Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumapili, Novemba 07, 2010

JOSEPH/YUSUPH

Jinsia: Mwanamme

Linakotumika: Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, kwa watumiaji wa Biblia.

Linavyotamkwa:
1. JO-SEF (Uingereza).
2. ZHO-ZEF (Kifaransa).
3. YO-ZEF (Kijerumani).

Linatokana na jina la kilatini lililotokana na jina la kiyunani (LOSEPHOS), lililotokana na jina la Kiebrania (YOSEF) likiwa na maana ya:

“ATAZIDISHA au ATAONGEZA” (He Will Add).

Katika agano la kale Biblia takatifu inaeleza Yusufu na Joseph ni mwana wa kumi na moja wa Yakobo (Israel).

Kwa sababu ya kupendwa sana na baba yake Yusufu alionewa wivu na ndugu zake, wakamchukia, wakamuuza akapelekwa Misri kisha wakaenda kumweleza baba yao uongo kwamba alikuwa amekufa.

Lakini huko Misri Yusufu aliongezewa neema ya Mungu akapandishwa cheo na kuwa Mshauri mkuu wa Farao.

Jina hili pia limetumiwa na watu wengine wawili ndani ya biblia takatifu waliocheza nafasi muhimu sana ya kiroho na kimaandiko ambao ni Yusufu mume wa Bikira Mariam na Yusufu tajiri wa Arimathaya aliyenunua kaburi la kifahari akalitumia kuhifadhi mwili wa Bwana Yesu Kristo baada ya kufa msalabani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni