Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumatatu, Machi 05, 2012

YALIYOJIRI WEEKEND HII





Ushindi SDA Choir ikiwa ktk mafunzo ya Muziki na mazoezi ya uimbaji. Ni moja kati ya kaya ninazo zikubali hapa Tanzania kwa sababu waliamua waimbaji wote wajifunze Muziki.




Ushindi SDA Church Choir ikiwa ktk mazoezi baada ya somo la Muziki toka kwa Mwalimu Heri Kaale, nilikuwepo hapo sijaoneka kwa sababu ndie nimefotoa hizi picha.


Kibweta kinavyoonekana kwa mbaaaaaaaali cha kanisa la Waadventista Ushindi

Mwalimu wa Muziki Heri Kaale.

Pianist Mic Ndimbo wakati wa zoezi la uimbaji.

Baadhi ya washuhudiaji ambao pia ni waimbaji wa kwaya ya vijana.




Geti la kuingilia na kutokea kanisani, mbele ni nyumba ya jirani.


Kisima cha kubatizia ktk mwelekeo wa kukisafisha.

Ndivyo kinavyoonekana.

Kwa ukaribu zaidi, hapa maji yapo usawa wa unyayo.


Kisima cha kubatizia ktk hatua za mwisho ili kifanyiwe usafi.

Jengo la Ushindi SDA Church ambapo chini ni kanisa na juu kutakuwa na Morning Star Tv Station.


Unapenda maua?

Mtangazaji wa Morning Star Radio 105.3 fm Kibaga Mwaipaja akiwa ktk kipindi cha Top 20 kinachoruka siku ya jumapili kuanzia saa 8:00 mchana hadi saa 10:00 jioni.


Kibaga Mwaipaja.


Vipi tena Dogo!!

Manase Rusaka Mtangazaji wa Morning Star Radio 105.3 fm akiwa ktk chumba cha habari.


Jamaa mmoja alitongoza msichana club usiku,wakati wanaondoka kufika njiani jamaa akapaki gari akaomba mchezo..walipomaliza kuvua nguo,bibie akamwambia jamaa subiri kwanza "Kabla hatujafanya nimesahau kukwambia mimi ni changudoa na nachaji elfu 20 kwa tendo" Jamaa akachukua wallet akampa hela yake game likaendelea.walipomaliza kuvaa demu akashangaa jamaa haendeshi gari waondoke anavuta sigara tu,akamuuliza "Mbn hatuondoki?"Jamaa akajibu "Kabla hatujaondoka nimesahau kukwambia mimi ni taxi driver na huko unakotaka twende nachaji elfu 25,lipa twende"

Daniel Ramadhani na Dr.Makalla wakirekodi kipindi cha Darubini ya Imani, ni kipindi kinachoichambua Biblia na Quar'an, wamezoea hiyo mikao kutokana na asili ya watu wanashughulika nao kiroho.

Wakati wmingine huwa wanafanya mihadhara na Waislam.

Ni ktk kujibu swali toka kwa msikilizaji.

Kazi hii ili uweze kuifanya unapewa mafunzo mbali mbali ya na historia waislam. Kanisa la Waadventitsa wa Sabato lilianzia kitu kinachoitwa Aadventist Muslim Relation AMR likiwa na lengo la kufanya mahusiano kati ya Waadventista Wa-Sabato na Waislam, na hawa ni miongoni mwa watenda kazi ktk kitengo hicho.




Nyumba za jirani na Ushindi SDA Church pamoja na Morning Star Radio 105.3 fm Mikocheni B/Bussnes Dar es salaam Tanzania.



Jamaa aliingia kanisani bila kuzima simu, wakati ibada inaendelea simu ikaita, akaingiza mkono mfukoni kuizima, kumbe ndio  kwanza kapokea, mara simu ikaaza kusema ''''mme wangu mbona hutaki kupokea simu? nimekumiss sana''' jamaa kusikia vile akabonyeza tena kuzima kumbe ndio kaweka loud spika,'''''' Sauti ikasikika kwa ukubwa ""Honey unanikera nimeletewa tetesi kumbe haupo safarini bali upo gesti na mke wa mtu'' Hebu piga picha watu ndani ya kanisa walikuwa ktk hali gani.
Baadaye kidogo basi mdau.

USHINDI NDANI YA KRISTO


Johari hii iliandikwa mnamo karne Zilizopita, lakini bado inasisimua na kuwa ya kweli kama wakati ule wa mwanzo ilipotiririka kutoka katika moyo wake na kuandikwa juu ya karatasi. Ninayafunua mawazo yangu ya ndani kabisa juu ya Upendo wa maisha yake - yaani, Muumbaji wetu.

Sio mimi ama Mchungaji, Padri, Shekhe anayetumegea hatua alizotembea katika matembezi yake na Kristo, ninamwalika kila mmoja au wote kujiunga kufaidi unono wa upendo wa Mungu. Furaha isiyoneneka juu ya "zawadi itolewayo bure kabisa" ya haki yake Mungu kwa watoto wake inabubujika katika kurasa hizi. 

Mwandishi, akigusa maisha yako binafsi, anaongea kwa moyo mkunjufu, habari za Baba yetu aliye mbinguni anayeijua fika njia ile tunayopita. Na hata hivyo Mungu huyu mwenye huruma daima husimama akiwa tayari kuongeza nguvu zake katika udhaifu wetu ili kutupatia ushindi dhidi ya dhambi, nafsi, utumwa wa kutawaliwa na hofu na mashaka. 

Kristo, kaka yetu, Kristo aliye umoja na Baba, Kristo Mwombezi wetu na Kuhani wetu Mkuu, alipigana vita ya maisha haya na kushinda, kwa niaba yetu, kwa ajili ya kila mtu. Ushindi ndani ya Kristo ni wetu sisi.

Kama vipi, pita na HAPA

Jumamosi, Machi 03, 2012

YALIYOWAHI KUTOKEA HIVI KARIBUNI.

Kutoka Kushoto: Pianist Chacha, Mtangazaji Maduhu aliyekaa mwenye miwani, Communication Director ambaye ni IT wa kanisa la Waadventista wa Sabato Manzese, Meneja wa Adventist World Radio mwenye suti na tai.

Kutoka kushoto: Pastor Katengu mmiliki wa Okoa fm iliyopo Morogoro, Pastor Mika Musa Communication Director wa Tanzania Union. Rais wa Waadventista Wa Sabato Tanzania Pastor Lekundayo, Ass.Communication Director kutoka makao makuu ya Waadventista wa Sabato Duniani Andre Brink, Communication Director wa Division ya Africa Mashariki na Kati Pastor Steven Bina, Katibu wa Confrence ya Mashariki mwa Tanzania.

Wachukua matukio kwa njia ya Picha ya mnato na kutembea.

Kutoka kushoto: Pastor Mika Musa Communication Director wa Tanzania Union. Rais wa Waadventista Wa Sabato Tanzania Pastor Lekundayo, Ass.Communication Director kutoka makao makuu ya Waadventista wa Sabato Duniani Andre Brink, Communication Director wa Division ya Africa Mashariki na Kati Pastor Steven Bina

Baadhi ya Communication Directors wakiwa nje, mimi ni mwenye miwani.

Baadhi ya Communication Directors wakiwa nje, mimi ni mwenye miwani.

Baadhi ya Communication Directors wakiwa nje, mimi ni mwenye miwani.

Umeniona hapo?


Mtangazji wa Morning Star Radio 105.3 fm Manase Rusaka.

Aliyeketi kushoto: ni Dr. Baraka Muganda Makamu wa Rais kwa ajili ya Wizara katika Chuo Kikuu cha Wasabato Washington kilichopo Marekani.  Pia is an accomplished youth ministries professional, an international motivational speaker, and a lecturer on youth ministries leadership.  He has organized and directed multiple youth leadership training programs, assisted in organizing an international conference on AIDS, advised the President of the General Conference on youth matters, and managed departmental publications on youth development. Soma habari zake zaidi  HAPA:

HAYA NI BAADHI YA MAMBO/MATUKIO/WASHIRIKI  WA  TANZANIA UNION COMMUNICATION CONVENTION

****************************************************************

DHAHAMA INAPOTOKEA KUNA HAJA YA KUUNDA TEAM ITAKAYOSHUGHULIKA NA HALI HIYO...(Kuitawala Dhahama). AINA YA WATU WANAOFAA KUTUMIKA KTK HIYO TEAM NI:
1.      KUWA NA WATU WANAOSHUGHULIKA NA MASUALA YA UFUNDI,
2.      IT,
3.      UMEME,
4.      WAANDISHI WA HABARI,
5.      WANASHERIA.
6.      MAFUNZO NI MUHIMU KWA HAWA WATU NA WAPEWE VIFAA.
7.      KTK KILA DHAHAMA VYOMBO VYA HABARI NI MUHIMU KUVITUMIA

****************************************************************

MWAKA HUU WA 2012 KUTAKUWA NA MKUTANO WA ADVENTIST TANZANIA PROFESSIONALS UTAKAOFANYIKIA DODOMA. 

MAMBO YATAKAYOFANYIKA KTK HUO MKUTANO WA  ATAP DODOMA 2012
  1. Kujilisha kiroho -  mahubiri, kaya na familia, maburudisho.
  2. Katiba –Kutakuwa na suala la kutengeneza katiba mpya.
  3. Mikakati ya kusukuma mbele gurudumu la injili.
  4. Kuchagua viongozi wapya.

Ijumaa, Machi 02, 2012

....Nisaidie kuelewa hili.


Mfano wa maada mango ni jiwe la mwamba, maada kiowevu ni maji, na maada gesi ni hewa. Hivyo plasma ama utegili ni hali ya nne ambayo si ya asili katika maisha yetu ya kila siku. Huonekana katika mifumo ya kimaada iliyo katika joto kali.

Plasma ni hali halisi ya jua. Lenyewe linafanyika na maada lakini si tena katika hali ya kawaida tunayoijua hapa duniani. Nayo ni kama gesi inayolipuka masaa yote na kufanya mnururiko wa nishati inayotufikia kama joto, mwanga na pia mawimbi ya plasma itufikiayo na kujidhihirisha kama aurora katika ncha ya kaskazini ya Dunia.

Ikiwa gesi ni ya joto kali sana elektroni zake zinaanza kuachana na atomu zao. Tabia ya hali hii ni tofauti na hali ya gesi yenyewe. Elektroni zisizoshikwa na atomu pamoja na atomu hizo katika hali ya ioni zote zinajibu kwa uga wa sumakuumeme.

Asilimia kubwa ya maada ulimwenguni iko katika hali ya utegili kwa sababu imo ndani ya nyota za angani. Kwa ajili ya matumizi ya mitambo hali ya utegili yaani ya kuionika husababishwa pia kwa leza au kwa uga wa sumakuumeme.

Utegili pia: plasma katika lugha ya fizikia, ni hali ya nne ya maada. Hali hiyo ni kama gesi ila ni ya kiioni. Nyinginezo ni hali mango (imara), kiowevu (majimaji) na gesi (kama hewa).