JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KUHUSU MATOKEO YANGU YA KIDATO CHA NNE 2008
KUHUSU MATOKEO YANGU YA KIDATO CHA NNE 2008
(Nimeiandika 8th, February 2009)
Kumbukumbu ya matokeo yalivyotoka na kunihusu mimi mdogo wako.
Hayo yote yalitokana na msichana mmoja ambaye niliwahi mpenda na kujikuta na zama katika kufeli mtihani na maisha yangu kupinda. Kisa hiki kina husu yale yote yaliyonikuta shuleni na hatimaye kushindwa kutimiza ahadi yangu, ilikuwa hivi:
Hayo yote yalitokana na msichana mmoja ambaye niliwahi mpenda na kujikuta na zama katika kufeli mtihani na maisha yangu kupinda. Kisa hiki kina husu yale yote yaliyonikuta shuleni na hatimaye kushindwa kutimiza ahadi yangu, ilikuwa hivi:
Nilikuwa nasoma shule moja iliyopo Arusha, kwa ujumla afya yangu haikuwa njema kwa kipindi chote cha masomo yangu. Niliugua sana muda wote wa maisha ya pale shuleni. Ndipo siku moja nikaaamua kwenda nyumbani kutibiwa.
Nilitumia mda mrefu kutibiwa baada ya hosipitali kushindwa kunitibu ndipo nikaacha shule ili niwe nyumbani kwa ajili ya matibabu, nilitibiwa kwa muda wa miezi sita hatimaye nikapata nafuu ya kuweza kuendelea na masomo ya sekondari kidato cha pili na nilifaulu mtihani wangu wa kidato hicho.
Baada ya hapo, ndipo nilipokutana na msichana mmoja aliyenipenda yeye mwenyewe nami nikajikuta nampenda kulingana na jinsi tulivyokuwa tumezoeana kwa muda mrefu, ni kweli tulipendana sana tena sana, tuliheshumiana na kila mmoja alimjali mwenzake.
Hapo ilikuwa mwezi wa kumi na mbili baada ya kumaliza mtihani wa kidato cha pili.
Matokeo yalipotoka, wote tulifaulu kuendelea na kidato cha tatu. Sasa huo ndio mda matatizo yalipoanzia hasa kwa upande wangu mimi. Ugonjwa ulianza tena kwa kasi ya ajabu ambayo muda wote ulinifanya mimi kuwa mgonjwa sana
Wakati huo huyo msichana kumbe yeye alikuwa na msela mwingine ambaye ni rafiki yangu sana, kadri nilipokuwa nikimuuliza na kumwambia kwamba yeye ana mtu mwingine alikuwa anakataaa kata kata kwamba hana. Tuliendelea na uhusiano wetu kwa muda, siku moja mimi mwenyewe nikamkuta akitoka kwao na huyo jamaa.
Kumbe alikuwa akienda mara kwa mara kwao, nikaamua kuachana nae kabisa. Kuna wakati aliniomba msamaha, alinisihi sana nami niliaamua kumsamehe kutokana na jinsi nilivyokuwa nikimpenda. Lakini kadri nilivyozidi kuwa nae ndivyo nilivyokuwa na ugua sana.
Mara kifua kuuma sana, mara malaria kali ambayo haikuwa inaisha katika mwili wangu nilivumilia sana mpaka tukamaliza kidato hicho cha tatu lakini kwangu ilikuwa shida sana. Baadae alianza dharau, chuki na kuniona mimi simfai, niliachana nae hapo sasa niliugua nusura kufa!!
Nakumbuka baada ya kuachana naye siku hiyo niliugua usiku huku akinitokea mimi akiniambia kwamba kwa nini nimemwacha huku akiniambia nitakiona. Kesho yake nilienda hospitali kupimwa nikakutwa nina malaria kali sana. Daktari aliamua kunichoma sindano za malaria nikaanguka chini nakupoteza fahamu.
Hiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza mimi kuzimia, baada ya hapo nilipozinduka na kupata nguvu niliamua kumfuata, nilienda nikamueleza yote, yeye alijibu kwamba aliomba kwa Mungu wake anifunulie mimi na kunionesha kwamba yeye alikuwa hana huyo ninaye hisi kwamba alikuwa naye.
Kwanza alicheka sana baada ya mimi kumwambia hayo yote yaliyonisibu, nikaamua kumuomba msamaha. Cha ajabu ni kwamba ugonjwa uliisha baada ya maongezi kwa muda na kesho yake nilikuwa mzima sana nikarudi shule.
Baada ya kurudi shule, niliendelea vyema na masomo yangu huku nikiendelea kumpenda na kumjali sana yeye kama mpenzi wangu, haukupita mda mrefu tukiwa kidato cha nne ndipo alipoamua kubadilika kabisa alinitenda alivyotaka. Baada ya kuona hayo mimi nikaamua kuachana nae tena kabisa mpaka mda wa wa kipindi cha mitihani kufika nilipatwa na tatizo la kufukuzwa shule na mwalimu wangu.
Kosa ni kufokeana na kiranja pale shuleni, huyo mwalimu hakujali hili wala lile akanifukuza shule. Kumbe huyo mwalimu alikuwa akitembea nae kwa maana ya mahusiano, ndipo alipopata nafasi ya kunifukuza shule huku akisema kwamba;…nilikuwa nakutafuta kwa mda mrefu.
Nilihangaika sana kuweza kumshauri huyo mwalimu anisamehe lakini alikataa kabisa nami niliamua kurudi nyumbani huku yeye akisema kwa marafiki zake kwamba amenikomoa sana mimi na kwamba alikuwa akinichukia sana mimi.
Baadae nilifanikiwa kurudi shule alipoona nimerudi akataka tena turudiane! mimi nikakataa, akawa ananitusi lakini sikuwahi hata kidogo kuongea nae jambo lolote lile hata kumjibu mpaka ikafikia hatua yeye alianza kujenga urafiki lakini nilikataa
Kwamba simtaki kabisa na kujiwekea msimamo wa aina hiyo mpaka sasa, lakini huyo mwalimu aliekuwa nae alisema jambo moja; tataona kama utafaulu mtihani wako wa mwisho!! Sikumjibu jambo lolote lile hata moja na kweli matokeo yalipotoka ndipo nikaamini kwamba nimefeli mtihani wangu lakini sikukata tama hata moja shule nitakwenda.
HII NDIO STORY YA MAISHA YALIYONIKUTA SHULENI, NIMESHINDWA LAKINI MUNGU HATANIACHA KAMWE.
Kaka, naomba kama kuna uwezekano wa mtu yeyote kutumia stori hii ili aweze kutoa mkanda ama kitabu sio jambo la uongo ni TRUE STORY. Sitasahau kamwe, jina la filamu iwe SELINA kuashiria matatizo yaliyonipata.
Mpaka sasa Yule msichana anataka turudiane lakini mimi nimeshaamua kuwa mwenyewe kabisa sitaki kupenda tena hata kidogo. Faida ya kupenda ndio hiyo iliyonikuta mimi na hasara ndio hiyo. Je, kama ni wewe ungefanyeje kuhusu yote hayo? Toa maoni yako kaka kwa kadri utavyoweza.
Hakika imeniuma sana na bado yeye anatuma salaam kwangu lakini mimi nilimjibu kwamba salaam zake ampe mpenzi wake ambaye alimuona anafaa kwake ndipo aliponitusi mimi mpaka na matusi ya mama yangu!! nilimuuliza mama yangu anamahusiano gani kati ya jambo hilo na yeye angepaswa anitusi mimi.
Kweli iliniuma sana mimi, lakini sitasahau kamwe mkasa huu ulionikuta mimi, ingawa mpaka sasa anatamani nimsamehe lakini mimi simtaki hata kidogo na wala jambo lolote kutoka kwake sihitaji kabisa.
Ahsante kunielewa.
Ni mimi mdogo wako,
E.D.M
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni