao katika kuthubutu kutenda mambo na hali zao za kutoogopa hasara
-Si watu wanaopenda suluhu na amani
-Unadhifu na usafi wao ni wa wastani
-Hawapendi starehe kwa wingi
-Ni watu wanaoweza kufurahia mazingira yenye dhiki na shida
-Siku zote huwa wanatafuta kufanya mambo ya kihistoria ili wakumbukwe hata baada ya kufariki
-Wanafurahia kushuhudia na kutazama hadithi, matukio na filamu zilizosheheni ukatili na za kutisha
-Mifano ya watu wa kundi hilo: Idd Amin, Hitler, etc
*SI TABIA ZOTE ZA KUNDI LAZIMA ZIANGUKIE SEHEMU MOJA

MAMBO MUHIMU UNAYOPASWA KUFAHAMU

-Kila mtu amezaliwa na tabia fulani zinazomfanya awe katika kundi fulani
-Huwezi kujibadilisha kundi
-Kujifahamu kundi lako kunakuwezesha kurekebisha madhaifu uliyonayo na kuimarisha mazuri uliyonayo. Pia inakusaidia kuwatambua watu wengine hivyo kuwa makini namna ya kuishi nao
-Inawezekana kabisa kujifahamu upo kundi gani na pia kwa kusoma na kutazama ni rahisi kutambua makundi ya wengine

*NITATAMBUAJE MIMI NI WA KUNDI GANI?

-Watu wengi wana tabia za makundi zaidi ya moja-Kwa wale tabia zaidi ya asilimia themanini kutoka kundi fulani hao wanaitwa pure (i.e pure sanguine etc)-Kama una tabia kutoka kundi zaidi ya moja, unaunganisha majina ya makundi mawili yenye tabia nyingi zaidi, unaanza jina la lile lenye asilimia nyingi zaidi. *Mfano: flag-coleick; cole-flagmetic, flag-colerick , sangu-melancolic, melanco-sanguine: etc —

Jumatatu, Novemba 17, 2014

MUZIKI WA JADI CHINA



Bw. Liu Tianhua (1895---1932) alikuwa mtungaji muziki mashuhuri, mwanamuziki na mwalimu wa ala za muziki za jadi. Bw. Liu Tianhua alizaliwa mwaka 1895 katika ukoo wa msomi wa wilaya ya Jiangyin, mkoani Jiangsu. 

Ndugu watatu wa ukoo huo wote ni hodari. Mwaka 1912 Bw. Liu Tianhua alishiriki kwenye bendi moja mjini Shanghai, na kujifunza nadharia ya muziki, piano, fidla na za aina nyingine. Alirejea kwao mwaka 1914 na kufundisha masomo ya muziki katika shule moja ya sekondari. 

Mwaka 1915 Bw. Liu Tianhua alifiwa na baba yake, ambapo katika majonzi makubwa alitunga muziki “kupiga kite”, na kuanza kushika njia ya utungaji wa muziki. 

Ili kujifunza muziki ya jadi ya China Bw. Liu Tianhua aliwatembelea wanamuziki wa jadi na kujifunza kutumia ala za muziki za kijadi. Alifanya mageuzi kuhusu upigaji wa zeze la kijadi na kufanya upigaji wa ala hiyo ya muziki kuoneshwa katika maonesho ya muziki na kufundishwa katika vyuo vya muziki. 

Katika miaka 10 ya kutoka mwaka 1922 hadi 1932, Bw. Liu Tianhua alikuwa profesa wa ala za muziki za zeze ya kijadi, gambusi na fidla. Katika utungaji wa muziki alirithi ufundi wa utungaji wa muziki wa kijadi huku akijifunza mbinu ya utungaji wa muziki ya nchi za magharibi. 

Toka alipokuwa na umri wa miaka 17 Bw. Liu Tianhua alianza kufundisha muziki katika shule za msingi na sekondari, na alikuwa na uzoefu mwingi wa kufundisha, na aliweka msingi wa mfumo wa elimu ya muziki wa kijadi. 

Alipoanza kuwa na mafanikio makubwa Bw. Liu Tianhua alianza kuugua, mwezi Mei mwaka 1932. Wakati alipofariki alikuwa na umri wa miaka 38 tu. 

Muziki safi aliotunga Bw. Liu Tianhua ni pamoja na “Kupiga kite”, “wimbo wa majonzi” na “Usiku mwema”. 

Chanzo:http://swahili.cri.cn

Jumatano, Novemba 12, 2014

WAMILIKI WA BLOG TANZANIA WATAKIWA KUFUATA MAADILI YA UANDISHI WA HABARI

Mhandisi wa TCRA,Andrew Kisaka akiwasilisha Mada kuhusu maadili ya Uandishi  na Utangazaji  wa Habari


 Serikali imewataka wamiliki na waandishi wa blog nchini kuzingatia maadili ya taaluma ya uandishi wa habari wakati wa mchakato wa kuelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwezi ujao na uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani.



Wamiliki wa blog mbalimbali waliohudhuria katika mkutano huo

 Akizungumza jijini Dar es salaam hii leo wakati wa ufungaji wa mkutano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Wamiliki wa blog mbalimbali nchini Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Tanzania Assah Mwambene amesema serikali inatambua blog zinafanya kazi ya kutoa habari sawa na vyombo vingine vya habari lakini vinapaswa kuzingatia uandishi wa mambo ya msingi kwa kufuata maadili ya uandishi wa habari.



Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo nchini Tanzania Assah Mwambene


 Mwambene ambaye pia ni Msemaji wa serikali ameeleza kuwa lazima wamiliki na waandishi wa blog wajue wamechukua wajibu mkubwa unaoendana na wajibu wa kuwajibika kwa wananchi wanaowandikia habari wa kuzingatia maadili.


Kamati ya muda ya wamiliki wa blog iliyochaguliwa leo

 Awali akizungumza kwenye mkutano huo Mkurugenzi wa Utangazaji wa TCRA Habbi Gunze amesema waandishi na wamiliki wa blog wananafasi ya kusaidia umma kuweza kuelewa masuala mbalimbali ya uchaguzi pasipo upendeleo wowote wala uchochezi.



Mwenyekiti wa Kamati ya wamiliki wa blog Joachim Mushi


Kumekua na malalamiko toka kwa  wananchi kutokana na habari mbalimbali zinazoandikwa kwenye baadhi ya blog kwa kutozingatia maadili ya uandishi wa habari na utamaduni wa mtanzania jambo ambalo ni changamoto kwa serikali kutokana na uhuru uliopo kwa wamiliki wa blogi hizo na ukosefu wa sheria zinazowaongoza.

Jumanne, Septemba 16, 2014

MNARA MREFU MSITU WA AMAZON, BRAZIL




Nchi ya Brazil imeanza rasmi ujenzi wa mnara mrefu zaidi duniani huko Manaus mjini Amazon.

Mnara huo kwa jina Amazon observation Tower, unatazamiwa kutumika katika utafiti wa mapana wa hali ya anga.

Utakuwa na vifaa maalum venye uwezo mkubwa wa kukusanya data kuhusu gesi chafu iliyo hewani, chembe chembe za erosoli na hali ya anga ya kila uchao katika msitu wa Amazon.

Eneo hilo la Amazon ndilo linalinaloshuhudia mvua kubwa zaidi kila msimu.

Wanasayansi wa Brazil na Ujerumani wanatumai kuutumia mnara huu katika uchunguzi wao wa vyanzo vya gesi chafu na mabadiliko ya hali ya anga.

Kutokana urefu wake, mnara huu utawezesha wanasayansi kuelewa mabadiliko ya mwelekeo wa upepo kwa kitalifa cha zaidi ya kilomita mia moja katika msitu wa Amazon.
Msitu wa Amazon umekuwa ukikatwa kwa muda
Msitu wa Amazon ni kati ya misitu mikubwa zaidi duniani inayoathiri mazingira kwani inahusika pakubwa katika kuongeza na kupunguza kiwango cha hewa aina ya (carbon) angani.

Kulingana na bw. Paulo Artaxo, mwelekezi wa mradi huo kutoka chuo kikuu cha Sao Paulo, amesema mnara huo utasaidia pakubwa katika juhudi za kutafuta majibu ya maswali mengi kuhusu mabadiliko ya hali ya anga duniani.

Aidha, mnara huu unatarajiwa kutumiwa pamoja na minara mingine midogo ambayo tayari imejengwa nchini humo.

Kulingana na wajenzi, mnara huu utafanana na ule uliojengwa Siberiaya kati katika mwaka wa 2006.

Jumatatu, Septemba 15, 2014

UHODARI NA MOYO WA USHUJAA





Ndugu mpendwa, ni vyema sana kuwa nawe tena katika eneo hili.

Tuko hapa duniani katika kipindi cha ajabu katika historia yake. Nafasi zetu karibu hazina kipimo, na bado tunakumbana pia na changamoto nyingi, baadhi yazo za kipekee kwa wakati wetu.

Tunaishi katika ulimwengu ambapo maadili yametupiliwa mbali kwa kiasi kikubwa, ambapo dhambi imeanikwa wazi, na ambapo majaribu kupotoka kutoka kwenye njia nyembamba na iliyosonga yanatuzunguka. Tunakabiliwa na mashinikizo yasiyokoma na ushawishi wa kudanganya unaoharibu kile ambacho ni cha heshima na kujaribu kukibadilisha na falsafa na utamaduni duni.

Kwa sababu hizi na changamoto zingine, maamuzi daima yako mbele yetu ambayo yanaweza kuamua hatima yetu. Ili kwetu sisi kufanya maamuzi sahihi, ujasiri unahitajika---ujasiri wa kusema hapana wakati tunapaswa, ujasiri wa kusema ndio wakati inafaa, ujasiri wa kufanya jambo la haki kwa sababu ni la haki.

Kwa sababu viwango vya jamii hivi sasa kwa haraka vinaachana kwa mbali na maadili na kanuni ambazo Bwana ametupa, sisi bila shaka tutaitwa kutetea kile ambacho tunaamini. Je, tutakuwa na ujasiri wa kufanya hivyo?

Rais J. Reuben Clark Jr., ambaye kwa miaka mingi alikuwa mshiriki wa Urais wa Kwanza, alisema: “Zinajulikana kesi ambapo [wale] wa imani ya kudhaniwa … wamehisi kwamba, kwa sababu ya kudhibitisha imani yao kamili huenda wakajiitia kejeli ya wenzao wasioamini, lazima aidha warekebishe au kuelezea vyema imani yao, ama kuizimua kiuangamizi, ama hata kujifanya kuitupilia mbali. Watu kama hao ni wanafiki.” Hakuna yeyote miongoni mwetu angependa kuitwa mnafiki, na bado tunasita kutangaza imani yetu katika hali fulani. ?

Tunaweza kujisaidia katika hamu yetu ya kufanya mema tukijiweka katika maeneo na kushiriki katika shughuli ambapo mawazo yetu yanashawishiwa kwa ajili ya mema na ambapo Roho wa Bwana atasikia vizuri kuwa.

Nakumbuka nikisoma hapo awali ushauri ambao baba alimpa mwanawe wakati akienda shule: “Ukiwahi kujipata mahali ambapo haupaswi kuwa, ondoka!” Nawapa kila mmoja wenu ushauri huo huo: “Ukijikuta wakati wowote mahali ambapo haupaswi kuwa, ondoka!”

Sote tunahitaji kila mara kuwa na ujasiri. Kila siku ya maisha yetu ujasiri unahitajika---si tu kwa ajili ya matukio makubwa, lakini mara nyingi zaidi tunapofanya maamuzi ama kutenda kwa ajili ya hali zilizo karibu nasi. Mshairi na mwandishi Mskoti Robert Louis Stevenson alisema: “Kila siku ujasiri una mashahidi wachache. Lakini ujasiri wako bado una heshima hata kama hakuna anayekutia moyo na hakuna umati unaokusifu.”

Ujasiri huja kwa njia nyingi. Mwandishi Mkristo Charles Swindoll aliandika: “Ujasiri hauko tu kwenye uwanja wa vita … ama kwa kumshika kiushujaa mwizi katika nyumba yako. Vipimo halisi vya ujasiri ni kimya sana. Ni majaribio ya kindani, kama vile kubaki mwaminifu wakati hakuna mtu anayeangalia, … kama kusimama peke yako wakati watu hawaelewi imani yako.”

Ningeongezea kwamba ujasiri huu wa ndani pia unajumuisha kufanya jambo la haki hata kama huenda kuwa unahofia, kutetea imani yetu katika hatari ya kudharauliwa , na kudumisha imani hizo hata baada ya kutishwa na kupoteza marafiki ama hadhi ya kijamii. Yule ambaye anasimama dhabiti kwa yale ambayo ni ya haki lazima ahatarishe kuwa wakati mwingine hakubaliwi na kukosa umaarufu.

Mtu mmoja alipokuwa akihudumu katika Jeshi la Majini la Marekani alikuja kujua kuhusu matendo ya ujasiri, matukio ya ushujaa, na mifano ya ujasiri. Mmoja ambao kamwe hakuwahi sahau ilikuwa ujasiri usio wazi wa mwana maji wa umri wa miaka 18---sio wa imani yetu---ambaye hakuogopa kusali. 

Kwa watu 250 katika kitengo chetu, alikuwa ndiye peke yake ambaye kila usiku alipiga magoti kando ya kitanda chake, wakati mwingine akiwa anakejeliwa na kuchekwa na wasioamini. Akiwa ameinamisha kichwa, alimwomba Mungu. Kamwe hakuogopa kuomba. Kamwe hakuyumba. Alikuwa na ujasiri.

Muda mfupi uliopita, nilisikiliza mfano wa mtu ambaye hakika alionekana kukosa ujasiri huu wa ndani. Rafiki alisimulia kuhusu mkutano wa kiroho na wa kukuza imani ambao yeye na mumewe walikuwa wamehudhuria katika kata yao. 

Mvulana aliyekuwa katika ofisi ya mkuhani katika Ukuhani wa Haruni aligusa mioyo ya mkusanyiko mzima alipozungumzia kweli za injili na furaha za kutii amri. Alishuhudia kwa dhati akisimama kwenye mimbari, akionekana kuwa msafi na nadhifu akiwa amevaa shati yake nyeupe na tai.

Baadaye siku hiyo hiyo, mwanamke huyu na mumewe walipokuwa wanaondoka kule, walimuona mvulana yule yule ambaye alikuwa amewavutia sana saa chache tu awali. Sasa, hata hivyo, alionekana kubadilika kabisa akitembea barabarani akiwa amevaa nguo chafu---na anavuta sigara. 

Rafiki yangu na mumewe hawakuwa wamesikitishwa sana na kuhuzunika tu, lakini pia walichanganyikiwa na jinsi angeweza kusadikisha kuonekana kuwa mtu mmoja katika mkutano wa kiroho na kisha haraka hivyo kuonekana kuwa mtu mwingine kabisa.

Ndugu, je, wewe ni mtu yule yule popote ulipo na katika chochote unachofanya---mtu Baba yetu wa Mbinguni anataka uwe na mtu unajua unapaswa kuwa?

Katika mahojiano yaliyochapishwa katika gazeti la kitaifa, mchezaji aliyejulikana wa mpira wa kikapu wa NCAA Mmarekani anayeitwa Jabari Parker, mshiriki wa Kanisa, aliombwa ashiriki ushauri bora kabisa aliokuwa amepokea kutoka kwa baba yake. Jabari alijibu, “[Baba Yangu] alisema, kuwa mtu yule yule unapokuwa peke yako na vivyo hivyo unapokuwa mbele ya watu.” Ushauri muhimu, ndugu zangu, kwetu sisi sote.

Maandiko yetu yamejaa mifano ya aina ya ujasiri unaohitajika na kila mmoja wetu leo. Nabii Danieli alionyesha ujasiri mkuu kutetea aliyoyajua kuwa ya haki na kwa kuonyesha ujasiri wa kuomba, ingawa alitishwa na kifo kama angefanya hivyo.

Abinadi aliishi maisha ya ujasiri, ilivyoonyeshwa na kukubali kifo badala ya kukana ukweli.

Sisi sote tunavutiwa na maisha ya vijana askari 2,000 wana wa Helamani, waliofundisha na kuonyesha umuhimu wa kuwa na ujasiri wa kufuata mafundisho ya wazazi, kuwa waadilifu na wasafi?

Pengine kila moja ya hadithi hizi za maandiko zimepambwa na mfano wa Moroni, ambaye alikuwa na ujasiri wa kustahimili katika haki hadi mwisho

Katika maisha yake yote, Nabii Joseph Smith alitoa mifano isiyohesabika ya ujasiri. Mojawapo wa mfano mkubwa zaidi ulitokea wakati yeye na ndugu wengine walifungwa minyororo pamoja---fikiria, kufungwa minyororo pamoja---na kufungiwa katika nyumba ambayo haijamalizika karibu na jumba la mahakama kule Richmond, Missouri. Parley P. Pratt, ambaye alikuwa miongoni mwa wale waliofungwa, aliandika kuhusu usiku mmoja: 

“Tulikuwa tumelala ni kama tuko usingizini mpaka saa ya usiku wa manane kupita, na tulikuwa tumehuzunika sana, wakati tulikuwa tumesikiliza kwa masaa kejeli mbaya, maneno mabaya, kashfa kubwa na lugha chafu ya walinzi wetu.”

Mzee Pratt aliendelea:

“Nilikuwa nimesikiliza hadi nikachukizwa, nikasikitika, nikahudhika , na kujawa na roho ya haki ya kukasirika kwamba ilikuwa vigumu kwangu kujizuia kusimama na kuwakemea walinzi, lakini [mimi] sikuwa nimemwambia Joseph chochote, ama mtu yeyote mwingine, ingawa nilikuwa nimelala karibu naye na nilijua kwamba alikuwa macho. Ghafla, alisimama na kuzungumza kwa sauti ya nguvu kama mgurumo wa simba, akisema, vyema ninavyoweza kukumbuka, maneno yafuatayo:

“‘NYAMAZENI. ... Katika jina la Yesu Kristo nawakemea ninyi, na kuwaamurisha mtulie; sitaishi dakika ingine na kusikia lugha kama hiyo. Komeni kuongea hivyo, ama ninyi au mimi nife SAA HII!’”

Joseph “alisimama wima katika enzi ya kutisha,” kama ilivyoelezwa na Mzee Pratt. Alikuwa amefungwa kwa minyororo, bila silaha, na bado alikuwa mtulivu na mwenye heshima. Aliwaangalia walinzi waliohofia, ambao walikuwa wanarudi nyuma kwenye kona wakijikunyata miguu. Watu hawa walioonekana kutorekebishika waliomba msamaha kwake na wakabaki kimya.

Si vitendo vyote vya ujasiri huleta matokeo ya kuvutia kama hayo ama ya mara moja, na bado yote huleta amani akilini na maarifa kwamba haki na ukweli umetetewa.

Ni vigumu kusimama wima wakati mtu anapanda mizizi yake kwenye changarawe inayonyong’onyea ya maoni na idhinisho linalobobea. Ujasiri kama ule wa Danieli, Abinadi, Moroni ama Joseph Smith unahitajika ili tubaki imara na dhabiti kwa yale tunayojua ni mema. Walikuwa na ujasiri wa kufanya kile ambacho akikuwa rahisi, bali kile kilichokuwa sahihi.

Sote tutakumbana na hofu, tutakejeliliwa, na kukutana na upinzani. Acheni sisi —sisi sote—tuwe na ujasiri kushinda yanayopendelewa na wengi, ujasiri wa kutetea kanuni zetu. Ujasiri, si kuridhisha, hutuletea tabasamu ya idhini ya Mungu. Ujasiri unakuwa sifa ya uwezo na ya kuvutia wakati unachukuliwa si tu kama nia ya kufa kidume lakini pia kama uamuzi wa kuishi kwa heshima. 

Tunavyosonga mbele, tukijitahidi kuishi kama tunavyopaswa, hakika tutapokea msaada kutoka kwa Bwana na tunaweza kupata faraja katika maneno Yake. Naipenda ahadi Yake katika kitabu cha Yoshua: “Sitakupungukia wala sitakuacha. …

“...Uwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa Bwana, Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako.”

Ndugu yangu mpendwa, kwa ujasiri wa imani yetu, tutangazeni, pamoja na Mtume Paulo, “Siionei haya Injili ya Kristo.”Kisha, kwa ujasiri huo huo, tufuateni ushauri wa Paulo : “Uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo, na katika roho na imani na usafi.”

Migogoro ya janga huja na kwenda, lakini vita vinavyopigwa kwa nafsi za watu vinaendelea bila kukoma. Kama mwito linakuja neno la Bwana kwenu, kwangu mimi, na kwa wenye ukuhani kila mahali: 

“Kwa sababu hiyo, sasa acha kila mtu na ajifunze wajibu wake, na kutenda kazi katika ofisi ambayo ameteuliwa, kwa bidii yote.” Kisha tutakuwa, kama vile Mtume Petro alivyotangaza, hata “ukuhani wa kifalme,”na umoja katika kusudi na kubarikiwa na nguvu kutoka mbinguni.

Acha kila mmoja wetu aondoke siku ya leo akiwa na dhamira na ujasiri wa kusema, pamoja na Ayubu wa kale, “Kwa kuwa uhai wangu ukali mzima ndani yangu,...sitajiondolea uelekevu wangu.” 

Naomba kwa unyenyekevu kwamba hii iweze kuwa hivyo katika jina la Yesu Kristo, Bwana wetu, Amina.

Jumatatu, Agosti 11, 2014

HISIA YA SITA


Naomba 'kushea' nawe kitu kinachojulikana kama TELEPATHY. Kwa kifupi, telepathy ni uwezo wa kuwasiliana na mtu mwingine bila kutumia hisia 5 za kawaida (kugusa, kuongea, kuona, kunusa au kusikia). Katika familia, walio na mapacha watakuwa wananielewa Kulwa  na Doto. 

 Kuna matukio mengi ya telepathy kuwahusu mapacha hao lakini nafasi hairuhusu kuyataja yote. Lakini si kwa mapacha tu.Mara nyingi kama upo mbali halafu msiba unatokea, kina uwezekano wa kuota ndoto inayohusiana na msiba usiku wa mkesha wa tukio hilo. Hiyo ni telepathy ya aina flani. 

Pia mara kadhaa unaweza kumfikiria mtu flani na muda huohuo akakupigia simu au kukutumia meseji. Hiyo pia ni telepathy. Au unaweza kutamani kuwasiliana na mtu flani, na ukicheki emails zako unakuta amekuandikia. Japo hakuna maelezo ya moja kwa moja kuhusu telepathy, inafahamika kuwa mtu anaweza kujifunza na kuboresha uwezo wake wa telepathy kwa kutumia meditation (sijui neno la Kiswahili ni nini). 

Mashushushu (spies) hufunzwa kuendeleza kitu kinachojulikana kama 'hisia ya sita' yaani zaidi ya hisia tano za kawaida nilizozitaja hapo juu. Hisia ya sita ambayo ni kama telepathy kwa namna flani huwawezesha kubashiri mambo karibu kabisa na usahihi. Lakini kama nilivyobainisha, hata mtu wa kawaida pia aweza kujifunza...lakini madhara yake ni pamoja na kufahamu matukio yatayojiri mbeleni bila kuwa na uwezo wa kuyazuwia. Anyway, I thought I should share with you about this interesting phenomenon.

Jumamosi, Agosti 02, 2014

MSAADA WA MAANA



Kwa sababu hiyo tunapaswa kutafuta majina tofauti kwa makala zinazohusu maana tofauti ya jina lilelile.

Mfano wa makala ya maana kuhusu "Mwezi"
Makala ya maana inakusanya maana hizi zote kwenye ukurasa wa pamoja. Haina maandishi marefu bali maelezo mafupi tu mfano: .

  1. mwezi (gimba la angani) - msindikizaji wa sayari
  2. mwezi (wakati) - mojawapo wa vipindi kumi na mbili vya mwaka
Vivyo hivyo:

  1. Ndege (mnyama) - aina wa wanyama ambao kwa kawaida wanaweza kuruka
  2. Ndege (uanahewa) - chombo cha usafiri kinachoweza kuruka wakati kikiwa na abiria au mizigo ndani yake
Isipokuwa kama maana mbalimbali yana historia ya pamoja au uhusiano wa pekee ni sawa kuongeza chini ya orodha ya viungo maelezo ya ziada. Zisihusu viungo moja-moja. Mfano:

Majengo inataja mahali pengi Afrika ya Mashariki kwa hiyo tunatofautisha Majengo (Kigoma), Majengo (Mbeya mjini) na kadhalika. Mitaa au kata hizi zote zina historia ya kufanana inayoelezwa chini ya orodha.

Jumanne, Julai 29, 2014

JIWE LA THAMANI BAHARINI


Ndani ya bahari samaki-gamba mkubwa sana anasonga polepole kati ya miamba, akila magugu-maji yanayoyumbishwa na mikondo ya bahari. Gamba lake la nje lililofunikwa kwa asidi na viumbe vidogo vya maji, hufanya isiwe rahisi kuona rangi zake nyangavu, yaani, rangi tofauti-tofauti za bluu, kijani, na zambarau zilizochangamana na manjano na waridi, na sehemu ndogo zilizo na rangi ya dhahabu na fedha.


Kiumbe huyo wa kushangaza ni paua, wa jamii ya moluska anayepatikana New Zealand peke yake. Kiumbe huyo na viumbe wengine wa jamii hiyo wanaishi chini ya maji karibu na pwani zenye miamba. Ingawa paua anapendwa kwa sababu ya rangi za kupendeza za gamba lake la ndani linaloweza kutumiwa kutengeneza vito maridadi, watu wengi wanapenda nyama yake tamu. Kwa kuongezea, lulu zenye kung’aa sana zinaweza kukuzwa ndani yake.


Kuna jamii zaidi ya 100 za moluska ulimwenguni pote zinazopatikana Afrika Kusini, California huko Marekani, Japani, Australia, na katika kisiwa cha Guernsey kilicho kwenye Mlango-Bahari wa Uingereza. Hata hivyo, katika eneo la kusini la bahari ya Pasifiki Kusini ndiko tu unaweza kupata moluska mwenye rangi nyangavu wa New Zealand, anayeitwa paua (Haliotis iris).


Muujiza wa Kibiolojia


Ndani ya gamba la paua, matabaka ya protini na kalisi hukusanyika na kutokeza rangi maridadi kama jiwe la thamani linaloitwa opali. Kwa sababu hiyo, paua amejulikana kuwa jiwe hilo la thamani la baharini. Kiwango cha joto baharini kinaposhuka, moluska hulala. Kisha matabaka ya magamba yao huchukua muda mrefu zaidi kukua. Mtaalamu mmoja anaamini kwamba rangi mbalimbali za paua huenda zinatokana na virutubisho katika maji na pia rangi mbalimbali za magugu-maji ambayo moluska hula.


Paua huchagua chakula chao kwa uangalifu na vilevile wao huchagua wataishi karibu na nani. Hawawezi kuishi karibu na mwanamizi mwenye miiba, au kina, kwa sababu wanakula aina zilezile za magugu-maji. Pia, kiti cha pweza ni adui hatari kwani wachache tu kati yao wanaweza kumaliza familia nzima ya paua. Kwa ujanja, kiti cha pweza huwekelea mnyiri kwenye mashimo ya kupumulia ya paua na hivyo kufanya asiweze kupumua. Kisha, paua anapoanguka kutoka kwenye jiwe alilolalia, kiti cha pweza humla kwa urahisi.


Matumizi Mbalimbali ya Paua


Ingawa sehemu nyeusi ya nje ya paua haipendezi sana, kwa karne nyingi wenyeji wa New Zealand wanaoitwa Wamaori wamekula paua. Sehemu inayoweza kuliwa ya paua ni musuli mkubwa, au mguu, ambao kiumbe huyo hutumia kusonga kwenye miamba. Pia Wamaori wametumia gamba lake katika mapambo na kama chambo cha kuvua samaki. Wametengeneza vito kwa kutumia magamba yake na wameyatumia kama macho katika michongo yao.


Sasa paua anapendwa sana kuliko wakati mwingine wowote. Watalii hawakosi kununua vito vya paua wanapotembelea New Zealand.


Leo, watu wanaopiga mbizi bila vifaa vya kupumua, wanawavua paua kwa wingi sana. Hiyo imekuwa biashara inayoletea New Zealand dola milioni nyingi sana kutoka kwa nchi za nje. Ili kuhakikisha kwamba paua hawaangamizwi huko New Zealand, serikali imeweka kiwango cha paua wanaoweza kuvuliwa kwa mwaka. Nyama nyingi hutiwa katika mikebe ili ikauzwe huko Asia, na nyingine hugandishwa na kutumwa Singapore na Hong Kong ambako paua wanapendwa sana ingawa wanauzwa kwa bei ghali sana. Mara nyingi, analiwa akiwa mbichi na kukatwa vipande-vipande. Ingawa kuna paua wengi sana huko New Zealand, wenyeji wengi hawajawahi kuonja nyama yake kwa sababu ya kuuzwa sana katika nchi za nje.


Ili waweze kutosheleza uhitaji wa kimataifa wa paua, wafanyabiashara wanatumia mbinu za kisasa kuwafuga. Wafanyabiashara huko Australia, Japani, na Marekani wamefaulu kutumia mbinu hiyo ili kufuga moluska wengine. Mbinu mpya kama hizo zimesaidia paua wafugwe katika matangi yenye mifumo ya kudumisha kiwango kinachofaa cha joto mbali sana na maeneo wanayopatikana kwa ukawaida.


Paua wa kufugwa wanakula kwa kiasi kilekile kama wale wa kiasili. Kila juma wanaweza kula chakula chenye uzito sawa na nusu ya uzito wao. Kwa kushangaza, paua pia wanaweza kusonga haraka. Wanapopinduliwa, wanaweza kujigeuza upesi sana. Ni kazi rahisi kufuga paua. Mtaalamu mmoja anasema kwamba “inafurahisha kufuga paua kwa sababu ni wapole na wenye adabu, na hawawasumbui wafugaji!”


Lulu za Paua


Zaidi ya kutokeza vito vinavyotengenezwa kutokana na magamba yao na kutumiwa kama chakula, paua wanaweza pia kutokeza lulu zenye kung’aa. Ni vigumu kupata lulu za asili katika paua wanaoishi baharini. Lakini wanaweza kutokezwa kupitia mbinu iliyobuniwa katika miaka ya 1890 na mwanasayansi Mfaransa Louis Boutan. Kito chenye umbo la yai kilicho na rangi za kuvutia kama za gamba la paua hutokezwa. Mbinu hiyo hufanya kazi jinsi gani?


Vipande vya udongo, mbao, mfupa, au chuma, huwekwa ndani ya gamba la paua katika sehemu tatu, yaani, mara mbili kwenye upande na mara moja mgongoni. Pole kwa pole, paua hufunika vipande hivyo vilivyoingizwa ndani ya gamba lake kwa matabaka ya lulumizi, yaliyotengenezwa kwa kalisi kaboni, na conchiolin. Kwa angalau miezi 18, maelfu ya matabaka hutokezwa na kufanyiza lulu ndogo. (Ona sanduku lililo chini.) Inachukua miaka sita ili kufanyiza lulu kubwa. paua 1 hivi kati ya 50 hutokeza lulu ambayo imekaribia kuwa kamili. Hii ni lulu laini, yenye rangi nyangavu, na inayong’aa kwa kustaajabisha.


Bado watafiti hawajafaulu kutokeza lulu yenye umbo la mviringo kutoka kwa paua. Hiyo ni kwa sababu, tofauti na chaza, paua ana musuli katika tumbo ambao hutema kitu chochote kinachowekwa katika mfumo wake wa kumeng’enya. Huenda siku moja mtu akagundua siri ya kutokeza lulu ya mviringo.


Kwa sasa, tunaweza kufurahia vitu tunavyopata kutoka kwa samaki-gamba huyu aliye na matumizi mengi, yaani, vito vyenye kupendeza, nyama tamu, na gamba lenye rangi maridadi. Je, hatumshukuru Mungu kwa kutupa zawadi yenye kupendeza kama hiyo?—Yakobo 1:17.

Jumamosi, Mei 31, 2014

Mazoezi Ya Kujenga Misuli Ya Mwili Bila Kunyanyua Vyuma.

Tofauti na unyayuaji vyuma vizito, zipo njia nyingine za kukuza misuli na kufanya mwili kuwa katika hali ya mvuto kuliko hata ya myanyua vyuma, na kuufanya mwili kujijenga kwa usawa bila kuwa na utofauti wa ukubwa wa misuli ambao wanyanyua vyuma vizito wengi wao walivyo, haya hapa ni mazoezi kumi na matano yatakayokuweka vizuri kiafya na kimuonekano...
  • Push up
  Ni zoezi linalopanua kifua, kujenga kifua, kukuza misuli ya mikono ya ndani na nje na ni zoezi zuri la kuanzia, kama unataka kuwa na mwili wa kujijenga vizuri anza na hili zoezi.

  • Pull ups
 Pull ups inafanyisha kazi kila misuli mwilini, hasa misuli ya mikono na mgongo, ukitaka uwe na nundu za mikono kama za Jean Claud Vandame hili ndo hasa zoezi lako.

  • Plank
Ukishikilia hili zoezi bila kutingishika kwa dakika kadhaa, wewe kweli utakua una nia na kuubadilisha mwili wako liwe hekalu la mvuto. Zoezi hili linahitaji mabega yaliyoshiba na linafanyisha kazi misuli ya mikono, kiuno, mgongo, shingo na miguu na zoezi hili lina zawadi moja, linafanya tumbo lako likatike mara sita.

  • Roll Out
    Hili zoezi linafanana na la nusu push up(Plank), ila linachobadilisha ni kusukuma nondo kuelekea mbele na kurudi, na jinsi unavyoendelea kusukuma nondo ndo ambavyo zoezi linavyozidi kuwa gumu, kwa hio unahitaji nia na kujitoa kweli, faida zake linajenga misuli ya mgongo, kiuno, kifua na kutanua mabega. 

  •  Glute bridge
    Zoezi hili linajenga mgongo na misuli yote inaouzunguka, ukiwa mkufunzi wa hili zoezi kinachofuata ni kuombwa namba tu na wasichana.

  • Iverted Row
    Hili zoezi ni la mgongo, fuata kama picha inavyolionyesha, faida zake linafanya kifua kiwe kipana zaidi na mikono iwe na stamina zaidi.

  • Close Hands Push ups
    Hili zoezi ni kwa ajili ya mikono, na ni kwa ajili ya nundu za ndani na nje ya mikono, na misuli yako inakua inakua kwa pamoja bila kutegeana, fanya hili zoezi na utaona mabadiliko makubwa kwenye mikono yako.

  • Star Plack
    Hili zoezi kidogo ni zito kidogo, na zoezi hili linalenga kifua na mabega pamoja na misuli ya miguu na mikono, na ni zuri kwa kukata tumbo.

  • Burpee
    Zoezi la kupunguza mafuta mwilini, zoezi hili linafanya mwili mzima uchemke kwa pamoja, ukiwa unafanya hili, unakua unafanyisha kazi kila kiungo cha mwili na kuondoa sehemu dhaifu mwilini.

  • Dip
    Zoezi la misuli ya nyuma ya mkono na linasaidia pia kwenye misui ya kifua na upanuaji wa mabega na kufanya kifua kikae vizuri, zoezi hili linahitaji nia na nguvu ili lifanyike kwa mpangilio unaotakiwa na linamzidi yule aliyelala kwenye benchi akinyanyua vyuma vizito.

  • Bulgaria Split Squart
    Kichura chura cha mguu mmoja nyuma, kinafanyisha kazi misuli ya mapajani na kukufanya uwe na stamina zaidi, ukifanya hili kwa wiki kadhaa, kama kichura chura cha kawaida kilikua kinakupiga chenga basi utakua unafanya mara mbili ya zaidi ulivyokua unafanya.

  • Suspended Push ups
     
    Push ups ni nzuri, ila ukiiongezea ugumu kidogo kwa kuiongezea suspenda, ni njia mojawapo ya kuiongezea misuli uzito, na kufanya iwe misuli yenye ujazo na ya muda mrefu tofauti na yule anaebeba vyuma vizito.

  • Prone Back Extension
    Hili zoezi linahimalisha kiuno, tumbo na mgongo kwa ujumla.

  • Pike Push ups
    Ukiwa mkongwe wa push ups, hili ndilo zoezi la mwisho la push ups na linasaidia kuimalisha mabega na kuongeza ubora wa viazi vyako vya mikono.

  • Swiss Ball Ro-------+++++++llout
    Zoezi linavyozidi kuwa gumu ndo misuli inavyozidi kuongezeka, ukiweza kuzingatia haya mazoezi utajishangaa baada ya wiki tatu mfululizo ukiwa unayafanya.
 Chanzo: waulize wanaume
  •