Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumatatu, Machi 05, 2012

USHINDI NDANI YA KRISTO


Johari hii iliandikwa mnamo karne Zilizopita, lakini bado inasisimua na kuwa ya kweli kama wakati ule wa mwanzo ilipotiririka kutoka katika moyo wake na kuandikwa juu ya karatasi. Ninayafunua mawazo yangu ya ndani kabisa juu ya Upendo wa maisha yake - yaani, Muumbaji wetu.

Sio mimi ama Mchungaji, Padri, Shekhe anayetumegea hatua alizotembea katika matembezi yake na Kristo, ninamwalika kila mmoja au wote kujiunga kufaidi unono wa upendo wa Mungu. Furaha isiyoneneka juu ya "zawadi itolewayo bure kabisa" ya haki yake Mungu kwa watoto wake inabubujika katika kurasa hizi. 

Mwandishi, akigusa maisha yako binafsi, anaongea kwa moyo mkunjufu, habari za Baba yetu aliye mbinguni anayeijua fika njia ile tunayopita. Na hata hivyo Mungu huyu mwenye huruma daima husimama akiwa tayari kuongeza nguvu zake katika udhaifu wetu ili kutupatia ushindi dhidi ya dhambi, nafsi, utumwa wa kutawaliwa na hofu na mashaka. 

Kristo, kaka yetu, Kristo aliye umoja na Baba, Kristo Mwombezi wetu na Kuhani wetu Mkuu, alipigana vita ya maisha haya na kushinda, kwa niaba yetu, kwa ajili ya kila mtu. Ushindi ndani ya Kristo ni wetu sisi.

Kama vipi, pita na HAPA

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni