Jinsia: Mwanamme
Linakotumika: Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, kwa watumiaji wa Biblia.
Linavyotamkwa:
1. JO-SEF (Uingereza).
2. ZHO-ZEF (Kifaransa).
3. YO-ZEF (Kijerumani).
Linatokana na jina la kilatini lililotokana na jina la kiyunani (LOSEPHOS), lililotokana na jina la Kiebrania (YOSEF) likiwa na maana ya:
“ATAZIDISHA au ATAONGEZA” (He Will Add).
Katika agano la kale Biblia takatifu inaeleza Yusufu na Joseph ni mwana wa kumi na moja wa Yakobo (Israel).
Kwa sababu ya kupendwa sana na baba yake Yusufu alionewa wivu na ndugu zake, wakamchukia, wakamuuza akapelekwa Misri kisha wakaenda kumweleza baba yao uongo kwamba alikuwa amekufa.
Lakini huko Misri Yusufu aliongezewa neema ya Mungu akapandishwa cheo na kuwa Mshauri mkuu wa Farao.
Jina hili pia limetumiwa na watu wengine wawili ndani ya biblia takatifu waliocheza nafasi muhimu sana ya kiroho na kimaandiko ambao ni Yusufu mume wa Bikira Mariam na Yusufu tajiri wa Arimathaya aliyenunua kaburi la kifahari akalitumia kuhifadhi mwili wa Bwana Yesu Kristo baada ya kufa msalabani.
DO NOT GIVE UP. THE BIGINNING IS ALWAYS THE H a r D e s t. "NI HERI KUFA KATIKA FIKRA ZINAZOISHI KULIKO KUISHI KATIKA FIKRA ZILIZOKUFA."
Mtayarishaji
Morning Star Radio
Jumapili, Novemba 07, 2010
Jumanne, Oktoba 19, 2010
KUPATA MORNING STAR RADIO FM
KUTUPATA KWA HOPE CHANNEL INTERTAIONAL
Big Satelite Dishes freq,04070 symbol rate 03003 vertical polrity 2/3.
Small Satelite Dishes freq,26657 vertical polrity 7-10,all frm intelsat Satelite located 68.5 degree east
Big Satelite Dishes freq,04070 symbol rate 03003 vertical polrity 2/3.
Small Satelite Dishes freq,26657 vertical polrity 7-10,all frm intelsat Satelite located 68.5 degree east
Jumamosi, Oktoba 16, 2010
MAPANGO YA AMBONI
Mapango ya Amboni yako katika eneo la Kiamoni, kata ya kiamoni, tarafa ya chumbageni, wilaya ya tanga, mkoa wa tanga. Ni eneo zuri la kupumzikia, kwa tafi za kihistoria, kijiografia, kijiolojia, n.k
Mapango haya yako umbali wa kilomita 8 toka tanga mjini kupitia barabara kuu inayoelekea Mombasa. Unaweza kufika katika hifadhi ya mapango kwa kupitia mojawapo ya njia zinazoelekea huko. Ya kwanza ni barabara ya changarawe iliyo upande wa kushoto meta 200 baada ya kuvuka daraja la hofu, ya pili iko kilometa 1.5 kutoka daraja la utofu katika kituo cha ukaguzi wa mazao ya misitu. Njia zote zinapitia katikati ya kijiji cha kiamoni.
Mapango haya yametokana na mabadiliko ya nguvu za asili zilizobadilisha maumbile ya miamba ya chokaa kipindi cha jurasiki (Jurassic period) kama miaka inayosadikiwa kuwa zaidi ya milioni 150 iliyopita. Kulingana na tafiti zilizokwishafanywa, eneo hili la mapango lilikuwwa tena chini ya maji miaka milioni 20 iliyopita na linakadiriwa kuwa na ukubwa wa kilometa za mraba 234 lenye mazingira ya miamba ya chokaa. Ni eneo ambalo linapitiwa na mito na limejaa uoto wa asili.
Miamba ya chokaaa kwa asili huundwa na madini ya kashiamu kabonate [ Calcium carbonate=CaCo3]. Miamba hii ni migumu kumomonyolewa na maji ya kawaida, lakini ni rahisi kuyeyushwa na maji yenye kiasi kidogo cha tindikali ya kaboni (Carbonic Acid). Tindikali ya kaboni iliyobadilisha maumbile ya miamba hii kwa kumomonyoa na kusababisha mapango yaweza kutokana na maji ya mvua yanapochanganyika na dioksidi ya kaboni (carbodioxide) hewani kabla ya kufika ardhini au na dioksidi ya kaboni inayopatikana ardhini. Maji yanapojipenyeza ardhini huendelea kupokea dioksidi ya kaboni kutoka muozo wa viumbe hai kama mimea na wanyama na kutengeneza tindikali. Tindikali ya kaboni inapopambana na madini ya kashiamu kaboneti (calcium carbonate) katika miamba ya chokaa husababisha kumomonyoka kwa miamba hii katika maeneo mbalimbali na kusababisha mapango. Mabadiliko haya huitwa kabonesheni (carbonation). Angalia mchanganuo wa kemikali ufuatao.
Wataalam wanaelezea njia mbalimbali zilizosababisha mapango katika eneo hili.
Kulingana na utafiti uliofanywa na mturi (1979), njia ya kwanza ni ile ya maji ya mvua yanapochanganyika na hewa ya “Carbondioxide” katika anga na kutengeneza tindikali (carbonic acid) ambayo inauwezo wa kuyeyusha madini ya calcium carbonate yanaunda sehemu kubwa ya miamba ya chokaa. Maji haya yenye tindikali husababisha mabadiliko kidogo yanapotelemka kuelekea ardhini. Yakifikia meza ya maji (water table) huku yakiendelea kuongezeka huzidi kuchanganyika na carbondioxide) iliyoko kwenye maji ardhini.
Kina cha maji kikiongezeka maji haya yenye tindikali huwa na uwezo wa kuyeyusha maungio ya miamba katika sehemu laini zaidi za miamba na kusababisha nyufa. Nyufa hizi huzidi kupanuliwa na maji yanayotembea na kusababisha baadhi ya mawe kuporomoka na kufanya mapango. Kasi ya maji inapozidi njia ndogondogo hupanuliwa na kuwa kubwa zaidi na upo uwezekano mapango madogo madogo hupanuliwa na kuwa kubwa zaidi na upo uwezekano mapango madogo madogo kuunganishwa na hatimaye kuwa na mfululizo wa mapango kama yanavyoonekana katika eneo hili.
Kina cha maji kinapopungua eneo huachwa likiwa kavu, lakini mabadiliko hayo huweza kuendelea kutokea chini zaidi na kusababisha njia na mapango mengine katika kina kingine ambapo hutokea muunganiko wa mapango kwa baadhi ya maeneo.
Njia nyingine ni pale ambapo inasemekana eneo hili lilikuwa chini ya usawa wa bahari yaani pembeni ya ufuko wa bahari. Mawimbi ya bahari yakamomonyoa miamba ya chokaa na kusababisha mapango. Baada ya bahari kurudi nyuma kutokana na kupungua kwa kina chake katika eneo hili, eneo la mapango likaachwa likiwa kavu.
Njia zote zilizoelezwa zimehusika katika kutokea kwa mapango haya, Mapango ya kwanza yatakuwa yalitokana na mmomonyoko wa miamba ya chokaa kutoka na maji ya ardhini yenye tindikali yaliyoyeyusha maungio ya miamba ya chokaa na kusababisha mapango. Kina cha bahari kilipopanda, maji ya bahari yalifikia eneo la mapango na mawimbi yake kusababisha kupanuliwa kwa mapango au mabadiliko katika kuta za nje na ndani ya mapango. Kina cha bahari kiliposhuka, eneo la mapango kilikuwa chini sana, maji ya mvua yenye tindikali yamekuwa na uwezo wa kuendelea kupanua na kubadilisha mfumo wa mapango.
Haijulikani mapango haya yaligunduliwa lini, bali taarifa zilizopo zinaonesha kwamba watu wa makabila yaliyoishi jirani na eneo la mapango: Wabondei, Wasambaa, Wadigo, na Wasegeju wamekuwa wakiya tumia kwa ajili ya matambiko ya mizimu tangu karne ya 16. Eneo hili la mapango kwa wakati huo lilijulikana kama eneo la mzimu wa mabavu.
Watu wanaamini habari za nguvu za mizimu katika kutatua matatizo ya uzazi, kuongeza kipato, magonjwa n.k. Kwa hivi sasa hutoka sehemu mbali mbali za Afrika Mashariki na kuja kuomba au kutambikia mizimu katika vijipango mbali mbali. Mbali na matumizi hayo, kampuni ya kigeni iliyojulikana kama “Amboni Limited” ilimiliki mashamba ya mkonge katika eneo la ta nga na kuweka eneo hili chini ya himaya yake mwaka 1892 ili kulitumia kama sehemu ya kupumzikia. Hii inatokana na mazingira mazuri na yenye utulivu ya mapango ya Amboni. Baadaye kampuni hii ilijulisha serikali kuhusu kuwepo kwa mapango haya. Serikali ilichukua hatua kutangaza eneo la mapango kuwa eneo la hifadhi mwaka 1922.
Mwaka 1937 ilipitishwa sheria ya mambo ya kale (Monuments Preservation Ordinace of 1937) iliyofuatiwa na ile ya 1953 (Monuments Preservation Ordinace of 1953) ambayo ingesaidia kulinda mambo ya kale ikiwa ni pamoja na mapango ya amboni. Mwaka 1963 serikali ya Tanganyika ikayaweka mapango chini ya usimamizi wa idara ya mambo ya kale. Mwaka 1964 serikali ilisimamisha sheria ya kikoloni ya 1937 na 1953 na kupitisha sheria ya mambo ya kale ya mwaka huo (The Antiquities Act of 1964) iliyofanyiwa marekebisho mwaka 1979 (Amendments Acts of 1979) kwa ajili ya kulinda mambo ya kale nchini. Kwa upande wa mapango ya Amboni, mbali na mambo mengine sheria inakataza kuandika au kuchora kwenye kuta za mapango.
Kuna miamba yenye maumbo ya kuvutia yanayofanana na Sofa/Kochi, Meli, Mamba, Tembo, Sanamu ya bikira maria n.k. Kuna vitu vinavyoonekana kama michoro inayofanana na unyayo wa mguu wa binadamu, na mnyama inayotokana na uchafu, hasa vumbi na udongo ambao hunywea pamoja na maji ya mvua na hatimaye kuganda katika paa la pango. Alama nyingine ni zile zilizosababishwa na popo wanaoishi mapangoni.
Kuna miamba inayokua au kuongezeka (Speleothems/Dripstones) kutokana na mabadiliko ya kikemikali katika miamba ya chokaa. Mabadiliko haya hutokana na maji yenye tindikali kuyeyusha madini ya “Calicium Carbonate”, kuyahamisha na kuya rundika katika eneo jingine. Mtokeo ni kupata miamba inayokuwa kutoka juu kuelekea chini (stalactite) au inayoelekea juu (stalagmite). Kulingana na utafiti uliofanywa na Mapunda na Msemwa (2005:101). Miamba ya aina hii huongezeka/kukua kwa kasi zaidi kipindi cha mvua kuliko kipindi cha kiangazi. Katika miaka kumi iliyopita, ukuaji wa miamba ya aina hii ni milimeta 0.5 kila baada ya miaka 100. Na kwamba iliwahi kuongezeka kwa kasi ya milimeta 7 katika kila miaka 100 kipindi cha kati ya miaka 38,000 na 34,000 (38 & 34 Ka)
Yapo masimulizi mengine yanayohusu mapango haya, mfano:
Kuna simulizi zinazoelezea njia za mapango zinazoelekea Mombasa, Maweni, Mkoa wa Kilimanjaro n.k. Vile vile zipo simulizi za Osale Otango (Samuel Otango) na (Paulo Hamis). Watu hawa waliwahi kutumia kituo namba tatu ndani ya pango kubwa kama sehemu yao ya kujificha kati ya mwaka 1952 na 1956 huku wakiendesha harakati za kupambana na walowezi waliokuwa wamewekeza katika maeneo ya Tanga. Walipora mali na kutishia maisha ya walowezi katika maeneo mbalimbali. Serikali ya kikoloni iliwatambua kama wahalifu na kujaribu kuwakamata bila mafanikio kwa kipindi kirefu. Mwaka 1957 Paulo Hamis alipigwa risasi maeneo ya Lushoto na kufariki. Wananchi wa kawaida wanawakumbuka kama mashujaa walioendesha harakati za ukombozi wa watu wanyonge kutoka katika mikono ya walowezi na watawala wa kikoloni.
NUKUU:
Habari hizi zimeandikwa kutokana na masimulizi pia maelezo kutoka katika vitabu mbalimbali:-
1. Institute of Curriculum Development: Geography Coourse Book for Secondary Schools Book 3.
2. Lutgens, F.K and Edward J.Tartbuck (2000). Essentials of GEOLOGY. SEVENTH EDITION. Upper Saddle River, New Jersey: Printice-Hall, Inc.
3. Mapunda, B.B.B and Paulo Msemwa (2005). Slavaging Tanzania’s culture Heritage, Dar es Salaam. Dar es Salaam University Press.
4. Mturi, A.A (1998). Archeology of Tanzania, Dar es Salaam: The Open University of Tanzania.
5. Mturi, A.A (1975). A guide to Tongoni Ruins, Dar es Salaam.
Ama, unaweza kupata maelezo zaidi kwa kuwasiliana kupitia mawasiliano haya:
Mapango ya Amboni.
S.L.P 5028,
TANGA.
Simu: +255 784 788 990 na +255 784 546 302.
Mapango haya yako umbali wa kilomita 8 toka tanga mjini kupitia barabara kuu inayoelekea Mombasa. Unaweza kufika katika hifadhi ya mapango kwa kupitia mojawapo ya njia zinazoelekea huko. Ya kwanza ni barabara ya changarawe iliyo upande wa kushoto meta 200 baada ya kuvuka daraja la hofu, ya pili iko kilometa 1.5 kutoka daraja la utofu katika kituo cha ukaguzi wa mazao ya misitu. Njia zote zinapitia katikati ya kijiji cha kiamoni.
Mapango haya yametokana na mabadiliko ya nguvu za asili zilizobadilisha maumbile ya miamba ya chokaa kipindi cha jurasiki (Jurassic period) kama miaka inayosadikiwa kuwa zaidi ya milioni 150 iliyopita. Kulingana na tafiti zilizokwishafanywa, eneo hili la mapango lilikuwwa tena chini ya maji miaka milioni 20 iliyopita na linakadiriwa kuwa na ukubwa wa kilometa za mraba 234 lenye mazingira ya miamba ya chokaa. Ni eneo ambalo linapitiwa na mito na limejaa uoto wa asili.
Miamba ya chokaaa kwa asili huundwa na madini ya kashiamu kabonate [ Calcium carbonate=CaCo3]. Miamba hii ni migumu kumomonyolewa na maji ya kawaida, lakini ni rahisi kuyeyushwa na maji yenye kiasi kidogo cha tindikali ya kaboni (Carbonic Acid). Tindikali ya kaboni iliyobadilisha maumbile ya miamba hii kwa kumomonyoa na kusababisha mapango yaweza kutokana na maji ya mvua yanapochanganyika na dioksidi ya kaboni (carbodioxide) hewani kabla ya kufika ardhini au na dioksidi ya kaboni inayopatikana ardhini. Maji yanapojipenyeza ardhini huendelea kupokea dioksidi ya kaboni kutoka muozo wa viumbe hai kama mimea na wanyama na kutengeneza tindikali. Tindikali ya kaboni inapopambana na madini ya kashiamu kaboneti (calcium carbonate) katika miamba ya chokaa husababisha kumomonyoka kwa miamba hii katika maeneo mbalimbali na kusababisha mapango. Mabadiliko haya huitwa kabonesheni (carbonation). Angalia mchanganuo wa kemikali ufuatao.
Wataalam wanaelezea njia mbalimbali zilizosababisha mapango katika eneo hili.
Kulingana na utafiti uliofanywa na mturi (1979), njia ya kwanza ni ile ya maji ya mvua yanapochanganyika na hewa ya “Carbondioxide” katika anga na kutengeneza tindikali (carbonic acid) ambayo inauwezo wa kuyeyusha madini ya calcium carbonate yanaunda sehemu kubwa ya miamba ya chokaa. Maji haya yenye tindikali husababisha mabadiliko kidogo yanapotelemka kuelekea ardhini. Yakifikia meza ya maji (water table) huku yakiendelea kuongezeka huzidi kuchanganyika na carbondioxide) iliyoko kwenye maji ardhini.
Kina cha maji kikiongezeka maji haya yenye tindikali huwa na uwezo wa kuyeyusha maungio ya miamba katika sehemu laini zaidi za miamba na kusababisha nyufa. Nyufa hizi huzidi kupanuliwa na maji yanayotembea na kusababisha baadhi ya mawe kuporomoka na kufanya mapango. Kasi ya maji inapozidi njia ndogondogo hupanuliwa na kuwa kubwa zaidi na upo uwezekano mapango madogo madogo hupanuliwa na kuwa kubwa zaidi na upo uwezekano mapango madogo madogo kuunganishwa na hatimaye kuwa na mfululizo wa mapango kama yanavyoonekana katika eneo hili.
Kina cha maji kinapopungua eneo huachwa likiwa kavu, lakini mabadiliko hayo huweza kuendelea kutokea chini zaidi na kusababisha njia na mapango mengine katika kina kingine ambapo hutokea muunganiko wa mapango kwa baadhi ya maeneo.
Njia nyingine ni pale ambapo inasemekana eneo hili lilikuwa chini ya usawa wa bahari yaani pembeni ya ufuko wa bahari. Mawimbi ya bahari yakamomonyoa miamba ya chokaa na kusababisha mapango. Baada ya bahari kurudi nyuma kutokana na kupungua kwa kina chake katika eneo hili, eneo la mapango likaachwa likiwa kavu.
Njia zote zilizoelezwa zimehusika katika kutokea kwa mapango haya, Mapango ya kwanza yatakuwa yalitokana na mmomonyoko wa miamba ya chokaa kutoka na maji ya ardhini yenye tindikali yaliyoyeyusha maungio ya miamba ya chokaa na kusababisha mapango. Kina cha bahari kilipopanda, maji ya bahari yalifikia eneo la mapango na mawimbi yake kusababisha kupanuliwa kwa mapango au mabadiliko katika kuta za nje na ndani ya mapango. Kina cha bahari kiliposhuka, eneo la mapango kilikuwa chini sana, maji ya mvua yenye tindikali yamekuwa na uwezo wa kuendelea kupanua na kubadilisha mfumo wa mapango.
Haijulikani mapango haya yaligunduliwa lini, bali taarifa zilizopo zinaonesha kwamba watu wa makabila yaliyoishi jirani na eneo la mapango: Wabondei, Wasambaa, Wadigo, na Wasegeju wamekuwa wakiya tumia kwa ajili ya matambiko ya mizimu tangu karne ya 16. Eneo hili la mapango kwa wakati huo lilijulikana kama eneo la mzimu wa mabavu.
Watu wanaamini habari za nguvu za mizimu katika kutatua matatizo ya uzazi, kuongeza kipato, magonjwa n.k. Kwa hivi sasa hutoka sehemu mbali mbali za Afrika Mashariki na kuja kuomba au kutambikia mizimu katika vijipango mbali mbali. Mbali na matumizi hayo, kampuni ya kigeni iliyojulikana kama “Amboni Limited” ilimiliki mashamba ya mkonge katika eneo la ta nga na kuweka eneo hili chini ya himaya yake mwaka 1892 ili kulitumia kama sehemu ya kupumzikia. Hii inatokana na mazingira mazuri na yenye utulivu ya mapango ya Amboni. Baadaye kampuni hii ilijulisha serikali kuhusu kuwepo kwa mapango haya. Serikali ilichukua hatua kutangaza eneo la mapango kuwa eneo la hifadhi mwaka 1922.
Mwaka 1937 ilipitishwa sheria ya mambo ya kale (Monuments Preservation Ordinace of 1937) iliyofuatiwa na ile ya 1953 (Monuments Preservation Ordinace of 1953) ambayo ingesaidia kulinda mambo ya kale ikiwa ni pamoja na mapango ya amboni. Mwaka 1963 serikali ya Tanganyika ikayaweka mapango chini ya usimamizi wa idara ya mambo ya kale. Mwaka 1964 serikali ilisimamisha sheria ya kikoloni ya 1937 na 1953 na kupitisha sheria ya mambo ya kale ya mwaka huo (The Antiquities Act of 1964) iliyofanyiwa marekebisho mwaka 1979 (Amendments Acts of 1979) kwa ajili ya kulinda mambo ya kale nchini. Kwa upande wa mapango ya Amboni, mbali na mambo mengine sheria inakataza kuandika au kuchora kwenye kuta za mapango.
VIVUTIO:
Yapo masimulizi mengine yanayohusu mapango haya, mfano:
Kuna simulizi zinazoelezea njia za mapango zinazoelekea Mombasa, Maweni, Mkoa wa Kilimanjaro n.k. Vile vile zipo simulizi za Osale Otango (Samuel Otango) na (Paulo Hamis). Watu hawa waliwahi kutumia kituo namba tatu ndani ya pango kubwa kama sehemu yao ya kujificha kati ya mwaka 1952 na 1956 huku wakiendesha harakati za kupambana na walowezi waliokuwa wamewekeza katika maeneo ya Tanga. Walipora mali na kutishia maisha ya walowezi katika maeneo mbalimbali. Serikali ya kikoloni iliwatambua kama wahalifu na kujaribu kuwakamata bila mafanikio kwa kipindi kirefu. Mwaka 1957 Paulo Hamis alipigwa risasi maeneo ya Lushoto na kufariki. Wananchi wa kawaida wanawakumbuka kama mashujaa walioendesha harakati za ukombozi wa watu wanyonge kutoka katika mikono ya walowezi na watawala wa kikoloni.
NUKUU:
Habari hizi zimeandikwa kutokana na masimulizi pia maelezo kutoka katika vitabu mbalimbali:-
1. Institute of Curriculum Development: Geography Coourse Book for Secondary Schools Book 3.
2. Lutgens, F.K and Edward J.Tartbuck (2000). Essentials of GEOLOGY. SEVENTH EDITION. Upper Saddle River, New Jersey: Printice-Hall, Inc.
3. Mapunda, B.B.B and Paulo Msemwa (2005). Slavaging Tanzania’s culture Heritage, Dar es Salaam. Dar es Salaam University Press.
4. Mturi, A.A (1998). Archeology of Tanzania, Dar es Salaam: The Open University of Tanzania.
5. Mturi, A.A (1975). A guide to Tongoni Ruins, Dar es Salaam.
Ama, unaweza kupata maelezo zaidi kwa kuwasiliana kupitia mawasiliano haya:
Mapango ya Amboni.
S.L.P 5028,
TANGA.
Simu: +255 784 788 990 na +255 784 546 302.
Ijumaa, Oktoba 15, 2010
HAMU HAIISHI LEO
NI MWANZO MGUMU LAKINI WENYE NEEMA, SIKU YA KULA MAZIWA NA ASALI. UNAWEZA DHANI NI SUALA LA KUFIKIRIKA LAKINI NI ZAIDI YA KIKOMO CHA MAWAZO NA FIKRA ZETU ZINAPOISHIA. SASA, TARAJIA ZAIDI MAANA MWENENDO WETU UNATULETEA MAMBO MAGUMU NA KUYAFANYA MAISHA KUWA KITU KISICHO MUHIMU NDIO MAANA LEO MWANAMKE AMA MWANAMME YUPO RADHI ASIKUPE RUHUSA YA KUCHEZEA AMA KUTUMIA GARI LAKE LINALOTUMIA MAFUTA IWE NI DIESEL AMA PETROL LAKINI MWILI UNAWEZA KUUFANYIA CHOCHOTE ILIMRADI ETI UNAITULIZA TAMAA!!! HAMU HAIISHI JAMANI.
Alhamisi, Mei 27, 2010
Jumanne, Mei 25, 2010
Jumamosi, Mei 22, 2010
CHANZO CHA KUFELI
JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KUHUSU MATOKEO YANGU YA KIDATO CHA NNE 2008
KUHUSU MATOKEO YANGU YA KIDATO CHA NNE 2008
(Nimeiandika 8th, February 2009)
Kumbukumbu ya matokeo yalivyotoka na kunihusu mimi mdogo wako.
Hayo yote yalitokana na msichana mmoja ambaye niliwahi mpenda na kujikuta na zama katika kufeli mtihani na maisha yangu kupinda. Kisa hiki kina husu yale yote yaliyonikuta shuleni na hatimaye kushindwa kutimiza ahadi yangu, ilikuwa hivi:

Nilikuwa nasoma shule moja iliyopo Arusha, kwa ujumla afya yangu haikuwa njema kwa kipindi chote cha masomo yangu. Niliugua sana muda wote wa maisha ya pale shuleni. Ndipo siku moja nikaaamua kwenda nyumbani kutibiwa.
Nilitumia mda mrefu kutibiwa baada ya hosipitali kushindwa kunitibu ndipo nikaacha shule ili niwe nyumbani kwa ajili ya matibabu, nilitibiwa kwa muda wa miezi sita hatimaye nikapata nafuu ya kuweza kuendelea na masomo ya sekondari kidato cha pili na nilifaulu mtihani wangu wa kidato hicho.
Baada ya hapo, ndipo nilipokutana na msichana mmoja aliyenipenda yeye mwenyewe nami nikajikuta nampenda kulingana na jinsi tulivyokuwa tumezoeana kwa muda mrefu, ni kweli tulipendana sana tena sana, tuliheshumiana na kila mmoja alimjali mwenzake.
Hapo ilikuwa mwezi wa kumi na mbili baada ya kumaliza mtihani wa kidato cha pili.
Matokeo yalipotoka, wote tulifaulu kuendelea na kidato cha tatu. Sasa huo ndio mda matatizo yalipoanzia hasa kwa upande wangu mimi. Ugonjwa ulianza tena kwa kasi ya ajabu ambayo muda wote ulinifanya mimi kuwa mgonjwa sana
Wakati huo huyo msichana kumbe yeye alikuwa na msela mwingine ambaye ni rafiki yangu sana, kadri nilipokuwa nikimuuliza na kumwambia kwamba yeye ana mtu mwingine alikuwa anakataaa kata kata kwamba hana. Tuliendelea na uhusiano wetu kwa muda, siku moja mimi mwenyewe nikamkuta akitoka kwao na huyo jamaa.
Kumbe alikuwa akienda mara kwa mara kwao, nikaamua kuachana nae kabisa. Kuna wakati aliniomba msamaha, alinisihi sana nami niliaamua kumsamehe kutokana na jinsi nilivyokuwa nikimpenda. Lakini kadri nilivyozidi kuwa nae ndivyo nilivyokuwa na ugua sana.
Mara kifua kuuma sana, mara malaria kali ambayo haikuwa inaisha katika mwili wangu nilivumilia sana mpaka tukamaliza kidato hicho cha tatu lakini kwangu ilikuwa shida sana. Baadae alianza dharau, chuki na kuniona mimi simfai, niliachana nae hapo sasa niliugua nusura kufa!!
Nakumbuka baada ya kuachana naye siku hiyo niliugua usiku huku akinitokea mimi akiniambia kwamba kwa nini nimemwacha huku akiniambia nitakiona. Kesho yake nilienda hospitali kupimwa nikakutwa nina malaria kali sana. Daktari aliamua kunichoma sindano za malaria nikaanguka chini nakupoteza fahamu.
Hiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza mimi kuzimia, baada ya hapo nilipozinduka na kupata nguvu niliamua kumfuata, nilienda nikamueleza yote, yeye alijibu kwamba aliomba kwa Mungu wake anifunulie mimi na kunionesha kwamba yeye alikuwa hana huyo ninaye hisi kwamba alikuwa naye.
Kwanza alicheka sana baada ya mimi kumwambia hayo yote yaliyonisibu, nikaamua kumuomba msamaha. Cha ajabu ni kwamba ugonjwa uliisha baada ya maongezi kwa muda na kesho yake nilikuwa mzima sana nikarudi shule.
Baada ya kurudi shule, niliendelea vyema na masomo yangu huku nikiendelea kumpenda na kumjali sana yeye kama mpenzi wangu, haukupita mda mrefu tukiwa kidato cha nne ndipo alipoamua kubadilika kabisa alinitenda alivyotaka. Baada ya kuona hayo mimi nikaamua kuachana nae tena kabisa mpaka mda wa wa kipindi cha mitihani kufika nilipatwa na tatizo la kufukuzwa shule na mwalimu wangu.
Kosa ni kufokeana na kiranja pale shuleni, huyo mwalimu hakujali hili wala lile akanifukuza shule. Kumbe huyo mwalimu alikuwa akitembea nae kwa maana ya mahusiano, ndipo alipopata nafasi ya kunifukuza shule huku akisema kwamba;…nilikuwa nakutafuta kwa mda mrefu.
Nilihangaika sana kuweza kumshauri huyo mwalimu anisamehe lakini alikataa kabisa nami niliamua kurudi nyumbani huku yeye akisema kwa marafiki zake kwamba amenikomoa sana mimi na kwamba alikuwa akinichukia sana mimi.
Baadae nilifanikiwa kurudi shule alipoona nimerudi akataka tena turudiane! mimi nikakataa, akawa ananitusi lakini sikuwahi hata kidogo kuongea nae jambo lolote lile hata kumjibu mpaka ikafikia hatua yeye alianza kujenga urafiki lakini nilikataa
Kwamba simtaki kabisa na kujiwekea msimamo wa aina hiyo mpaka sasa, lakini huyo mwalimu aliekuwa nae alisema jambo moja; tataona kama utafaulu mtihani wako wa mwisho!! Sikumjibu jambo lolote lile hata moja na kweli matokeo yalipotoka ndipo nikaamini kwamba nimefeli mtihani wangu lakini sikukata tama hata moja shule nitakwenda.
HII NDIO STORY YA MAISHA YALIYONIKUTA SHULENI, NIMESHINDWA LAKINI MUNGU HATANIACHA KAMWE.
Kaka, naomba kama kuna uwezekano wa mtu yeyote kutumia stori hii ili aweze kutoa mkanda ama kitabu sio jambo la uongo ni TRUE STORY. Sitasahau kamwe, jina la filamu iwe SELINA kuashiria matatizo yaliyonipata.
Mpaka sasa Yule msichana anataka turudiane lakini mimi nimeshaamua kuwa mwenyewe kabisa sitaki kupenda tena hata kidogo. Faida ya kupenda ndio hiyo iliyonikuta mimi na hasara ndio hiyo. Je, kama ni wewe ungefanyeje kuhusu yote hayo? Toa maoni yako kaka kwa kadri utavyoweza.
Hakika imeniuma sana na bado yeye anatuma salaam kwangu lakini mimi nilimjibu kwamba salaam zake ampe mpenzi wake ambaye alimuona anafaa kwake ndipo aliponitusi mimi mpaka na matusi ya mama yangu!! nilimuuliza mama yangu anamahusiano gani kati ya jambo hilo na yeye angepaswa anitusi mimi.
Kweli iliniuma sana mimi, lakini sitasahau kamwe mkasa huu ulionikuta mimi, ingawa mpaka sasa anatamani nimsamehe lakini mimi simtaki hata kidogo na wala jambo lolote kutoka kwake sihitaji kabisa.
Ahsante kunielewa.
Ni mimi mdogo wako,
E.D.M

Najaribu kufanya kile kitakachosaidia wazo lililoanza.
Wakati mwingine unaweza dhani kuwa hii siyo kawaida lakini ukweli unaonesha MAISHA ni sawa na mashindano ya aina yoyote yanayofanyika.
Kwa nini nasema hivi;
KILA SIKU INAHITAJI WAZO JIPYA, NAMNA JINSI UTAKAVYOJIKWAMUA KATIKA HALI UNAYOKABILIANA NAYO KATIKA MAZINGIRA ULIPO.
Kwa maana hiyo basi, naanza kuashiria mwanzo uliokwisha anza.
NINA MENGI YA KUONESHA
VIPI KAMA HALI HII INGEKUWA HIVYO SIKU ZOTE BILA KUBADILIKA
(No Jioni Wala Mchana na Hata Asubuhi)
**************
SIKU YA KWANZA
Ni simulizi ya kweli, iliyotokea halisi.
Tangu mwanzo hata sasa tunapoendelea.
SIKU YA KWANZA mara baada ya kuanza jambo.
Kumbuka siku ya kwanza wewe kupanda ndege.Au hivi, ile siku ya kwanza uliyokutana na ambaye kwa sasa!!, naamaanisha sasa hivi (kwa aliyeoa) ndie mama mkwe wako wakati ule ulipoenda kutoa posa.
**********
Mimi siku ya kwanza kula wali hata siikumbuki! Lakini nakumbuka siku ya kwanza kupanda gari!!... ni kisa cha kuchekesha sana kwa namna flani hivi ingawa ndani yake kuna fundisho. Hivyo ndivyo binadamu anavyokabiliana na mazingira.
************
Maisha yanaendelea kuwa na maana kutokana na mapitio, changamoto tunazokutana nazo na jinsi tunavyokabiliana nazo. Nitakupatia mfano mmoja, jinsi kipimo cha upendo kilivyo baina ya mwanamke na mwanamme. Angalia mapitio na changamoto walizokutana nazo vijana hawa wawili, kila mmoja kwa muda wake na mazingira aliyokuwemo.****************SIKU YA KWANZA NI SIMULIZI INAYOGUSA MAISHA HALISI YA BINADAMU.
Yusuph D. Mcharia.
Radio Presenter,
Story & Song wrighters, Producer and much more...!
Watoto Wanapenda Kucheza Kwenye Maji.
Jumamosi, Aprili 10, 2010
HII NI ISHARA TU, MOJA YA MAJUKUMU TUNAYOKABILIANA NAYO KILA MAWIO YANAPOFIKA NA HATA MACHWEO YANAPOJITOKEZA.
KAMA UNAWEZA JIULIZE JUU YA JUKUMU LINALOKUKABILI KILA SIKU INAYOPITA. DHAMIRA YANGU TANGU MDOGO NDIO HII NILIYOIFIKIA UKUBWANI, MTAYARISHAJI.
SASA, NAKULETEA MUHIMU YANAYOTUHUSU SOTE MAANA NATAMBUA WENGI TUNAPENDA BURUDANI.
NAYASEMA HAYA KWA SABABU NIMEMUDU KUFIKIA, ENDELEA BLOGINI...

Jumatatu, Machi 29, 2010
Hellow wote mtandanoni!!
Ni yangu imani kuwa haujambo msomaji wa blog hii.
Ni kwa siku nyingi nimekuwa kimya bila kuendeleza nia ya fikra zangu.
Namshukuru Mungu kwa jinsi anavyoendelea kuniweka katika namna ambayo kwa hakika sikuitaraji.
Kwa ufupi napenda kusema nimerejea tena.
MUZIKI WA ACAPPELLA NDIO JAMBO AMBALO LIMENICHUKULIA MDA WANGU MWINGI LENGO NIKUUFANIKISHA KWA KUUFIKISHA KATIKA NGAZI INAYOTAKIWA, WENGI WANAIITA YA KIMATAIFA.
Jumanne, Desemba 01, 2009
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)

.jpg)